Wanajamvi, hapo nyuma kidogo nimechokoza tu mjadala kwa kuuliza maswali mawili nayo ni;
Kama kawaida bingwa wa hadithi anayejulikana kama Mohamed Said, haraka haraka, akadakia kwa kutoa majibu na nanukuu tu sehemu ya simulizi ambazo anadai alipewa na wazee wake wa Gerezani.
Hilo hapo juu ndilo jibu la Mohamed Said kuhusu viongozi wakuu walioiongoza AA toka kuasisiwa kwake mwaka 1929 hadi ilipobadilika na kuwa TAA na badaye kuundwa TANU mwaka 1954. Kwa hilo jibu peke yake Mohamed Said anathibitisha hila zake za kichochezi na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika (na Zanzibar?) kama mtoa hii mada alivyoainisha.
Je ni kitu gani kimejificha katika hili jibu la Mohamed Said? Ukilisoma hili jibu kwa haraka haraka utadhani AA haikuwa na Kiongozi Mkuu. Kwa nini hataji kuwa AA ilikuwa na Raisi aliyeiongoza? AA haikuwa kikao kama cha wanywa kahawa ambapo watu wanapasishana kikombe bila kujali "protocol" yoyote. Je huyo Kleist anayetajwa mara mbili, ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa AA?
Mwalimu Cecil Matola, myao ambaye nyumbani kwake ndiko kulikofanyika mkutano wa kwanza wa TAA yeye akiwa ndiye Raisi wa kwanza, mbona anatajwa mwisho kama vile hana umuhimu wowote? Je baada ya kufariki kwake mwaka 1933, kwa nini AA ilizorota na hakuweza kupatikana kiongozi mwingine wa kuiongoza AA hadi alipoingia kijana msomi kutoka Makerere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Raisi wa kwanza wa TAA?
Dr. Kyaruzi aliiongoza TAA kwa miaka miwili hadi 1951 na hata alipohamishiwa mikoani na kushindwa kumudu kuiongoza TAA kwa nini hakupatikana Kiongozi mwingine hadi mwaka 1953 alipoingia kijana mwingine msomi kutoka Edinburgh, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere? Kwa nini wazee wa Mohamed ambao anadai ndio walikuwa vinara wa mwamko wasimchague mmoja wao kuwa Raisi?
Je ni kweli kuwa chombo cha kwanza kilichowaunganisha waafrika kilianzia Dar es Salaam? Vipi Msomi Martin Kayamba aliyeanzisha TTACSA (Tanganyika Territory African Civil Service Association) huko Tanga mwaka 1922? Je si kweli kuwa TAA iliasisiwa kwa kufuata unyayo na misingi iliyoanzishwa na TTACSA? Ni TTACSA iliyowawezesha wafanya kazi kukutana pamoja bila kubaguana kikabila, kirangi wala kidini.
Tuendelee na mjadala...
Unachanganya habari.
Unaandika na hamaki.
Hapo ndipo zinaingia kejeli za kahawa nk. nk.
Huu ni mjadala tu kama nimekosea mahali unasema tu kiungwana.
Kleist alikuwa na kipaji cha hali ya juu katika uongozi.
Licha ya kuwa katibu muasisi wa AA mkwaka 1933 alikuwa katibu muasisi
wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika)
Mzee bin Sudi akiwa rais.
Matola alikuwa rais kweli lakini mambo yote akifanya Kleist kwa kuwa Kleist
alikuwa kijana tajiri.
Hii ilimwezesha kufanya mambo mengi sana kwa urahisi.
Cecil Matola alikuwa kiongozi wa African Association na alipoondoka akaingia
Mzee bin Sudi kama rais.
African Association ilizorota mwaka 1933 baada ya kutokea ugomvi kati ya Erika Fiah
na Kleist.
Kleist alijitoa katika uongozi.
Ipo barua aliyoandika Mzee bin Sudi aliyoanza kwa Bismillah Rahman Rahim.
Barua hii Mzee bin Sudi alimwandikia Kleist kumbembeleza arudi AA wakiongoze
chama.
Habari hizi zipo katika mswada wa maisha ya Kleist.
Habari hii inaweza halikadhalika kupatika katika Illife (Modern Tanzanians)
''The Townsman Kleist'' Sykes kama alivyoandika mjukuu wake.
Dr. Kyaruzi aliingia TAA na Abdu Sykes 1950 na hakumaliza hata mwaka
Waingereza wakampa uhamisho Kingolwira Prison kisha Nzega.
Sababu ya uhamisho wa Dr. Kyaruzi ni ile TAA Political Sub Commttee waliyounda
wajumbe wakiwa Sheikh Hassan bin Amir, Abdu Sykes, Dr Kyaruzi, Said Chaurembo,
John Rupia, Hamza Mwapachu na Steven Mhando.
Kamati hii ilimchukua mwanasheria wa Kibyamuda Earle Seaton kama mshauri.
Seaton alikuwa rafiki yake Abdu Sykes.
Habari ni nyingi nisimame hapa kwa sasa.
Kwa ufupi TAA ikawa inafanya kazi kama chama cha siasa halisi.
Huo ndiyo ukawa ndiyo mwisho wake wa uongozi wake kama rais wa TAA.
kuanzia 1951 Abdu Sykes akawa Acting President na Secretary na 1952
Abdu akawa rais wa TAA.
Kuhusu Martin Kayamba nakusihi tufanye subra tutamzungumza.
Kwanza hebu linganisha haya niliyoandika hapa na hayo uliyoandika wewe.
Tukimaliza Insha Allah tutakuja kwa Martin Kayamba Mdumi.
Tuendelee Insha Allah na mjadala.