OK. Nakupongeza kama umeelewa kuwa nimechagua upande unaosimamia 'hoja za ukweli'. Kama unanifikiria nipo upande mwingine mbali na huo, basi pole sana. Tuendelee.Sijakwazika na chochote unapofanya mjadala wakati umeishachagua upande hata ukitoa hoja zako zinakosa nguvu.
rudi kwenye sheria za nchi kisha uone rais anamamlaka gani hasa kipengele cha kumuweka mtu kizuizini.
Ni mkosaji yupi hustahili kuwekwa kizuizini na yupi hupelekwa mahakamani,
mwaka ule wa vuguvugu za uasi wa baba yako na wazee wengine ndipo sheria ile iliridhiwa, yote hiyo nikatika kuwajali na kuwaheshimu tu, mwalimu alikuwa na uwezo wa hata kuwanyonga tena hadharani, lakini busara zake zilizotukuka akaamua kuwaweke kizuizini tu.
Hilo tu linampa sifa ya kipekee ulimwenguni, kwani hakuna kiongozi barani afrika aliyeweza kuwaweka vizuizini waasi wa serikali halali, wengi waliwanyonga tu.
sasa naamini kwamba mwanakijiji anampinga kikwete kwa sababu ni muislam tu. Mbona nyerere anampamba sana huku akisahau kwamba ndie alietufikisha hapa kwa umaskini?
nimekueleza historia ya babu yangu.
Babu yangu kapigania uhuru wa nchi hii.
Historia hii ninayoeleza humu ndiyo shahidi.
Hakuwa msaliti.
Kilichompelekea kufungwa jela ni hofu ya nyerere.
Aliogopa kupambana na yeye siku za baadae katika
uwanja tambarare wa siasa.
Huyu ni mtu aliyeongoza mgomo uliodumu siku 82.
Hiki ndicho kilichomtisha nyerere.
Ile ati babu yangu alikuwa anaandaa jeshi la kumpindua
nyerere ni uongo uliokubuhu.
Ndiyo maana alitengeneza orodha yake ya waongo, vibaraka
na wasaliti.
Akifurahi alikuwa akiwataja.
Kuanzia pale alijitoa tanu akajipinda katika kilimo cha tumbaku
urambo na akafanikiwa sana.
Kafa katuachia nyuma hazina ya kumbukumbu ndiyo hii leo
nami nawarithisheni urithi wake.
Mzee Mohamed Said hongera sana!!! inaonyesha upeo wako ni mkubwa sana, na umejaaliwa uwezo mkubwa wa kutetea na kujibu hoja kwa weledi wa hali ya juu, pamoja na kwamba unashambuliwa na watu wenye upeo tofauti na wenye mtazamo hasi juu yako pamoja na kwamba unawajibu hoja zao kwa ukamilifu lakini kwa sababu tayari wameshakuhukumu kua ni mchochezi na mdini, basi hata ukiwaelewesha kwa ustadi wa namna gani abadan hawatakuelewa wala kukubaliana na wewe, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa umetoa somo ambalo hawakulijua hapo kabla na wamefaidika nalo a sio wao tu kila aliyepitia huu uzi kuna kitu amejifunza tofauti na tulivyoaminishwa zamani kutokana na historia ya nchi yetu.mm sikua mchangiji wa hii mada lakini nimekua naifuatilia hii mada tangu mwanzo na sio tu hii mada hua nasoma mada karibu zote hapa jf, na hata wachangiaji wote wa huu uzi wengi wanaokukejeli asilimia kubwa wanajulikana kua wao wako mrengo gani na wameonyesha wazi wazi ni wanaipinga dini fulani, kuazia Yericho nyerere, Jasusi na Jogoo aka Nguruvi hawa jamaa wana ule ubishi wa jadi na wanaile tabia ya kutaka kujifunza kitu kipya kwa njia ya ubishi, kwa kutoa kejeli, jazba na kutoa hoja zisizo kua mashiko kwa sababu tu umegusa sehemu ambayo wao hawapendi iguswe au ipewe shutuma.
basi julius angeonekana ana busara zaid kama angeamua kuwafungulia mashitaka ya uhaini ili kuujuza ummah wa watanzania juu ya hila kuu iliyokawa inafanywa na wazee wale kuliko kuwaweka kizuizini,ni wazi kabisa kwa kufanya vile alikuwa anahofia ukweli kudhihiri pindi pale wananchi wataamua kuhoji,na leo tumehoji kisha ukweli unadhihiri namna hii..!
Wewe unaonekana mvivu kusoma vitabu na historia kubwa unayoijua ni ile ya kupita darasani, tena ile ya tuliyosoma shule ya msingi, umekuwa muumini wa vitu vipya kwa sababu huvijui na huna uhakika navyo...unameza tu...soma ndugu
a
Bwana Nyerere,
Wazee wangu hawakuwa waasi kwa serikali kwani hiyo
serikali waliiweka madarakani wao wenyewe kwa mikono yao.
Nakuwekea hapa kwa ufupi kipi kilimpeleka babu yangu jela.
Nawaachia wanaukumbi waseme kama babu yangu alikuwa msaliti
au mzalendo.
Soma ukiwa akili yako umeifungua.
Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa,
kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislam
wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Wakristo
serikalini. Mashuhuri miongoni mwao walikuwa:
Sheikh Hassan bin Amir, Abdillah Schneider Plantan, Sheikh
Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi
Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein
Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela,
Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh
Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah,
Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha
Mbuzi na wengine wengi.
Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa
na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa.
Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana
na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa Nyerere.
Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu
walihusika na msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako
Sheikh Hassan bin Amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo
roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa
yake kila magharibi pale msikitini.
Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba walihamishiwa Kenya,
walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika
harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa
waangalizi wa msikiti wa Badawiy.
Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara
alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa
kivuli cha sheikh.
Hakuna katika orodha hii ya masheikh hata mmoja aliyefikishwa
mahakamani kwa kesi ya uhaini.
Jina lenye mstari Salum Abdallah ni babu yangu.
Salum Abdallah aliongoza mgomo (General Strike) wa 1947.
Salum Abdallah alikuwa mfadhili wa AA hadi TAA Tabora.
Salum Abdallah alikuwa katika kamati ya siri ya kuibuka na TANU
1954akihudhuria mikutano yote ya ''uchochezi'' dhidi ya Waingereza.
Salum Abdallah alitoa fedha nyingi kupita wote kumpa Germano Pacha
kuja Dar es Salaam kuwakilisha Western Province katika kuasisi TANU.
Salum Abdallah ni mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU
Salum Abdallah 1955 alikuwa rais muaisisi wa Tanganyika Railway
African Union (TRAU) chama hiki kilipigana bega kwa bega na TANU
katika kupigania uhuru.
Katibu wake akiwa Chrisant Kassanga Tumbo.
Salum Abdallah aliongoza mgomo wa Railway wa 1960 uliodumui siku
82 mgomo kama huu wa miezi 3 haujapata kutokea.
Viongozi wa TRAU walipokea msaada kutoka chama cha wafanyakazi wa
Reli Uingereza na chama cha wafanyakazi kutoka Ujerumani ya Mashariki.
Hiki ndicho kilichoiwezesha TRAU kudumu katika mgomo kwa miezi 3.
Wafanyakazi wakipata posho kuzikimu familia zao.
Salum Abdallah katika mkutano wa Moshi 1962 alimpinga Nyerere
katika suala la kuweka vyama vya wafanyakazi chini ya TANU.
Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kuzuizini.
Babu yangu hakuwa haini.
Babu yangu alikuwa mzalendo mpigania uhuru kwa vitendo toka
enzi za African Association akiwa akiwa Dar es Salaam.
Nyerere alipata hofu ya wazalendo kama hawa waliokuwa na uwezo
wa kuwakusanya wananchi pamoja kudai haki zao.
Mgomo ule wa 1960 ndiyo uliomfanya Nyerere apate hofu na Salum
Abdallah.
Akiwa jela ya Uyui taarifa zikamfika Salum Abdallah kuwa TRAU
na vyama vyote vya wafanyakazi vimevunjwa na Nyerere na chama
kimoja cha vibaraka NUTA kimeundwa kuwawakilisha wafanyakazi wa
nchi nzima.
Salum Abdallah hadi anaingia kaburini alikuwa na orodha ya watu wake
akiwaita waongo, vibaraka, wasaliti na wengi katika hao walikuwa katika
NUTA, TANU, na serikalini...
Julius Nyerere...
Michael Kamaliza...
Rashid Kawawa...
Wanaukumbi tafuteni majina ya watu hawa ambao babu yangu
aliwaorodhesha kama waongo, vibaraka na wasaliti.
Si tabu kuwajua.
Alipokufa 1974 TANU walifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
babu yangu na kumwita mzalendo aliyejitolea kwa hali na mali yake
kuipigania nchi yake.
Huyu alikuwa Mmnanyema kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika baba
yake Samitungo Mwekapopo aliingia nchini kama askari katika jeshi la
Wajerumani.
Bwana Nyerere huyu ndiye babu Salum Abdallah yangu ambae kaanza
harakati za kupigania uhuru wa nchin hii wala hamjui Nyerere.
Ikiwa una maana ya Dentation Act ya 1962 ndiyo naifahamu vyema.
Siyo kuijua tu naifahamu hata historia yake na ilichukuliwa kutoka wapi
na nani aliitilia bidii itumike.
Lakini haya tuyaache majibu ya kifedhuli yana shida zake Waswahili tunasema
itakuwa nipe nikupe mpate mpatae.
Heshima na taadhima zitaondoka.
Hii si nzuri kwa afya ya mnakasha.
Lakini kuna kisa cha Chief Kidaha Makwaia aliyefungwa Tunduru.
Taarifa zake vipi na yeye alikuwa ana mpango wa kupindua serikali?
Ndugu zangu wote mnaofuatilia mjadala huu kwa siku ya 12 leo,
Naomba nimfungue macho na akili rasmi Mzee wetu huyu mpigania Dini kwa mgongo wa Uhuru wa nchi hii.
Nitaeleza kwa kifupi tu yale anayoyalilia Mohamed Said juu ya WAZEE wake.
Ukweli nikuwa kuanzia mwaka 1955 kulianza kuibuka milengo tofauti kwa baadhi ya washarika wa ukombozi ndani ya TANU,
Hasa hasa milengo hiyo ilikuwa ni kuweka DINI mbele yaani iwe ndio tiketi halisi yakupigania uhuru na sio Utanganyika wao, na baada tu ya kupata uhuru, baadhi ya wazee waliokuwa beba kwa bega na Mwalimu WALIASI rasmi nakuanza kuendesha vita ya chini kwa chini yakumpindua Mwalimu chini DINI.
Mwalimu Nyerere kwakutumia falsafa ya malengo yake ya tangu akiwa Tabora Boys Sec Schoo, Makerere University, na pale Scotland akiwa sambamba na wanaukombozi wasomi wenzie waliweza kuanzisha mfumo stahiki wa kufuta UDINI, UKABILA, Urangi, Ukanda nk.
Waliamua kuwafanya Watanganyika kuwa kitu KIMOJA.
Sasa mgogoro ulikuja kwa WAASI, kwakuwa hawakukubaliana na sera za Serikali mpya ya Mwalimu, wakaziidisha vurugu kwakushawishi makundi kadhaa ya kiroho yaenzi uasi huo, hilo lilipelekea serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi yao!
Ndiomaana mashehe wengi walitiwa kizuizini na wengine kufukuzwa nchini.
Hilo halikuwakumba waislamu tu kwani uasi huo ulikuwa hata kwa makasisi waliotaka itikadi zao ipewe kipaumbele zaidi na serikali ya Mwalimu Nyerere.
Mohamed Said kuwa mkweli, waambie ukweli watanzania (waislamu) kuwa wazee wako waliasi serikali mpya ya mwalimu na ndipo madhila hayo wakayapata.
Mzee Mwanakijiji, Mohamed Said, Nguruvi3, Jasusi,
..yaani hata kwenye winter la Edinburgh SCOTLAND Mwalimu alikuwa anadunda na kaptura, suruali ameijua alipokutana na wazee wa D'Salaam??
Companero,
..ile document uliyosema utatuletea vipi mkuu?
..au umeanza likizo mpya?
nipo kaka Mohamed Said 'atamuua' huyu kijana
Anampa ngumi za KO
Mzee Said, babu yako si alikuwa miiongoni mwa wale "radical Muslims" wa mwaka 1957 ambao walitaka kumuondoa Nyerere kama kiongozi wa TANU kwa sababu ya Ukristu wake? na ilikuwa ni mara ya pili kujaribu kufanya hivyo?
Mzee Said, babu yako si alikuwa miiongoni mwa wale "radical Muslims" wa mwaka 1957 ambao walitaka kumuondoa Nyerere kama kiongozi wa TANU kwa sababu ya Ukristu wake? na ilikuwa ni mara ya pili kujaribu kufanya hivyo?