Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Moh' Said na vijana wako akina Boko Haram!Sometimes huwa tunajiuliza weledi wenu nyie kama wasomi hasa mnaposhabikia vitu mnavyojua kabisa kuwa ni propaganda.Moh' Said, unasema habari za EAMWS kuhusishwa na radical islamists miaka hiyo mpaka kupigwa marufuku kwake, ilikuwa ni propaganda tu.Yes, ilikuwa ni propaganda kwa sababu unataka kuhusisha kanisa na Nyerere kwamba ndio wali-collude.Lakini kuhusu Chadema kuwa chama cha kikatoliki kwa vile tu mgombea wake aliwahi kuwa Padre- hizi sio propaganda, si ndio?Kwa mtaji huo mtaendelea kutumiwa na wanasiasa mpaka mchanganyikiwe (kama bado hamjachanganyikiwa).
Hivi hamjui kuwa ni CCM iliyotuma state agents (mashushu) ndani ya misikiti mwaka 1995, wakijifanya maustaadh, huku wakipiga kelele kuwa waislam wachague CUF ambacho kilikuwa na mgombea muislam? Hamjui kwamba walikuwa wanafanya makusudi ili wapiga kura wakione CUF kuwa chama cha kidini? Njama kama hizo walizifanya na kwa NCCR-mageuzi ionekane ni ya wachaga. Na ndio propaganda kama hizo zinatumika dhidi ya Chadema. Lakini nyie ni wepesi wa kuamini lolote lile mnaloambiwa na viongozi wenu, hata mnapoingizwa chaka! Na ndani ya chaka mmeingizwa! Si waliwaambia CCM itawapa mahakama ya kadhi, tutajiunga na OIC, msichague chama kinachoongozwa na padre, na mpaka sasa bado mnaamini hivyo?
Boko Haram na wafuasi wenzio:
Mnaaminishwa kwamba waislam wamekuwa sidelined kwenye maendeleo hapa nchini. Yet, tunaona matajiri wakubwa ni waislam. Eti wanaonewa na NECTA kwenye elimu, yet, tunaona maprofessor wengi waislam (hasa wenye asili ya bara) ambao wamepitia mfumo huo huo wa elimu. Mnasema waislam wengi ni maskini kwa sababu ya mfumo kristo, lakini sisi tuliotembea vijijini tunaona hakuna tofauti ya umasikini kati ya wanavijiji wa imani mbalimbali. Mnaaminishwa kuwa uhuru ulipiganiwa na waislam. Tukikosoa na kuwapa ukweli kuwa ulipiganiwa na wazalendo bila kujali imani zao, nyie mnasema tumekaririshwa kumsifia Nyerere na kwamba tunampinga Moh Said kwa vile yeye ni Muislam na sisi ni wakristo (hata sijui mnajuaje kuwa members ni wakristo au waislam-kwa kuangalia majina kama alivyofanya Moh kwenye simulizi zake?). Moh' Said akiwaambia nchi hii haina wapagani, ila ina waislam na wakristo, nyie mnaamini tu, almradi aliyewaambia ni ustaadh MS aliyefanya "research". Hata hapa jamvini wala hamumsomi vizuri. kiasi kuwa mmeshindwa kujua kuwa huyu mtu ana hidden motive iliyopelekea yeye ku-fabricate stories ambazo anaziita historia. Hamuwezi kumkosoa Kikwete eti tu kwa sababu ni muislam, Kimsingi, ni watu kama nyie ndio mtatucheleweshea maendeleo ya nchi. Stuka, fikirieni nje ya boksi la dini, mpate ukweli.
Nanren,
Hii forum huru kila moja na mawazo yake jitahidi kuwa mvumilivu ukisoma michango ambayo inakukera.
Sijui kwa nini unapenda kutumia neno wafuasi wa Mohamed Said, sijui wewe mfuasi wa nani?
Hata kama unapingana ki mawazo na msimamo na Mohamed Said, lakini kuna vitu unachota kwako kutoka kwenye historia ya Tanganyika.
Last edited by a moderator: