Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Moh' Said na vijana wako akina Boko Haram!Sometimes huwa tunajiuliza weledi wenu nyie kama wasomi hasa mnaposhabikia vitu mnavyojua kabisa kuwa ni propaganda.Moh' Said, unasema habari za EAMWS kuhusishwa na radical islamists miaka hiyo mpaka kupigwa marufuku kwake, ilikuwa ni propaganda tu.Yes, ilikuwa ni propaganda kwa sababu unataka kuhusisha kanisa na Nyerere kwamba ndio wali-collude.Lakini kuhusu Chadema kuwa chama cha kikatoliki kwa vile tu mgombea wake aliwahi kuwa Padre- hizi sio propaganda, si ndio?Kwa mtaji huo mtaendelea kutumiwa na wanasiasa mpaka mchanganyikiwe (kama bado hamjachanganyikiwa).

Hivi hamjui kuwa ni CCM iliyotuma state agents (mashushu) ndani ya misikiti mwaka 1995, wakijifanya maustaadh, huku wakipiga kelele kuwa waislam wachague CUF ambacho kilikuwa na mgombea muislam? Hamjui kwamba walikuwa wanafanya makusudi ili wapiga kura wakione CUF kuwa chama cha kidini? Njama kama hizo walizifanya na kwa NCCR-mageuzi ionekane ni ya wachaga. Na ndio propaganda kama hizo zinatumika dhidi ya Chadema. Lakini nyie ni wepesi wa kuamini lolote lile mnaloambiwa na viongozi wenu, hata mnapoingizwa chaka! Na ndani ya chaka mmeingizwa! Si waliwaambia CCM itawapa mahakama ya kadhi, tutajiunga na OIC, msichague chama kinachoongozwa na padre, na mpaka sasa bado mnaamini hivyo?

Boko Haram na wafuasi wenzio:
Mnaaminishwa kwamba waislam wamekuwa sidelined kwenye maendeleo hapa nchini. Yet, tunaona matajiri wakubwa ni waislam. Eti wanaonewa na NECTA kwenye elimu, yet, tunaona maprofessor wengi waislam (hasa wenye asili ya bara) ambao wamepitia mfumo huo huo wa elimu. Mnasema waislam wengi ni maskini kwa sababu ya mfumo kristo, lakini sisi tuliotembea vijijini tunaona hakuna tofauti ya umasikini kati ya wanavijiji wa imani mbalimbali. Mnaaminishwa kuwa uhuru ulipiganiwa na waislam. Tukikosoa na kuwapa ukweli kuwa ulipiganiwa na wazalendo bila kujali imani zao, nyie mnasema tumekaririshwa kumsifia Nyerere na kwamba tunampinga Moh Said kwa vile yeye ni Muislam na sisi ni wakristo (hata sijui mnajuaje kuwa members ni wakristo au waislam-kwa kuangalia majina kama alivyofanya Moh kwenye simulizi zake?). Moh' Said akiwaambia nchi hii haina wapagani, ila ina waislam na wakristo, nyie mnaamini tu, almradi aliyewaambia ni ustaadh MS aliyefanya "research". Hata hapa jamvini wala hamumsomi vizuri. kiasi kuwa mmeshindwa kujua kuwa huyu mtu ana hidden motive iliyopelekea yeye ku-fabricate stories ambazo anaziita historia. Hamuwezi kumkosoa Kikwete eti tu kwa sababu ni muislam, Kimsingi, ni watu kama nyie ndio mtatucheleweshea maendeleo ya nchi. Stuka, fikirieni nje ya boksi la dini, mpate ukweli.


Nanren,

Hii forum huru kila moja na mawazo yake jitahidi kuwa mvumilivu ukisoma michango ambayo inakukera.

Sijui kwa nini unapenda kutumia neno wafuasi wa Mohamed Said, sijui wewe mfuasi wa nani?

Hata kama unapingana ki mawazo na msimamo na Mohamed Said, lakini kuna vitu unachota kwako kutoka kwenye historia ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru sana ndugu yangu Mohamed Said kwakuamua sasa kuwapa ukweli halisi wanajamvi wanaotufuatlia hapa!

Ndugu zangu wanajamvi, Mashehe aliowataja hapo juu na baadhi ya makasisi wa kikristu, ndio wali ASI serikali ya TANU iliyokuwa chini ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,

Tuipongeze serikali ya TANU kwakuzima maasi yale ya chini kwa chini na kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi na waambata wao wote wa maasi dhidi ya ukombozi wa nchi yetu takatifu.

Mohamed Said, mimi ninajua mengi huenda kuliko hata kukuzidi wewe, kinachonishangaza, mbona hukutaka kuwaambia ukweli kwenye Kitabu chako mashabiki wako hasa waislamu wenzio wanaokuunga mkono?


Waambie tu usiogope, waambie kuwa "wazee wetu akina Sheikh Hassan bin Amir waliasi, na wakakumbana na mkono wa sheria ya nchi"!

Hongera kwa vijana wa wakizalendo wa usalama wa taifa Sawaya na Kayugwa waliojitolea nafsi zao kupambana na mashehe hawa walioasi, kwakuwa walifanya kazi nzito katika mazingira magumu na wakafanikiwa.

Si umeona jina la babu yake Salum Abdallah kwenye list ya waasi walioswekwa ndani?
Siri nzima ya chuki ya Moh' Said kwa Nyerere inaanzia hapa. Simulizi za akina Sykes ilikuwa ni uchochoro tu wa kupitishia hasira zake. Na ili apate support among unsuspecting muslims, akaamua ku-concoct conspiracy ya kanisa na Nyerere na mfumo kristo dhidi ya waislam na uislam... Ndio maana tukimuuliza, kama kanisa katoliki lilikuwa na uadui na waislam, na kanisa katoliki tunajua lina mtandao mkubwa, kwanini lifanye hayo mambo hapa TZ tu? kwanini halikuwafanyia waislam wa uganda, Kenya, Mozambique, Malawi? Yeye atakujibu, "hayo sina ujuzi nayo, mimi nasimulia historia ya wazee wangu". Wafuasi wake wanamsaidi kujibu eti " ndio maana Nyerere anafanyiwa mchakato wa kuwa mwenye heri, kwa sababu amelifanyia kanisa mambo mengi". Yote haya ni kutokujua chanzo cha hizi chuki za Moh Said. The guy has grudges!
 
muogope Mungu wako mzee Said;
ukiambiwa uthibitishe unakimbilia kusema wazee wangu walinihadithia

Ithibati gani unataka kuliko haya ninayokueleza?

Ukiwa unataka ithbati ya kimahakama itabidi tufungue
kesi na tulete ushahidi mahakamani na vielelezo vingine.

Mahakama wahoji watu waliotuhumiwa kwa dhulma
na Waislam walete ushahidi.

Ikiwa serikali wanalitaka hilo naamini Waislam tuko tayari.
 
Bwana Nyerere,

Wazee wangu hawakuwa waasi kwa serikali kwani hiyo
serikali waliiweka madarakani wao wenyewe kwa mikono yao.

Nakuwekea hapa kwa ufupi kipi kilimpeleka babu yangu jela.

Nawaachia wanaukumbi waseme kama babu yangu alikuwa msaliti
au mzalendo.

Soma ukiwa akili yako umeifungua.

Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa,
kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislam
wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Wakristo
serikalini. Mashuhuri miongoni mwao walikuwa:

Sheikh Hassan bin Amir, Abdillah Schneider Plantan, Sheikh
Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi
Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein
Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela,
Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh
Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah,
Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha
Mbuzi na wengine wengi.


Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa
na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa.

Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana
na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa Nyerere.

Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu
walihusika na msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako
Sheikh Hassan bin Amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo
roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa
yake kila magharibi pale msikitini.

Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba walihamishiwa Kenya,
walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika
harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa
waangalizi wa msikiti wa Badawiy.

Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara
alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa
kivuli cha sheikh.


Hakuna katika orodha hii ya masheikh hata mmoja aliyefikishwa
mahakamani kwa kesi ya uhaini.
Jina lenye mstari Salum Abdallah ni babu yangu.

Salum Abdallah aliongoza mgomo (General Strike) wa 1947.

Salum Abdallah alikuwa mfadhili wa AA hadi TAA Tabora.

Salum Abdallah alikuwa katika kamati ya siri ya kuibuka na TANU
1954akihudhuria mikutano yote ya ''uchochezi'' dhidi ya Waingereza.

Salum Abdallah alitoa fedha nyingi kupita wote kumpa Germano Pacha
kuja Dar es Salaam kuwakilisha Western Province katika kuasisi TANU.

Salum Abdallah ni mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU
Salum Abdallah 1955 alikuwa rais muaisisi wa Tanganyika Railway
African Union (TRAU) chama hiki kilipigana bega kwa bega na TANU
katika kupigania uhuru.

Katibu wake akiwa Chrisant Kassanga Tumbo.

Salum Abdallah aliongoza mgomo wa Railway wa 1960 uliodumui siku
82 mgomo kama huu wa miezi 3 haujapata kutokea.

Viongozi wa TRAU walipokea msaada kutoka chama cha wafanyakazi wa
Reli Uingereza na chama cha wafanyakazi kutoka Ujerumani ya Mashariki.

Hiki ndicho kilichoiwezesha TRAU kudumu katika mgomo kwa miezi 3.
Wafanyakazi wakipata posho kuzikimu famila zao.

Salum Abdallah katika mkutano wa Moshi 1962 alimpinga Nyerere
katika suala la kuweka vyama vya wafanyakazi chini ya TANU.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kuzuizini.
Babu yangu hakuwa haini.

Babu yangu alikuwa mzalendo mpigania uhuru kwa vitendo toka
enzi za African Association akiwa akiwa Dar es Salaam.

Nyerere alipata hofu ya wazalendo kama hawa waliokuwa na uwezo
wa kuwakusanya wananchi pamoja kudai haki zao.

Mgomo ule wa 1960 ndiyo uliomfanya Nyerere apate hofu na Salum
Abdallah.

Akiwa jela ya Uyui taarifa zikamfika Salum Abdallah kuwa ya TRAU
na vyama vyote vya wafanyakazi vimevunjwa na Nyerere na chama
kimoja cha vibaraka NUTA kimeundwa kuwawakilisha wafanyakazi wa
nchi nzima.

Salum Abdallah hadi anaingia kaburini alikuwa na orodha ya watu wake
akiwaita waongo, vibaraka, wasaliti na wengi katika hao walikuwa katika
NUTA, TANU, na serikalini...

Julius Nyerere...
Michael Kamaliza...
Rashid Kawawa...

Wanaukumbi tafuteni majina ya watu hawa ambao babu yangu
aliwaorodhesha kama waongo, vibaraka na wasaliti.

Si tabu kuwajua.

Alipokufa 1974 TANU walifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
babu yangu na kumwita mzalendo aliyejitolea kwa hali na mali yake
kuipigania nchi yake.

Huyu alikuwa Mmnanyema kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika baba
yake Samitungo Mwekapopo aliingia nchini kama askari katika jeshi la
Wajerumani.

Bwana Nyerere huyu ndiye babu Salum Abdallah yangu ambae kaanza
harakati za kupigania uhuru wa nchin hii wala hamjui Nyerere.

Asante sana mkuu, hayo ni madai upande wa kwanza, je upande wapi (Serikali) wayajua?

Zingatia niliyokupa pale juuuu! Yale ndio madai halisi ya upande wa pili mkuu.
 
Nyerere kwenye moja ya hotuba yake alishawahi kusema kuwa alimwachia aliesema ameiweka tanzania mfukoni baada kuwasiliana na bishop Makarius lakini haikuwahi kutokea majadiliano yenye muafaka kati wa masheikh na nyerere.
 
Nanren,

Hii forum huru kila moja na mawazo yake jitahidi kuwa mvumilivu ukisoma michango ambayo inakukera.

Sijui kwa nini unapenda kutumia neno wafuasi wa Mohamed Said, sijui wewe mfuasi wa nani?

Hata kama unapingana ki mawazo na msimamo na Mohamed Said, lakini kuna vitu unachota kwako kutoka kwenye historia ya Tanganyika.

Sijui kwanini imeku-touch!?! Au...
Mimi mtu wa bara nisamehe. Kiswahili sikijui sana. Labda neno sahihi badala ya neno wafuasi ni mashabiki. Kama ni sahihi, basi, naomba kwenye post zangu huko nyuma uelewe hivyo. Otherwise, samahani kwa yeyote aliyekwazika.
 
bwana nyerere,

wazee wangu hawakuwa waasi kwa serikali kwani hiyo
serikali waliiweka madarakani wao wenyewe kwa mikono yao.

Nakuwekea hapa kwa ufupi kipi kilimpeleka babu yangu jela.

Nawaachia wanaukumbi waseme kama babu yangu alikuwa msaliti
au mzalendo.

Soma ukiwa akili yako umeifungua.

Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa,
kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na waislam
wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa wakristo
serikalini. Mashuhuri miongoni mwao walikuwa:

sheikh hassan bin amir, abdillah schneider plantan, sheikh
abdulkarim abdulwahid, maalim popo saleh, suleiman masudi
mnonji, ali migeyo, mufti sheikh hassan bin amir, sharff hussein
badawiy, shariff mwinyibaba, shariff adnan, bilali rehani waikela,
sheikh jumanne bias, maalim matar, abdalah mwamba, sheikh
hashim haji abdallah, sheikh nurdin hussein, salum abdallah,
sheikh mzee ali comoriam, sheikh al amin maftah, rajab kiguu cha
mbuzi na wengine wengi.


lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa
na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa.

Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana
na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa nyerere.

Maalim matar na shariff adnan walifungwa jela kwa sababu tu
walihusika na msikiti wa badawiy mjini dar es salaam ambako
sheikh hassan bin amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo
roho ya waumini wa tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa
yake kila magharibi pale msikitini.

Shariff hussein na nduguye mwinyibaba walihamishiwa kenya,
walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika
harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa
waangalizi wa msikiti wa badawiy.

Sheikh mzee ali comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara
alikuwa akifuatana na sheikh hassan bin amir kama vile alikuwa
kivuli cha sheikh.

Hakuna katika orodha hii ya masheikh hata mmoja aliyefikishwa
mahakamani kwa kesi ya uhaini.
Jina lenye mstari salum abdallah ni babu yangu.

Salum abdallah aliongoza mgomo (general strike) wa 1947.

Salum abdallah alikuwa mfadhili wa aa hadi taa tabora.

Salum abdallah alikuwa katika kamati ya siri ya kuibuka na tanu
1954akihudhuria mikutano yote ya ''uchochezi'' dhidi ya waingereza.

Salum abdallah alitoa fedha nyingi kupita wote kumpa germano pacha
kuja dar es salaam kuwakilisha western province katika kuasisi tanu.

Salum abdallah ni mmoja wa wanachama wa mwanzo wa tanu
salum abdallah 1955 alikuwa rais muaisisi wa tanganyika railway
african union (trau) chama hiki kilipigana bega kwa bega na tanu
katika kupigania uhuru.

Katibu wake akiwa chrisant kassanga tumbo.

Salum abdallah aliongoza mgomo wa railway wa 1960 uliodumui siku
82 mgomo kama huu wa miezi 3 haujapata kutokea.

Viongozi wa trau walipokea msaada kutoka chama cha wafanyakazi wa
reli uingereza na chama cha wafanyakazi kutoka ujerumani ya mashariki.

Hiki ndicho kilichoiwezesha trau kudumu katika mgomo kwa miezi 3.
Wafanyakazi wakipata posho kuzikimu famila zao.

Salum abdallah katika mkutano wa moshi 1962 alimpinga nyerere
katika suala la kuweka vyama vya wafanyakazi chini ya tanu.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kuzuizini.
Babu yangu hakuwa haini.

Babu yangu alikuwa mzalendo mpigania uhuru kwa vitendo toka
enzi za african association akiwa akiwa dar es salaam.

Nyerere alipata hofu ya wazalendo kama hawa waliokuwa na uwezo
wa kuwakusanya wananchi pamoja kudai haki zao.

Mgomo ule wa 1960 ndiyo uliomfanya nyerere apate hofu na salum
abdallah.

Akiwa jela ya uyui taarifa zikamfika salum abdallah kuwa trau
na vyama vyote vya wafanyakazi vimevunjwa na nyerere na chama
kimoja cha vibaraka nuta kimeundwa kuwawakilisha wafanyakazi wa
nchi nzima.

Salum abdallah hadi anaingia kaburini alikuwa na orodha ya watu wake
akiwaita waongo, vibaraka, wasaliti na wengi katika hao walikuwa katika
nuta, tanu, na serikalini...

Julius nyerere...
Michael kamaliza...
Rashid kawawa...

Wanaukumbi tafuteni majina ya watu hawa ambao babu yangu
aliwaorodhesha kama waongo, vibaraka na wasaliti.

Si tabu kuwajua.

Alipokufa 1974 tanu walifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
babu yangu na kumwita mzalendo aliyejitolea kwa hali na mali yake
kuipigania nchi yake.

Huyu alikuwa mmnanyema kizazi cha kwanza kuzaliwa tanganyika baba
yake samitungo mwekapopo aliingia nchini kama askari katika jeshi la
wajerumani.

bwana nyerere huyu ndiye babu salum abdallah yangu ambae kaanza
harakati za kupigania uhuru wa nchin hii wala hamjui nyerere.


wanataka i'lmu gani nyingine zaid ya hiii??

Chukua nukuu hii ndugu yangu,,
"maa aamanat' kablahum' min qariyatin' aha'lakna haaa..!afahum yuu'mi nuun'??
'hawakuamini wengi miongoni mwa ummah zilizoumbwa kabla yao,je wataamin hawa??narudia tena kauli hii,hawawez amini,inawakera na kuwaumiza kuona ukweli huu ukimwaga wazi wazi,hadhwarani pasi na tozo ya aina yoyote ile...!
Basi mungu na akulipe kheri ndugu moh' said kwa maarifa haya unayoyatoa kwa ndugu zako watanzania,kwa kweli wenye kunufaika tunanufaika,na wenye kukaidi wewe zidi tuh kuwashushia nondo,mioyoni mwao yanawaingia haya.
 
Kama babu yangu angekuwa msaliti angepelekwa mahakamani
na kufunguliwa mashtaka.

Hilo halikufanyika si kwake yeye hata kwa wengine.

Walokuwa wahaini walisimamishwa kizimbani na hili
kila mtu analijua na adhabu walizopewa katika hukumu
yao.

Bado mimi nimuugope Mungu?
 
Asante sana mkuu, hayo ni madai upande wa kwanza, je upande wapi (Serikali) wayajua?

Zingatia niliyokupa pale juuuu! Yale ndio madai halisi ya upande wa pili mkuu.

Nimependa sana staili yako ya kujifunza baada ya kukosa hoja umeamua kuja na mbinu mbadala anachosema Mohamed Said, unakigeuza kuwa jibu lako. Hoja ya uchochezi imepotea saizi umejikita kwenye hoja ya uasi.

Bado tunasubiri majibu ya waasi waliopewa msamaha na Nyerere na wengi kupewa vyeo na wengine kuwa mabalozi.
 
Sijui kwanini imeku-touch!?! Au...
Mimi mtu wa bara nisamehe. Kiswahili sikijui sana. Labda neno sahihi badala ya neno wafuasi ni mashabiki. Kama ni sahihi, basi, naomba kwenye post zangu huko nyuma uelewe hivyo. Otherwise, samahani kwa yeyote aliyekwazika.

Sijakwazika na chochote unapofanya mjadala wakati umeishachagua upande hata ukitoa hoja zako zinakosa nguvu.
 
ndiyo maana ndugu yangu vyuo vingi vinanialika
na wanafunzi wengi huja kwangu kwa ushauri.

Hawaendi chuo cha kivukoni.

kabisa kabisa,mtu aende chuo cha kivukoni kusoma kitu gani??
Aende kivukoni kuisoma siasa chafu ya ccm?zao la julius lililopotoka?

Abadan asilani mwerevu hawezi kwenda kivukoni,labda kama anaenda kunywa supu ya pweza na samaki wabichi,lakini sio kwenda kuongeza maarifa,pale utaambulia upotofu na mafunzo ya ufisadi tuh yanayoigharam nchi hii kwa sasa.
 
Kama babu yangu angekuwa msaliti angepelekwa mahakamani
na kufunguliwa mashtaka.

Hilo halikufanyika si kwake yeye hata kwa wengine.

Walokuwa wahaini walisimamishwa kizimbani na hili
kila mtu analijua na adhabu walizopewa katika hukumu
yao.

Bado mimi nimuugope Mungu?

Rudi kwenye sheria za nchi kisha uone rais anamamlaka gani hasa kipengele cha kumuweka mtu kizuizini.

Ni mkosaji yupi hustahili kuwekwa kizuizini na yupi hupelekwa mahakamani,

Mwaka ule wa vuguvugu za uasi wa baba yako na wazee wengine ndipo sheria ile iliridhiwa, yote hiyo nikatika kuwajali na kuwaheshimu tu, mwalimu alikuwa na uwezo wa hata kuwanyonga tena hadharani, lakini busara zake zilizotukuka akaamua kuwaweke kizuizini tu.

Hilo tu linampa sifa ya kipekee ulimwenguni, kwani hakuna kiongozi barani afrika aliyeweza kuwaweka vizuizini waasi wa serikali halali, wengi waliwanyonga tu.
 
Hapana sina chuki na mtu.
Kuacha chuki ikutawale ni sawa na kujitia jela.

Nimeandika historia hii kwa kuwa naijua.

Mke wa Kleist Sykes akiitwa Bi Mluguru biti Mussa.
Mke wa Salum Abdallah akiitwa Bi Zena biti Farijallah.

Majirani hapa Dar es Salaam.
Waume marafiki na wake zao mashoga.

Nimekuwekea taarifa hizi kujivua shutuma yako kuwa
nimepitia kwa akina Sykes kutoa dukuduku langu kuhusu
ugomvi wa babu yangu na Nyerere.

Si hivyo Kleist na babu yangu hao wote ni wazee wangu na
historia zao zimefungamana pamoja na kushikana na historia
ya Tanganyika.
 
Mzee Mohamed Said hongera sana!!! inaonyesha upeo wako ni mkubwa sana, na umejaaliwa uwezo mkubwa wa kutetea na kujibu hoja kwa weledi wa hali ya juu, pamoja na kwamba unashambuliwa na watu wenye upeo tofauti na wenye mtazamo hasi juu yako pamoja na kwamba unawajibu hoja zao kwa ukamilifu lakini kwa sababu tayari wameshakuhukumu kua ni mchochezi na mdini, basi hata ukiwaelewesha kwa ustadi wa namna gani abadan hawatakuelewa wala kukubaliana na wewe, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa umetoa somo ambalo hawakulijua hapo kabla na wamefaidika nalo a sio wao tu kila aliyepitia huu uzi kuna kitu amejifunza tofauti na tulivyoaminishwa zamani kutokana na historia ya nchi yetu.mm sikua mchangiji wa hii mada lakini nimekua naifuatilia hii mada tangu mwanzo na sio tu hii mada hua nasoma mada karibu zote hapa jf, na hata wachangiaji wote wa huu uzi wengi wanaokukejeli asilimia kubwa wanajulikana kua wao wako mrengo gani na wameonyesha wazi wazi ni wanaipinga dini fulani, kuazia Yericho nyerere, Jasusi na Jogoo aka Nguruvi hawa jamaa wana ule ubishi wa jadi na wanaile tabia ya kutaka kujifunza kitu kipya kwa njia ya ubishi, kwa kutoa kejeli, jazba na kutoa hoja zisizo kua mashiko kwa sababu tu umegusa sehemu ambayo wao hawapendi iguswe au ipewe shutuma.
 
Nimekueleza historia ya babu yangu.
Babu yangu kapigania uhuru wa nchi hii.

Historia hii ninayoeleza humu ndiyo shahidi.
Hakuwa msaliti.

Kilichompelekea kufungwa jela ni hofu ya Nyerere.
Aliogopa kupambana na yeye siku za baadae katika
uwanja tambarare wa siasa.

Huyu ni mtu aliyeongoza mgomo uliodumu siku 82.
Hiki ndicho kilichomtisha Nyerere.

Ile ati babu yangu alikuwa anaandaa jeshi la kumpindua
Nyerere ni uongo uliokubuhu.

Ndiyo maana alitengeneza orodha yake ya waongo, vibaraka
na wasaliti.

Akifurahi alikuwa akiwataja.

Kuanzia pale alijitoa TANU akajipinda katika kilimo cha tumbaku
Urambo na akafanikiwa sana.

Kafa katuachia nyuma hazina ya kumbukumbu ndiyo hii leo
nami nawarithisheni urithi wake.
 
Back
Top Bottom