Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hili ndilo tatizo la maandishi yako mzee mwenzangu; unatutaka tuamini maneno yako kwa vile umeyasema hata kama hakuna ushahidi wowote. Kwamba tukitaka ushahidi hasa wa kihistoria utasema "amini kama hutaki basi". Sasa hiyo siyo historia. Unapoandika historia you only write on that which you have evidence of.
Lakini hili si kweli; katika kitabu cha aliyekuwa mke wa Du Bois (ambaye alimhoji Nyerere mwanzoni mwa miaka ya sitini pale Dar) aliandika hili. Na katika kitabu cha We Must Run While They Walk cha William Edget Smith Nyerere ameeleza kwa kirefu sana jinsi alivyoingia kwenye TAA.
Nilishasoma haya kwenye kitabu chako; unachotoa hapa kama ushahidi ni maandishi yako wewe na madai (assertions) zako wewe. Unataka tukubali kwa vile umezisema hata kama ulichoandika hakina ushahidi.
Sawa
Lakini hili si kweli. Nyerere alianza siasa akiwa Makerere siyo Dar. Hata kusema 'uongozi wa kisiasa" Nyerere hakuanzia Dar.
Hili pia si la kweli kwani alishaanza harakati hizi tangu akiwa shuleni (Tabora) mwanafunzi.
Ndio lakini walikuwa wanafahamika kwa sababu kwanza walikuwa ni mamluki wa Ujerumani ambao walikuja kkupigana na watu weusi ili kumtetea Mjerumani na hawakuwa very fond na Waingereza. Na katika maandishi yako unaonesha kuwa kina Sykes walikuwa na resentment kukbwa sana kwa Waingereza hasa kwa vile Uingereza haikufanya kile kilichotarajiwa kwa ex German Soldiers.
Wengine (kama mimi) wanaweza kusema kuwa Abdule Sykes alimpinga Muingereza sana si kwa sababu ya maslahi ya Watu weusi wengine au Tanganyika bali zaidi wa sababu ya walivyomfanyia baba yake. Unaweza kulielewa hili katika maandishi yako kumhusu Sykes.
Tukubali kwa sekunde kuwa ni kweli waliongoza harakati dhidi ya ukoloni. Je ni ushahidi gani ulio nao ambapo kina Sykes waliongoza harakati dhidi ya Mjerumani? Au Mjerumani hakuwa Mkoloni?
Once again ni madai yako haya (assertion) lakini nikiuliza kuna ushahidi gani kukwa kina Abdulwahid na wenzie walikuwa tayari wameshaamua kumpa Nyerere urais? utasema ni maneno uliyosimuliwa. Maana kama walikuwa tayari wamekubali kumpa kwanini Sykes bado aligombea wakati mgombea mwingine alijitoea kama nakumbuka vizuri?
Kwa kweli mimi sina tatizo na fikra zako kama ulizoandika hapo juu.
Yote ni maswali ambayo mtu yoyote anaweza akajiuliza baada ya
kusoma kitabu changu.
Mathalan chuki ya Wazulu Kleist, Plantan dhidi ya utawala wa Kiingereza
hili lilijitokeza wazi kupitia Schneider Abdillah Plantan katika uchaguzi wa
TAA wa 1950.
Kafanya vurugu mbele ya maofisa Waingereza waliohudhuria kikao kile pale
Ukumbi wa Arnautoglo kupelekea hadi uchaguzi ukafanyika.
Mdogo wake Ramadhani Mashado Plantan alikuwa na gazeti Zuhra ambalo ndilo
lilikuwa sauti ya Waafrika wa Tanganyika na gazeti la kwanza kuitangaza TANU
na kumnukuu Nyerere.
Tahariri zake zilikuwa zikiishambulia sana serikali ya kikoloni (nakala za gazeti hili
zipo East Africana, maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).
Mifano ya chuki hii ipo mingi.
Hilo la Kleist kupinga utawala wa Wajerumani ni kweli hakuna popote katika nyaraka
zake na maisha yake hilo limejitokeza sana sana alikuwa Aide de Camp wa Von Lettow
Vorbeck katika Vita ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918).
Huu ni ukweli hakuna anaeweza kuupinga.
Ni ukweli pia mlezi wake Affande Plantan ndiye aliyekuwa mkuu wa Germany Contabulary
na nafasi hii ndiyo iliyofanya watoto wote wa askari wa Kizulu akina Klest, Mashado, Thomas
nk. wapate elimu ya juu kwa wakati ule.
Huu ni ukweli wa historia na hakuna anaeweza kuukataa.
Lakini hiyo siasa aliyofanya Nyerere Makerere ni ipi basi?
Mimi binafsi nimesoma nyaraka nyingi sana kuhusu Nyerere na sijapata kuvutiwa na yeye mpaka
alipofika Dar es Salaam na kuingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953.
Sasa hapa kuna kitu watu wengi hawakifahamu na yeye mwenyewe kwa kuwa hakupenda kunasibishwa
na harakati za Abdulwahid habari hizi hazikupata kujulikana.
Nyerere alipochukua uongozi wa TAA 1953 chama kilikufa.
Ukipenda na wanaukumbi wakiona kuna haja naweza Insha Allah nikaeleza kwa kirefu nini kilitokea.
Hilo la Nyerere kutotoa jina lake akamwachia Nyerere kupita bila kupingwa vilevile ikiwa ni lazima
naweza nikalieleza hapa.
Iwe itakavyokuwa naheshimu fikra zako.