Tunarudi pale pale ndugu yangu. Research methodology, nakuomba ukasome jinsi ya kufanya research. Lakini nikwambie kitu, mtu akininong´oneza kitu sitoiita fact. Lakini, watu 10, 20, 30....100 wakiwa wananinong´oneza jambo hilo hilo kuwa ni A, nitawajibika na nitalazimika kuiita kuwa ninacho nong´onezwa ni fact. Nikuulize kitu. Kwa mtazamo wako, research aliofanya mzee Mohamed Said unadhani amesikiliza simulizi ya mtu mmoja au ya watu wengi? Na si pia simulizi tu, ametumia sources tafauti katika kuwasilisha kile alichokiuna kwenye research yake. Nawasilisha
Iko siku nazungumza na rafiki yangu mmoja.
Yeye ni Harvard graduate. Tumejuana katika haya haya mambo ya tafiti na kuandika. Baba yake alisoma Oxford 1945. Nilimpa kitu nilichoandika kuhusu Peter Colmore. (wanaukumbi wanaweza kumtafuta kwenye google).
Akanipigia simu kutoka Washington anakoishi.
Tukazungumza sana maana kilichomgusa sana ni kuwa wale wote niliowataja katika paper ile mimi nikiwajua kabisa wakati ni mdogo.
Nikamwambia kuwa mimi nilipokuwa mtoto wa miaka kama 12 nikimjua Peter Colmore na nikenda hadi ofisini kwake kwani ofisi yake ilikuwa karibu na tulipokuwa tukiishi.
Akaniuliza yaani hawa wote wewe ukiwajua? Nikamwabia sio nikiwajua na wao wakinijua. Kumtuliza nikamwambia kuwa kwa wakati ule hawa walikuwa watu kama watu wengine wakija kwetu kwa baba yangu.
Wakati ule miaka ya 1960 hakuna aliyewaza kuwa haya mambo yatakuja kuwa makubwa kiasi hiki kiasi ukilkhadithia habari zao hii leo uonekane muongo kwa jinsi ya umaarufu wao.
Nikamwambia baba yangu alimjua Nyerere kwa kutambulishwa na Abdu Sykes na wakampokea kama kijana mwenzao.
Baba yangu na Abdu Sykes wakati ule wote walikuwa na miaka 28.
Nyerere alikuwa na umri wa miaka 30 mkubwa kidogo kwao.
Huwa nasema mtoto yoyote yule kama engelizaliwa katika wakati ule na watu hawa basi hii elimu angeipata maana ni vitu nikiviona na
vingine nikihadithiwa.
Ndiyo maana hucheka ninapoambiwa mbona hukumhoji yule na yule na yule.
Niwahoji nini na hao wametoka bara wamakuja Dar es Salaam baba yangu kawaona?
Mimi wazee wangu wananitosha kwa rejea ya historia ya uhuru.
Natafuta kitu nikikipata Insha Allah nitakiweka hapa ukumbini ili tufahamiane vyema.