Kwanza nikupongeze mkuu, na nikupe pole kwani mjadala wewe unachukua karibu wiki ya tatu sasa,
Nimeamua kuuleta hapa peupe kwakuwa kule mjadala huu ulijificha chini ya Tamko la maaskofu, lakini hapa tunapata uwanja mpana wakujadiliana kwa hoja kile ukiitacho historia upande wa pili na kile nikiitacho mimi kuwa ni uchochezi na uhaini.
Nikirudi kwenye majibu ya maswali yangu, Jibu lako la kwanza tu linakutoa kwenye maana ya ulichoandika!
Mfano: Unasema,
"Nimeathirika kwa kuona wazee wangu hawamo katika historia kwa hiyo hawatakuwamo katika kumbukumbu kama mashujaa wazalendo waliopigana kuung'oa ukoloni Tanganyika".
Hii inakupa nguvu ya kusema ni historia ya uhuru upande wapili?
Unataka kukiambia kizazi hiki kuwa kila aliyesikia au kuhisi mzazi wake alishiriki katika uhuru wa nchi hii na hayumo kwenye historia aje na kitabu na kukiita historia mpya ya UHURU na kubeza vingine kikiwemo chako?
Katika majibu yako unajichanganya sana, mara useme ni historia ya uhuru upande wa pili, mara histori ya waislamu na sasa unasema ni historia ya wazee wako, Je sisi tusimamie wapi?
Weka sawa kwenye jibu la kwanza tu hapo ili twende mbele mkuu!