Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Labda nikuulize kwa nini unataka maswali hayo yote nijbu mimi peke yangu ilhal humu ukumbini
ni jamajamala?

Huu ukumbi hauna ubaguzi kila mtu yuko huru kuchangia na ndiyo maana unaona mijadala inastawi.
Huu mjadala ukishakuwa baina ya watu wawili, mie na wewe utapoteza maana.

Mkuu Mohamed Said, ningependa unijibu wewe kwa vile, tofauti zetu kwenye mijadala ya nyuma, ilikuwa ni kati ya wewe na waliokuwa "wanakuelewa" kwa upande mmoja na sisi ambao tulikuwa "hatukuelewi" kwa upande mwingine. Masimulizi yako ndio yalikuwa yakitenganisha hizi pande mbili.

Lakini pia, ni kwamba, ninapendelea uungwana wako katika kujibu, ukilinganisha na wengine wa upande huo.

Hivyo, basi, naomba urejee tena post yangu ya awali, ambapo nimekuuliza kama bado unaamini ile misingi ya "kutofautiana kwetu". Post yenyewe ni hii hapa chini

Swali kwa @[Mohamed said]

Siku za nyuma, kwenye threads zako tulitofautiana katika mambo kadhaa, wewe ukiwa unasaidiwa na barubaru, mdondoaji, faizafoxy na topical just to mention a few. Katika mambo ambayo tulitofautiana ni pamoja na misingi ya "historia" yako kwamba:

1. Vita ya maji maji ilikuwa ni baina ya Waislam na Wakristo.

2. Hapa nchini kuna waislam na wakristo tu, hamna wapagani.

3. Majina yanaashiria dini fulani, kwa mfano Ally Songea lazima alikuwa muislam, na John Smith lazima alikuwa mkristo.

4. Kwamba kwa ujumla, waislam Tanzania ni wengi kuliko wakristo, ila kwasabau ya kukandamizwa/uonevu kwa waislam, ndio maana waislam wanakuwa wachache katika elimu ya juu, makazini na serikalini

5. Kwamba kanisa katoliki (Tanzania) lilikuwa na bado lina uadui na uislam na lina mpango mkakati wa kudhoofisha uislam afrika mashariki.

6. Mkatoliki Nyerere alikuwa anatimiza maagizo ya kanisa kuutokomeza uislam na ndio maana hata wizara ya elimu iliwahi kuongozwa na padre, na kwamba hata kupendekezwa kwake na kanisa kwenye sainthood kunatokana na kazi aliyofanya ya kudhibiti uislam.

Je bado unaamini kama nilivyoeleza hapo juu? Kama bado unaamini nitaomba ufafanuzi japo kidogo, sababu ya kuamini kwako.

Naomba swali hili lijibiwe na Mohamed Said na si mwingine wa "upande" huo.
 
Nyerere aliitumia gari hiyo 1955-1960,dereva alikuwa Said Tanu,baadaye akaikabidhi kwa Tanu Youth League.Gari inaitwa Austin Morris

Ni kweli kabisa, ipo makumbusho ya Taifa hapa Dar,

Kama bado upo jirani hapo Makumbusho mda huu hebu sogea upige picha gari ya kwanza kabisa kutoka kushoto mwa banda hilo, gari hiyo ya kwanza kushoto ni nyeupe hivi, alipewa na D. Azizi kama sikosei kidogo,
 
Mkuu Jokakuu,

Nimesoma maelezo ya Mohamed Said kuhusu Mshume Kiyate alivyomkirimu mwalim hadi kumpa pesa, chakula n.k.
Mohamed akaenda mbali zaidi na kusema Ditopile alipoelezea mchango wa Kiyate, Magazeti yalipotosha kwa kusema alimdhalilisha Nyerere kwa maneno ''kulishwa''. Hapa Mohamed anatuambia kuwa kuna kusoma habari na kupotosha habari kunakoweza kutokea. Fair enough!

Ukisoma maelezo ya vitabu tuhumiwa utaona kilichotokea ni kuchukua baadhi ya mistari na kupoteza dhana nzima.
Sina maana kila kinachosemwa hakikuandikwa, ninamaanisha kuwa kuna sehemu imechukuliwa sentensi tu na kuacha maudhui ya aya nzima. Sina hakika kama hakuna upotoshaji kama ule aliofanyiwa Ditopile.

Lakini pia lazima watu wasome vitabu vya ngano za Mzee Said kwa kufahamu kuwa yapo mambo yaliyokuwa pre-determined kuandikwa na hivyo hutafutiwa eneo tu.

Ukisoma majibu kwa Yericko Nyerere kuhusu Mshume Kiyate, Mohamed ameelekeza tuhuma zake kwa Nyerere hasa pale anapodai kuwa kulikuwa na zipo hujuma za jina lake kutopewa mtaa. Kwamba Nyerere alifanya hivyo kama sehemu ya dharau na chuki kwa wazee wake.

Anachosahau Mohamed ni kuwa Tangu Uhuru, madiwani wa jiji la Dar es Salaam kwa asilimia zaidi ya 80 hadi sasa ni Waislam wakiongozwa na Mameya Waislam tena wazee wake akina Kitwana Kondo, Sykes, Abouu n.k.
Hakuna kumbu kumbu kama walifanya chochote na kuzuiwa zaidi ya wao kuwa sehemu ya mabadiliko ya majina kama UWT/Bibi Titi n.k. Why Nyerere na sio madiwani? Kwanini Moshi waenzi watu wao Dar washindwe? Ni kosa la nani!

Mfano huu ni kuonyesha kuwa yapo mazingira yaliyoandaliwa ili kujenga mazingira yenye ushahidi usiokuwepo.
Hapo ndipo ''vitabu husika'' huelezwa kwa undani kwasababu kuna mstari mmoja au miwili inayoweza chomolewa na ku-fit the purpose.

Fikiria hivi, mambo yote yaliyotokea kati ya 1954 hadi 1985 yalimhusu Nyerere kama mtu. Leo Mohamed anasema serikali ikae na Waislam iongee nao kuhusu tatizo. Kwanini Waislam wasitake kukaa na Mwinyi, Mkapa au Kikwete bali serikali.
Lini mambo ya taifa yametoka kwa mtu na kuwa serikali? Mbona huko nyuma haitajwi serikali anatajwa Nyerere na kwanini leo hatajwi Kikwete inatajwa serikali.

Nitamwelewa kama atasema hivi, Waislam wanataka kukaa kitako na Kikwete kuelezea kadhia yao wasikilizwe.
Asiishie hapo tu, ni lazima na ni wajibu wa mtu anayetafuta suluhu kuweka kila kitu mezani.
Mohamed hawezi kutuambia kuna kadhai lakini hatuambia anafikiri suluhisho ni nini.

Hii ni kwasababu tayari ameshajenga mazingira ya ''wasikilizwe'' na wala si kusikilizwa bali kutekelezewa.
Hiyo ndio pre-determined condition ambazo zinashangaza ndani ya masimulizi na ngano za mzee wetu.

Ametoa madai kitabu kimepigwa marufuku, hajaeleza ni tamko la nani na lini! Ameshauriwa viwekwe hapa anatoa bei ya vitabu! Yote haya ni kwa kujua kuwa vitabu hivyo vikitua jamvini kwa wale wasiovisoma awali au waliosoma kwa ushabiki, ngano inaweza kuchukua mweleko mpya kabisa.

Mzee wangu Mohamed Said naomba nitendee haki mjukuu wako nahitaji kuyaelewa haya;

nakuomba sana sana mzee wangu jibu hizo hoja za nguruvi3 hapo juu wengine hapa ni kizazi cha 1990's kwa hakika napata faida kubwa sana nikifuatilia mjadala kama huu.

Na tangu uanze mnakasha huu nimekuwa nafuatilia hoja juu ya hoja pasipo kuweka neno; kwakuwa mimi ni maamuma katika hili... lakini mtima wangu haujaridhika kwa tokumjibu Nguruvi3 Tafadhali fanyia kazi ombi langu.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa, ipo makumbusho ya Taifa hapa Dar,

Kama bado upo jirani hapo Makumbusho mda huu hebu sogea upige picha gari ya kwanza kabisa kutoka kushoto mwa banda hilo, gari hiyo ya kwanza kushoto ni nyeupe hivi, alipewa na D. Azizi kama sikosei kidogo,

Ahsante sana.
Insha Allah nitafanya hivyo.

Nakuwekea hapa taazia ya Grimshaw kwa Kiingereza uone ilivyosomeka katika
uhalisia wake:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 601"] When Abdulwahid died the Ministry of Information issued a press release announcing that the President had attended the funeral of Abdulwahid Sykes.[1] Surprisingly the press release gave few details of his government service, completely eclipsing his checkered political career. It was an Englishman, Brendon Grimshaw, the editor of Tanganyika Standard, who published a fitting obituary to Abdulwahid describing him as: ‘one of the architects of the independence movement and one of the men who helped launch President Nyerere on his political carrier...'

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] The obituary also paid glowing tribute to the family on its contribution to the political development of Tanganyika by mentioning that ‘much of the desire among Africans for a powerful political party in Tanzania came from the drive of the Sykes family'. [2] It is said that this recognition of Abdulwahid as one of the founding fathers of the nation became a focus of attack from certain members of the TANU leadership. They were overheard grumbling in the corridors of the TANU headquarters in Dar es Salaam that Ally and Abbas Sykes were trying to glorify their elder brother.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[1] See Press Release A/2746/68 IT/1.322 of 13 th October, 1968. East Africana, University of Dar es Salaam.

[2] Sunday News, 20 th October, 1968.
 
Abdulwahid alipofariki Wizara ya Habari ilitoa taarifa ikieleza kuwa Rais Nyerere
amehudhuria maziko ya Abdulwahid Sykes.

Kingine kinachostaajabisha ni kuwa taarifa ile ilitoa maelezo machache ya uajiriwa
wake katika serikali na kuacha maelezo muhimu ya Abdulwahid katika siasa.

Ilikuwa Mwingereza, Brendon Grimshaw, mhariri wa Tanganyika Standard, ndiye
aliyempa Abdulwahid heshima na hadhi anayostahili baada ya kifo chake kwa
kuchapisha taaízia ambayo ilimweleza Abdulwahid kama: ''mmoja wa wapangaji
wa vuguvugu la kudai uhuru na mmoja wa watu waliomsaidi Nyerere kuingia katika
siasa.''

Taazia ile ilitoa sifa kemkem kwa ukoo wa Sykes katika kuleta maendeleo ya siasa
Tanganyika kwa kusema kuwa, ''msukumo mkubwa wa Waafrika wa Tanganyika kupata
chama cha siasa chenye nguvu ulitokana na juhudi za ukoo wa Sykes.''

Inasemekana taaízia hii iliyompa marehemu Abdulwahid heshima na sifa za uzalendo wa
hali ya juu iliwaudhi baadhi ya viongozi katika TANU.

Viongozi hao wakawa wakisikika wakisema kuwa Ally na Abbas Sykes walikuwa wanajaribu
kumtukuza kaka yao.

(''Tanganyika Standard'' 20th October 1968).

Hali hii ilijitokeza tena wakati CCM ilipokuwa ikitafiti historia yake.

Hassan Upeka,[1]mmoja katika wasaidizi wa utafiti ule alipeleka katika jopo lile la utafiti na
uandishi wa historia ya TANU, mahojiano aliyofanya na Abdulwahid miaka mingi iliyopita
kuhusu historia ya TANU.

Hassan Upeka alifahamishwa kuwa historia inayoandikwa haimhusu Abdulwahid Sykes.

Uandishi huo wa historia ya TANU ndio uliomjumuisha Kreluu na ndio uliozaa Historia ya TANU ya Kivukoni?

Uliratibiwa na serikali ya Mzee Nyerere?

Kwanini Abdulwahid Sykes walimtenga na historia hiyo kwakusema haimuhusu?
 
Mzee wangu Mohamed Said naomba nitendee haki mjukuu wako nahitaji kuyaelewa haya;

nakuomba sana sana mzee wangu jibu hizo hoja za nguruvi3 hapo juu wengine hapa ni kizazi cha 1990's kwa hakika napata faida kubwa sana nikifuatilia mjadala kama huu.

Na tangu uanze mnakasha huu nimekuwa nafuatilia hoja juu ya hoja pasipo kuweka neno; kwakuwa mimi ni maamuma katika hili... lakini mtima wangu haujaridhika kwa tokumjibu Nguruvi3 Tafadhali fanyia kazi ombi langu.

Hebu Insha Allah niwekee hayo maswali kwa mpangilio wa swali la kwanza ni kitu kadhaa,
swali la pili ni kitu kadhaa nk.
 
Ni kweli kabisa, ipo makumbusho ya Taifa hapa Dar,

Kama bado upo jirani hapo Makumbusho mda huu hebu sogea upige picha gari ya kwanza kabisa kutoka kushoto mwa banda hilo, gari hiyo ya kwanza kushoto ni nyeupe hivi, alipewa na D. Azizi kama sikosei kidogo,
Nasikia huyu D aziz alikufa akiwa masikini na eti kuhuduria mkutano wa kizota,ambao waasisi wote walialikwa,ilibidi apewe msaada wa nguo Mohamed Said hii habari inawezekana vipi kuwa ya ukweli,wakati huu ni ukoo unaojiweza-au ndio propaganda za kumkandamiza Nyerere
 
Last edited by a moderator:
Uandishi huo wa historia ya TANU ndio uliomjumuisha Kreluu na ndio uliozaa Historia ya TANU ya Kivukoni?

Uliratibiwa na serikali ya Mzee Nyerere?

Kwanini Abdulwahid Sykes walimtenga na historia hiyo kwakusema haimuhusu?

Historia ya kwanza ilikuwa ndiyo hiyo ya Abdu na Dk. Kleruu.
Hii siyo ya Kivukoni.

Historia ya Kivukoni ni hii ya pili ambayo walikataa Abdu asitajwe.

Kwa nini Abdu asitajwe ni lile tatizo la kutaka historia ya uhuru ianze
na Nyerere.

Sasa ukishamleta Abdu itabidi umlete na baba yake kama waasisi wa
harakati dhidi ya Waingereza.

Nyerere hakupenda jambo hili.

Wakati ule Nyerere ndiye alikuwa kwenye kiti.
 
Nasikia huyu D aziz alikufa akiwa masikini na eti kuhuduria mkutano wa kizota,ambao waasisi wote walialikwa,ilibidi apewe msaada wa nguo Mohamed Said hii habari inawezekana vipi kuwa ya ukweli,wakati huu ni ukoo unaojiweza-au ndio propaganda za kumkandamiza Nyerere

Amini ndugu yangu.
Mimi nimekwenda kwa Dossa Mlandizi.

Alinipeleka Ally Sykes.
Niliona hali ya Dossa ''patheitic.''

Kisa cha Dossa na nguo nikumbushe
wakati mwingine nitakihadithia hapa Insha Allah.

Hata mimi kama wewe nilijiuliza inawezekanaje?
Huu ndiyo ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nyerere mbele ya kadamnasi alisema hakumbuki Abdu
alikuwa na cheo gani katika TAA.

kasema maneno haya mbele ya Wazee wa Dar es Salaam
mwaka 1985 katika hotuba yake ya kuaga baada ya kustaafu
urais wa Tanzania.

Hotuba ile wanaogopa hata kuirudia kwa sababu ni fedheha
kubwa kwa Nyerere.

Kama kuna mwanaukumbi anaweza kuipata na atuwekee hapa
tuisikilize.
 
Mradi huo wa uandishi wa historia ya TANU uliosimamiwa na Abdu na Dk. Kleruu ulifanikiwa kuzaa kitabu?

Uandshi wa pili uliomtenga Abdu, Unatumia ushahidi upi kuhalalisha kauli yako kuwa Mzee Nyerere hakupenda jambo hilo?.
 
Hebu Insha Allah niwekee hayo maswali kwa mpangilio wa swali la kwanza ni kitu kadhaa,swali la pili ni kitu kadhaa nk.
Remote,
nayaweka maswali katika mpangilio anaoutaka Mohamed ili tulitendee jamvi haki nikizingatia maoni ya wanajamvi wengi walioyaona na kuyaelewa. Nategemea naye atayajadili kwa mpangilio ulioletwa. Nitarejea
 
Hakuna KIPYA kitachozalishwa katika mpango huo, bali makusanyo yaleyale ya kweli ndio yaunde historia ili kuondoa dhana ya kila mtu/watu kuamini lake katika Historia ya Nchi hii.

Kwaujumla historia huwa inajiandika, tunachofanya sisi nikukusanya tu kumbukumbu hizo nakuhifadhi katika maandishi.

Bwana Yericko,
Unasema kuwa Mwalimu Nyerere aliwakusanya vijana wa Dar es Salaam akaunda TANU.

Nakuwekea hapa chini watu waliohudhuria mkutano wa kwanza wa
TANU Ukumbi wa Arnatouglo kisha niambie katika hawa Nyerere
alikuwa akifahamiana na nani kwa undani amwendee amuambiye
mambo yakuanzisha chama cha siasa.

Elewa kuwa katika miaka ile 1950 hilo lilikuwa jambo la hatari sana:

''mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban
watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa
Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza,
Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha
Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio,
Denis Phombeah na wengineo.
..''

Ukipitia hiyo orodha hapo juu waliokuwa wakimjua Nyerere walikuwa Abdu
na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate na wengineo.

Unataka kusema kuwa Nyerere ndiyo aliwaendea hawa?
Wengi katika hawa kumbuka walikuwa watu wazima hawakuwa vijana.

Vijana uliowakusudia ndiyo hawa?
Schneider Plantan, Makisi Mbwana na Iddi Tulio?

Nyerere aliwajulia wapi wazee hawa?
 
Amini ndugu yangu.
Mimi nimekwenda kwa Dossa Mlandizi.

Alinipeleka Ally Sykes.
Niliona hali ya Dossa ''patheitic.''

Kisa cha Dossa na nguo nikumbushe
wakati mwingine nitakihadithia hapa Insha Allah.

Hata mimi kama wewe nilijiuliza inawezekanaje?
Huu ndiyo ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nyerere mbele ya kadamnasi alisema hakumbuki Abdu
alikuwa na cheo gani katika TAA.

kasema maneno haya mbele ya Wazee wa Dar es Salaam
mwaka 1985 katika hotuba yake ya kuaga baada ya kustaafu
urais wa Tanzania.

Hotuba ile wanaogopa hata kuirudia kwa sababu ni fedheha
kubwa kwa Nyerere.

Kama kuna mwanaukumbi anaweza kuipata na atuwekee hapa
tuisikilize.
Hii haingii akilini, sasa serikali imemtupa D Aziz,ina maana na mwanae wa kumzaa Hamza Aziz nae alimtupa baba yake-how there is something being hidden from the world- baada ya kufariki wanae wakaanza kugombania nyumba zake kariakoo-sasa mtasemaje alikuwa hajiwezi AU mlitaka fadhila ilipwe mara 100
 
Mohamed Said,

Kuna huyu mtu anaitwa Dome Okochi Budohi, raia wa Kenya mmoja wa viongozi wa TAA na muasisi wa TANU.

Kuna mwanabodi yeyote anayejua habari zake.

Huyu mtu muhimu sana kwenye historia ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Nasikia huyu D aziz alikufa akiwa masikini na eti kuhuduria mkutano wa kizota,ambao waasisi wote walialikwa,ilibidi apewe msaada wa nguo Mohamed Said hii habari inawezekana vipi kuwa ya ukweli,wakati huu ni ukoo unaojiweza-au ndio propaganda za kumkandamiza Nyerere

Sio kweli, Dossa Azizi alikuwa na ukwasi wakutosha, kwa lugha nyingine tunaweza kusema kuwa alikuwa sehemu ya matajiri wazalendo wa Tanganyika, kama walivyokuwa akina Chifu Marealle, Chifu Sapi na wengine.

Hata wanae wamerithi utajiri mkubwa wa majengo mitaa ya kariakoo. Alihamia Kibaha kama ilivyo desturi ya wazarendo wa kiafrika kutopenda vurugu za kimaendelea (kukaa sehemu iliyotulia)

Hizo ni propaganda zilezile!
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka ilikuwa tarehe 27 mwezi wa nne mwaka 1985 Mwalimu Nyerere alitoa medali 3,979 katika viwanja vya Ikulu.

Medali hizo aliziita za waliochangia katika maendeleo ya taifa kuna mwanabodi yeyote anaweza kutuwekea orodha ya hao watu.

Ili darsa linatufunza mengi sana.
 
Mradi huo wa uandishi wa historia ya TANU uliosimamiwa na Abdu na Dk. Kleruu ulifanikiwa kuzaa kitabu?

Uandshi wa pili uliomtenga Abdu, Unatumia ushahidi upi kuhalalisha kauli yako kuwa Mzee Nyerere hakupenda jambo hilo?.

Ushahidi wa kimahakama huwezi kuupata katika utafiti kama huu.

Lakini Abdu alijitoa na alisema kuwa anajitoa kwa kuwa Nyerere
hafurahishwi na jinsi yeye alivyokuwa anaeleza historia ya uhuru.

Mradi ule ulizaa kitabu.
Mswada ule wa Kleruu uliibiwa pale TANU Hq.

Huyo jamaa aliouiba akafanya mabadiliko katika kazi ile kisha
akatoa kitabu.

Na kitabu hicho hakina tofauti na kitabu cha Kivukoni College.
 
Nakumbuka ilikuwa tarehe 27 mwezi wa nne mwaka 1985 Mwalimu Nyerere alitoa medali 3,979 katika viwanja vya Ikulu.

Medali hizo aliziita za waliochangia katika maendeleo ya taifa kuna mwanabodi yeyote anaweza kutuwekea orodha ya hao watu.

Ili darsa linatufunza mengi sana.

Mwenyekiti wa Kamati ya Medali yu hai.
Naogopa hata kumtaja jina lake.

Sasa hivi ni mstaafu.

Alikuwa mtu mkubwa sana katika CCM na serikali yake.
Kashika nyadhifa za juu sana ndani na nje ya nchi.

Alimuuliza Nyerere mbona naona hapa katika orodha yako
hawapo watu waliokupokea Dar es Salaam?
 
Sio kweli, Dossa Azizi alikuwa na ukwasi wakutosha, kwa lugha nyingine tunaweza kusema kuwa alikuwa sehemu ya matajiri wazalendo wa Tanganyika, kama walivyokuwa akina Chifu Marealle, Chifu Sapi na wengine.

Hata wanae wamerithi utajiri mkubwa wa majengo mitaa ya kariakoo. Alihamia Kibaha kama ilivyo desturi ya wazarendo wa kiafrika kutopenda vurugu za kimaendelea (kukaa sehemu iliyotulia)

Hizo ni propaganda zilezile!

Mimi si nia yangu kubishana katika vitu nilivyokuwa na yakini navyo.
Nawaachia wasomaji wenyewe watumie akili zao.

Siku Nyerere alipokwenda Mlandizi kuhani.

Aliona kwa macho yake mwenyewe hali ya makazi ya Dossa.

Nyerere alilia.

Mbele ya nyumba yake ilikuwapo Landrover ya Dossa aliyonunua katika
miaka ya 1950.

Ilikuwa imekwisha ni dude tu liko pale.

Dossa alinambia kazunguka Tanganyika nzima na Nyerere ndani ya Landrover
ile wakati wa kupigania uhuru.

Huenda Nyerere alikumbuka mbali.
Nyerere alizungumza kuhusu Dossa na katikati ya hotuba yake alilia machozi.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Medali yu hai.
Naogopa hata kumtaja jina lake.

Sasa hivi ni mstaafu.

Alikuwa mtu mkubwa sana katika CCM na serikali yake.
Kashika nyadhifa za juu sana ndani na nje ya nchi.

Alimuuliza Nyerere mbona naona hapa katika orodha yako
hawapo watu waliokupokea Dar es Salaam?

Hebu funguka kidogo tupate darsa.

Na kwa nini alitoa hizo medali wakati kaishaondoka madarakani.
 
Back
Top Bottom