Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wakati mwingine hunijia huruma kwa kuwa mimi najua mengi katika haya
kupita hawa ninaojadiliananao.

Kuna habari nyingine huwa siona sababu ya kuziweka hapa na ni nyingi.

Nyerere si kama hakujibu.
Alikubali kuandika maisha yake na humo ataeleza upande wake wa historia.

Kazi hiyo alimpa Prof. Haroub Othman.
Wakati mwingine sisi ndiyo huwa tunakuonea huruma ndugu yangu.
Hapo juu umesema Nyerere si kama hakujibu.
Haya turudi nyuma kidogo kabla sijapigwa ban. Angalia post yangu ya #823 kwenye uzi wa "Maaskofu wakemea udini na ukanda".
Niliquote hii kitu kutoka paper yako.
The late Prof. Haroub Othman after reading Sheikh Ali Muhsin's book Conflict and Harmony in Zanzibar and the writer's book The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 -1968 The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press, London 1998 and having come across hitherto unknown information on Nyerere was devastated because he was a great admirer of Nyerere as a patriot and a nationalist . The two books had painted him differently. Prof. Haroub confronted Nyerere and told him that the allegations in those two works have tarnished his image and he advised him to respond to them. Nyerere never did.

Linganisha hapo kwenye buluu halafu naomba unifafanulie labda mimi lugha inanichenga
 
Mzee Said wewe mwenyewe kwenye kitabu chako unaonesha kuwa Sykes aligombea dhidi ya Nyerere na alishindwa? Skykes alikataliwa na wazee wenzie wa Dar na Nyerere alikubaliwa. Ndivyo ulivyoandika unless nimesoma vibaya kuwa Skyes alijitoa kwenye uchaguzi ili kumpisha Nyerere.

Ungesoma kitabu changu usingesema, ''Sykes alikataliwa na wazee wenzake.''
Kwanza Abdu hakuwa mzee alikuwa na umri wa miaka 29 na Nyerere alikuwa
na miaka 31.

Uongozi wa ndani wa TAA uliamua kumpa uongozi Nyerere na aliyeongoza kampeni
ya kuchaguliwa Nyerere ni Abdu.

Kwa kweli ni bahati mbaya sana Nyerere hakupata kueleza vipi aliingia TAA Dar es
Salaam na ndiyo maana nyie wenzangu msiojua historia ya TANU mnababaika na
mengi ambayo hamkupata kuyasikia wala kuyasoma kabla.

Hebu soma hapa chini kisha tuendelee na mjadala:

''Uchaguzi baina ya aliyekuwa rais wa TAA, Abdulwahid na mwalimu wa shule asiyefahamika vyema pale mjini, Julius Nyerere,
ulifanyika kwenye Ukumbi wa Arnatouglo tarehe 17 Aprili, 1953.

Nje ya uongozi wa TAA ambao ulimpendekeza kugombea nafasi hiyo, Nyerere alikuwa mgeni kabisa kwa wote aliokuwa akiwaomba
kura zao.

Maisha ya Nyerere katika siasa yalianza hapo.

Nyerere alikuwa mgeni na alikuwa hana historia ya kuongoza mapambano ya umma dhidi ya serikali ya kikoloni.

Ukoo wa Sykes ulikuwa unatambulikana katika siasa za Dar es Salaam kwa takriban robo karne.

Ukoo huu ndiyo ulioanzisha na kuongoza vyama vyote viwili, African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Ukoo wa Abdulwahid, mtoto wa Kleist Sykes ulikuwa unafahamika kwa kuongoza mapambano dhidi ya serikali.

Ushahidi wa haya ulikuwa unapatikana katika nyaraka kati ya ukoo huu na serikali ya kikoloni.

Katika kipindi cha miaka zaidi ya ishirini, serikali kwa nyakati tofauti, kati ya mwaka 1929 hadi 1953 ilikuwa na barua za Kleist Sykes na
za mwanae Abdulwahid wakiwa viongozi wa African Association kuhusu madhila tofauti yaliyokuwa yakiwakabili wananchi. [1]

Uchaguzi ulikuwa kwa kunyoosha mikono.

Denis Phombeah [1]aliyekuwa akifanya kazi Ukumbi wa Arnatouglo ndiye alikuwa msimamizi wa uchaguzi.

Phombeah aliwaomba Abdulwahid na Nyerere kutoka nje ya ukumbi ili uchaguzi uanze.

Wiki nzima kabla ya uchaguzi Phombeah alikuwa akizunguuka mji mzima na pikipiki yake akimfanyia kampeni Nyerere.

Lakini kwa hakika hakukuwa na haja ya kufanya hivyo.

Uongozi wa ndani wa TAA wa Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz na Rupia ulikuwa tayari
umekwishaamua kumpa Nyerere urais wa chama.''
 
Ndugu yangu umefanya haraka.
Ushahidi uko hapo.

Nastaajabu vipi hukuuona.
Angalau basi ungeuliza kiungwana.

Mzee ushahidi uko wapi?
Insha Allah ningekujibu.

Umenitukana na kuniita muongo bila ya
sababu, mchochezi nk.

Angalia hizo footnote gazeti la Majira
ndilo lililomnukuu Kadinali Pengo.

Ikiwa wewe ni mjuzi katika mambo haya
utaelewa kwa nini ilikuwa muhimu nibandike
hicho kipande.

Hii ni dhihaka...Kama huna ushahidi sema tu huna ushahidi na usizidi kujishushia hadhi. Kuwa mkweli. Kama Cardinal Polycarp Pengo angetoa tamko kama hilo, leo hii ndiyo lingekuwa rejea ya kila kitu kinachohusiana na Mfumo Kristo kama vile vitabu vya Sivalon na Van Bergen...!

[1] Majira, 24 July, 1995. Amidst this conflict between Muslims and the government, it was published by the press that Muslims were to embark on a systematic campaign to elect a Muslim president in the elections of 1995. This in its entirety was a mere psychological warfare unleashed by the Christian Lobby upon Muslim ministers in the cabinet who anyway were far from Muslim politics. The bombardment from the press and within the Parliament was so overwhelming to those Muslims ministers mentioned by Muslims as possible presidential candidates that they had to stand up in the Parliament as Muslims to deny their capability to lead the country and disassociated themselves from the Muslim movement. Prof. Malima refused to be humiliated; he was of the opinion that the move by Muslim ministers was un-called for and unnecessary. To him Muslim ministers were just as qualified as any Christian to aspire for the presidency. His signature was not among those which Muslim ministers issued to the press as binding document of their commitment not to aspire for the highest office in the land. Jakaya Mrisho Kikwete later to become president of the country was among the signatories.
 
Mohamed Said, wimbi la mbele,

..hivi mnaweza kutuletea vitabu vya van Bergen na John Sivalon ambavyo mara nyingi mmekuwa mkivinukuu?

..nadhani ili mjadala huu uweze kupendeza tunapaswa na kuviona vitabu hivyo ambavyo mnadai vina ushahidi wa uonevu wa Mwalimu Nyerere dhidi ya Waislamu.

..kama kuna tatizo mnaweza kuwasiliana na Maxence Melo au moderator kuona taratibu gani zitumike vitabu hivyo vifike hapa kwa ajili ya mjadala wetu.

cc: Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Companero, Jasusi

Mkuu mnataka kuniharibia likizo - likizo yenyewe fupi. Jumatano narudi shule. Kitabu cha Bergen nilikibeba ili niandike pepa ya econometric kuhusu long-run effects ya wamisionari na shule zao katika kujenga tabaka la wateule (elites) hapa Tanzania. Regressions na Correlations zote zilionesha kuwa hakuna hiyo effect na hivyo kuthibitisha aliyoyasema Bergen kuhusu Tanzania ilivyokuwa tofauti na nchi zingine kwenye sual la taathira ya ukristo. Sasa nahitaji data zaidi ili nijiridhishe 100% kuwa hivyo ndivyo hali ilivyokuwa hasa. NITA-SCAN Appendix 13 ya kitabu cha Bergen yenye huo waraka confidential wa Nyerere akiwakiana na priests wa Kikatoliki. Ilikuwa ni transcript (si barua) ya mkutano wake na hao mapriests na kuna jibu la father wa Kitanzania pia. Kwa kiasi kikubwa inaonekana Nyerere alishinikizwa sana ila aliwadhibiti sana hao wakuu wa hilo dhehebu linalodai eti ni la watu wote (universal).
 
Mkuu inaelekea una mambo mazito...mchango wako unahitajika sana hapa...!
 
Mohamed Said, unaweza kuwatambua hawa kwa majina baada ya ushindi wa kimbunga wa viongozi wa TANU 1958?
nyerere_and_TANU_leaders_1958.jpg
 
Wakati mwingine hunijia huruma kwa kuwa mimi najua mengi katika haya
kupita hawa ninaojadiliananao.

Kuna habari nyingine huwa siona sababu ya kuziweka hapa na ni nyingi.

Nyerere si kama hakujibu.
Alikubali kuandika maisha yake na humo ataeleza upande wake wa historia.

Kazi hiyo alimpa Prof. Haroub Othman.

Katika maelezo yao huko nyuma ya uzi huu na ule wa tamko la maaskofu ulisema wazi kuwa Prof H.Othuman baada ya kusoma kitabu chako alimfuata Mwalimu Nyerere kumuomba aandike chochote kujibu kitabu hicho la si hivyo heshima yake itashuka, lakini Mwalimu hakujibu!

Sasa hivi unasema mwalimu alijibu? Haya tuambie alijibuje na wapi alijibia?
 
Wanasema ukiwa muongo, unatakiwa uwe na kumbukumbuku kali sana.
 
Mkuu mnataka kuniharibia likizo - likizo yenyewe fupi. Jumatano narudi shule. Kitabu cha Bergen nilikibeba ili niandike pepa ya econometric kuhusu long-run effects ya wamisionari na shule zao katika kujenga tabaka la wateule (elites) hapa Tanzania. Regressions na Correlations zote zilionesha kuwa hakuna hiyo effect na hivyo kuthibitisha aliyoyasema Bergen kuhusu Tanzania ilivyokuwa tofauti na nchi zingine kwenye sual la taathira ya ukristo. Sasa nahitaji data zaidi ili nijiridhishe 100% kuwa hivyo ndivyo hali ilivyokuwa hasa. NITA-SCAN Appendix 13 ya kitabu cha Bergen yenye huo waraka confidential wa Nyerere akiwakiana na priests wa Kikatoliki. Ilikuwa ni transcript (si barua) ya mkutano wake na hao mapriests na kuna jibu la father wa Kitanzania pia. Kwa kiasi kikubwa inaonekana Nyerere alishinikizwa sana ila aliwadhibiti sana hao wakuu wa hilo dhehebu linalodai eti ni la watu wote (universal).

Mkuu asante sana mkuu kwakurudi kwako kwenye mnakasha huu, wewe ni mtu mhimu sana,

Nafahamu uelewa wako kati ya kanisa na utawala wa Nyerere lakini ningependa kufahamu zaidi kutoka kwako juu ya kanisa na harakati za ukombozi tangu uwepo walo Tanganyika au vyovyote vile.
 
Mkuu niwe mkweli nisimamie weledi wa mambo.

Sio kwamba yote yaliyo katika kitabu chako ni batili la hasha, yapo mengi mazuri kama ilivyo kwenye kitabu cha Kivukoni.

Leo hii mimi nikitaka kuandika historia hii, yapo nitakayonukuu katika kitabu chako na cha kivukoni!

Kinachoondoa nguvu ya kitabu chako ni kuweka hisia zako ama za mitaani kuwa ndio uhalisia wa Mzee Nyerere na Sykes.

Hata post yako hii hapo juu unasema wazi kuwa Mwalimu Nyerere alihujumu mpango wa Dr Kreluu na Addu wa kuandika historia ya TANU, lakini tukisema uthibitishe hili utakuja na ushahidi kutoka kwenye kitabu chako hichohicho tunachokipinga kuwa ni cha kufikirika.

Hayo ni sehemu ya mapungufu makuu katika andiko lako mkuu!
Akiondoa UISLAMU aloowavika wazee wake hawa, akaondoa na ukristo wa Mwalimu kwenye kazi zake za UONGOZI wa TANU na Urais wa nchi hii, akatambua kabisa kwamba wazee wake hawa na Mwalimu walifanya kazi pamoja kudai uhuru wa NCHI hii kule UN kwa UZALENDO wao, Mzee Mohamed Said anaweza kuandika kitu kizuri mno kwa taifa letu hili.

Hakuna ulevi na kasumba mbaya kama DINI na hasa ukiichanganya na mambo mengine. Tuweke dini kando kama nia ni kuandika historia ya nchi hii.
 
Huu mjadala hauwezi kwisha leo au kesho.
Inavyoonekana dhahiri kuna mengi ya kujifunza.

Na inavyodhihiri Mzee Mohammed Said amefinyanga mengi. Laiti kama angekuwa haweki hisia zake na
chuki dhidi ya Nyerere vitabu vyake vingekuwa na heshima miongoni mwa jamii yetu yote na vingejenga uzalendo.

Na bila shaka kwa kadri jitihada kubwa ya kuligawa Taifa kidini inavyoendelea ndivyo itakavyokuwa vigumu kukubali huu upungufu.
 
Duh WildCard akiondoa UISLAM wa wazee wake wa GEREZANI,akiondoa UKRISTO wa Nyerere akaweka UZALENDO na UTAIFA wa TANGANYIKA unadhani madhumuni ya kitabu chake bado yatakuwepo !.Mkuu wa unapaswa kutambua kwanza nia na madhumuni ya Mohamed Said kabla ya kumwelekeza vinginevyo utakuwa unajisumbua bure.

Akiondoa UISLAMU aloowavika wazee wake hawa, akaondoa na ukristo wa Mwalimu kwenye kazi zake za UONGOZI wa TANU na Urais wa nchi hii, akatambua kabisa kwamba wazee wake hawa na Mwalimu walifanya kazi pamoja kudai uhuru wa NCHI hii kule UN kwa UZALENDO wao, Mzee Mohamed Said anaweza kuandika kitu kizuri mno kwa taifa letu hili.

Hakuna ulevi na kasumba mbaya kama DINI na hasa ukiichanganya na mambo mengine. Tuweke dini kando kama nia ni kuandika historia ya nchi hii.
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli kabisa mkuu,
 
Wakati mwingine hunijia huruma kwa kuwa mimi najua mengi katika haya
kupita hawa ninaojadiliananao.

Kuna habari nyingine huwa siona sababu ya kuziweka hapa na ni nyingi.

Nyerere si kama hakujibu.
Alikubali kuandika maisha yake na humo ataeleza upande wake wa historia.

Kazi hiyo alimpa Prof. Haroub Othman.
Hapa ndipo unaponiacha hoi kwa kudhani kuwa wewe unajua mengi kuliko watu wote. Hii inatokana na kutowasoma watu wengine wanachokiandika kwenye magazeti na majarida mbalimbali ya humu nchini. Unachagua mno mambo ya kusoma na unaikataza kabisa akili yako kukubaliana na mambo usiyoyataka wewe.

Kwa kuwa uko hivo na kwa umri wako wa sasa hakuna unachoweza kubadili. Unaipa DINI yako umuhimu mkubwa mno usiostahili wakati dini ni kama mke/mme tu. Unaweza kuibadili, kuiacha, kuisusa au hata kuitelekeza tu. Wazee wako hawa akina Sykes, Plantan,..., walitokea kwenye ukristo. Naamini hata Mwalimu angebadili dini usingemwandika hivi!
 
Duh WildCard akiondoa UISLAM wa wazee wake wa GEREZANI,akiondoa UKRISTO wa Nyerere akaweka UZALENDO na UTAIFA wa TANGANYIKA unadhani madhumuni ya kitabu chake bado yatakuwepo !.Mkuu wa unapaswa kutambua kwanza nia na madhumuni ya Mohamed Said kabla ya kumwelekeza vinginevyo utakuwa unajisumbua bure.

Hilo ni kweli Kitabu chake kimemfunga mwenyewe.
Ni kama kumwambia mtu akate tawi alilokalia. Hawezi, inahitaji ujasiri wa aina yake.

Kumbuka amewavuta baadhi ya Waislam kumfuata kwenye huu ubaguzi kutokana na haya anayoandika.
Leo watamwelewa vipi akigeuka?

Ndio maana haishi kukwepa hoja hasa akijua anajadiliana na watu wanaomjua.
 
Kwa kweli kama ninavyosisitiza najibu swali ambalo nalijua.
Nisilojua siwezi kujibu.

Au lile ninaloona halina tija huwa silijibu.
Kwa ufupi sijibu kila post.

Katika hili tuwiane radhi na Insha Allah tusonge mbele kwa mengine.
 
Hapa ndipo unaponiacha hoi kwa kudhani kuwa wewe unajua mengi kuliko watu wote. Hii inatokana na kutowasoma watu wengine wanachokiandika kwenye magazeti na majarida mbalimbali ya humu nchini. Unachagua mno mambo ya kusoma na unaikataza kabisa akili yako kukubaliana na mambo usiyoyataka wewe.

Kwa kuwa uko hivo na kwa umri wako wa sasa hakuna unachoweza kubadili. Unaipa DINI yako umuhimu mkubwa mno usiostahili wakati dini ni kama mke/mme tu. Unaweza kuibadili, kuiacha, kuisusa au hata kuitelekeza tu. Wazee wako hawa akina Sykes, Plantan,..., walitokea kwenye ukristo. Naamini hata Mwalimu angebadili dini usingemwandika hivi!

Nielewe ndugu yangu.

Ninayoyajua mengi siyo kwenye kila kitu.
Nasisitiza sijui mengi kwenye kila kitu.

Mimi najua mengi kuhusu historia ya wazee wangu tu.
Ndiyo maana nimeweza hata kuandika kitabu.

Hayo mengine sidhani kama nina haja ya kuyasemea.
 
Akiondoa UISLAMU aloowavika wazee wake hawa, akaondoa na ukristo wa Mwalimu kwenye kazi zake za UONGOZI wa TANU na Urais wa nchi hii, akatambua kabisa kwamba wazee wake hawa na Mwalimu walifanya kazi pamoja kudai uhuru wa NCHI hii kule UN kwa UZALENDO wao, Mzee Mohamed Said anaweza kuandika kitu kizuri mno kwa taifa letu hili.

Hakuna ulevi na kasumba mbaya kama DINI na hasa ukiichanganya na mambo mengine. Tuweke dini kando kama nia ni kuandika historia ya nchi hii.

Mbona nimekusihini siku nyingi sana kuhusu kuandika historia ya TANU?
Hakika mnahitaji kuandika nami nitatoa ushirikiano.

Nina hazina ya picha na nyaraka nyingi kuhusu kipindi kile.
Naahidi kukupeni zote Insha Allah.

Halikadhalika Insha Allah nitakujulisheni kwa koo za wajukuu wa hawa wazalendo.
Haya yote ikiwa mtataka.
 
Mohamed Said, unaweza kuwatambua hawa kwa majina baada ya ushindi wa kimbunga wa viongozi wa TANU 1958?
View attachment 79866

Kwanza nikufahamishe kuwa hiyo picha ni kutoka ''Jumbe Tambaza Collection''
niliyopiga kutoka kwa picha zilizoko kwa wajukuu wa Jumbe Tambaza.

Picha hizo kaniruhusu Msakala Mohamed Jumbe Tambaza kuzipiga upya
katika digitali.

Mimi ndiyo niliyeweka picha hii katika mtandao.

Huyu Msakala ni mjukuu wa Jumbe Tambaza na ni mtoto wa marehemu
Mohamed Tambaza.

Mzee Mohamed Tambaza (marehemu) tukifahamiana kwa muda mrefu.

Mbele aliyetangulia ni Nyerere na nyuma yake ni Dossa Aziz.

Hao wengine siwafahamu.
 
Back
Top Bottom