Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hili ndilo tatizo la maandishi yako mzee mwenzangu; unatutaka tuamini maneno yako kwa vile umeyasema hata kama hakuna ushahidi wowote. Kwamba tukitaka ushahidi hasa wa kihistoria utasema "amini kama hutaki basi". Sasa hiyo siyo historia. Unapoandika historia you only write on that which you have evidence of.

Lakini hili si kweli; katika kitabu cha aliyekuwa mke wa Du Bois (ambaye alimhoji Nyerere mwanzoni mwa miaka ya sitini pale Dar) aliandika hili. Na katika kitabu cha We Must Run While They Walk cha William Edget Smith Nyerere ameeleza kwa kirefu sana jinsi alivyoingia kwenye TAA.

Nilishasoma haya kwenye kitabu chako; unachotoa hapa kama ushahidi ni maandishi yako wewe na madai (assertions) zako wewe. Unataka tukubali kwa vile umezisema hata kama ulichoandika hakina ushahidi.

Sawa

Lakini hili si kweli. Nyerere alianza siasa akiwa Makerere siyo Dar. Hata kusema 'uongozi wa kisiasa" Nyerere hakuanzia Dar.

Hili pia si la kweli kwani alishaanza harakati hizi tangu akiwa shuleni (Tabora) mwanafunzi.

Ndio lakini walikuwa wanafahamika kwa sababu kwanza walikuwa ni mamluki wa Ujerumani ambao walikuja kkupigana na watu weusi ili kumtetea Mjerumani na hawakuwa very fond na Waingereza. Na katika maandishi yako unaonesha kuwa kina Sykes walikuwa na resentment kukbwa sana kwa Waingereza hasa kwa vile Uingereza haikufanya kile kilichotarajiwa kwa ex German Soldiers.

Wengine (kama mimi) wanaweza kusema kuwa Abdule Sykes alimpinga Muingereza sana si kwa sababu ya maslahi ya Watu weusi wengine au Tanganyika bali zaidi wa sababu ya walivyomfanyia baba yake. Unaweza kulielewa hili katika maandishi yako kumhusu Sykes.

Tukubali kwa sekunde kuwa ni kweli waliongoza harakati dhidi ya ukoloni. Je ni ushahidi gani ulio nao ambapo kina Sykes waliongoza harakati dhidi ya Mjerumani? Au Mjerumani hakuwa Mkoloni?

Once again ni madai yako haya (assertion) lakini nikiuliza kuna ushahidi gani kukwa kina Abdulwahid na wenzie walikuwa tayari wameshaamua kumpa Nyerere urais? utasema ni maneno uliyosimuliwa. Maana kama walikuwa tayari wamekubali kumpa kwanini Sykes bado aligombea wakati mgombea mwingine alijitoea kama nakumbuka vizuri?

Kwa kweli mimi sina tatizo na fikra zako kama ulizoandika hapo juu.
Yote ni maswali ambayo mtu yoyote anaweza akajiuliza baada ya
kusoma kitabu changu.

Mathalan chuki ya Wazulu Kleist, Plantan dhidi ya utawala wa Kiingereza
hili lilijitokeza wazi kupitia Schneider Abdillah Plantan katika uchaguzi wa
TAA wa 1950.

Kafanya vurugu mbele ya maofisa Waingereza waliohudhuria kikao kile pale
Ukumbi wa Arnautoglo kupelekea hadi uchaguzi ukafanyika.

Mdogo wake Ramadhani Mashado Plantan alikuwa na gazeti Zuhra ambalo ndilo
lilikuwa sauti ya Waafrika wa Tanganyika na gazeti la kwanza kuitangaza TANU
na kumnukuu Nyerere.

Tahariri zake zilikuwa zikiishambulia sana serikali ya kikoloni (nakala za gazeti hili
zipo East Africana, maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).

Mifano ya chuki hii ipo mingi.

Hilo la Kleist kupinga utawala wa Wajerumani ni kweli hakuna popote katika nyaraka
zake na maisha yake hilo limejitokeza sana sana alikuwa Aide de Camp wa Von Lettow
Vorbeck katika Vita ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918).

Huu ni ukweli hakuna anaeweza kuupinga.

Ni ukweli pia mlezi wake Affande Plantan ndiye aliyekuwa mkuu wa Germany Contabulary
na nafasi hii ndiyo iliyofanya watoto wote wa askari wa Kizulu akina Klest, Mashado, Thomas
nk. wapate elimu ya juu kwa wakati ule.

Huu ni ukweli wa historia na hakuna anaeweza kuukataa.

Lakini hiyo siasa aliyofanya Nyerere Makerere ni ipi basi?

Mimi binafsi nimesoma nyaraka nyingi sana kuhusu Nyerere na sijapata kuvutiwa na yeye mpaka
alipofika Dar es Salaam na kuingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953.

Sasa hapa kuna kitu watu wengi hawakifahamu na yeye mwenyewe kwa kuwa hakupenda kunasibishwa
na harakati za Abdulwahid habari hizi hazikupata kujulikana.

Nyerere alipochukua uongozi wa TAA 1953 chama kilikufa.

Ukipenda na wanaukumbi wakiona kuna haja naweza Insha Allah nikaeleza kwa kirefu nini kilitokea.

Hilo la Nyerere kutotoa jina lake akamwachia Nyerere kupita bila kupingwa vilevile ikiwa ni lazima
naweza nikalieleza hapa.

Iwe itakavyokuwa naheshimu fikra zako.
 
Ushawahi kujiuliza kwanini barabara za lami zipo siku nyingi kutoka dar kwenda Mbeya?nataka arusha Moshi kuja dar?na kwanini hakuna mawasiliano ya kutoka Mtwara lindi kwenda sehemu yoyote kwenye jamhuri hii?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, sisi ambao hatukuwepo, tunajikuta tukiendelea kudanganywa na simulizi kama hizi za Maalim, Mohamed Said simply kwa sababu yeye ame document alichosimuliwa!, kama amedangaywa na hao wasimulizi wake, na yeye akaishia kutudanya sisi kwa kuamini uwongo ule kuwa ndio ukweli, historia itakuja kuishia kubaki na records za uwongo huo kuonekana ndio ukweli wenyewe simply because ukweli halisi, "was not told!, was not documented!". Ikumbukwe tuu kuwa "half truth" huonekana kama ndio "full truth" as long as the other half is never told!, Hiyo half truth can only be defeated if the other half is told and that is the only way of getting "the full truth!". Mohamed Said played his part, got his "half" toka simulizi za babu zake, lets get the other "half" from other nayo iwe compiled, vinginevyo hiyo "half" ya wazee wake Mohamed Said ndio itakayokuja kuishia kuonekana kama ndio the only "full truth!".

Nakumbuka kuna wakati mwandishi Kanyama Chiume (Rip). alipewa kazi ya kuandika historia ya Tanu, sijui iliishia wapi maana hata historia yetu tuu, tulimtegemea Mmalawi!. Kwa nini waandishi kama nyinyi, msijitolee kui compile historia ya mapambao toka machapisho mbalimbali, ikaandikwa kwenye kitabu na kitabu hicho kichapishwe ili ku defeat upotoshwaji kama huu unaofanywa na Maalim Mohamed Said, as of now, Maalim yuko right ku preserve historia ya Wazazi wake kama alivyosimuliwa, na mimi naendelea kukiri wazi kuwa kwa vile napenda simulizi za hadithi, naendelea ku enjoy simulizi za hadithi za Mohamed Said.
Pasco.

Napenda kusahihisha jambo dogo.

Mzee Chiume ile historia alokuwa anataka kuandika haikuwa historia ya TANU
bali historia ya vyama vya ukombozi wa Africa pamoja na TANU.

Mimi nilimjua kupitia Ally Sykes.

Mzee Kanyama Chiume alikuwa hana pa kuanzia kuhusu TANU kwa shida ya nyaraka.
Kwa hiyo alikwenda kwa Ally Sykes kumuomba nyaraka ili aanze utafiti.

Hapo ndipo Bwana Ally Sykes akanikutanisha na Mzee Chiume.
 
Hilo la Kleist kupinga utawala wa Wajerumani ni kweli hakuna popote katika nyaraka
zake na maisha yake hilo limejitokeza sana sana alikuwa Aide de Camp wa Von Lettow
Vorbeck katika Vita ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918).

Huu ni ukweli hakuna anaeweza kuupinga.
Ni ukweli pia mlezi wake Affande Plantan ndiye aliyekuwa mkuu wa Germany Contabulary
na nafasi hii ndiyo iliyofanya watoto wote wa askari wa Kizulu akina Klest, Mashado, Thomas
nk. wapate elimu ya juu kwa wakati ule.

Huu ni ukweli wa historia na hakuna anaeweza kuukataa.

Kwa hiyo kusema kuwa kina Sykes walikuwa wanaongoza harakati za kupinga ukoloni kama ulivyosema hapo juu kuwa:

Ukoo wa Abdulwahid, mtoto wa Kleist Sykes ulikuwa unafahamika kwa kuongoza mapambano dhidi ya serikali.

Ushahidi wa haya ulikuwa unapatikana katika nyaraka kati ya ukoo huu na serikali ya kikoloni.

Kwa hiyo siyo KWELI kwamba ukoo wa Sykes uliongoza mapambano dhidi ya serikali isipokuwa kama unamaanisha kuwa 'serikali' hapa unaizungumzia ile ya Mwingereza tu.

Je, siyo KWELI kwamba Sykes aligeuka dhidi ya serikali ya Mwingereza kwa sababu walimuondoa Mjerumani na ukoo wake ulifanya hivyo hivyo kwa sababu yule waliyemtumikia kwa maisha yao na ambaye kwake walipata ujira wao aliondolewa na Mwingereza? Kwamba harakati za Sykes dhidi ya Mwingereza hazikuwa kwa sababu ya kutaka uhuru wa Mwafrika zaidi kuliko kumuondoa aliyemwondoa kipenzi chao - Mjerumani?

Lakini hiyo siasa aliyofanya Nyerere Makerere ni ipi basi?

Mimi binafsi nimesoma nyaraka nyingi sana kuhusu Nyerere na sijapata kuvutiea na yeye mpaka

alipofika Dar es Salaam na kuingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953.

Naomba - ikikupendeza - ututajie angalau maandishi au nyaraka tatu tu za Nyerere kabla ya 1953 ambazo umezisoma na ambazo hazikukuvutia hadi alipokuja Dar in 1953. Maana fikra za Nyerere kisiasa hazikuanza kujengwa alipokuja Dar na kujiunga na TAA; zilikuwa zimejengwa miaka mingi nyuma na aliziweka wazi hivyo.

Kwa maana mimi nina maandishi yake akiwa Chuo Kikuu cha Edinburg (1949-1952) hivi ambapo mawazo yake juu ya Ukoloni na Demokrasia yalikuwa tayari yamekomaa. Na yapo maandishi yake wakati akiwa Makerere vile vile ambayo yanaonesha political maturity. Aliyoyafanya Dar baada ya kutoka Uingereza ulikuwa tayari ni mwendelezo wa fikra zake ambazo alikuwa tayari ameanza kuzijenga mapema. Siyo Sykes wala Rupia au mzee mwingine wa Dar waliochangia mabadiliko makubwa ya kifikra hasa dhidi ya Ukoloni ndani ya Mwalimu. Alipokuja Dar alikuwa tayari anajua nini anataka kufanya.

Katika mahojiano yake na jarida la New Internationalist Mwalimu Nyerere mwenyewe anaelezea fikra zake zilivyokua dhidi ya ukoloni na kweli haikutokea Dar. Anasema hivi alipoulizwa juu ya ni jinsi gani alipata mawazo ya kupinga utawala wa kikoloni.

I cannot say I encountered the idea of liberation in a totality like a flash of light. I did not have an experience like Paul on the road to Damascus. For me it was a process – something that grew inside of me...

World War Two and what it was fought for – democracy and freedom – started the process for many people, especially those who were in the Army. For me the transformation came later. At Makerere in 1943 I started something called the Tanganyika African Welfare Association. Its main purpose was not political or anti-colonial. We wanted to improve the lives of Africans. But inside us something was happening.

I wrote an essay in 1944 called The Freedom of Women. I must be honest and say I was influenced by John Stuart Mill, who had written about the subjugation of women. My father had 22 wives and I knew how hard they had to work and what they went through as women. Here in this essay I was moving towards the idea of freedom theoretically. But I was still in the mindset of improving the lives and welfare of Africans: I went to Tabora to start teaching.

Then came Indian independence. The significance of India's independence movement was that it shook the British Empire. When Gandhi succeeded I think it made the British lose the will to cling to empire. But it was events in Ghana in 1949 that fundamentally changed my attitude. When Kwame Nkrumah was released from prison this produced a transformation. I was in Britain and oh you could see it in the Ghanaians! They became different human beings, different from all the rest of us! This thing of freedom began growing inside all of us. First India in 1947, then Ghana in 1949. Ghana became independent six years later. Under the influence of these events, while at university in Britain, I made up my mind to be a full-time political activist when I went back home. I intended to work for three years and then launch into politics. But it happened sooner than I planned.

Kutokana na kauli ya Nyerere mwenyewe siyo kusimuliwa na watu anasema kuwa mawazo yake ya kisiasa na kujishughulisha na siasa vilianzia kabla ya Kuja Dar na kuanza kazi na kina Sykes in 1953 kama unavyotaka watu waamini. Tunaweza tukakubali kuwa ilikuwa miaka 10 kabla au angalau miaka minne kabla akiwa Uingereza. Kama hili ni kweli - na sioni unaweza vipi kupingana na kauli yake mwenyewe - basi madai yako kuwa ni kina Sykes waliomuingiza Nyerere kwenye siasa na kuwa ni Dar ndiko alikoanzia siasa hayawezi kuwa kweli. Sivyo?

Sasa hapa kuna kitu watu wengi hawakifahamu na yeye mwenyewe kwa kuwa hakupenda kunasibishwa
na harakati za Abdulwahid habari hizi hazikupata kujulikana.

Nyerere alipochukua uongozi wa TAA 1953 chama kilikufa.

Ukipenda na wanaukumbi wakiona kuna haja naweza Insha Allah nikaeleza kwa kirefu nini kilitokea.

Hilo la Sykes?? kutotoa jina lake akamwachia Nyerere kupita bila kupingwa vilevile ikiwa ni lazima
naweza nikalieleza hapa.

Iwe itakavyokuwa naheshimu fikra zako.

Miye nitafurahi ukiweka kwani itatupa mwanga wa kuuliza mengi zaidi na kujifunza mengi zaidi. Tafadhali tuwekee hapa mheshimiwa
 
Mzee Mohamed Said, jee huyu Bi Mluguru biti Mussa mama yake Abdu, ndiye huyu aliyekuwa akiiishi pale Upanga, opposite Califonia Dreamer?.

Naomba utuhadithie hicho kisa cha Nyerere "kulishwa sumu!".
Pasco.

Hapana huyo wa pale Upanga ni mama yetu.
Mke wa Abdu Sykes mama yake Daisy, Kleist, Adam na Omar (marehemu).

Bi Mluguru biti Mussa ni mama yake Abdu Sykes.
 
Kwa hiyo kusema kuwa kina Sykes walikuwa wanaongoza harakati za kupinga ukoloni kama ulivyosema hapo juu kuwa:

Kwa hiyo siyo KWELI kwamba ukoo wa Sykes uliongoza mapambano dhidi ya serikali isipokuwa kama unamaanisha kuwa 'serikali' hapa unaizungumzia ile ya Mwingereza tu.

Je, siyo KWELI kwamba Sykes aligeuka dhidi ya serikali ya Mwingereza kwa sababu walimuondoa Mjerumani na ukoo wake ulifanya hivyo hivyo kwa sababu yule waliyemtumikia kwa maisha yao na ambaye kwake walipata ujira wao aliondolewa na Mwingereza? Kwamba harakati za Sykes dhidi ya Mwingereza hazikuwa kwa sababu ya kutaka uhuru wa Mwafrika zaidi kuliko kumuondoa aliyemwondoa kipenzi chao - Mjerumani?

Naomba - ikikupendeza - ututajie angalau maandishi au nyaraka tatu tu za Nyerere kabla ya 1953 ambazo umezisoma na ambazo hazikukuvutia hadi alipokuja Dar in 1953. Maana fikra za Nyerere kisiasa hazikuanza kujengwa alipokuja Dar na kujiunga na TAA; zilikuwa zimejengwa miaka mingi nyuma na aliziweka wazi hivyo.

Sasa hapa kuna kitu watu wengi hawakifahamu na yeye mwenyewe kwa kuwa hakupenda kunasibishwa
na harakati za Abdulwahid habari hizi hazikupata kujulikana.

Miye nitafurahi ukiweka kwani itatupa mwanga wa kuuliza mengi zaidi na kujifunza mengi zaidi. Tafadhali tuwekee hapa mheshimiwa

Nashukuru kuona kile nilichojaribu kumuuliza Mohamed Said juu ya wasifu wa Mzee Nyerere kisiasa akiwa Makerere na akiwa Misheni Pugu

Lakini kwa bahati mbaya mzee Mohamed Said hakujibu inavyostahiki!

Na lengo la kumuuliza hivyo nilitaka kuijibu hoja yake kuwa Mwalimu aliingizwa katika siasa na Abdu alipofika Dar jambo ambalo sio kweli.
 
Ndugu yangu tusifanye mjadala wa nipe nikupe kwa kawaida wasomaji hawanufaiki sana.
hata hivyo nitakujibu.

Kuhusu ukoloni wa Kijerumani na Kleist nimekueleza lakini naona unafanya msisitizo.
Mimi sina ugomvi na fikra na uchambuzi wako.

Binadamu lazima tupishane namna tunavyoona mambo.
Hili lisitukwamishe.

Napenda nikuonye mimi ni msomaji nimemsoma Nyerere kwingi hata sikumbuki vitabu vingine. Nyerere nimemsoma kwa John Hatch, hicho cha Smith, Judith Listowel, Ali Mazrui, Kivukoni College, Kimambo, Lupatu, Mwenegoha, Nimitz, Muhsin, nyaraka zake katika mafaili ya Sykes, vitabu vyake vyote alivyoandika mwenyewe nk. nk.

Sasa kuhusu kusinzia kwa TAA baada ya uchaguzi wa 1953 Nyerere alipingia madarakani:

''Mara baada ya Nyerere kuchukua uongozi wa TAA chama kikaanza kusinzia, ushupavu na bidii iliyokuwepo wakati wa uongozi wa Abdulwahid vilitoweka.

Kwa hakika ilikuwa wakati mmoja tukatika historia ya Dar es Salaam ambapo mkristo Erikah Fiah, alikamata bendera dhidi ya serikaly ya kikoloni. historia ya Dar es Salaam, Mkristo akakamata bendera dhidi ya serikali ya kikoloni.

Nyerere alikuwa akikaa nje ya mji na alikuwa akija Dar es Salaam mwishoni mwa juma tu. Kwa kiasi fulani hii iliathiri shughuli za chama.

Kwa muda wanachama walionekana kama wamepoteza hamu ya chama.

Wajumbe wa kamati ya utendaji mara nyingine hawakutokea kwenye mikutano ijapokuwa Dossa aliwapitia majumbani kwao na gari yake kuwachukua.

Dossa anakumbuka kuwa alikuwa akisimama nje ya nyumba ya mwanakamati na kupiga honi. Mtoto au mke wa mwanakamati angetoka mlangoni kutoa habari kuwa hakuwapo, katoka ilhali yupo ndani.

Kwa muda kidogo ilionekana kama Nyerere alikuwa kikwazo cha maendeleo ya TAA.

Na huu ndiyo ulikuwa mwendo wa TAA, nguvu yake ilikuwa ikitegemea uwezo wa viongozi wake.

Awamu ya kwanza ya uongozi wa Kleist Sykes na Mzee Bin Sudi katika makao makuu TAA ilipiga hatua kubwa.

Vivyo hivyo katika zama za Ali Juma Ponda na Hassan Suleiman katika tawi la Dodoma, TAA ilikuwa ikisikika sana na uongozi wake uliheshimiwa hata nje ya Tanganyika.

Abdulwahid alikuwepo kama makamu wa rais lakini alipendelea kumwona Nyerere akiendesha ofisi na kufanya maamuzi yake mwenyewe kama rais.

Akakihofia kufa kwa chama, Abdulwahid aliwataka shauri viongozi wenzake wa ndani katika TAA - Ally, Dossa, Tewa na Rupia kuwa kipi kifanyike ili kudhibiti hali ile iliyojitokeza.

Ilikuwa dhahiri tatizo lilikuwa ni katika kubadilisha uongozi.

Wanachama walikuwa hawana imani na uongozi mpya katika ngazi ya juu.

Hili linaweza kueleweka ikifikirika kuwa ilikuwa ni miaka mitatu tu huko nyuma wakati Abdulwahid na Dr Kyaruzi walikifufua baada ya kupoteza mwelekeo baada ya Vita Kuu ya Pili.

Iliamuliwa kuwa wazee Waislam wa mjini Dar es Salaam waombwe kumuunga mkono Nyerere...''
 
Kwa hiyo kusema kuwa kina Sykes walikuwa wanaongoza harakati za kupinga ukoloni kama ulivyosema hapo juu kuwa:

Kwa hiyo siyo KWELI kwamba ukoo wa Sykes uliongoza mapambano dhidi ya serikali isipokuwa kama unamaanisha kuwa 'serikali' hapa unaizungumzia ile ya Mwingereza tu.

Je, siyo KWELI kwamba Sykes aligeuka dhidi ya serikali ya Mwingereza kwa sababu walimuondoa Mjerumani na ukoo wake ulifanya hivyo hivyo kwa sababu yule waliyemtumikia kwa maisha yao na ambaye kwake walipata ujira wao aliondolewa na Mwingereza? Kwamba harakati za Sykes dhidi ya Mwingereza hazikuwa kwa sababu ya kutaka uhuru wa Mwafrika zaidi kuliko kumuondoa aliyemwondoa kipenzi chao - Mjerumani?

Naomba - ikikupendeza - ututajie angalau maandishi au nyaraka tatu tu za Nyerere kabla ya 1953 ambazo umezisoma na ambazo hazikukuvutia hadi alipokuja Dar in 1953. Maana fikra za Nyerere kisiasa hazikuanza kujengwa alipokuja Dar na kujiunga na TAA; zilikuwa zimejengwa miaka mingi nyuma na aliziweka wazi hivyo.

Nashukuru kuona kile nilichojaribu kumuuliza Mohamed Said juu ya wasifu wa Mzee Nyerere kisiasa akiwa Makerere na akiwa Misheni Pugu

Lakini kwa bahati mbaya mzee Mohamed Said hakujibu inavyostahiki!

Na lengo la kumuuliza hivyo nilitaka kuijibu hoja yake kuwa Mwalimu aliingizwa katika siasa na Abdu alipofika Dar jambo ambalo sio kweli.

Kwa Dar es Salaam Nyerere aliingizwa katika siasa na Abdu Sykes.

Hakuna mtu aliyekuwa anamjua Nyerere katika siasa za Dar es Salaam hadi
Abdu alipomleta ofisi ya TAA New Street.

Hiki wala si kitu cha kificho watu wote wa Dar es Salaam katika harakati zile za
1950 wanajua.

Ikiwa unaamini kuwa Nyerere alijitambulisha mwenyewe sawa siwezi kukulazimisha.
 
Hapana huyo wa pale Upanga ni mama yetu.
Mke wa Abdu Sykes mama yake Daisy, Kleist, Adam na Omar (marehemu).

Bi Mluguru biti Mussa ni mama yake Abdu Sykes.
Nilipelekwa pale Upanga na Mwamvua, na kuna vitu kuhusu Maria Nyerere, Mama yenu alinihadithia, yeye ndiye aliyempokea na kuishi nao nyumbani kwao mara baada ya Mwalimu kuacha kazi na ikawa ndio kama Mama Maria kaletwa kwa "kungwi", wakamfundisha kila kinachofundishika kuanzia kusukuma chapati, kuokota vifuu na makumbi kwa ajili ya biashara ndogo ndogo, hadi biashara za kuuza vitumbua!. Kwa vile mimi sio mwandishi sikuweza kuandika, ila kwa vile Mama Maria yuu hai, ni busara simulizi yake ikarekodiwa na kuwa documented, vinginevyo itaja siku ya siku, hatakuwepo tena, na ikitokea simulizi kama ya huyo mama yenu, ikasimuliwa upande mmoja, itakuja onekana ni uongo!.
Kwa Watanzania wengi, wanamfahamu Mama Maria kama mama wa nyumbani tuu, simulizi ya mama yenu kuhusu Maisha ya Mwalimu na Mama Maria wakiwa ni wageni wao, wakiishi nyumba moja kabla ya Mwalimu kupatiwa nyumba pale Magomeni, leaves much to be desired!.
Nimewahi kukutana na mama Maria several times na mara ya mwisho ni last December tumesafiri same flight next seat nilitamani kuomba appointment, yule bodyguard wake anakuwa too protective, kumzuia Mama asizungumze hata maongezi ya kawaida tuu!. Nadhani moja ya kazi za hawa ma body guard sio tuu kuzuia asidhurike, bali ni gate keepers kuhakikisha nothing goes out!.
I wish panapo majaaliwa, nitafuata the right channels nimrekodi huyu mama, just for record keeping na sio kusubiri zile simulizi za "..alikuwa".
Pasco.
 
Iliamuliwa kuwa wazee Waislam wa mjini Dar es Salaam waombwe kumuunga mkono Nyerere...''

Tuanzie hapa tu niache huko kwingine; uamuzi huu wa kutaka 'Wazee Waislamu wa mjini Dar waombwe" ulichukuliwa na nani na lini? Lakini siyo wazee wote Waislamu waliokubali kumuunga mkono Nyerere sivyo? Ni wazee gani maarufu wa Dar ambao hawakuwa tayari kumuunga mkono Mwalimu na kwanini?
 
Kwa Dar es Salaam Nyerere aliingizwa katika siasa na Abdu Sykes.

Hakuna mtu aliyekuwa anamjua Nyerere katika siasa za Dar es Salaam hadi
Abdu alipomleta ofisi ya TAA New Street.

Hiki wala si kitu cha kificho watu wote wa Dar es Salaam katika harakati zile za
1950 wanajua.

Ikiwa unaamini kuwa Nyerere alijitambulisha mwenyewe sawa siwezi kukulazimisha.

Bado unasimamia kauli yako kuwa safari ya kisiasa ya Nyerere ilianzia 1953? na aliingizwa katika siasa na kina Sykes? Kabla ya kuja Dar Nyerere aliwahi kuanzisha taasisi au chama chochote kwa ajili ya kupigania maslahi ya waafrika? au kujaribu kujiingiza TAA kabla ya kukutana na Sykes na wazee wa Dar?
 
Hili linaweza kueleweka ikifikirika kuwa ilikuwa ni miaka mitatu tu huko nyuma wakati Abdulwahid na Dr Kyaruzi walikifufua baada ya kupoteza mwelekeo baada ya Vita Kuu ya Pili.

Iliamuliwa kuwa wazee Waislam wa mjini Dar es Salaam waombwe kumuunga mkono Nyerere...''
Mkuu Maalim, Mohamed Said, nimenote katika sumulizi zako, linapotokea jina kama Dr. Kyaruzi na Abdulwahid, hata kama Dr. Kyaruzi ndio aliyekuwa mkuu, wewe utaanza na Abdulwahid na kufuatia Dr. Kyaruzi, hivyo kupelekea kuonekana kana kwamba anaye play the leading role ni Abdulwahid na Dr. Kyaruzi kuonekana kama ni subordinate tuu wakati ukweli halisi unaujua fika kuwa japo ni kweli "the masses" behind harakati za uhuru kwa Dar es Salaam ni "Wazee wa Darisalama", ila the main players, "the brain behind" ni watu kama kina Nyerere, Kyaruzi and the like, na sio Wazee wa Darisalama!.
Pasco.
 
Bado unasimamia kauli yako kuwa safari ya kisiasa ya Nyerere ilianzia 1953? na aliingizwa katika siasa na kina Sykes? Kabla ya kuja Dar Nyerere aliwahi kuanzisha taasisi au chama chochote kwa ajili ya kupigania maslahi ya waafrika? au kujaribu kujiingiza TAA kabla ya kukutana na Sykes na wazee wa Dar?

Hapana inawezekana huko alikotoka alifanya makubwa.
Lakini kwa Dar es Salaam ambako ndiko hasa siasa zilikuwa
kali hakuna aliyepata kusikia jina la Nyerere.

Ukipenda pitia magazeti ya Zuhra ya mwaka 1950 upime hali
ya siasa ilikuwaje.

Hebu soma hapa chini kama unaweza kupata kitu:

Mwaka wa 1952 Julius Kambarage alikuja Dar es Salaam kama mwalimu akisomesha St. Francis College, Pugu. Historia ya Nyerere katika siasa inafungamana pakubwa na historia ya Hamza Kibwana Mwapachu. Hamza Mwapachu alisoma na Nyerere Makerere College Uganda na wakawa pamoja Tabora mwaka wa 1945 na baadaye wakawa tena pamoja nchini Uingereza kwa masomo ya juu.

Mwapachu na Nyerere walikaa kati bweni moja walipokuwa wanafunzi Makerere wakati ambapo Kasella Bantu na Nyerere walifundisha pamoja hapo Tabora. Nyerere alitangulia kurudi Tanganyika akitokea Chuo Kikuu Cha Edinburgh, Uskochi akamwacha Mwapachu akiendelea na masomo Chuo Kikuu cha Wales, Cardiff.

Mwapachu alimpa barua Nyererere amfikishie kwa Abdulwahid Sykes. Katika hotuba ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam aliyoitoa tarehe 5 Novemba, 1985 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Nyerere aliwaambia waliohudhuria kuwa Kasella Bantu ndiye aliyempeleka nyumbani kwa Abdulwahid na kumtambulisha.

Barua ya Hamza Mwapachu kwa rafiki yake Abdulwahid Sykes ilikuwa inamtambulisha Nyerere kwa Abdulwahid na ikimueza Nyerere kama mtu mwenye fikra nzuri zinazoweza kuisaidia TAA kufikia malengo yake.

Nyumba hii hivi sasa haipo tena badala yake hivi sasa Ally Sykes anajenga nyumba ya gorofa tano.

Wakati ule mwaka 1952 Abdulwahid ndiye alikuwa rais wa TAA na akifanya kazi kama Market Master, soko la Kariakoo.

Hotuba hii ya Diamond Jubilee ndiyo ilikuwa mara ya kwanza Nyerere kuzungumza hadharani siku zake za mwanzo Dar es Salaam na ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuihusisha katika kadamnasi historia yake na TANU na kulitaja jina la Abdulwahid Sykes.

Bahati mbaya sana hotuba ile ilivurugika na kitu kidogo sana. Nyerere alipokuwa anaeleza nafasi za uongozi katika TAA alisema hakumbuki marehemu Abdulwahid alikuwa na cheo gani.

Hili kwa hakika lilikuwa jambo lililoshangaza wazee wengi katika hadhira ile kwani wengi wao wasingelimfahamu Nyerere sama na kuletwa Makao Makuu ya TAA pale New Street na marehemu Abdulwahid Sykes.

Hata hivyo hotuba ya Nyerere ilimpamba sana Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo na Mohamed Jumbe Tambaza. Nyerere alieleza mchango wa wazee hawa kwa maneno na visa vya kupendeza.

Ukimtoa Dossa Aziz aliyekutana na Nyerere kwa muda mfupi katika mkutano mkuu wa TAA Dodoma Aprili 1946, Kasella Bantu mwenyewe na Denis Phombeah, hakuna mtu mwingine aliyewahi kusikia habari za Nyerere. Katika kukutana huku kati ya Nyerere na Abdulwahid Sykes mapenzi makubwa yalimea kati yao na kwa njia hii Nyerere akatiwa katika kundi la ndani katika TAA, kundi la vijana wasomi waliokuwa wakipanga mikakati ya kumng'oa Muingereza katika ardhi ya Tanganyika.

Vijana waliokuwa pale New Street walikuwa Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Steven Mhando, Dunstan Omar na wengineo pamoja na Mzee John Rupia. Vijana hawa walikuwa wakikutana kila Jumapili nyumbani kwa Dossa Aziz Mbaruku Street kona na Congo au nyumbani kwa Abdulwahid, Stanley Street kona na Sikukuu. Hizi ndizo zilikuwa baraza mbili ambazo wazalendo walikuwa wakikutana kujadili mustakabali wa Tanganyika.

Kuongezeka kwa Nyerere kulitia nguvu sana baraza hii.

Mijadala ya siasa miongoni mwa vijana hawa sasa ilivuka kutoka manung'uniko ya ndani ya nchi kama migomo ya wafanyakazi na matatizo ya ardhi ya Wameru na kuingia kujadili masuala ya kimataifa ya mrengo wa kushoto na hasa kuhusu kuwa na utawala wa Waafrika Tanganyika.

Kwa ufupi mijadala sasa ililenga katika kuutokomeza utawala wa Waingereza katika Tanganyika. Nyerere alimwona Abdulwahid kama mtu mwenye akili sana, kijana aliyejiweza kihali na mtu mwenye moyo mkubwa usiokuwa na hasad wala choyo.

Watu walioishi na marehemu Abdulwahid wanasema alikuwa mtu karimu sana hujapatapo kuona na mwenye haiba ya kupendeka.

Abdulwahid alimuona Nyerere, kama mtu aliyeelimika vizuri kati yao na mwenye ustadi katika mijadala. Nyerere alipata nafasi ya kuifahamu dunia vizuri lau kama alikulia kijijini.

Zaidi Nyerere alikuwa amepata uerevu wa siasa kutokana na uhusiano wake na Fabian Society, wakati alipokuwa mwanafunzi Uingereza. Mijadala mizito sana ilijitokeza katika vile vikao vya kila Jumapili wakati akili na ujuzi wa siasa wa Abdulwahid vilipopambana na uhodari wa majadiliano wa Nyerere.

Abdulwahid alipata uzoefu mkubwa wa uongozi katika siasa nyumbani kwao kwa baba yake aliyeasisi African Association kisha wakati wa vita Burma na baada ya vita serikali ya kikoloni ilipomteua kuwa katibu wa kwanza wa chama cha wafanyakazi Dockworkers Union akiwa kijana mdogo wa miaka 24.

Nyerere hakuwa na wa ujuzi wowote katika siasa ukimlinganisha na Abdulwahid. Wakati African Association Tabora kiliposhiriki katika mgomo wa mwaka 1947 ambao chanzo chake kilikuwa mgomo wa makuli Dar es Salaam, Nyerere hakujihusisha na harakati zile za wafanyakazi ingawa yeye ndiye alikuwa katibu wa African Association pale Tabora.

Jukumu kubwa la mgomo ule lilibebwa na Salum Abdallah na wanachama wa kawaida katika African Association. Salum Abdallah baada ya kuundwa kwa TANU mwaka 1955 alikuwa rais muasisi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) katibu akiwa Christopher Kassanga Tumbo. TRAU na TANU vilishirikiana vizuri sana katika kupambana na serikali ya kikoloni.

Kutokana na Nyerere kuingia katika harakati zile pale New Street pakawa na kuheshimiana na mapenzi makubwa baina yake, Abdulwahid, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia.

Kila Jumapili Nyerere alikuwa akisafiri kutoka Pugu hadi Dar es Salaam kuhudhuria baraza lile lililokuwa likijadili siasa za Tanganyika. Baada ya kikao, Dossa Aziz au Dunstan Omar alimrudisha Nyerere kwa gari hadi Pugu.

Hivi ndivyo Nyerere alivyokuja kuingia ndani ya TAA Makao Makuu na hatimaye akaja kupendekezwa kugombea cheo cha juu kabisa cha uongozi wa chama mnamo Aprili, 1953.

Uongozi wa TAA ulimpendekeza Julius Nyerere ili kukiimarisha chama kwa kuwa na Waafrika wenye elimu ya juu ndani yake. Ilibakia kwa Nyerere kukubali au kukataa.

Kujadili siasa haikuwa sawa na kuongoza chama kilichokusudia kunyakua madaraka kutoka kwa serikali ya kikoloni. Hivi vilikuwa ni vita dhidi ya ukoloni na ilibidi mtu ajitayarishe kwa lolote ambalo lingetokea.
 
Mkuu Maalim, Mohamed Said, nimenote katika sumulizi zako, linapotokea jina kama Dr. Kyaruzi na Abdulwahid, hata kama Dr. Kyaruzi ndio aliyekuwa mkuu, wewe utaanza na Abdulwahid na kufuatia Dr. Kyaruzi, hivyo kupelekea kuonekana kana kwamba anaye play the leading role ni Abdulwahid na Dr. Kyaruzi kuonekana kama ni subordinate tuu wakati ukweli halisi unaujua fika kuwa japo ni kweli "the masses" behind harakati za uhuru kwa Dar es Salaam ni "Wazee wa Darisalama", ila the main players, "the brain behind" ni watu kama kina Nyerere, Kyaruzi and the like, na sio Wazee wa Darisalama!.
Pasco.

anapozungumzia Wazee wa Dar hazungumzii watu kama kina Rupia, Kyaruzi, Mhando n.k... ana maana yake maalum. Tulishaelewa hilo na ukumbuke hataki kuzungumzia ya Wazee waliosahaulika (including hawa kina Rupia, Kyaruzi n.k) yeye ana ndugu yetu anaposema "wazee" ana maana ya Wazee wa Kiislamu na kuwa walikuwa na nafasi ya pekee. Ili kukamilisha hili narrative ni lazima awataje wazee wa Kiislamu kwa namna ya kipekee kuliko wengine ili narrative yake ikamilike. Ni lazima umsome ndugu yetu huyu hivyo.

Ukitaka kuzungumzia mchango wa wazee wengine wasiokuwa Waislamu wakati wa harakati za uhuru na waliokuwa Dar inabidi uandike stori hiyo kuelezea juu ya "wazee wako" kwani yeye kaandika juu ya wazee "wake" a.k.a Wazee wake Waislamu.
 
Inawezekana lakini ndiyo wewe unaniambia sasa.
Haikunipitia kabisa.

Kuhusu ''brains'' baba yangu ananiambia kuwa yeye na Abdu walianza kusomeshwa mashaf
yaani Qur' an siku moja.

Abdu kamaliza kabla ya wenzake wote na akaja kuwa ndiyo mwalimu wao maalim asipofika darasani.

Cambridge alitoka first class.

Kyaruzi alipata kusema kuwa kama si ile mipango ya Mwapachu na Abdu ya 1950 Tanganyika isingepata
uhuru 1961.

Alikuwa mtu wa kipaji sana.
Si ajabu historia ya Nyerere ukimleta Abdu.

Matatizo tayari.

Dar es Salaam ya 1950s ilikuwa nyingine.
Kyaruzi "was playing second fiddle."

Huu ndiyo ukweli wa siasa za miaka ile.
Nani anamjua Kyaruzi?
 
Kwa Dar es Salaam Nyerere aliingizwa katika siasa na Abdu Sykes.

Hakuna mtu aliyekuwa anamjua Nyerere katika siasa za Dar es Salaam hadi
Abdu alipomleta ofisi ya TAA New Street.

Hiki wala si kitu cha kificho watu wote wa Dar es Salaam katika harakati zile za
1950 wanajua.

Ikiwa unaamini kuwa Nyerere alijitambulisha mwenyewe sawa siwezi kukulazimisha.

Ninachofurahi ni kuwa sasa hivi umebadili maana ya sentensi hiyo na sasa umeongeza kuwa "KWA" Dar es Salaam Nyerere alitambulishwa katika siasa na Abdu,

Sasa maana yote ya ile hoja imebadilika, na imesimamia kwa tunaomjua kuwa wasifu wa siasa za Mzee Nyerere hazikuanzia Dar, bali akiwa sekondari pale Tabora, akiwa Makerere pale Uganda, na akiwa Uingereza kote huko aliacha alama ya isiyofutika, hata wale waliosoma nae walishamtabiria makubwa hata kabla ya hatamu stahiki.
 
anapozungumzia Wazee wa Dar hazungumzii watu kama kina Rupia, Kyaruzi, Mhando n.k... ana maana yake maalum. Tulishaelewa hilo na ukumbuke hataki kuzungumzia ya Wazee waliosahaulika (including hawa kina Rupia, Kyaruzi n.k) yeye ana ndugu yetu anaposema "wazee" ana maana ya Wazee wa Kiislamu na kuwa walikuwa na nafasi ya pekee. Ili kukamilisha hili narrative ni lazima awataje wazee wa Kiislamu kwa namna ya kipekee kuliko wengine ili narrative yake ikamilike. Ni lazima umsome ndugu yetu huyu hivyo.

Ukitaka kuzungumzia mchango wa wazee wengine wasiokuwa Waislamu wakati wa harakati za uhuru na waliokuwa Dar inabidi uandike stori hiyo kuelezea juu ya "wazee wako" kwani yeye kaandika juu ya wazee "wake" a.k.a Wazee wake Waislamu.

Kitabu changu nimeandika habari za wazee wangu na hili nalisema kila siku.
Siwezi kuandika habari za watu ambao mimi siwafahamu.

Hao wengine nimewataja kama ilivyo ada katika kueleza jambo.
Nisingeweza kueleza habari za watu wote hata wale ambao habari zao
sizijui.

Mimi ni Muislam na katika historia ile ya Kivukoni na mengi yaliyoandikwa
Waislam walitupwa nje.

Hii ndiyo sababu ya kuwarudisha katika historia.
Sasa nyie mngelimjuaje Sheikh Hassan bin Amir kama nisingelimwandika?
 
Ninachofurahi ni kuwa sasa hivi umebadili maana ya sentensi hiyo na sasa umeongeza kuwa "KWA" Dar es Salaam Nyerere alitambulishwa katika siasa na Abdu,

Sasa maana yote ya ile hoja imebadilika, na imesimamia kwa tunaomjua kuwa wasifu wa siasa za Mzee Nyerere hazikuanzia Dar, bali akiwa sekondari pale Tabora, akiwa Makerere pale Uganda, na akiwa Uingereza kote huko aliacha alama ya isiyofutika, hata wale waliosoma nae walishamtabiria makubwa hata kabla ya hatamu stahiki.

Narudia kusema tena mimi sina tatizo na historia ya Nyerere huko nyuma
kama amefanya makubwa ya kuhadithiwa ni haki yake hayo yaenziwe.

Kinachonishangaza ni pale makubwa ya wengine yanapokataliwa na magazeti
kutiwa moto.

Pale ndipo nilipojiuliza.

Nyerere anaogopa nini?

Kama TANU yeye hakuasisi kama hivyo anavyotaka watu waamini.
Kuna habari lazima isemwe hadi tumfikie yeye 1953.

Hapo ndipo niliponyanyua kalamu.

Ndiyo maana leo Abdulwahid Sykes kaja kujulikana pamoja na wazalendo
wenzake.
 
Swali 1: Je, vitabu vya Bergen na Silvalon haviwezi kuwa vimefanyiwa upotoshaji kama ule uliofanywa kwa Ditopile?
Mohamed Said;5487489 Kitabu kimetoka na waandishi wake hawajasema kuna tatizo la upotoshaji.
1.Uwezekano ni mdogo sana
MS anaamini kuwa Ditopile anaweza kuwa alitendewa vibaya na magazeti yanayosimamiwa na wakristo lakini yeye na kundi lake wana haki ya kuaminiwa kuwa hakuna upotoshaji hata pale ambapo imedhihirika kuwa kulikuwa na upotoshaji wa hali ya juu. 1. Kuhusu namba za mitihani, 2. Kuhusu kupigwa marufuku kitabu chake UDSM ''by Christian lecturers'' n.k. Anachotaka ni ku-provoke mtafaruku kama alivyowahi kuwataka maaskofu wajibu hoja za kitabu pengine kulenga kuamsha hisia na kuchochea vurugu kwa uwazi kwasababu Ponda si peke yake.
Swali 2: a) Kuna ushahidi gani kuwa madiwani, mameya na viongozi wengine wa jiji walipigwa marufuku kutoa jina la mtaa wa Mshume Kiyate(b) Je, aliyebadilisha jina la bara bara kama UWT/Bibi titi ni Nyerere au ni madiwani wa jiji(c)Kwanini Moshi waenzi watu wao Dar washindwe? Ni kosa la nani?
(a) Mohamed Said;5487489 Katika mambo ya hujuma shida kupata ushahidi isipokuwa watendaji wanakuwa hawafanyi kinachotakiwa
Hapa anatupa ushahidi kuwa hana uthibitisho bali hisia zake zinamtuma kusema hivyo. Tena bila haya MS amekua akitumia neno ''huo ni ukweli'' sidhani kama kuna ukweli usiothibitika. Tunaposema historia asemayo imejengwa katika hisia, ushihidi ni kama huo.Hata kama maandishi yake yanaweza kuleta vurugu, MS yupo bize na toleo la tatu, take care of today, tommorrow will take care of itself.

Waliobadili majina ya mitaa ni madiwani wa Dar es salaam. Walioshindwa kuwaenzi wakazi na wanaharakati ni madiwani na wananchi wa Dar es salaam. Kuna nyakati Mwenyekiti wa CCM mkoa, Wilaya, Mkurugenzi, Meya na Madiwani wote walikuwa wazee wake. Anajua fika kuwa kosa si la Nyerere ni la wazee wake kama akina tambalizeni ambao badala ya kufikiria namna ya kuboresha maisha ya wakazi na wenyeji wamebaki kuandika ngonjera kama hizi tunazoziona.

MS hapaswi kutumia muda mwingi kumhukumu Nyerere kwa jina la mtaa mmoja ambao mtendaji wa kata angeweza kukaa na wananchi na madiwani wao wakafanya hivyo.

MS anapaswa aangalie picha kubwa zaidi. Je,kuna kitu gani cha kumbu kumbu ya Mzizima walikoishi wenyeji wetu?
Je, kiwanja cha Chang'ombe kiendelezwe vipi kwa faida ya wakazi wa jiji.
Je, kifanyike nini wakazi wa kariakoo-mzizima wanufaike na ardhi na rasilimali zilizopiganiwa na akina Abdul Sykes na Kiyate. Kwanini wahamishwe kwa kupewa milioni 15 kwa kitu chenye thamani ya milioni 400 n.k.
Kufikiria street moja tu ni tatizo kabla ya tatizo.

Walioifikisha Dar hapo ilipo ni wazee wako, Nyerere anafanywa Bangusilo tena kwasababu tu ya jina Julius.
Anahukumiwa kwa uzembe, ujinga na ututusa usiomhusu.
Nyerere hakuwa diwani Moshi, Mwanza au Mbeya! kimeshindikana nini Dar!
MS warithishe watoto werevu na kujitambua kwasababu dunia ya leo majungu haujawa mtaji wa maana the least to say
Swali 3( a) Kwanini Waislam wasitake kukaa na Mwinyi, Mkapa au Kikwete bali serikali?
b)Mbona yaliyotokea nyuma hayatajwi kama ni matatizo ya serikali yanasemwa ni ya Nyerere na kwanini leo hayasemwi kama ya Kikweteyanasemwa kuwa ni ya serikali?
Mohamed: Sijui hilo swali wanaweza kujibu viongozi wa Waislam (b) Sijui waulizwe viongozi wa Waislam
Sasa kama unajua hujui na huna majibu, kwanini ujihusishe na kuwa msemaji wa waislam?

Ukweli ni kuwa unaogopa kusema Mwinyi, Mkapa au Kikwete kwasababu kufanya hivyo utagusa wazee wako.
Tunarudi nyuma kuwa tuhuma dhidi ya Nyerere ni za kupikwa kwasababu historia inamsuta MS.
Huwezi ukawa na tukio moja katika historia ukachagua namna ya kulijadili au kuliandika kwa nyakati tofauti.
Chuki dhidi ya Nyerere ni kwasababu tu ya kumhusisha na dini yake.

MS unapaswa kwenda kujadiliana na Kikwete kwanza, kwasababu Nyerere ni marehemu. Kuendelea kumsukumia lawama hakumdhuru bali kunaidhuru jamii yako. Kumzushia yaliyomshinda Mwinyi na Kikwete ni ubaguzi wa ajabu sana.
Ubaguzi ni dhambi mbaya sana na humdhalilisha awaye
Swali (a)Kwa vile tunatafuta muafaka wa kitaifa, yeye ana maoni yapi kuhusu suluhu ya duku duku hilo.
Nini suluhisho ili kuondoa dhulma anayoidai.Nini kifanyike
(i) katika kuleta uwiano wa madarakaii)uwiano wa elimuiii) n.k.
Mohamed: Dukuduku ni kwanza serikali ikubali lipo tatizo
Nyerere aliwahi kulieleza na maandishi yapo. Mkapa kalizungumzia hotuba ipo.
Kikwete hajawahi kulizungumzia. Tatizo lipo lakini si kwa namna unayoielewa wewe na kundi lenu.

Kwanza hamtafuti suluhu mnachotaka ni kuvuruga nchi. Mtu mwenye suluhu hawezi kuwa anapiga mdomo na ikifika mahali anaulizwa tufanye nini anajibu haya
Hayo mengine matatu ni Waislam wanyewe waseme uwiano nk
MS anachotaka ni kuita majina na kuwapa watu madaraka. Kuita majina na kuwapa watu kazi za taaluma.
Kwamba kwake Daktari anaweza patikana kwa uwiano au kupiga kura!!!

Kibaya zaidi MS anaamini kuwa mtu anayeitwa Abdallah Husein Bin Suein au John William Walace basi huyo ni muumini wa dini. Tatizo la watu kama akina MS ni kutochukua kioo na kujiangalia!Ni kunajisiwa fikra zao na ukoloni wakidhsni kuwa dini ni jina hata kama awaye ni mzushi, jambazi, muongo.

Hivi unapata wapi mtaalam au kiongozi kutoka Kilwa kama shule zinafungwa kwa kukosa wanafunzi.
Shule ifungwe kwenda kusikiliza kesi ya Ponda!! Hayo si tatizo kwa MS,tatizo ni Nyerere!
MS waambie watu wako ukweli acha kuwadanganya ili uuze nakala za vitabu, unawapotezea muda wa kusonga mbele.
Swali 4 (a)Kitabu cha Bergen Kimepigwa marufuku kwa tamko la nani na lini!
b) Kitabu cha Mohamed kilichozuiliwa kuwa reference UDSM, ni kwa tamko la nani na lilitoka lini
Mohamed :Kitabu kuzuiwa hilo haliwekwi dhahir ila wanafunzi wa historia wanaambiwa hivyo
MS hana ushahidi wa maswali yote mawili, bado anasema alichoandika ndio ukweli. Huu ni ushahidi kuwa sehemu kubwa ya ngano hii imejengwa kwa fikra zake binafsi zikichagizwa na uzushi.

Mwanafunzi hawezi kuja kusema na mtafiti akakubali tu kwasababu ni mwanafunzi huyo ni Mwislam.
Hili kama si majungu ni nini. Uliposema ndani ya kitabu kuwa christian lecturers at UDSM... ulichotaka ni kujenga chuki tu.

Huko Ulaya wasikojua hali ya Tanzania hawawezi kukuuliza uwape ushahidi. Ndio maana tunasema MS ni mpotoshaji, mzushi na mjenzi wa historia kwa kutumia majina na matukio huku akichomeka mbegu yake ya chuki miongoni mwa jamii.

Kusema jambo usilo na uhakika nalo ni uzushi na ni uongo. Dini ya kiislam haitaki hivyo na imekataza.
Unapaswa umuogope mwenyezi mungu kwanza kabla ya mauzo ya kitabu.
Muogope mola wako kabla hujazua balaa maana hilo limekatazwa.

Sasa tuna mambo mengi sana ambayo Mohamed ameyaandikia kurasa na kurasa na ameshindwa kuyatetea kwa mantiki,
hoja na hekima. MS nani asiyejua kwanini unakimbia hoja na maswali na umebaki kukata vipande vya kitabu.

Ninafikiria hivi kama kuna mwanafunzi anaandika thesis na amefanyia reference kitabu hiki, atawezaje kuitetea thesis yake kama mwandishi hawezi kutetea maandiko yake. Sad!
 
Back
Top Bottom