Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Wameeshiwa hao. mwenyezimungu ametwambia. muislam 1 sawa na wakiristo 10. nimeona mwenyewe katika mjadala huu
 
Mzee wangu, unakataa jambo linaloonekana kwa macho na akili?
 
Bwana Nyerere siku zote nakuasa.
Tulia, soma, fanya utafiti kisha andika.

Hebu kanunue kitabu changu usome.

Zogo lililotishia kukigawa chama halikuwa 1957.
Ilikuwa 1958 katika Kura Tatu na kufuatiwa na
ugomvi wa Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere.

Ndipo Saleh Muhsin, Mashado Plantan, Abdallah
Mohamed na wana TANU wengine wakajitoa TANU
na kuunda AMNUT.

Babu yangu hakuwaunga mkono hawa ndugu zake.

Cha kustaajabisha alikuwa tayari kesha kuwa na ugomvi
na Waislam wenzake katika msikiti alosaidia kujenga.

Kwake yeye Nyerere alikuwa mtu wake hataki aguswe na mtu.
 
Hapana Mzee Mohamed. Hapa hauusemei moyo wako. Hakuna binadamu aliyeumbwa hivo. Hata mimi ningekuwa wewe ningetafuta namna ya kulipiza kisasi kwa Mwalimu. Elewa tu kwamba Mwalimu hayupo, hatarudi. Wazee wako hawa hawapo, hawatarudi. Tanzania na Watanzania wapo, wataendelea kuwepo kizazi hadi kingine. Uislam na Ukristo upo, utaendelea kuwepo. Tusiivuruge NCHI

Kwa kweli nilikuwa nashangaa mno kuwa ni DINI peke yake ilikusukuma kuandika ulioyaandika. Nikupe pole sana kwa yaliyomkuta babu yako. Kujenga nchi isiyo na DINI wala KABILA haikuwa kazi ndogo. Wapo waliokumbwa dhoruba hizi. Hata waliomuua Mzee Karume kule Kisiwandui ni kwa sababu ya visasi kama hivi.
 
Ona sasa! Kati ya hawa wazee wako na Mwalimu ni nani hasa alikuwa MDINI? AMNUT ilikuwa ya kidini?
 


wape wapee...!
Wakimeza wakitema ni khiayari yaoo,
ukweli dawa yake ni kuusema tuh.
Nawewe katu usichoke kuusema.
 
Bwana Nyerere,
Vipi Chief Kidaha Makwaia.

Kasota sana Tunduru kizuizini.

Unazo taarifa zake kuwa alikuwa
anaandaa majeshi kupindua serikali?

Je, Chief Msabila Lugusha...
Dr Wilbard Mwanjisi...
Dr Michael Lugazia...

Walii wa Allah Maalim Mohamed Matar
Mtu ambae hakujishughulisha na lolote katika
mambo ya kidunia ila dhikr na kusomesha Qur'an...
 
mzee said, babu yako si alikuwa miiongoni mwa wale "radical muslims" wa mwaka 1957 ambao walitaka kumuondoa nyerere kama kiongozi wa tanu kwa sababu ya ukristu wake? Na ilikuwa ni mara ya pili kujaribu kufanya hivyo?

busara za mzee mwanakijiji leo zaporomokea kwenye udini??
Afanalekii..!,,what a shame.!
Chutama mzee mwanakijiji,aibu hii tunaishuhudia.,udini haufai mzee mwanakijiji.
 
Nyerere unazungumza hayo ya nchi kutokuwa na dini leo?
Mbona tuko humu tunapambana?

Mambo yeshavurugika.
Legacy ya Nyerere ndiyo hii.

Historia inaanza kuhukumu.
Mwalimu aliacha NCHI moja. Isiyo na DINI. Alisimamia kwa dhati KATBA na sheria za nchi. Sasa tumeacha msingi huo. Tunarudi tulikokua huku kila mtu hata Rais mwenye nguvu nyingi kikatiba analialia kuliko hata sisi. Nimemsikia akilia hata huko Ufaransa.
 
Nyerere unazungumza hayo ya nchi kutokuwa na dini leo?
Mbona tuko humu tunapambana?

Mambo yeshavurugika.
Legacy ya Nyerere ndiyo hii.

Historia inaanza kuhukumu.

Nipo hapa kwaajili ya kuzuia mbegu ya uasi uliyoipanda isienee kwa wasio wako!
 
Mkuu ninafahamu vema jinsi Machifu walivyopokea sera ya mwalimu yakuvunja himaya zao na madhila waliyokutana nayo,

Wengi waliwekwa kizuizini kwakukaidi sera hiyo ya kuliweka taifa pamoja!

Chifu Kidaha ni mmoja wao wawalioonja joto la jiwe.
 
Siwezi kuweka chuki.
Hatujapata kuwa na chuki. Wazee wangu walipofukuzwa TANU Office 1963.
Walirejea majumbani kwao wakakaa hadi umauti ulipowafika.

Hapana Mohamed Said hawakurejea majumbani kwao na kukaa, baada ya AMNUT kukataliwa na Watanganyika kwa umoja wao, Waislaam kwa Wakristo, waliivamia jumuiya iliyoanzishwa na Wahindi, Isma'ili Khoja ya Aga Khan na kujaribu kuendeleza chokochoko zao za kisiasa kupitia mgongo wa EAMWS. Jinsi ile ile walivyoleta chochoko ndani ya TANU ndiyo hivyo hivyo unaleta uchochezi wako na sasa wenye uelewa mdogo wamevamia jukwaa kwa lengo moja tu, kuvuruga mjadala...hakuna hatari kama ya wenye uelewa mdogo wanapotumiwa na watu kama wewe. Lakini kama walivyoshindwa wazee wako, hivyo hivyo utashindwa na njama zako za kupandikiza chuki. Kama kuna urithi waliokuachia wazee wako ni chuki kwa Mwalimu Julius Nyerere na hii chuki itakutafuna hadi unaungana nao.
 

Ndiyo uzuri wa darsa tunajifunza mengi Mag3, tudadavulie hicho kisa jinsi walivyovamia EAMWS tupe na orodha yao hao wazee.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ninafahamu vema jinsi Machifu walivyopokea sera ya mwalimu yakuvunja himaya zao na madhila waliyokutana nayo,

Wengi waliwekwa kizuizini kwakukaidi sera hiyo ya kuliweka taifa pamoja!

Chifu Kidaha ni mmoja wao wawalioonja joto la jiwe.
Ngoja tuone hii issue Mohamed Said atavyo e overblow beyond all proportions
 
Last edited by a moderator:

Jamaa kapigwa butwaa, alidhani atawaokota kumbe kaokotwa!
 
Ndiyo uzuri wa darsa tunajifunza mengi Mag3, tudadavulie hicho kisa jinsi walivyovamia EAMWS tupe na orodha yao hao wazee.
Ritz, umewahi kujiuliza kwa nini walioianzisha EAMWS, Aga Khan, hawakulalamika na badala yake wanaolalamika ni wazee wa Mohamed Said? Mbona Aga Khan na jamii ya isma'ili waliendelea kushirikiana na TANU na serikali hadi leo. Mtu mzuri wa kumwuliza hilo swali ni huyo bingwa wenu wa simulizi na anapata wanaoziamini ngano zake. Kwa kukusaidia tu tafuta listi ya viongozi waliokuwa nyuma ya AMNUT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…