Wanajamvi wakati AA na TAA ikiwa under serious scrutiny nawarudisha kwenye Mapinduzi ya Zanzibar kidogo.
Mnakumbuka Mohamed Said alileta vipande viwili na kimoja ni hicho hapo juu kama majibu japo hayakuwa majibu.
Wickam aliomba reference na haraka Mohamed akaomba radhi kuwa hawaweza kutoa hizo reference.
Ikumbukwe kuwa suala la Kipumbwi si geni na amelishaliandikia na kuslisema sana huko nyuma. Kwahiyoo excuse ya kuwa source ni siri ima kwa kuzuia uandishi unaoendelea kama upo au kumkinga mtu si kweli na haina mashiko.
Nimeleta vkpengele hivyo kwasababu ukisoma kwa makini sana hiyo ni 'self quote' na hakuna mahali Mohamed amenukuu. Ni kawaida ya yeye kuji-quote na kusema ni reference. Narudia tena hiyo ni "self-quote''
Soma nukuu nambari moja between he lines kuna kitu kipo hapo ambacho kinaonyesha maandiko aliyonukuu si siku nyingi, pengine ni ya jana.
Natoa changamoto kwa Mohamed Said kufanya haya
Asitaje jina la mtu wala makala, kitabu, gazeti au paper na asitaje title.
Na wala asitaje mwaka, tunamuomba atoe muda (range) kwamba maneno hayo yalisemwa kati ya (mfano 1976-1986) basi
Kinyume chake iliombe radhi jamvi!
Muheshimiwa Nguruvi3,
Salaam ndugu yangu. Bado nakufuatilia bayana zako kwa makini.
Tafadhali/tafadhalini,muombeni Yericko Nyerere(kama apendavyo kujiita) atupatie sources ya Informations/statistics zake zoote hapa jamvini. Khasa tukianzia na ile khutba ya ufunguzi wake wa mada/shutuma hizi tunazozijadili kwa kina hapa jamvini.
Mengineyo yoote anayojadili au kupingana nayo hapa,lazim pia atupatie sources zake zoote. Haiyumkiniki tu kiwavi fulani akurupuke na kudai kitu fulani ni urongo au haikua vile,au kama anavyopenda kutumia neno "hakuna mantiki/logic" ,na utumbo wake mwingineo mwingi mno...
Kwa sasa inalazim tujue/atutajie hizo hoja zoote anazopinga ni kwa kutumia kigezo/sources zipi!? Au nayeye pia anatumia tu hisia na opinions zake,huku akishangiliwa!?ahaha!!
Kama kuna vitabu vyoyote,Articles,manuscripts,majina ya Historians na mengineyo mengi mno tunaomba aorodheshe hapa.
Lau kama pia alikhadithiwa naye na hao Wazee wenu huko Mikoani/kijijini atokeako au hata web- links/site na mengineyo mengi mno. Au kama kuna baadhi ya vitu/mambo yalitokea nae alikuwapo au alishuhudia enzi hizo,pia tutafurahika kuyapokea toka kwake.
Natumai ombi langu hili chechefu,utalizingatia kwa makini ndugu yangu na kuhakikisha utekelezwaji wake...kwa hishma ya kitaaluma ya Wanajamvi soote.
Niwie radhi kama kuna lolote nimenena kwenye huo uchechefu wangu,nawe labda limekukera au hukupendezwa nalo.
Ahsanta sana.
Cc;Shariff Ritz,Al Khalifa The Big Show,JokaKuu,Talib Boko Haram,Barubaru