Yericko Nyerere,
IMEKUWAJE UMEHAMA KWENYE ILE POST YA AWALI UMEFUNGUA NYINGINE KWA SOMO HILI HILI?
Wanaukumbi rudini kwenye post ile ya ''Maaskofu...'' nimeweka postings huenda mkafaidika Insha Allah.
Nimekupa majibu ya maswali yako kwenye ile post ya mwanzoni.
Hata hivyo nakuwekea majibu yangu hapa chini:
1) Nimeathirika kwa kuona wazee wangu hawamo katika historia kwa hiyo hawatakuwamo katika kumbukumbu kama mashujaa wazalendo waliopigana kuung'oa ukoloni Tanganyika.
2) (Hilo la taifa sina haki ya kulijibu watajibu wenyewe wenye mamlaka mimi nitawajibia Waislam). Kizazi kijacho hakitajua ushujaa wa Waislam katika kupinga dhulma kama moja ya mafunzo ya Allah. Pili hawatajua nguvu iliyokuwapo katika Uislam Tanganyika katika karne ya 20 nguvu iliyopelekea kupigana na Wajerumani katika vita vya Maji Maji 1905.
3) Babu yangu Salum Abdallah alikuwa katika African Association na TANU na aliongoza mgomo (general strike) ya 1947 Tabora na 1953 yeye na wenzake walifanya mkutano wa mwisho na wa siri wa TAA kutayarisha mjumbe Germano Pacha kuhudhuria kuasisiwa kwa TANU Dar es Salaam 7 Julai 1954. Juu ya haya alikuwa mmoja wa wafadhili wa chama. 1955 aliasisi Tanganyika Railway African Union (TRAU) akiwa mwenyekiti wa kwanza. 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82. Huu hadi leo umebaki mgomo wa kihistoria hawajaweza wafanyakazi kugoma kwa miezi 3.
4) Nilitegemea Nyerere angeliwaadhimisha katika uhai wake angalau kwa kuwataja au kuwapa heshima zao stahiki lakini akawa anakebehi juhudi za TAA na kufikia kusema kuwa hakumbuki Abdulwahid Sykes alikuwa na nafasi gani katika chama yeye alipoingia TAA Dar es Salaam mwaka 1953. (Nikawa na taarifa nyingine kuwa hakuwa anapenda Waislam wahisishwe na juhudi za kuikomba Tangnayika au yeye binafsi kuhusishwa na Abdu Sykes, Kiyate Mshumi, Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir na wengine wengi.) Kabla ya kustaafu alitoa medali 3, 979 kuwaadhimisha Watanzania walioifanyia makubwa nchi yetu. Hata mmoja katika wale waliopigania uhuru wa Tanganyika alikuwa katika ile orodha.
5) (Sijalielewa swali labda unifafanulie).
6) Najua mengi kiasi changu katika historia ya Uislam duniani lakini kitabu changu ni kuhusu Waislam wa Tanganyika.
7) Nilichoandika ni historia ya uhuru wa Tanganyika na mchango wa Waislam katika vita ile. Jina la kitabu linajieleza.
8) Huwezi kulazimisha watu sina uwezo huo nilichoandika ni historia ya wazee wangu wakati wa kupigania uhuru. Halikadhalika sina uwezo wa kulazimisha vyuo vinialike. Naalikwa kwa kuwa wameona watanufaika na elimu yangu katika somo hilo.
9) Nawatambua wote 17 na najua hadi historia zao. Kuna wengine walistahili wawepo katika ile orodha ya waasisi wa TANU lakini hakuwapo kwa kuwa mkutano usingeweza kuhudhuriwa na kila mtu. Mfano Sheikh Hassan bin Amir, Dk. Michael Lugazia, Ali Migeyo, Hamza Mwapachu na wengine wengi.