Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Unaamini Sivalon ndie sauti ya Wakristu kama wewe unavyojipa mamlaka ya sauti ya Waislamu nchini?
 

"GOAT" Mohamed Said,

Umenikumbusha mbali umemtaja marehemu Sheikh Mohamed Ayoub, zamani nikienda Tanga lazima nipite kumsikiliza, nikitoka hapo nakwenda Kigombe kwa kina mzee Mohamed Kizigo, napita Madaga, kupata muogo wa nazi kwa tasi, pamoja na ndizi malindi, ha haa ha gombesugu, upo Al Habiby.

CC: kahtaan, hargeisa,
 
Last edited by a moderator:
Unaamini Sivalon ndie sauti ya Wakristu kama wewe unavyojipa mamlaka ya sauti ya Waislamu nchini?

Yericko,

Hilo swali labda wewe ndiyo wa kulitafutia jibu.

Kitabu kimechapwa Ndanda na kikajauzwa hapa
Dar es Salaam Cathedral Bookshop.

Kuhusu nafasi yangu kwa Waislam hilo mie siwezi
kujibu kitu.

Waulize Waislam wenyewe.
 

Yericko,

Hilo swali labda wewe ndiyo wa kulitafutia jibu.

Kitabu kimechapwa Ndanda na kikajauzwa hapa
Dar es Salaam Cathedral Bookshop.

Kuhusu nafasi yangu kwa Waislam hilo mie siwezi
kujibu kitu.

Waulize Waislam wenyewe.
Waislam umewavuruga na kuwagawa mapande na kitabu chako. Kwa kweli dhambi hii mbaya itakutafuna hadi kaburini
 

Yericko,

Hilo swali labda wewe ndiyo wa kulitafutia jibu.

Kitabu kimechapwa Ndanda na kikajauzwa hapa
Dar es Salaam Cathedral Bookshop.

Kuhusu nafasi yangu kwa Waislam hilo mie siwezi
kujibu kitu.

Waulize Waislam wenyewe.

Kuchapywa Ndanda na kuuzwa kwenye maduka ya vitabu ya kikristu hiyo ni tiketi ya sauti ya ukristu?

Mbona wewe kitabu chako kinauzwa misikitini lakini sio Sauti ya Waislamu?

Hoja nikuwa mawazo ya mtu yasichukuliwe kuwa ndio sauti ya taasisi!
 



Naam.,
Swadakta kabisa Mwalimu Wangu,
Na tunafaham watu kama hao nia yao ni kuja kuharibu hali ya hewa na kukutusi huku wakijua ya kwamba wewe huwez na huna tarbia ya kujibishana na waungwana kwa lugha za aina hiyo,
Sisi hali hiyo inatupa simanzi sana,cha ajabu yericko anawaambia heko na kuwapongeza,
Insha allah sisi tupo hapa kusoma maarifa,
Tupo kwa utuvu na ustahimilivu wa hali ya juu sana,Tunakufuatilia kwa makini sana,
Hatuishii tuh kumeza meza kama wanavyodhani,bali tunasoma na kupima kisha tunasadikisha...
 
Kuchapywa Ndanda na kuuzwa kwenye maduka ya vitabu ya kikristu hiyo ni tiketi ya sauti ya ukristu?

Mbona wewe kitabu chako kinauzwa misikitini lakini sio Sauti ya Waislamu?

Hoja nikuwa mawazo ya mtu yasichukuliwe kuwa ndio sauti ya taasisi!


Yericko,

Kama kuchapwa Ndanda na kitabu kuuzwa Cathedral Bookshop si tija mimi sina
la kusema.

Kuwa mimi ni sauti ya Waislam.
Hilo nimeshakueleza bora uwaulize Waislam kwanza kabla ya wewe kuwasemea.

Ila nitakujuvya kitu kimoja.

Nishaalikwa kuzungumza misikiti mingi sana hapa Dar es Salaam na nje ya Dar
es Salaam.

Nimekuwekea hapa vyuo nilivyozungumza nk. nk.
Na mada zangu zinahusu Uislam katika Tanzania.

Unaweza wewe mwenyewe kuchuja.
 

The Big Show,

Natambua mnataabika sana kwa yale yanipatayo humu.

Huwa nakutana na vijana mjini wengine wala siwajui.

Wananipongeza na kusema kuwa wanafaidika kwa huu
mnakasha ingawa na wao husema huumia sana wanapoona
nakashifiwa nk. nk.

Juu ya haya yote ni lazima tustahamili na tusomeshe asa kheri
huenda faida kubwa ikapatikana.

Wapi tungepata uwanja wa kuwaelimisha watu tena kwa wepesi
kama si fursa hii ya hapa JF?

Haya yatukutayo ndiyo gharama yake.
Tuwe na subra.
 
Waislam umewavuruga na kuwagawa mapande na kitabu chako. Kwa kweli dhambi hii mbaya itakutafuna hadi kaburini


Hapo mwanzo ndio kweli tulikuwa tumevurugwa kwa kutojua ukweli na uhalisia,
Ila kwa sasa tuvurugwe kwa kipi sasa??
Yan ukweli uje utuvuruge tena??
Umeshawahi skia waislam wanalumbana eti kisa kuelezwa kwa historia hii??
Sisi tumekaa zetu kimyaa,na kuwashangaa kwa mshangao wa ajabu wale waliokadhani ya kwamba ukweli huu utaendelea kufichwa milele na milele,
MIMI NADHANI WATU WALIOVURUGWA SIO WAISLAM,BALI MLIOVURUGWA NI NYINYI MLIOKAWA MNAIAMINI ILE HISTORIA YA KIVUKONI KAMA MASAHAFU AU MAANDIKO MATAKATIFU..
YANAPOKUJA KUFUMULIWA MAMBO KAMA HAYA AMBAYO MLIKUWA HAMYAJUI KWA KWELI MMECHANGANYIKIWA NA MMEVURUGWA MOJA KWA MOJA...
 

Ndugu Mohamed Said,
Mwalimu,Nimekufaham vyema,
Nimefarijika kwa kusikia hayo kutoka kwako,
SHUKRANI JAZILLAH...
 
Last edited by a moderator:
Waislam umewavuruga na kuwagawa mapande na kitabu chako. Kwa kweli dhambi hii mbaya itakutafuna hadi kaburini

Wild Card,

Una ushahidi wa hayo usemayo?

Facts on the ground hazisemi hivyo.

Kila shughuli, kila hafla ya shule, msikiti nk.nk mialiko
inamiminika nyumbani.

Nikenda kuswali ile misikiti ya pembeni najificha maana
lazima nitasimamishwa Waislam wanione nk. nk.

Alhamdulilah.
Wewe unasema nimewagawa Waislam!

Lete ushahidi.
Propaganda hizo ziliwezekana 1968 wakati wa mgogogro wa EAMWS.

Kwa sasa ni mchuzi uliochujuka.
 


Ati yeye anadhani tumevurugika,mambo sasa yamefika hadi bungeni kina Zitto Kabwe wanayazungumza bila hofu bila kufumba fumba macho,yeye anadhani kuanza sasa kwa kupingwa kwa bakwata na mifano kama hiyo yeye anadhani ni kuvurugwa..!!!
Ukweli unawezaje kumvuruga mtu??fumbo lilifumbwa kisha limekuja kufumbuliwa kisha mtu abakie kwenye kitendawili tuh??
Waliovurugwa ni wao na washirika wao,waislam tupo imara na moyoni hatuna chuki,bali tuna furaha kwa kuwa tuna uhakika hadi wao wenyewe wanajua kuwa ukweli sisi tumeujua,
Kazi kwao,kusuka ama kunyoa,kila mtu aamin kile anachokiamin,
Wanasema ni nchi ya kidemokrasia hii,sasa ntima nyongo wa nini??
 
Last edited by a moderator:
Mfano mdogo tu Mohamed; Sasa hivi ipo misikiti ya wanaBAKWATA na isio. Mufti wa Tanzania sio wa Waislam wote. Wewe mwenyewe hakuna hafla hata moja inayoandaliwa na BAKWATA utahudhuria!

Wewe na akina Ponda tu. Unawaandalia uvamizi wa Markaz, unaandaa hotuba zao misikitini,...

Umoja wa Waislam unaonekana kidogo kwenye kugawana vyeo na madaraka serikalini tu. Uliona juzi waziri wa elimu alivyolindwa na Wabunge Waislam?
 
Hakuna wa kuibadili historia ile ya Kivukoni. Ndio inayofundishwa mashuleni, vyuoni. Unatarajia kitabu cha Mohamed kibadili historia ilioandikwa na wengi?

Wanafunzi wataendelea kufundishwa kuwa Rais na Mwenyekiti pekee wa TANU tangu ilipoanzishwa hadi kifo chake ni Mwalimu. Ni kichaa tu anayeweza kufundisha wanafunzi kuwa TANU ilianzia Burma!
 


Wild Card,
Huenda unajua lakini unapenda tupimane ubavu hapa jamvini.

Nitakupa mfano mwepesi wa wewe kuuelewa.

Bakwata kwa Waislam ni sawa na Wanamaombi kwa Wakatoliki.

Hivi unaweza kuwaambia Wakatoliki kuwa mmegawika kwa sababu
miongoni mwemu kuna Wanamaombi na nyie hamtaki kuwatambua.

Nataka tuagane na hii.
BBC 1960s mahojiano kati ya mtangazaji wa BBC Mwingereza na
Nyerere.

Huyu Mzungu akijulikana sana kwa maswali yake ya kuwafedhehesha
watu na alikuwa anayapanga na kuyaleta bado dakika chacha kipindi
kumalizika.

Basi wakati kipindi kinasogelea ukingoni akamtumbukizia Nyerere, ''Mr
Pressident what about these persisitng civil unrests in many African
countries, what have you got to say about this.''

Nyerere kwanza akajifanya kama kashangaa, kashtuka swali zito limempiga.
Alipofungua kinywa kusema akasema maneno haya, ''I think we should begin
with Northern Ireland.''

Mzungu kinywa kimejaa mate.
Control Room jamaa anampiga signal kuwa muda unayoyoma.

Mzungu alikuwa amekutana na saizi yake.

Wild Card,
Mambo ndiyo hayo.

Unaweza kumwambia Kadinali Pengo awaheshimu Wanamaombi au ahudhurie
shughuli yao yoyote?
 


Wild Card,

Hayo ulosema ni kweli kabisa.

Hakuna wa kuibadili historia ya Kivukoni.

Ni kweli kuwa itaendelea kufundishwa mashuleni.

Lakini sisi hufundisha hiyo na hufundisha historia ya kweli.

Vijana wanaelewa.

Wild Card,

Mimi nimetembea kwingi duniani nasomesha hii historia na sidhani kama
mimi ni mwendawazimu.
 

Nicholas,

Nadhani umesoma kuna mtu amenishauri nikupuuze.
Kwanza hujajitetea kuwa huna mizaha...na uhuni ktk kujibu hoja za msingi.

Kunipuuza kutaamanish akitu kimoja umekula kona...Pia ujue mimi sipo hapa kuku appease au kuvutika na utetezi wako wa hisia na dhana tuu.

Kwa hiyo naomba ujikaze tuu na kuwa strong...hatutaacha "...any stone unturned....".So km umezoea kupewa "All knowing status..".Now expect something very different.Tumeshaona madhara ya hii mizaha yako.Hooligans wanaanza ongezeka nchini.Wewe ndio kiumbe pekee unayeamini watu ambao hawajawahi jega chohcote ktk maisha yao binafsi wajifiche ktk "uongo wako"..Kanisa katoliki linaweza mfanya masikini mvuvi wa pemba?
Lakini kabla sijafanya hilo ningependa kwanza usome kipande hiki.
Huenda kikakusaidia kunielewa:
Unaanza tena kuogea vitu vingine,wakati umeulizwa kitu kingine..Una divert bila haya aibu tena kiholela tuu.Nikisoma hapa nitawaelewa walichoandika wengine na si wewe.Kwani wewe ndie character ndani ya hivyo vitabu hadi nikuelewe wewe kwa kuvisoma?

Hizi logic zenu sijui mmezipata wapi?

Ni udogo tuu wa fikra zako...ila Uislam ni Adui wa Ukrstu tangu day one,kwa hiyo huwezi potosha watu kuwa umeanza kuwa adui Tanzania.Pamekuwa na vita ya uislam na Ukristu Tangu....Tagu uislam kuiteka Uturuki, syria, lebanon, uislam kuteka na kugeuza spain kuwa taifa la kiislam huku makanisa yakigeuzwa kuwa misikiti, Uturuki kuishambulia ulaya....."Pirates wa Morocco" walikuwa hatari kuliko wasomali na wao walikuwa wakiwauza mateka hadi wa kizungu kuwa watumwa na wanawake kuwekwa ktk madanguro..Islam ni adui wa Wabudha kuanzia burma,thailand na hata china....wahindu tangua walipoingi ana kujenga Taj Mahal hadi leo....Uislam ni Adui wa wayahudi na siku zote wanaangalia kuwaangamiza.

Kwa Tanzania raia(Watu) walikuwa ktk amani aliyoijenga Nyerere, kumbuka nilikuwambia Nyerere alikuwamwadilifu na mpenda haki hadi waingereza walijiona kuwa salama ktk mikono ya nyerere hata kama walitoautiana sana ktk mitizamo.Kwa hiyo hakuna mahali kanisa lingetangaza kuwa uislam ni adui number moja wakati lipo wazi...Ila watakuwa walitangaza kuwa threat..Na ililkuwa wazi sana ...hata kabla wamissionary hawajaamua kuhamia Pugu ili kuwa salama.

Kwa upande mmoja unataka dhania kuwa waislam nao hawakuwa ktk mikakati..waislam walisumbu asana ktk kupata uhuru. waislam wameapotosha sana Historia ya Ukristu ktk ukombozi na maendeleo ya hii nchi.Wamegeuza taifa letu kuwa la Kuwakilisha uislam na utamaduni wa kiarabu. Sasa hivi vitu vya kiislam, na kiarabu zimegeuzwa na kuitwa za kitanzania na kiafrica.

Maharamia wa kiislam wamegeuzwa kuwa mashujaa wa nchi, serikali muda wote imekuwa ikitumikia misikiti, Bakwata inatumia hela ya serikali, hija imekuwa ikigharamiwa na serikali, vurugu za waislam zimekuwa zikiigharimu sana serikali.Siku hizi dini ya kiislama ndio kipaumbele, ibada zao zimeingizwa ktk maisha ya kawadia ya wasio waislam.Kwanini srikali inatumia nguvu nyingi kuhakikisha waislam wanafanya ibada ya kuchinja,tena kuchinja hata ktk ibada za wengine?

Sasa hivi waislam ndio wapo huru kuchoma makanisa, kuuwa viongozi wa makanisa kirahisi tuu km wanavyokwenda kufanya tambiko.

Nani ni victima hapa?Badala ya ke waislam wamejaribus ana kuplay VICTIMS.

Kanisa lilijua kuwa walihitajia kujipanga na kufanya mambo kwa akili ili isitokee wakajikuta wanafanyia kilichotokea halafu viongozi waaanze chekelea au kuwahukumu wakristu kwa mashitaka y akijinga km kukojolea copy ya quran ambayo kanunua aliyeikojoloea au kuichoma.

Harakati za waislam wa mwazo wala hazikuhitaji kuambiwa kuw azilikuwa na malengo maovu....ndio maana hata wakahamishia makao makuu dar...Kenya walishazimika..hadi leo Agha Khan anafanya juhudi kubwa sana....na kipindi cha JK hawa jamaa wamezidi imarika sana ktk killa Nyanja...mashitaka mengi ya watumishi na taasisi shirika na Agha Khan...huwa JK huaymaliza mwenyewe.

The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa.
Si ajabu kuona mwislam mwenye hela iliyo idle akifanya mambo ya hatari km kufadhili ugaidi na mengine.Hiyo POLITICAL POWER INAYOSEMWA inakuumbua tuu hapa.Unasema waislam walibaguliwa wakati hapa unanukuu jinsi walivyokuwa na nguvu za kisiasa.

Nashukuru kwa hilo.
Nicholas,
Who is targeting who?

Na nani afanyae mzaha hapa JF?

Pitia posts zangu.

Hizo zitakufungulia mlango wa kupita unijue kama mimi
ni mtu makini ama mtu wa mizaha.
Mbona unazidi ongeza mizaha?Naona uanuliza maswali ulitakiw auwe umejibu muda mrefu...sasa maswali km "nani? sijui nini" hayaonyeshi km unatakiwa kubali au kataa na kujinasua ktk nilichokuambia.Nimekuambia "Unaleta Mizaha hapa".ni statement rahisi inayokueleza wewe na unachofanya...sasa kona nyingi za nini?

Yaani unanipa assignment ya kukutoa ktk shutuma dhidi yako?Inawezekana vipi "Mshtakiwa amtake mshtaki akatafute facts za kumtetea mshtakiwa?".Something might be very wrong in you mind.

umeanza porojo za kwenye chai,...Nilishakuambia possibility za watu hata wasio wasomi au wasio wajuzi sana kukaribishwa ktk vyuo vikuu ili kupresent kwa watu vitu fulani.Ila hapa nataka kukuonyesha ujinga ktk hiyo statement yako.

Wapi utapata watu wanaotaka watu wenye ujuzi wa kuyaelezea matatizo yao ambayao wao wameayaona na wanataka kuyajua kwa undani?Watu wanawaiata watu wa KUJA WAPA SOLUTIONS NA SI MABINGWA WA KUELEZEA MATATIZO YAO.Mtu mwenye kansa atakaje wewe umwelezea kwa undaji jinsi anpata maumivu,au mwenye njaa umwelezee kwa uandani kuhusu maumivu ya tumbo badala ya tiba na chakula?

NI WEWE MTU WA KWANZA UANYEDHANI WATU WANAHITAJI WATU WANAOJUA KUELEZEA MATATIZO YAO NA SI MAJIBU YAKE.

Ni aibu sana pamoja kwenda kote huko hujui ulikwenda fanya nini na walikuita kwa sababu gani...?Pole sana ,ndio maana nakuambia unakwenda chafua sana Africa,na fikra zenu za kiislama na kiarabu mkidhani dunia itakaa ikubali kuwa ni za kiafrica.Pengine wanakutafuta ili kuweza break network ya ugaidi na wafadhili wake.Its not a joke,majasusi wa US huweza facilitate,vitu bila criminal kujua....watu vijana wabeba unga au magaidi ambao wakifika ubalozi tuu wanashangaa ,viza yao haisumbui km kwa wale wanaotaka kwenda kihalali, baadaye hawa wabeba unga/magaidi mambo yao huenda vizuri sana lakin baadaye hujasaidia sana kuwakamata wafadhili wao.

Kwa hiyo hata wewe unaweza kuwa ktk List..
 

Sasa kma unajua hawezi ibadili kwanini usimwambie aachane na huo mpango?
 

Huyo ndie Mwalimu. Kwa nini migogoro ya Africa ndio inayokuzwa tu huku NI wanachinjana. Jibu hilo la Mwalimu linafanana kimaudhui na lile alilotoa kwa yule mwandishi wa Nairobi juu ya utawala wa Mzee Mwinyi na Mwalimu.

Wanamaombi na Kanisa Katoliki ni tofauti sana na BAKWATA na Waislamu wa Tanzania. Labda kama umeanza kufikiri na kuzeeka vibaya. Sidhani kama unawaelewa wanamaombi na Padre Nkwera na mambo yao vinginevyo usingewalinganisha na BAKWATA ambayo imejaa viongozi makini sana wa dini ya Kiislam, wanaoweka utaifa MBELE.
 
Ndugu

Habari za sijui kumpuuza au kumuweka mtu kwenye list hilo huliwezi kabisa ndugu yangu!

Wewe vumilia hoja na upambane nazo tu mpaka kieleweke!

Haha..jamaa wamepeana dili ili akimbie...soon ataanza kukulia hivyohivyo..Nataka danganya watu kuwa yeye hafanyi uhuni na mizaha kwa vile anaamini yeye ni mheshimiwa na mstaarabu...wakati badala ya kujibu kitu alichoulizwa anaweka quotes za mamabo tofauti, au ahat anapotezea kwa kufnaya dedications zao, au anahdithia vitu tofauti...na kuna sehemu kageuza kauliza uliyomwambia kuwa wewe ni maji.Alichojibu alijipunuza na kuwa mdogo sana.Kwa tunaolewa ktk maandiko ya kiislam matusi yemkuwa ni sehemu ya mizaha ya kawaida kabisa ktk kipindi cha mtume, kwa hiyo haishangazi sana kuona uhuni, na mizaha ya huyu jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…