Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Huwa sijibu swali kama anavyotaka muulizaji.
Najibu swali kwa ufahamu wangu.

Hilo swali nimelijibu.

Nimesema wanafunzi wa Masters wakija kwangu kwa msaada huwa
sioni kitabu changu kwenye literature review yao.

Nikiwauliza kulikoni?
Wanasema kitabu chako kinatisha walimu wetu.

Hawataki hata kitiwe katika bibliography.
Kama hukuridhika na jibu hili langu basi sina la kufanya.

Lakini hebu na wewe jishughulishe kidogo.

Pitia ''dissertations'' za miaka 10 nyuma zilizofanya utafiti unaohusu historia
ya Tanganyika uangalie kama kitabu changu kipo katika bibliography.

Fika hapa Idara ya Historia uangalie na Insha Allah utujuvye.

Majina ya walimu Idara ya Historia si siri.
Lakini tujaalie nimesema fulani na fulani.

Ndiyo iwe nini.
Na wao wakasema nimewasingizia.

Ndiyo itakuwa nini.
Hakuna tija.

Sana sana nitakuwa nimewafedhehesha na watu ''source'' zote zitaniogopa.
Sijui kuweka siri.
Sawa sawa kabisa. Kwahiyo wanafunzi hao wangesema chochote wewe ungeweka katika kitabu unachosema umefanyaia research.

Lakini hujaeleza kama wanasema ni wahadhiri wakristo.
Hapa ni wazi umechomeka neno wahadhiri wakristo kwa hisia tu ulizokuwa nazo lakini huna ushahidi wa hilo kutokea.
Bado unaamnisha umma kuwa wewe hukutunga na kwamba umefanya research.

Sioni kwanini uogpe kutaja majina endapo umeweza kutaja jina la B.W. Mkapa wakati huo akiwa mhariri wa gazeti na jinsi alivyoshiriki kuua EAMWS.

Kwa wale mnaoamini kuwa kitabu kikiwa published basi kimejaa ukweli, huu ni ushihidi usio na shaka kuwa ndani ya kitabu hicho kuna mengi sana ambayo si ya kweli na hayana utetezi achilia mbali ushahidi.
Ushahidi kuwa reserach ina walakini kama si duara, na ushahidi kuwa hii ni script ya ngano iliyotumia majina,nyakati na matukio katika mpangilio maridhawa ili kufikia kilichokusudiwa.

Jitihada kubwa katika suala la UDSM ilikuwa ni kuonyesha jinsi gani mfumokristo unavyoonea waislam hadi vitabu vyao haviruhusiwi kufanyiwa reference. Jinsi gani historia ya ''kweli'' ya Tanganyika inavyofichwa na wakristo.
The bottom line is simply to associate christianity with the mission to ignite fury, angst and misunderstand in our society.

Mzee Said, upo tayari kwa jingine la pili !
Hili halikuwa na split decision, lilikuwa clean and well executed upper cut
 
Mohamed Said, naja

Nakukaribisha na kitu hiki:

Baada ya kuundwa BAKWATA, ili kuondoa wasiwasi na kuwarudishia imani Waislam, Katibu wa Tume ya Waislam, Mussa Kwikima alitoa taarifa iliyosema:

''Hakuna anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali, lakini si watu binafsiÖhata ikiwa mikoa yote kumi na saba ikijitoa haitamaananisha kuwa jumiya imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.''

Wakati ilipotoka taarifa hii BAKWATA ilikuwa bado haijaandikishwa rasmi na Msajili wa Vyama. Kisheria ilikuwa haiwezekani kwa kundi la Adam Nasibu kuunda jumiya mpya iliyokuwa na malengo sawa na jumuiya ambayo tayari ishaandikishwa.

Kwa muda wa siku tatu BAKWATA na EAMWS zikawepo kwa wakati mmoja. Ilionekana kama kwamba EAMWS itashinda vitimbi vya serikali na vya kundi la Adam Nasibu.

Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa BAKWATA Cerificate of Exemption na kuifungia EAMWS.[1] Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:

''Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[1]

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza. Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe. Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa. Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa.

Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa kingine. Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.

Huu ndiyo ukawa mwisho wa kile kilichokuwa kikijulikana kama mgogoro wa Waislam ulivyomalizika. Mgogoro ambao ulianza pale mwalimu wa shule ya msingi asiyefahamika na yeyote alipofanya maandamano katika mitaa ya Bukoba akimuunga mkono Julius Nyerere na Azimio lake la Arusha na ukaishia kwa mwalimu huyu akiwa na nafasi juu katika jumuiya ya Kiislam ambayo ilikuwa ikichukiza machoni mwa Waislam.

Mwalimu huyu ambae sasa amekuwa Makamu Katibu Mkuu wa BAKWATA alianza kazi yake kwa kuwashutua Waislam.

Katika mkutano wa waandishi wa habari Adam Nasibu aliiomba TANU na ASP kujikinga na watu wanaohujumu umoja wa nchi kupitia dini. Akaendelea na kusema kuwa BAKWATA ni sawa na Baraza la Kikristo la Tanzania. [1]

Kwa kuwa Waislam walinyimwa fursa ya kujadili ìmgogoroí hivi sasa kilichobaki na dhana tu, kuwa nini kingelitokea endapo wangeliruhusiwa kufanya mkutano ule ulioitishwa na EAMWS.

Waislam wa Bukoba ambao ilitaarifiwa kuwa walifanya maandamano kuunga mkono Azimio la Arusha hawakutayarisha maandamano ya kuunga mkono BAKWATA. Dar es Salaam na katika miji mingi ya Tanzania, neno BAKWATA halina tofauti na tusi.

Kumuita Muislam kuwa yeye ni mwanachama wa BAKWATA ni sawa na kumuita Mkristo mfuasi wa Yuda Iscariot, aliyemsaliti Yesu kwa vipande thelathini vya fedha.

(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
 
Sawa sawa kabisa. Kwahiyo wanafunzi hao wangesema chochote wewe ungeweka katika kitabu unachosema umefanyaia research.

Lakini hujaeleza kama wanasema ni wahadhiri wakristo.
Hapa ni wazi umechomeka neno wahadhiri wakristo kwa hisia tu ulizokuwa nazo lakini huna ushahidi wa hilo kutokea.
Bado unaamnisha umma kuwa wewe hukutunga na kwamba umefanya research.

Sioni kwanini uogpe kutaja majina endapo umeweza kutaja jina la B.W. Mkapa wakati huo akiwa mhariri wa gazeti na jinsi alivyoshiriki kuua EAMWS.

Kwa wale mnaoamini kuwa kitabu kikiwa published basi kimejaa ukweli, huu ni ushihidi usio na shaka kuwa ndani ya kitabu hicho kuna mengi sana ambayo si ya kweli na hayana utetezi achilia mbali ushahidi.
Ushahidi kuwa reserach ina walakini kama si duara, na ushahidi kuwa hii ni script ya ngano iliyotumia majina,nyakati na matukio katika mpangilio maridhawa ili kufikia kilichokusudiwa.

Jitihada kubwa katika suala la UDSM ilikuwa ni kuonyesha jinsi gani mfumokristo unavyoonea waislam hadi vitabu vyao haviruhusiwi kufanyiwa reference. Jinsi gani historia ya ''kweli'' ya Tanganyika inavyofichwa na wakristo.
The bottom line is simply to associate christianity with the mission to ignite fury, angst and misunderstand in our society.

Mzee Said, upo tayari kwa jingine la pili au tuuishie hapa!

Kwanza ngoja nikusahihishe kidogo.

Hilo sakata la kitabu changu kukwepwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
sikusema katika kitabu changu.

Hayo maneno yapo katika paper yangu ya ZMO, Berlin - ''Christian Hegemony...''

Nimekusoma fikra zako.
Ndiyo dunia ilivyo watu sharti waghitilafiane.

Niulize swali lolote na Insha Allah ikiwa ninalo jibu nitakupa.

Nami nimekupa changamoto vipi utakwenda kuchunguza ''bibliography''
za ''dissertations'' ulete jibu hapa ukumbini?
 
Mohamed Said;5509546]Nakukaribisha na kitu hiki:

Baada ya kuundwa BAKWATA, ili kuondoa wasiwasi na kuwarudishia imani Waislam, Katibu wa Tume ya Waislam, Mussa Kwikima alitoa taarifa iliyosema:

''Hakuna anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali, lakini si watu binafsiÖhata ikiwa mikoa yote kumi na saba ikijitoa haitamaananisha kuwa jumiya imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.''

Wakati ilipotoka taarifa hii BAKWATA ilikuwa bado haijaandikishwa rasmi na Msajili wa Vyama. Kisheria ilikuwa haiwezekani kwa kundi la Adam Nasibu kuunda jumiya mpya iliyokuwa na malengo sawa na jumuiya ambayo tayari ishaandikishwa.

Kwa muda wa siku tatu BAKWATA na EAMWS zikawepo kwa wakati mmoja. Ilionekana kama kwamba EAMWS itashinda vitimbi vya serikali na vya kundi la Adam Nasibu.

Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa BAKWATA Cerificate of Exemption na kuifungia EAMWS.[1] Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:

''Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[1]

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS
Wanajamvi,nawaomba msome vizuri maneno ya MS. Kumbe EAMWS ilivunjwa kwa amri ya serikali. Sasa serikali hiyo si ilikuwa na waziri wa mambo ya ndani Sadi Ali Maswanya na kwa upande wa kulia wa Nyerere alikuwepo Makamu wa Rais na Waziri mkuu Rashid Mfaume kawawa!
Hivyo basi suala zima ni la serikali ya Tanzania ikiongozwa na Nyerere na si amri ya Nyerere.

Kwa muktadha huo kauli za nyuma(ushahidi upo) za MS kuwa Nyerere kwa kushirikiana na kanisa waliua EAMWS si za kweli. Si za kweli kwasababu hakuna mahali MS ameonyesha ushiriki wa kanisa.
Unless aondoe neno serikali libaki Nyerere mkatoliki, MS hana justification za allegation against christians.
Nadhani angeangalia zaidi within his own society rather than fabricating unfounded allegation.
 
Swali la pili,
Cecil Matola, Klemens Kiiza,Joseph Melingo na Martin Kayamba na wengine walifanya ya AA aliyoyataja Mag3 katika post yake?
 
Mohamed Said, naja

Wanaukumbi naweka hapa maisha ya siasa kama nilivyo nakili katika
tovuti ya Baba wa Taifa.

Nakuulizeni wana ukumbi mnijibu kwa haki liliah kweli hii ndiyo historia
ya Nyerere ya kweli?

Hii ndiyo historia ya TANU?

Political career

On his return to Tanganyika, Nyerere took a position teaching History, English, and Kiswahili at St. Francis' College, near Dar es Salaam. It is at St. Francis' College that he founded TANU. His political activities attracted the attention of the colonial authorities, and he was forced to make a choice between his political activities and teaching.

He was reported as saying that he "was a schoolmaster by choice and a politician by accident." He resigned and continued with his work on his goal to bring a number of different nationalist factions into one grouping, which was achieved in 1954. Nyerere traveled throughout the country, speaking to common people and tribal chiefs, trying to garner support for the movement towards independence. He also spoke on behalf of TANU to the Trusteeship Council and Fourth Committee of the United Nations, in New York.

His oratory skills and integrity helped Nyerere achieve TANU's goal for an independent country without war or bloodshed. The cooperative British governor Sir Richard Turnbull was also a factor in the struggle for independence. Nyerere entered the Colonial Legislative council in 1958, and was elected chief minister in 1960. In 1961, Tanganyika was granted self-governance and Nyerere became its first Prime Minister on December 9, 1961. A year later, Nyerere was elected President of Tanganyika when it became a Republic. Nyerere was instrumental in the union between the islands of Zanzibar and the mainland Tanganyika to form Tanzania, after a 1964 coup in Zanzibar toppled Jamshid bin Abdullah, who was the Sultan of Zanzibar.

Kweli ndugu zangu TANU iliundwa Pugu?
Sina la kuongeza nakuachieni wanaukumbi.

Tembeleeni tovuti ya Nyerere muone mambo.
Inaitwa ''Nyerere Centre for Peace and Research''

Nakawaandikia nikawaeleza ukweli.
Kimya.
 
Wanajamvi,nawaomba msome vizuri maneno ya MS. Kumbe EAMWS ilivunjwa kwa amri ya serikali. Sasa serikali hiyo si ilikuwa na waziri wa mambo ya ndani Sadi Ali Maswanya na kwa upande wa kulia wa Nyerere alikuwepo Makamu wa Rais na Waziri mkuu Rashid Mfaume kawawa!
Hivyo basi suala zima ni la serikali ya Tanzania ikiongozwa na Nyerere na si amri ya Nyerere.

Kwa muktadha huo kauli za nyuma(ushahidi upo) za MS kuwa Nyerere kwa kushirikiana na kanisa waliua EAMWS si za kweli. Si za kweli kwasababu hakuna mahali MS ameonyesha ushiriki wa kanisa.
Unless aondoe neno serikali libaki Nyerere mkatoliki, MS hana justification za allegation against christians.
Nadhani angeangalia zaidi with his society who had an upper hand rather than fabricating unfounded allegation.

Nilishasema na nitasimamia hapo kuwa Mohamed Said ni mchochezi!

Anawarubuni watanzania wasiojua historia ya nchi yao ili waamini udini wake! Hii ni hatari sana!
 
Wanajamvi,nawaomba msome vizuri maneno ya MS. Kumbe EAMWS ilivunjwa kwa amri ya serikali. Sasa serikali hiyo si ilikuwa na waziri wa mambo ya ndani Sadi Ali Maswanya na kwa upande wa kulia wa Nyerere alikuwepo Makamu wa Rais na Waziri mkuu Rashid Mfaume kawawa!
Hivyo basi suala zima ni la serikali ya Tanzania ikiongozwa na Nyerere na si amri ya Nyerere.

Kwa muktadha huo kauli za nyuma(ushahidi upo) za MS kuwa Nyerere kwa kushirikiana na kanisa waliua EAMWS si za kweli. Si za kweli kwasababu hakuna mahali MS ameonyesha ushiriki wa kanisa.
Unless aondoe neno serikali libaki Nyerere mkatoliki, MS hana justification za allegation against christians.
Nadhani angeangalia zaidi within his own society rather than fabricating unfounded allegation.

Yote uliyosema ni kweli kabisa.
Lakini si kweli yote.

Said Maswanya si Kawawa walikuwa na sauti.

Lakini ukitaka jibu jepesi hayo uliosema yanatosheleza sana.
 
Nilishasema na nitasimamia hapo kuwa Mohamed Said ni mchochezi!

Anawarubuni watanzania wasiojua historia ya nchi yao ili waamini udini wake! Hii ni hatari sana!
Unajua Mohamed anapenda sana watu waamini tu bila fikra. Hivi kweli Nyerere anaweza kuamka asubuhi na kumfukuza sheikh Amir bila sababu ya msingi! Hivi ingekuwa wakati wa Nyerere na akaamua kumweka magereza Sheikh Ilunga kungekuwa na uonevu gani?

Kuna swali moja huwa hataki kulijibu. Huwa namuuliza MS, hivi akina Bomani, Paul Rupia, Vedastus Kyaruz huwa wanaangukia kundi gani katika kitabu chake? Wazee wake au marafiki wa wazee wake au hakuna kabisa.

Hivi ni kwanini Nyerere alimshinda Abdul Sykes katika uchaguzi wa chama ili hali majority ilikuwa ni wazee wake waliotaka kupigania uhuru wa Waislam!
 
Mzee miye wala sina shida kwani nimekuelewa vizuri; tatizo langu ni kuwa watu wanaweza kufikiria unaandika historia ya harakati za Tanganyika za majina ya watu waliosahauliwa. Ni vizuri watu wakusome kama unavyosema unachoandika wewe ni kwa ajili ya kuzipamba harakati za WAislamu na ili hili lifanikiwe ni lazima Wakristu wengine ambao nao walikuwa na mchango mkubwa wawekwe pembeni.

Kimsingi unachomtuhu Nyerere kukifanya kwa Waislamu (au waandishi wa historia ya Nyerere) ndicho wewe unakifanya dhidi ya wazee wa Kikristu walioshiriki harakati zile zile. Kwamba historia ya Waislamu ilifutwa au kuwekwa pembeni na ni muhimu kuirudisha lakini wakati huo huo wewe mwenyewwe unajitahidi kuweka pembeni majina ya wazee Wakristu ili kkupamba wazee wa Kiislamu.

Utakuwa na tofauti gani na wale walioandika historia ya Nyerere basi?

Kama hajaelewa hapa basi tena...sikio la kufa...
 
Unajua Mohamed anapenda sana watu waamini tu bila fikra. Hivi kweli Nyerere anaweza kuamka asubuhi na kumfukuza sheikh Amir bila sababu ya msingi! Hivi ingekuwa wakati wa Nyerere na akaamua kumweka magereza Sheikh Ilunga kungekuwa na uonevu gani?

Kuna swali moja huwa hataki kulijibu. Huwa namuuliza MS, hivi akina Bomani, Paul Rupia, Vedastus Kyaruz huwa wanaangukia kundi gani katika kitabu chake? Wazee wake au marafiki wa wazee wake au hakuna kabisa.

Hivi ni kwanini Nyerere alimshinda Abdul Sykes katika uchaguzi wa chama ili hali majority ilikuwa ni wazee wake waliotaka kupigania uhuru wa Waislam!

Hapo ndipo nabaki kustaajabu ya filauni tu,

Mohamed Said anahisi watanzania wote ni wajinga,

Mwalimu atambulishwe 1952 akiwa ni mgeni kabisa katika siasa za TAA na akiwa nimchanga kabisa wa siasa, kisha mwaka mmoja tu baadae yani 1953 amshinde Abdul Sykes kwa kishindo aliyekuwa rais wa chama hicho, mtu maarufu na mkongwe na zaidi mwasisi wa chama hicho? Mwenye ushawishi mkubwa kwa wazee wa kariakoo?

Haiingii akilini hata kidogo na hii Mohamed Said amewadhara na kuwatusi wale anaodai ni wazee wake!

Nahisi washamlaani kwa aina ya maandiko yake!
 
acha vitisho lete ushahidi

mwenzio yericko nyerere alisema ataweka ushahidi mpaka sasa kimya
Nina ushahidi umetunga! Nikiweka ushahidi huo utaamuomba mwenyezi mungu radhi? Kuna mahali hakuna research niweke hapa na ikithibitika uombe jamvi radhi?
 
kaka naona povu laendelea kukutoka

vipi ulishaleta ule ushahidi ulosema utauweka hapa jamvini?
Kwa muda kidogo nilikuwa sipo

cc @kichwakigumu Barubaru Ritz
Nilishasema na nitasimamia hapo kuwa Mohamed Said ni mchochezi!

Anawarubuni watanzania wasiojua historia ya nchi yao ili waamini udini wake! Hii ni hatari sana!
 
Last edited by a moderator:
Swali la pili,
Cecil Matola, Klemens Kiiza,Joseph Melingo na Martin Kayamba na wengine walifanya ya AA aliyoyataja Mag3 katika post yake?

Kwanza nataka nimzungumze Cecil Matola.

Katika wale waasisi wa AA hakuna aliyeacha kumbukumbu aloandika
kwa mkono wake isipokuwa Kleist Sykes.

Cecil Matola kaingia kwenye uongozi wa AA kama rais pamoja na Kleist
mwaka 1929.

Kumbukumbu za Kleist zinasema juhudi za kuasisi AA zilitokana na yeye
binafsi baada ya mazungumzo na Dk. Aggrey mwaka 1924.

Hii ilikuwa AA iliyoasisiwa Dar es Salaam.

Baada ya Cecil Matola rais akawa Mzee bin Sudi na mwaka 1933 Kleist na
Mzee bin Sudi wakaasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Sasa kuhusu Kiiza, Joseph Melingo sina taarifa ya mafanikio ya chama chao.

Ila Martin Kayamba alikuwa kibaraka wa Waingereza.

Erika Fiah alikuwa na haya ya kusema katika kifo cha Kayamba:

Katika rambirambi alizotoa za kijeuri na za dharau juu ya kifo cha Martin
Kayamba,[1]Fiah aliomboleza kwa kusema kwamba:

''Waafrika hawakunufaika kwa elimu ya Kayamba wala kwa wadhifa wake
kama karani wa Kaimu Katibu Mkuu.''[1]

Hapa chini mimi nazungumza katika kitabu changu:

''Vyama vilivyoonekana kama kwamba viliundwa kulinda maslahi ya wafanyakazi
vilikuweko tangu miaka ya 1930.

Serikali ya kikoloni, pamoja na kuanzisha sheria yaTrade Union Ordinance ya mwaka 1932,
ilikuwa bado inapinga umoja wowote wa wafanyakazi ulioundwa kudai haki zao.[1

Lakini jambo hili halikuwazuia wafanyakazi wasipiganie haki zao bila ya kujali kitisho cha
wakoloni.

Hakuna chama au jumuiya iliyoundwa iliyoamsha hamasa ya tabaka la wafanyakazi wa
Tanganyika kama harakati zile za makuli wa mji wa Dar es Salaam.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya Tanganyika Territory Civil Servants Association (TTACA)
iliyoundwa mwaka 1922 na Martin Kayamba na Chama cha Makuli, katika uongozi na mwelekeo.''

TTACA kilikuwa chama halisi cha ustawi wa jamii ambacho hakikuwa na taathira yoyote
dhidi ya ukoloni; TTACA ilikuwa ''kilabu ya makarani na waalimu, ikiwa na magazeti na timu
ya kandanda, ikisaidiwa na kuungwa mkono na serikali.1]

Chama hiki na vingine vya namna hii vilivyoundwa na kuongozwa na wasomi havikufanikiwa
chochote.''[1]

Nadhani mpaka hapa unayo picha ya hali ya siasa iivyokuwa.
Hata John Iliffe alipokuja kuhariri kitabu chake Modern Tanzanians wanasiasa ambao waliandikwa
maisha yao ni hawa wafuatao: Kleist Sykes, Ali Juma Ponda, Hassan Taufiq Suleiman na Martin
Kayamba.

Si Kiiza, Matola na wengineo walitiwa katika kitabu kile.

Na hata kilipokuja kuandikwa kitabu kingine kuhusu siasa za Kanda ya Ziwa Mutahaba alichagua
kuandika maisha ya Ali Migeyo ''The Portrait of a Nationalist.''
 
Unajua Mohamed anapenda sana watu waamini tu bila fikra. Hivi kweli Nyerere anaweza kuamka asubuhi na kumfukuza sheikh Amir bila sababu ya msingi! Hivi ingekuwa wakati wa Nyerere na akaamua kumweka magereza Sheikh Ilunga kungekuwa na uonevu gani?

Kuna swali moja huwa hataki kulijibu. Huwa namuuliza MS, hivi akina Bomani, Paul Rupia, Vedastus Kyaruz huwa wanaangukia kundi gani katika kitabu chake? Wazee wake au marafiki wa wazee wake au hakuna kabisa.

Hivi ni kwanini Nyerere alimshinda Abdul Sykes katika uchaguzi wa chama ili hali majority ilikuwa ni wazee wake waliotaka kupigania uhuru wa Waislam!

kwenye;

RED- huyo ustaadhi naweza sema alitakiwa ainishwe kama mtu hatari zaidi kwa sasa hapa TZ kwa kuhatarisha umoja wa kitaifa..

BLUE- Hakika najifunza mengi sana kwa mara nilipomsikia mzee MS radio imaan; pamoja na wachagizaji wake hakika waliniteka akili.
 
Hapo ndipo nabaki kustaajabu ya filauni tu,

Mohamed Said anahisi watanzania wote ni wajinga,

Mwalimu atambulishwe 1952 akiwa ni mgeni kabisa katika siasa za TAA na akiwa nimchanga kabisa wa siasa, kisha mwaka mmoja tu baadae yani 1953 amshinde Abdul Sykes kwa kishindo aliyekuwa rais wa chama hicho, mtu maarufu na mkongwe na zaidi mwasisi wa chama hicho? Mwenye ushawishi mkubwa kwa wazee wa kariakoo?

Haiingii akilini hata kidogo na hii Mohamed Said amewadhara na kuwatusi wale anaodai ni wazee wake!

Nahisi washamlaani kwa aina ya maandiko yake!

Wanaukumbi oneni mambo hayo.
TANU iliasisiwa Pugu.

Hii inatoka katika Tovuti ya Baba wa Taifa:

On his return to Tanganyika, Nyerere took a position teaching History, English, and Kiswahili at St. Francis' College, near Dar es Salaam. It is at St. Francis' College that he founded TANU. His political activities attracted the attention of the colonial authorities, and he was forced to make a choice between his political activities and teaching.

He was reported as saying that he "was a schoolmaster by choice and a politician by accident." He resigned and continued with his work on his goal to bring a number of different nationalist factions into one grouping, which was achieved in 1954. Nyerere traveled throughout the country, speaking to common people and tribal chiefs, trying to garner support for the movement towards independence. He also spoke on behalf of TANU to the Trusteeship Council and Fourth Committee of the United Nations, in New York.

His oratory skills and integrity helped Nyerere achieve TANU's goal for an independent country without war or bloodshed. The cooperative British governor Sir Richard Turnbull was also a factor in the struggle for independence. Nyerere entered the Colonial Legislative council in 1958, and was elected chief minister in 1960. In 1961, Tanganyika was granted self-governance and Nyerere became its first Prime Minister on December 9, 1961. A year later, Nyerere was elected President of Tanganyika when it became a Republic. Nyerere was instrumental in the union between the islands of Zanzibar and the mainland Tanganyika to form Tanzania, after a 1964 coup in Zanzibar toppled Jamshid bin Abdullah, who was the Sultan of Zanzibar.
 
kwenye;

RED- huyo ustaadhi naweza sema alitakiwa ainishwe kama mtu hatari zaidi kwa sasa hapa TZ kwa kuhatarisha umoja wa kitaifa..

BLUE- Hakika najifunza mengi sana kwa mara nilipomsikia mzee MS radio imaan; pamoja na wachagizaji wake hakika waliniteka akili.

Ukienda kwa mtindo huo wa hamaki na kejeli huu mjadala utaharibika.

Hivi nyie hamuwezi kufanya mjadala hadi mtie lugha za kihuni?

Tulizaneni kwanza kisha mrudi humu ukumbini na adabu tuendelee na mjadala.

Ndugu zanguni kipi hapa kinachokupandisheni hasira?

Haya maneno ya ''ustaadhi,'' ''mtu hatari,'' ''wachagizaji'' yanakujaje?
 
Wanaukumbi oneni mambo hayo.
TANU iliasisiwa Pugu.

Hii inatoka katika Tovuti ya Baba wa Taifa:

On his return to Tanganyika, Nyerere took a position teaching History, English, and Kiswahili at St. Francis’ College, near Dar es Salaam. It is at St. Francis’ College that he founded TANU. His political activities attracted the attention of the colonial authorities, and he was forced to make a choice between his political activities and teaching.

He was reported as saying that he "was a schoolmaster by choice and a politician by accident." He resigned and continued with his work on his goal to bring a number of different nationalist factions into one grouping, which was achieved in 1954. Nyerere traveled throughout the country, speaking to common people and tribal chiefs, trying to garner support for the movement towards independence. He also spoke on behalf of TANU to the Trusteeship Council and Fourth Committee of the United Nations, in New York.

His oratory skills and integrity helped Nyerere achieve TANU's goal for an independent country without war or bloodshed. The cooperative British governor Sir Richard Turnbull was also a factor in the struggle for independence. Nyerere entered the Colonial Legislative council in 1958, and was elected chief minister in 1960. In 1961, Tanganyika was granted self-governance and Nyerere became its first Prime Minister on December 9, 1961. A year later, Nyerere was elected President of Tanganyika when it became a Republic. Nyerere was instrumental in the union between the islands of Zanzibar and the mainland Tanganyika to form Tanzania, after a 1964 coup in Zanzibar toppled Jamshid bin Abdullah, who was the Sultan of Zanzibar.

Ndugu yangu, sio kila mzungu ni padre,

Hivi unamfahamu anaeiendesha hiyo tovuti?

Fanya utafiti ummfahamu kisha njoo tuendelee na mjadala huu
 
Back
Top Bottom