Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kijana unatisha!

Fikra za mtu kama wewe unadhani zitaingia kwenye kitabu ambacho ni authority kama cha mzee wetu?
Mtu unayesema kuwa threads ni sawa sawa na kitabu?
Mtu ambaye hujui the significance of a work of academia being published?
Mtu ambaye hutambui the weight of Cambridge, Oxford na Harvard kukipitisha?

Kama utajaaliwa kufanya research na utabeza research yako from threads za JF, mdogo wangu utafeli vibaya na utachekwa
Kwani Ahmed Salman Rushdie kapata tuzo ngapi nzito kabisa kwa ile "fiction" yake ya "Satanic Verses"?
 
Huyo Mzee Mohamed Said, kitu muhimu kwake ni kuwa kitabu chake kimekubaliwa na kusomwa USA na UK tu! Lakini ajabu analalamika kuwa UDsm Wahadhiri hawakubali kufanyiwa marejo, na kwa kuwa Wahadhiri hao wamekataa kitabu chake; basi ni Wakristo.
Ajabu ni kuwa hao wa UK na US ambako kinatumika kwenye vyuo vyao, hawataji kwa dini zao!

Silalamiki.
Hebu lifuatie hili neno na ''ulalamishi.''

Neno hili linapendwa sana humu.
Ni tusi la rejareja ni vizuri wanaukumbi tukaliepuka.

Linavunja staha zetu.

Mimi nimeeleza hizo habari sikulalamika.
 
Nakuomba radhi.

Angalia unavyojiharibia muruwa wako.
Ilitosha kunambia kuwa siyo mimi.

Mimi nikakutaka radhi.
Hapakuwa na haja ya kuongeza hayo mengine.

Huo ni ujuvi.
Na ujuvi si sifa ya mtoto aliyefunzwa adabu na mama yake.

Usiwatukanishe wazee wako kuwa hawakukufunza adabu.
Adabu, tabia njema ni silaha utapendwa popote.
Kauli zako nyingine zinafanana na matusi lakini usipate shida. Mishale umerushiwa mingi mno humu JF ingawa mingi unaikwepa. Nakusifu jinsi unavyoweza kujisimamia mwenyewe.
 
Kwani Ahmed Salman Rushdie kapata tuzo ngapi nzito kabisa kwa ile "fiction" yake ya "Satanic Verses"?

unaruka mada sasa. Tunazungumzia kitabu cha mzee wetu wewe unarukia Rushdie. Nusu karne and you cannot keep your eye on the ball!
 
Kuna haja gani ya vitisho.
Weka ushahidi hapana tabu.
Hebu twende kidogo kidogo,
Mohamed, Ndani ya kitabu chako kuna maandishi yasemayo '' wahadhiri wa kikristo katika chuo kikuu cha UDSM wamepiga marufuku kitabu chako kistumike..’’
Una jina la mhadhiri mmoja tu aliyetoa kauli hiyo? Na kama yupo, je, ni kauli yake, kanisa au chuo kikuu.
 
... Hivi mwenzetu hauna aibu? Tuonyeshe basi hiyo dhulma wanayofanyiwa waislam ...

Nilimuliza Mzee Said kwenye uzi wake, anitajie shule ngapi za Waislam zilitaifishwa, dhidi ya shule za Wakristo, hakujibu.
Ktk kila mkoa, Kanisa / madhehebu ya Kikristo lilikuwa na shule tena hata ile mikoa inayodaiwa kuwa na Waislamu wengi.
Mkoa naotoka, shule ya Sekondari ilikuwa moja tu ambayo pia Nyerere alitaifishia na serikali haikuwahi kujenga shule hadi miaka ya 90!
 
Hebu twende kidogo kidogo,
Mohamed, Ndani ya kitabu chako kuna maandishi yasemayo '' wahadhiri wa kikristo katika chuo kikuu cha UDSM wamepiga marufuku kitabu chako kistumike..’’
Una jina la mhadhiri mmoja tu aliyetoa kauli hiyo? Na kama yupo, je, ni kauli yake, kanisa au chuo kikuu.

Bwana Nguruvi,

Ikiwa nitakupa majina na hao walonipa taarifa hizi nishawaponza.
 
Bwana Nguruvi,

Ikiwa nitakupa majina na hao walonipa taarifa hizi nishawaponza.
Je, si kweli kuwa umetunga hili jambo na kwamba hukufanya research? Sina haja unipe jina la ''source'' ninachotaka utueleze kama yupomhadhiri kwa jina ABCD na ametoa tamko hilo kama yeye, kanisa au chuo kikuu
 
Bwana Nguruvi,

Ikiwa nitakupa majina na hao walonipa taarifa hizi nishawaponza.

Je marufuku hiyo imetolewa na chuo au mhadhiri mmoja au wengi?
Ni kitu gani kilichokufanya uione marufuku hiyo kimtazamo wa dini,
Ni nini kilichokufanya uwaone wahadhiri hao kwa dini zao na sio WAHADHIRI WA CHUO KIKUU TU?
 
Hivi nguruvi3 na bigirita, wanenu wakipata admissions za kusomea african studies UDSM na Harvard au Oxbridge, mtawapeleka wapi? kwa mitazamo yenu

Naomba majibu
 
Hivi nguruvi3 na bigirita, wanenu wakipata admissions za kusomea african studies UDSM na Harvard au Oxbridge, mtawapeleka wapi? kwa mitazamo yenu

Naomba majibu

Rather uncalled for.

Anyway, nitawapeleka huko kuliko na mfumo Kristo original.
Wewe utawapeleka wapi?
 
Hivi nguruvi3 na bigirita, wanenu wakipata admissions za kusomea african studies UDSM na Harvard au Oxbridge, mtawapeleka wapi? kwa mitazamo yenu
Naomba majibu
Bw Kichwa ngumu,
Mimi nadhani unataka kuvuruga mwenendo wa hoja. Nakushauri uungane na MS kujibu hoja.
Haya mambo ya watoto watasoma wapi hayahusiani na swali
 
Je, si kweli kuwa umetunga hili jambo na kwamba hukufanya research? Sina haja unipe jina la ''source'' ninachotaka utueleze kama yupomhadhiri kwa jina ABCD na ametoa tamko hilo kama yeye, kanisa au chuo kikuu
Mzee Said, swali hilo hapo vipi?
 
Kwa hakika ninajifunza mambo mengi sana kupitia mtanange huu wa historia ya wazee wa Gerezani kariakoo.

Shukurani za pekee ziwafikie Nguruvi3, Mzee mwanakijiji, Yericko Nyerere na WildCard.

Maana mtu au watu wowote wanaofatilia mtanange huu hapa bila ushabiki ni lazima atakuwa ameamka kifikra
na kuachana na propaganda za mzee wetu MS kwa huu mchango wenu uliosheheni hoja za maana.
 
Mzee Said, swali hilo hapo vipi?

Huwa sijibu swali kama anavyotaka muulizaji.
Najibu swali kwa ufahamu wangu.

Hilo swali nimelijibu.

Nimesema wanafunzi wa Masters wakija kwangu kwa msaada huwa
sioni kitabu changu kwenye literature review yao.

Nikiwauliza kulikoni?
Wanasema kitabu chako kinatisha walimu wetu.

Hawataki hata kitiwe katika bibliography.
Kama hukuridhika na jibu hili langu basi sina la kufanya.

Lakini hebu na wewe jishughulishe kidogo.

Pitia ''dissertations'' za miaka 10 nyuma zilizofanya utafiti unaohusu historia
ya Tanganyika uangalie kama kitabu changu kipo katika bibliography.

Fika hapa Idara ya Historia uangalie na Insha Allah utujuvye.

Majina ya walimu Idara ya Historia si siri.
Lakini tujaalie nimesema fulani na fulani.

Ndiyo iwe nini.
Na wao wakasema nimewasingizia.

Ndiyo itakuwa nini.
Hakuna tija.

Sana sana nitakuwa nimewafedhehesha na watu ''source'' zote zitaniogopa.
Sijui kuweka siri.
 
Kwa hakika ninajifunza mambo mengi sana kupitia mtanange huu wa historia ya wazee wa Gerezani kariakoo.

Shukurani za pekee ziwafikie Nguruvi3, Mzee mwanakijiji, Yericko Nyerere na WildCard.

Maana mtu au watu wowote wanaofatilia mtanange huu hapa bila ushabiki ni lazima atakuwa ameamka kifikra
na kuachana na propaganda za mzee wetu MS kwa huu mchango wenu uliosheheni hoja za maana.
Asante sana kwakutambua mchango wetu katika kuiangaza historia ya nchi yetu
 
Back
Top Bottom