Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

unapenda sana kanisa lihusishwe na harakati za uhuru wa tanganyika.Umejaribu kutoa historia ya kanisa na kushirikiana na sheikh uliyemwita issa bin ameir.Dah nilikuwa na jamaa zangu tulicheka sana.Tunakisubiri kitabu chako nawe
Nashukuru ndugu yangu, nikweli kabisa umeeleza historia iliyokuwa haifahamiki,

Naomba nikuulize swali moja tu:

Umeamini ushiriki wa kanisa katika harakati za ukombozi Tanganyika kama nilivyoeleza hapo juu?
 
umeshindwa hoja unaanza kejeli na kashfa.Kinachofurahisha mpaka sasa hamjatoa historia mbadala iliyosahihi.Nyinyi mnapinga yaliyoelezwa na Mohamed Said.Haya basi leteni hiyo historia iliyo sahihi hamna.Mjadala mmeuanzisha wenyewe sasa unawatoa jasho.
Mimi hutaniona natoa tena kitu hapa. Mawe yote yameshafunuliwa na ukweli umejulikana. Wajerumani wa ZMO wanasemagaje!? Viel Spass noch...
 
Last edited by a moderator:
Labda tumuulize Bw. Said swali jingine la moja kwa moja: Je Dossa Aziz aliwahi kukutana na Nyerere au kushiriki na Nyerere mkutano wowote wa TAA kabla ya 1953? Wapi na Nyerere alishiriki kama nani?
 
udini ulianzishwa na waislam kumbe. Na waislam wenyewe enzi hizo wakiwa hawajui ni jinsi gani ya kumtoa mkoloni hadi walipoazima nguvu toka kwa wasomi wakristo wachache. Nakumbuka kitambo kile kabla hii mikanda ya x haijaingia kulikuwa na majarida ya x. Sasa jamaa akaniazima kisha akaniambia, 'usije ukachana kurasa...' Nikasema moyoni kumbe inawezekana kuchana? Kweli nilichana peji moja. Asingeniambia wala nisingechana. Ni enzi hizoo.

Sasa huyu Takadir alipoleta hoja ya udini, wenzake walikuwa hawana habari na hayo. Walikuwa na lengo moja tu-kuongoza mapambano dhidi ya mkoloni kwa ajili ya mtanganyika! Bwana Said unadhani chozi la Nyerere lilitoka bure? Kwa nini kumshutumu mtu kwa jambo ambalo hakuwa na wazo nalo? Naye akajua kumbe inawezekana? Lakini Nyerere hakutaka kutumia elimu na ukatoliki wake kuwaburuza waislam ambao wengi walikuwa hawajasoma. Dhambi waliyofanya waislam ni kujishuku! Hadi leo hili tatizo lipo. Utasikia mfumo kristo. Utasikia hatutaki sensa. Utasikia wizara ya elimu ina hujuma. Utasikia MOU, na mengine mengi. Inawezekanaje mfumo kristo wakati cream ya uongozi Tanzania ni Islam Islam? Kujishuku. Waislam mnapojenga mazingira ya kujishuku mjue mnawatahadharisha wasio waislam kuwa wenzetu sio wenzetu. Kwa kuwa udini ulianzishwa na uislam, uislam uwe wa kwanza kukemea udini. Na uislam uwe wa mwisho kutekeleza udini!
 
Tunasubiri ile ahadi ya kutuwekea hapa ukumbini yale majina ya viongozi wa uasi waliochiwa huru.Leo ni siku ya tatu kimya.Hayo meneno ya red yatafakari vizuri na ahadi yako
cc @Rirtz Barubaru kichwakigumu
Nahisi mzee sasa hajui hata cha kudanganya, kila uongo wake unagonga ukuta!

Ataendelea kuwaburuza wenye akili mgano tun nao wakielevuka wanakana na kumchukia kupita kiwango.
 
Last edited by a moderator:
kasome athari za watu waangaliao picha za x,halafu angalia nafasi yako ktk mjadala huu
udini ulianzishwa na waislam kumbe. Na waislam wenyewe enzi hizo wakiwa hawajui ni jinsi gani ya kumtoa mkoloni hadi walipoazima nguvu toka kwa wasomi wakristo wachache. Nakumbuka kitambo kile kabla hii mikanda ya x haijaingia kulikuwa na majarida ya x. Sasa jamaa akaniazima kisha akaniambia, 'usije ukachana kurasa...' Nikasema moyoni kumbe inawezekana kuchana? Kweli nilichana peji moja. Asingeniambia wala nisingechana. Ni enzi hizoo.

Sasa huyu Takadir alipoleta hoja ya udini, wenzake walikuwa hawana habari na hayo. Walikuwa na lengo moja tu-kuongoza mapambano dhidi ya mkoloni kwa ajili ya mtanganyika! Bwana Said unadhani chozi la Nyerere lilitoka bure? Kwa nini kumshutumu mtu kwa jambo ambalo hakuwa na wazo nalo? Naye akajua kumbe inawezekana? Lakini Nyerere hakutaka kutumia elimu na ukatoliki wake kuwaburuza waislam ambao wengi walikuwa hawajasoma. Dhambi waliyofanya waislam ni kujishuku! Hadi leo hili tatizo lipo. Utasikia mfumo kristo. Utasikia hatutaki sensa. Utasikia wizara ya elimu ina hujuma. Utasikia MOU, na mengine mengi. Inawezekanaje mfumo kristo wakati cream ya uongozi Tanzania ni Islam Islam? Kujishuku. Waislam mnapojenga mazingira ya kujishuku mjue mnawatahadharisha wasio waislam kuwa wenzetu sio wenzetu. Kwa kuwa udini ulianzishwa na uislam, uislam uwe wa kwanza kukemea udini. Na uislam uwe wa mwisho kutekeleza udini!
 
teh teh teh,kidogo kidogo mtakubali huyu Mohamed Said ni mwalimu wa historia ya tanganyika.Endeleeni tu kuuliza.Anafundisha historia na adabu pia.Tena bure
Labda tumuulize Bw. Said swali jingine la moja kwa moja: Je Dossa Aziz aliwahi kukutana na Nyerere au kushiriki na Nyerere mkutano wowote wa TAA kabla ya 1953? Wapi na Nyerere alishiriki kama nani?
 
Last edited by a moderator:
Muuliza maswali kuwa na msimamo katika kuuliza ili tujue muongo nani na zaidi ya yoote tufaidike kwani wengine kwanza ndo 2napata habari hizi na inaonekana nyeti. Ebu uliza swali mojamoja alitolee maelezo halafu tupime cc, nani mkweli nani mdini.
 
Sasa tunasubilia kitabu cha historia iliyo sahihi na sio hii ya uchonganishi na uchochez wa mohammed said. Kumbe watu wanajua historia halafu wanazielezea kwenye kahawa tu bwana ebu tiriiiiiiiriiiiiken tujue ukweli.
 
Yerico umekili historia imepotoshwa irekebishe sasa tupime na hii ya mohammed said usitake umaarufu kwa kubisha na kutaka ufafanuzi wa somalia wakati mzee anaeleza historia ya tanganyika. Hiyo ya somalia afghan n.k ni maada ya kesho leo tanganyika.
 
Yerico umekili historia imepotoshwa irekebishe sasa tupime na hii ya mohammed said usitake umaarufu kwa kubisha na kutaka ufafanuzi wa somalia wakati mzee anaeleza historia ya tanganyika. Hiyo ya somalia afghan n.k ni maada ya kesho leo tanganyika.

Nsame.
Nakushauri usome posts zote kwenye uzi huu, kuanzia ukurasa wa kwanza.
 
Na sasa tunaanza kugundua kwamba Dosa Aziz alifahamiana na Nyerere mwaka 1946. Kwa hiyo Nyerere alipokuja Dar-es-Salaam 1952 hakuwa mgeni sana kwa wana harakati. In fact tayari alikuwa mwenzao ila tu kwamba hakuwa mtu wa Dar-es- Salaam. Very interesting.
Tena kaweka wazi kabisa. Ndio maana nilisema lile bandiko lake la ukurasa fulani hapo nyuma sijui aliliweka kwa makusudi au bahati mbaya.

Limeonyesha hata Nyerere alivyokaa na akina Sykes kutafuta mstakabali wa Tanganyika siyo Waislam.
 
Kwa nini Julius Nyerere alihudhuria mkutano wa African Association Dodoma mwaka 1946? Kama nani? Akitokea wapi? Je, hakuna mjumbe/wajumbe kutoka Dar es Salaam aliyehudhuria/waliohudhuria mkutano huo? Kama wapo inakuwaje mwaka 1952 (miaka sita baadaye) unadai hakuna hata mmoja kati ya wazee wako wa Dar es Salaam aliyewahi kumsikia Julius Nyerere? Kwa nini unadai kuwa safari ya kisiasa ya Nyerere ilianzia 1953? na aliingizwa katika siasa na kina Sykes? Je uko tayari kukiri kuwa ujio wa Mwalimu ndiko kulileta mwamko, msisimko na mawazo mapya ndani ya TAA? Je uko tayari kukiri uwongo ambao umekuwa ukiueneza kwa chuki kwa watu ambao hawaijui historia sahihi? Do you know even the meaning of the word "truth"?

Mtu yeyote anayetafuta msaada wa matusi na name-calling katika intellectual discourse, ananipa wasi wasi na veracity ya anayoyasema!
 
Mtu yeyote anayetafuta msaada wa matusi na name-calling katika intellectual discourse, ananipa wasi wasi na veracity ya anayoyasema!
Unfortunately this is JF! Hapa nyani giledi anakomwa bila kumwangalia uso...here a spade is called a spade and that is whether one likes it or not. Intellectual discourse? Nafikiri umedandia mada, rudi uanzie mwanzo or get back into your shell.
 
Mzee Mwanakijiji, Mohamed Said, Nguruvi3, Jasusi,

..yaani hata kwenye winter la Edinburgh SCOTLAND Mwalimu alikuwa anadunda na kaptura, suruali ameijua alipokutana na wazee wa D'Salaam??
Companero,

..ile document uliyosema utatuletea vipi mkuu?

..au umeanza likizo mpya?

Tatizo kuwa wapo watu kabisa - na wana akili timamu - wanaamini kuwa Nyerere aliingia siasa alipokuja Dar na ni wazee wa Dar walimfundisha kuvaa suruali. Kama kuna watu wanaamini Nyerere alifunga safari toka Pugu kwenda sokoni Kariakoo akiombea kuokoa hela njiani hadi alipokutana na rafiki yake kwa bahati mbaya aliyempatia fedha za kununua vitu sokoni wapo wanaoweza kuamini lolote.

Kama watu hawajifunzi kuuliza maswali na badala yake wanaamini chochote wanachoambiwa kama vifaranga vya ndege tunduni nani ataweza kuwasaidia?
 
Hoja za kipuuzi huletwa na watu wapuuzi kama wewe. hivi kuna mjinga gani waleo utakaemdanganya na utumbo wako huu? nani asiyejua wapigania uhuru wa nchi hii ni waislam tangu ukoloni wa kijerumani, soma akina Abshiri, Hasan Omar Bin Makunganya na wengineo walionyongwa (mungu awarehemu) walivyopinga utawala wa wakoloni. narudia tena, hivi huoni hata aibu kuleta mada ya uongo kama hii? mchana kweupe na uongo weupe? Mirembe panakufaa sana wewe.
Nimesoma maandiko ya ndugu yangu Mohamed Said aliyoyaweka katika kitabu chake akiitacho Historia ya Uhuru upande wa Pili,
Katika maandishi yake ameonyesha wazi kulazimisha dunia iamini kuwa waislamu wamedhulumiwa katika historia ya Uhuru wa nchi hii,
Katika matakwa yake Mohamed Said anataka historia ya Uhuru ingetazama itikadi za kidini kwanza kabla ya kusimamia maudhui halisi ambayo ni Uhuru,

Nikubaliane nae kuwa historia ya nchi yetu inamapungufu na inahitaji masahihisho, lakini kwa hili la Mohamed si masahihisho bali ni upotoshaji mkubwa, Uchochezi na ni Uhaini kwa nchi. Kwa bahati mbaya bwana Mohamed Said histori anayoisimamia ameiakisi kuanzia miaka ya 1950+ tu,

Hajajishughulisha kuutazama utawala wa Kiingereza wala kuutazama upya utawala wa Kijerumani ambao ndio uliosimika misingi ya utawala na mifumo mingi ambayo leo tunaitumia! Mjerumani mfumo wake wa utawala kwa ASILI ni wa kikristu na kwa Tanganyika walisimama hivyo bila kutetereka! (Yaani mfumo kristu 100%)

Akaja Muingereza na yeye mfumo wa utawala wake wa ASILI ni wakikristu!

Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.

Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 – 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.

Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake.

Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake,

Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa.

Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.

Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao.



Elimu,

Woga



Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake.

Mnamo tarehe 7/71954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranda) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir)


Mpaka hapo ndugu yangu Mohamed Said angalau umepata picha kwa KIFUPI tu ya harakati za uhuru chini ya kanisa.

Nikipata wasaa nitakuletea picha za Mwalimu Nyerere na Edger Aristide Maranta

Kwanini Kasisi huyu wa kikatoliki Edger Aristide Maranta hatajwi popote katika historia ya nchi? Kwanini kanisa katoliki halilalamiki kutokuwepo kwenye kitabu cha kivuko?

Yote hayo nitakushushia taratibu kadiri mnakasha huu unavyoenda.

Sasa nini kilifuata baada ya uhuru?

Nitaeleza kwakifupi tu:

Mwalimu Nyerere baada ya kukadhiwa mamlaka kamili ya kushika dola na Malkia wa Uingereza alianza mageuzi ya kubadili mfumo huo hasa mwanzoni mwa 1964 baada ya kuunganisha nchi ya Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa kwa Tanzania!

Juhudi hizi zilikwenda taratibu na kwa ufanisi wa hali ya juu kwakupitia hatua kadhaa ambazo ni pamoja na, kutaifisha huduma za jamii zote zilizokuwa chini ya makanisa, kuanzisha sera ya elimu ya msingi kuwa ni ya LAAZIMA kwa watanzania wote nk, Kumbuka Mjerumani amekaa zaidi ya karne tatu akitumia mfumo kristu kutawala, Muingereza nae akalowea karne kadhaa akitawala kwa mfumo huohuo, Lakini ndani ya miongo miwili tu ya utawala wa Mwalimu Nyerere huku nchi ikitoka kwenye dimbwi la ukoloni aliweza kubadili sura na mfumo huo wa kikoloni na kuwa wawatanzania wote bila kujali dini, kabila rangi au kanda.


Kazi aliyofanya mzee Nyerere ni kubwa na alikumbana na vikwazo vingi sana kutoka kwa wakatoliki, rejea kitabu cha Van Bergen kuna barua nzito ya Mwalimu Nyerere kwenye Appendix 15 kwenda kwa makasisi wa kikatoliki akiwatolea karipio kuu kwakukwamisha juhudi zake, katika hii hakuchukua karne kadhaa kuumaliza mfumo uliodumu kwa mvua na mvua.

Japokuwa hakumaliza chembe za mfumo huu lakini kwangu naona ni zaidi ya 98% alimaliza, palipobaki ni mimi, wewe na wale ndio wenye dhamana ya kumalizia.

Uthabiti na tunu aliyoifanya Mzee Nyerere inathibitishwa kwa Hotuba yake ya tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Mzee Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilikuwa thabiti na yenye kuvuta nyoyo za waungwa, Baba wa Taifa Mzee Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wakiwemo Bin Amir ambae Mohamed Said anamlilia, wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Mzee Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisemakuwa "upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake":

Inakera kuona wewe Mohamed unarudisha nyuma juhudi za wanaukombozi wetu na kupandikiza chuki miongoni mwa dini hizi mbili!
Faida unayopata ni ndogo na niyakwako tu kuliko hatari inayolikumba taifa hivi leo!
Sipingi kusahihisha historia ya nchi hasa kama kuna mema yaliyoachwa lakini kupotosha na kuchochea kunatulazimisha tuhoji mamlamla za usalama wa nchi zimelala wapi? Hivi tukisema kila mtu aingie katika historia ya uhuru wa nchi hii mbona itakuwa vurugu sana?

Leo mapinduzi matukufu ya Zanzibar, Mohamed Said anataka kutuaminisha kuwa Wanamapinduzi hawa wa Zanzibar waliwadhulumu waislamu wa Zanzibar na kuweka mfumo kristu anaodai upo au mfumo huo upo kwa Tanganyika tu?!
Juzi nimemuuliza maswali katika mjadala flani hapa, lakini majibu yake yamenifanya nijiridhishe kuwa Mohamed Said ni muhaini na mchochezi mkubwa wa nchi hii, Ameudhihaki Uislamu nchini na duniani kote,


Nilimuuliza hivi:

Naomba unijibu maswali haya kwaufasaha mwanazuoni Mohamed Said:

1) Uliathirika vipi kwa baadhi ya wazee waliopigania uhuru wa nchi hii kutokuwemo kwao katika histori ya nchi hii kama unavyodai?

2) Taifa na waislamu waliathirika vipi kwa baadhi ya wazee unaodai wewe walipigania uhuru wa nchi hii na hawamo katika historia?

3) Ulijuaje kuwa wazee hao walipigania uhuru ilihali hawapo katika historia stahiki ya nchi hii?

4) Unaposema historia ya uhuru wa nchi hii haiwakumbuki ama haiwatambui, ulitaka wakumbukwe katika maandishi ya vitabu au katika nyaraka za serikali za historia ya uhuru wetu?

5) Unatambua kuwa historia ya nchi yoyote ile duniani huwa wapi?

6) Upeo wako umegota kwenye historia ya waislamu wa Tanganyika na Nyerere tu, au historia ya waslamu duniani kote? Kama ndivyo, je matatizo ya waislamu wa Nigeria, Somalia, Sudani, nk Nyerere ndiye kayapeleka?

7) Je ulichokiandika ni historia ya Uhuru wa Tanganyika au ni historia ya baadhi ya Waislamu wa Tanganyika na mapito yao kisiasa?

8) Kwanini unaulazimisha umma kwa maandishi yako uamini kuwa ulichoandika ndio historia sahihi ya Uhuru wa Tanganyika?

9) Je ni kweli Mohamed Said huwajui na huwatambui wale wazee 17 waliosimama kidete kudai uhuru wa nchi yetu? Je wote walikuwa wakrstu?

Naomba majibu ili tujenge hoja mpya yamjadala huu kwa mafaa ya taifa letu!




Lakini maswali mengine yamsingi yaliulizwa na wadau wengi kama Nguruvi3, Mwanakijiji na moja lililonivutia lilikuwa hili hapa chini:


By adolay:


Ninakuuliza somalia na nyerere kwasababu waislam wa somalia wanamatatizo makubwa ya kijamii, kisiasa, kieliemu, afya nk

Nani mchawi maana hapa kwetu kwa mujibu wa hadithi zako ni Nyerere. (Tunaongelea matatizo ya waislamu na wanaowahujumu)

Watanzania (Waislam, wakristu pia wa imani zingine na wasio amini) wanamatatizo aghalabu si makubwa kama ya wasomali.

1. Kwanini useme waislam wa Tanzania ni hujuma za nyerere na kwanini wasiwe waislam wa somalia? kunatofauti ya uislam wa somalia na ule wa tanzania?

2. Je katika historia yako ufahamu wako umegota Tanzania kwa hayati JK Nyerere peke yake? kama ndivyo nini ubora na ufahamu wako kujisifu mwanahistoria makini kama sio mbabaishaji?

Tafadhali rejea maswali kutushawishi kwamba wewe ni mkweli na kashifa zako dhidi ya Nyerere ni uwongo na majungu.

Tuanze na Somalia, nataka usome swali uelewe ujibu kama nilivyouliza sio kuniwekea hadithi za maandishi zisizoakisi maudhui ya swali.

1. Nani amewahujumu/aliwahujumu wasomali na uislamu wa somalia mpaka wamefikia hapa walipo je? ni nyerere

2. Ni mfumogani unatumika katika kuitawala somalia kiasi kwamba wamefika hapo walipo ilituutupie lawama

a) Mfumo kristo ndiyo maana wamefika hapo walipo

b) Mfumo islam, mahakama ya kadhi nk

c) hufahamu nakama hufahamu nini mtazamo wako.

Ninakuuliza maswali haya lengo nikutaka kuujuwa ukweli wa pengine Nyerere huyu pia yupo somalia, afghanistan, pakistani, lebanon, syria, libya nk nakwamba machafuko yote yanayoendelea huko ni hujuma za Nyerere na mfumo kristo kama unavyowapotosha watanzania na kuwachochea!

Naomba majibu ya maswali yangu hapo juu kuthibitisha kwamba wewe sio mchochezi na mchonganishi wa waislamu na wakristo kwa kubuni vitu visivokuwepo.

Mohamed Said, baada ya utangulizi huo narejerea maswali yangu ya jana kwa ufafanuzi. Angalizo jibu maswali kama yalivyoulizwa na sio siasa au funika kombe mwanaharamu apite kwa nukuu za maandishi zisizobeba maana wala majibu ya hayo maswali




MAJIBU YA MOHAMED SAID:

quote_icon.png
By Mohamed Said

Umeingiza mambo mengi sana.
Kuna Zanzibar, elimu ya Waislam, matokeo mabaya ya shule za Kiislam, kuchinja.

Itakuwa tabu kufanya mjadala uliokuwa hauna mwelekeo ulionyooka.

Lakini kwa mukhtasari ukitaka historia ya Zanzibar na maendeleo yake itabidi tuanza kwa kuvamiwa
kwa Zanzibar na jeshi mamluki la Wamakonde kutoka Kipumbwi wakifadhiliwa na utawala wa Nyerere.

Kuanzia hapa tutaingia katika tatizo la Muungano na kwa nini leo Wazanzibari wanadai nchi yao.

Kuhusu elimu ya Waislam itatubidi tuje katika njama za Nyerere kuhujumu chuo kikuu cha Kiislam
kilichokuwa kijengwe Dar es Salaam mwaka 1968 na jinsi alivyotumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS
na kuunda taasisi kibaraka BAKWATA.

Vipi shule za Waislam hazifanyi vyema inabidi tuje katika hujma ya NECTA kwa wanafunzi wa Kiislam na
tuupitie waraka wa marehemu Prof. Malima kuhusu yale aliyoyakuta Wizara ya Elimu mwaka 1987.

Wizara ya Elimu na NECTA vimegeuzwa vigango vya kanisa.

Kubwa zaidi ni kuwa Waislam kwa muda mrefu hatukuruhusiwa kujioganaizi nje ya BAKWATA kibaraka
wa serikali.

Makanisa mnaendelea kwa kupendelewa na serikali iliyojaza watendaji Wakristo sisi tungepewa hayo
mabilioni ya MoU kati ya Makanisa na Serikali tusingekuwa kama hivi.

Yapo mengi sasa chagua tuanze na lipi katika hayo hapu juu niliyokugusia.

Wajerumani waliwaweka Wayahudi katika ghetto kisha wakawa wanawalaumu kwa uchafu.
Kwenye ghetto hakuna maji wala misala sasa watu wafanyeje?

Mnatusimanga kwa hospitali mnazoendesha kwa hela ya kodi ya serikali kodi inayolipwa na raia
wote.

Tunabanwa na mfumokristo kisha mnatulaumu hatuna maendeleo







Mohamed said

katika pita pita zangu nimekutana na post yako hii ya tare 4 January 2013 #914

Umeongelea kunyanyaswa kwa waislamu katika elimu ni njama ya JK Nyerere - Elimu ya somalia ipo taabani sana na Nyerere hayupo huko

Nakwamba Nyerere alitumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS - lakini ghilba wala uongo wa nyerere haupo Somali na inateketea vibaya

Necta imegeuka vigango vya kanisa - Somalia haina vigango vya makanisa katika taasisi zake hususani elimu lakini ipo taabani

Serikali imejaza wakristo kwa upendeleo na kuwaacha waislam - Somalia serikali takribani yote ni waislam hakuna maendeleo

Wakristo
wanawasimanga kwa hospitali zilizo jengwa kwa kodi ya watanzania- wasomali pia wanatoa na kukusanya kodi hakuna afya bora, elem wala siasa safi!

Waislamu wanabanwa na
mfumo kristo
- Somalia kuna mfumogani unaowabana wasiendelee



 
Hoja za kipuuzi huletwa na watu wapuuzi kama wewe. hivi kuna mjinga gani waleo utakaemdanganya na utumbo wako huu? nani asiyejua wapigania uhuru wa nchi hii ni waislam tangu ukoloni wa kijerumani, soma akina Abshiri, Hasan Omar Bin Makunganya na wengineo walionyongwa (mungu awarehemu) walivyopinga utawala wa wakoloni. narudia tena, hivi huoni hata aibu kuleta mada ya uongo kama hii? mchana kweupe na uongo weupe? Mirembe panakufaa sana wewe.

Pole sana kwakughadhibika ndugu,

Tulia soma andiko hilo na zama katika tafakuri ya nera kisha njoo uchangie hapa,

Tatizo lenu lilelile mkilishwa hamhoji "chakula hiki kitamu kimetoka wapi?" Nyie mwabugia tu.

Tangu sasa nimewapeni mwangaza halisi wakubadili medula oblongata zenu
 
Sasa tunasubilia kitabu cha historia iliyo sahihi na sio hii ya uchonganishi na uchochez wa mohammed said. Kumbe watu wanajua historia halafu wanazielezea kwenye kahawa tu bwana ebu tiriiiiiiiriiiiiken tujue ukweli.

Nsame hawawezi kuandika chochote watu hawa.
Hiyo historia hawana.

Huko nyuma nilisema unaweza kuwaambia Wachina waandike
historia yao ya ''holocaust?''

Jibu ni kuwa hapana.
Kwa nini?

Kwa sababu hiyo si historia yao.

Ndiyo maana unaona wanalazimisha kila kitu kianze na Nyerere.

Sasa ukiwaeleza ukweli ulivyokuwa cha kwanza ni kuhamaki cha
pili kejeli na matusi.
 
Back
Top Bottom