Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hawawezi kwa kuwa hawana hiyo historia.

Kuwapa changamoto hiyo ni sawasawa
kuwaambia Wachina waandike historia
ya ''holocaust.''

Sasa Wachina wataanzia wapi wakati
historia hiyo ni ya Wayahudi?

Ile historia ya uhuru wa Tanganyika
Allah alijaalia iwe ya Waislam.

Sasa si unaona matatizo haya?

Tovuti ya Baba wa Taifa inasema Nyerere
kaasisi TANU Pugu.

Mwanae anasema hiyo tovuti ni ya mitaani
haina uhusiano wowote na Baba wa Taifa.

Ana maana tovuti ya Baba wa Taifa inapotosha.

Inapotosha kweli lakini mbona mmekuwa kimya siku
zote?

Sasa swali la kujiuliza ni hili yaani Nyerere kakosa
hadhi kiasi mtu yoyote anaweza akachezea
jina lake?

Tovuti hiyo ilipokuwa inapotosha taarifa za
Baba wa Taifa wahusika walikuwa wapi?

Hakika ni kitendawili kisichokuwa na mteguaji
Umeshapewa majibu mazuri tu juu ya tovuti hiyo. Sasa sijui unataka wafanyeje, watoe fatwa kwa aliyeianzisha kama ile aloopewa Salman Rushdie? MfumoKristo hauna adhabu za aina hiyo!
 
Inawezekana kweli hukuwa na hasira nisamehe ndugu yangu.

Mimi nitafute uhalai wa nini kwa kutaka nini na kwa nani.
Nitafuta kuungwa mkono na nani na kwa lipi?

Hii historia ndiyo ilivyo hivyo hivyo huwezi kuibadili.

Sheikh Hassan bin Amir alikuwapo, Sheikh Suleiman Takadir,
Sheikh Mohamed Ramia, Sheikh Ysuf Badi na masheikh wengi tu
walikuwa TANU mstari wa mbele.

Baraza la Wazee wa TANU lilikuwapo na walikuwa Waislam watupu.
Haya yote ni ukweli wa historia haukwepeki.

Hataki kukubali kuwa watu hao, wenye kuamini dini ya kiislam, walishiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Ameshaweka akilini kuwa alichosomeshwa shule kinatosha. Haishughulishi akili yake kutaka kujua mengine. Haweki nafasi akilini mwake ku-expand kile anachokijua. Kuendelea kujibizana naye unatukosesha sisi uhondo wa kuijua historia yetu mzee wangu. Mpuuze
 
Nasaha zako Mzee wangu unazichanganya na maneno makali mno; unapomwambia mtu huna adabu, asiyefunzwa na mamaye, na lugha kama hizo, nashindwa kuelewa kama ni nasaha kweli kutoka kwa mtu kama wewe!

Hivyo ndivyo watu wazima wanavyowakanya watoto wasio
na adabu.

Hivi ndivyo watu wa pwani tunavyolea wana.

Huanza kwa nasaa kuwa usifanye hivyo na hivyo haifai.

Hasikii.
Anaendelea na kibri chake.

Anaendelea na utovu wake wa adabu.

Sasa ndiyo anatajiwa mama yake kumzindua.
Unaona baada ya kutaja mama sasa naulizwa.

Baada ya hapa kama matusi yakiendelea nitajua
huyu ni nunda.

Hawezekani.
 
kuna hili mzee ms kuwa nyerere alikuja mshamba anavaa kaptula na wazee wako ndo walio mfundisha kuvaa suluali.
Je? Ni kweli? Huwa najiuliza mwalim kasomea uingereza kwa wavaa suti iweje aje afundishwe kuvaa na watu wa kariakoo?

Hapo ndipo uyashangae maajabu ya Mohamed Said,

Mwalimu kasoma Chuo chenye hadhi kubwa barani Afrika Makelele nchini Uganda, kisha kaenda Scotland Uk ambako ni sehemu muhimu kwa ustaarabu wa mwanadamu, eti leo aje afundishwe kuvaa suruali na shati au kuvaa suti na vijana wa kariakoo???? Hii ni dharau sana!

Mbona hakuiga kuvaa misuli ama kubadili dini yake?

Mohamed Said anahisi watz sote ni majuha!
 
Inawezekana kweli hukuwa na hasira nisamehe ndugu yangu.

Mimi nitafute uhalali wa nini kwa kutaka nini na kwa nani.
Nitafuta kuungwa mkono na nani na kwa lipi?

Hii historia ndiyo ilivyo hivyo hivyo huwezi kuibadili.

Sheikh Hassan bin Amir alikuwapo, Sheikh Suleiman Takadir,
Sheikh Mohamed Ramia, Sheikh Mohamed Yusuf Badi na masheikh wengi tu
walikuwa TANU mstari wa mbele.

Ali Migeyo, Dharura bint Abdulrahman, Mama bint Maalim, Halima Selengia,
Amina Kinabo,Zena Maua, Abdallah Rutababzibwa, Sued Kagasheki, Hawa
Bint Maftah, Tatu bint Mzee, Shariffa
Bint Mzee Msham Awadh, Rajab Sisso...

Hawa hamuwajui lakini walikuwapo na walikuwa mstari wa mbele kupambana
na ukoloni.

Baraza la Wazee wa TANU lilikuwapo na walikuwa Waislam watupu.
Haya yote ni ukweli wa historia haukwepeki.
Ikafika mahala Mwalimu akawambia Masheikh hawa: Serikali ninayoiongoza mimi haina DINI. Nikuulize kaswali kadogo tu Mzee Mohamed, ni historia ya nchi gani imeandikwa ikawakumbuka watu wote? Tena kwa DINI na makabila yao?
 
Hataki kukubali kuwa watu hao, wenye kuamini dini ya kiislam, walishiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Ameshaweka akilini kuwa alichosomeshwa shule kinatosha. Haishughulishi akili yake kutaka kujua mengine. Haweki nafasi akilini mwake ku-expand kile anachokijua. Kuendelea kujibizana naye unatukosesha sisi uhondo wa kuijua historia yetu mzee wangu. Mpuuze

Ahsante ndugu yangu.

Darsa inaendelea Insha Allah.

Sheikh Hassan bin Amir alipokuwa anadarsisha
alikuwa anaulizwa maswali ya mtego na wanafunzi wake.

Sheikh alikuwa yeye lile analijibu kwa njia ndefu.

Atalijibu kwa kusomesha kwanza misimamo ya wanazuoni
mbalimabli katika ule mushkel.

Anatoa faida na hasara kama anavyoona kwa kila msimamo.

Kisha kujumuisha ataeleza kawaida ya jambo lile kwa Waislam
wa Afrika Mashariki.

Anapomaliza yule mwanafunzi mpenda ubishi anakuwa kasoma
sana na matokeo yake huwa anatulia hataki tena maswali ya
mitego ili aende kukoga wenzake katika minakasha.
 
Hapo ndipo uyashangae maajabu ya Mohamed Said,

Mwalimu kasoma Chuo chenye hadhi kubwa barani Afrika Makelele nchini Uganda, kisha kaenda Scotland Uk ambako ni sehemu muhimu kwa ustaarabu wa mwanadamu, eti leo aje afundishwe kuvaa suruali na shati au kuvaa suti na vijana wa kariakoo???? Hii ni dharau sana!

Mbona hakuiga kuvaa misuli ama kubadili dini yake?

Mohamed Said anahisi watz sote ni majuha!

nime highlight sehemu za bold kukujuza kuwa unamvunjia adabu mzee Mohamed Said. Huko nyuma ya mnakasha alishakwambia kuwa yeye ni mkubwa kwako, lakini still unavunja heshima yake. Sasa kwa namna hii munakasha hauwezi kuendelea uzuri

Pili, kusema "Scotland UK ambako ni sehemu muhimu kwa ustaarabu wa mwanadamu" nadhani hujui unachokisema. Sidhani kama unajua Scotland wanaume wanavaa sketi mpaka hii leo. Kama huu ni ustaarabu wa mwanadamu, basi nakuonea huruma wewe na vizazi vyako

Asante
 
Duh

Kijana unatisha.

Huishughulishi akili yako kujua zaidi. Ushaiwekea kikomo. Umekunywa nusu karne na mawazo yako ndo haya, nakuonea huruma wewe na vizazi vyako
Kwa kweli wewe ni kichwakigumu! unadandia hoja kwa mbele. Hautaelewa. Wala usichukue neno mojamoja kwenye sentensi. Utajichanganya.
 
Last edited by a moderator:
Hawawezi kwa kuwa hawana hiyo historia.

Kuwapa changamoto hiyo ni sawasawa
kuwaambia Wachina waandike historia
ya ''holocaust.''

Sasa Wachina wataanzia wapi wakati
historia hiyo ni ya Wayahudi?

Ile historia ya uhuru wa Tanganyika
Allah alijaalia iwe ya Waislam.

Sasa si unaona matatizo haya?

Tovuti ya Baba wa Taifa inasema Nyerere
kaasisi TANU Pugu.

Mwanae anasema hiyo tovuti ni ya mitaani
haina uhusiano wowote na Baba wa Taifa.

Ana maana tovuti ya Baba wa Taifa inapotosha.

Inapotosha kweli lakini mbona mmekuwa kimya siku
zote?

Sasa swali la kujiuliza ni hili yaani Nyerere kakosa
hadhi kiasi mtu yoyote anaweza akachezea

jina lake?

Tovuti hiyo ilipokuwa inapotosha taarifa za
Baba wa Taifa wahusika walikuwa wapi?

Hakika ni kitendawili kisichokuwa na mteguaji
Tulisema wengine...senility senility senility...
Kama kichwa kingekuwa kimekaa sawa wala usingeandika hivyo vitu hapo juu...
 
Hapo ndipo uyashangae maajabu ya Mohamed Said,

Mwalimu kasoma Chuo chenye hadhi kubwa barani Afrika Makelele nchini Uganda, kisha kaenda Scotland Uk ambako ni sehemu muhimu kwa ustaarabu wa mwanadamu, eti leo aje afundishwe kuvaa suruali na shati au kuvaa suti na vijana wa kariakoo???? Hii ni dharau sana!

Mbona hakuiga kuvaa misuli ama kubadili dini yake?

Mohamed Said anahisi watz sote ni majuha!

Yericko mdogo wangu.

Mimi siwezi kukosa adabu nifike mahali pa kusema maneno
kama hayo.

Nyerere ni umri wa baba yangu kwa hiyo ananizaa.

Sisi Waswahili mama zetu wametufunza adabu lau
kama kuna watu nunda hawasikii.

Mimi siwezi kuingia katika majibishano yasiyo na maana kama hayo.

Hili swali limelitolea kauli hapo nyuma.

Inalelekea Yericko wewe ni kuandika, kuandika, kuandika tu husomi
hutafakari.

Nakuomba hebu kwa dakika moja nifikirie kwa dhana njema.

Soma hapa chini:

''Hayo maneno yanasemwa sana lakini watu wanapoghadhibika.

Ni kukosa adabu na ustaarabu kutoa maneno kama hayo ya
kudhalilisha watu.

Kila mahali watu kama hao wasema ovyo huwezi kuwakosa.

Uniform aliyokuwa akivaa Abdu Sykes kama Market Master
pale Sokoni Kariakoo ilikuwa kaptula stockings na shati jeupe.

Waafrika wengi walikuwa wakivaa hivyo haikuwa kioja kwa
Nyerere.

Lakini kama ulivyosema akutukanae hakuchagulii tusi.''
 
nime highlight sehemu za bold kukujuza kuwa unamvunjia adabu mzee Mohamed Said. Huko nyuma ya mnakasha alishakwambia kuwa yeye ni mkubwa kwako, lakini still unavunja heshima yake. Sasa kwa namna hii munakasha hauwezi kuendelea uzuri

Pili, kusema "Scotland UK ambako ni sehemu muhimu kwa ustaarabu wa mwanadamu" nadhani hujui unachokisema. Sidhani kama unajua Scotland wanaume wanavaa sketi mpaka hii leo. Kama huu ni ustaarabu wa mwanadamu, basi nakuonea huruma wewe na vizazi vyako

Asante

Kha ...huyu naye!? Ulitaka wavae KANZU ndiyo uwaone wastaarabu? Mambo ya utamaduni mkuu wala usiumize kichwa vinginevyo utaonekana una upeo mfupi...turudi kwenye mjadala...
 
Kwa kweli wewe ni kichwakigumu! unadandia hoja kwa mbele. Hautaelewa. Wala usichukue neno mojamoja kwenye sentensi. Utajichanganya.

Context: Wewe kuja na hoja zisizokua na mashiko yoyote kwa madai eti "unam-challenge" mzee Mohamed Said
Quote: "Historia nilioisoma shuleni inatosha kabisa"

Meaning huweki nafasi akilini kukubali other info.
Nimekudadafulia jinsi unavofikiri

How is that kudandia kwa mbele?
 
Last edited by a moderator:
Tulisema wengine...senility senility senility...
Kama kichwa kingekuwa kimekaa sawa wala usingeandika hivyo vitu hapo juu...

Sweke ''senility'' kweli ipo lakini siyo kwa umri wangu.
Huna haja ya kunitukana kaka.

Ungesema ulitakalo tu.
 
Hawawezi kwa kuwa hawana hiyo historia.

Kuwapa changamoto hiyo ni sawasawa
kuwaambia Wachina waandike historia
ya ''holocaust.''

Sasa Wachina wataanzia wapi wakati
historia hiyo ni ya Wayahudi?

Ile historia ya uhuru wa Tanganyika
Allah alijaalia iwe ya Waislam.

Sasa si unaona matatizo haya?

Tovuti ya Baba wa Taifa inasema Nyerere
kaasisi TANU Pugu.

Mwanae anasema hiyo tovuti ni ya mitaani
haina uhusiano wowote na Baba wa Taifa.

Ana maana tovuti ya Baba wa Taifa inapotosha.

Inapotosha kweli lakini mbona mmekuwa kimya siku
zote?

Sasa swali la kujiuliza ni hili yaani Nyerere kakosa
hadhi kiasi mtu yoyote anaweza akachezea
jina lake?

Tovuti hiyo ilipokuwa inapotosha taarifa za
Baba wa Taifa wahusika walikuwa wapi?

Hakika ni kitendawili kisichokuwa na mteguaji

Mzee Mohamed Said, jitahidi kuweka adabu kama sisi tunavyojitahidi kudhiibiti ghadhabu zetu katika mjadala huu, umekuwa mwepesi wakuhitaji kuheshimiwa lakini ni mzito wakutoa heshima hiyo kwa wengine!

Mimi naamini kinachokusukuma useme hatuwezi kuandika historia ya Uhuru wa taifa letu takatifu ni kwakuwa sisi HATUWEZI kutunga/kubuni historia ya nchi yetu.

Mimi naamini wote tunaojadiliana hapa na wele wanaotufatilia wote tunao uwezo mkubwa wakukusanya historia halisi ya uhuru na kuiweka katika maandishi ya kitabu.

Ikiwa ni kutunga tu basi naamini wengi hatuwezi kama usemavyo, lakini kama ni kuandika yale yaliyotukia basi yeyote aweza kuandika ilimradi tu afuatilie vyanzo vyote muhimu ikiwemo na mnakasha huu!
 
Hapo ndipo uyashangae maajabu ya Mohamed Said,

Mwalimu kasoma Chuo chenye hadhi kubwa barani Afrika Makelele nchini Uganda, kisha kaenda Scotland Uk ambako ni sehemu muhimu kwa ustaarabu wa mwanadamu, eti leo aje afundishwe kuvaa suruali na shati au kuvaa suti na vijana wa kariakoo???? Hii ni dharau sana!

Mbona hakuiga kuvaa misuli ama kubadili dini yake?

Mohamed Said anahisi watz sote ni majuha!

Yericko.

Mimi nimeishi na nimesoma Uingereza.
Uingereza naijua vizuri sana kwa sababu siyo nimekwenda mara moja.

Naijua kuanzia Wales, England hadi Scotland.

Waskotishi ni washamba kwa namna yao.

Nimetembea Ulaya nchi nyingi na nimewaona Wazungu wastaarabu
kwa vigezo vyote.

Kule kaskazini wanapoishi Waskochi...huwezi kufananisha na kwengine
hapo Uingereza na Ulaya ''continental.''

Hawezi mtu kujifunza ustaarabu unaosema huko.
 
Mohamed Said, hivi kweli mtu utakuwa sawa kichwani kama unaandika hivi...

Angalau leo umefunguka...

Mie nimefunguka leo!

Si nimeeleza kuwa nina series za Africa Events katika 1980s
magazeti yalikusanywa yakachomwa moto!

Unasema leo nimefunguka!

Nisome kwa utulivu.
Jifunze kunisoma katikakati ya mistari.

Unajua kusoma maandiko magumu?
Unaweza kujifunza.

Mchukue Chaucer kwa kuanzia au Shakespeare.
Faida kubwa utapata.

Ukitaka kuwa mpigaji guitar mzuri jifunze ''cromatics.''
Usijifunze kupiga nyimbo.

Ukitaka kuwa mchezaji mzuri wa mpira jifunze kupiga danadana.
Mpira usiguse chini.
 
Mzee Mohamed Said, jitahidi kuweka adabu kama sisi tunavyojitahidi kudhiibiti ghadhabu zetu katika mjadala huu, umekuwa mwepesi wakuhitaji kuheshimiwa lakini ni mzito wakutoa heshima hiyo kwa wengine!

Mimi naamini kinachokusukuma useme hatuwezi kuandika historia ya Uhuru wa taifa letu takatifu ni kwakuwa sisi HATUWEZI kutunga/kubuni historia ya nchi yetu.

Mimi naamini wote tunaojadiliana hapa na wele wanaotufatilia wote tunao uwezo mkubwa wakukusanya historia halisi ya uhuru na kuiweka katika maandishi ya kitabu.

Ikiwa ni kutunga tu basi naamini wengi hatuwezi kama usemavyo, lakini kama ni kuandika yale yaliyotukia basi yeyote aweza kuandika ilimradi tu afuatilie vyanzo vyote muhimu ikiwemo na mnakasha huu!

Usinihukumu wewe kwa kauli hiyo ya kusema ''hamuwezi.''

Waachie wanaukumbi wahukumu kama hilo ni tusi.
Narudia kusema tena hamuwezi.

Laiti mngekuwa na historia ya kuandika mfano wa hii ya wazee
wangu kitabu kingekuwa tayari kipo mitaani.

Lakini nakuapia hamuwezi kwa kuwa hamna cha kuandika.
Huwezi kuandika kile kisichokuwapo.
 
Hapo ndipo uyashangae maajabu ya Mohamed Said,

Mwalimu kasoma Chuo chenye hadhi kubwa barani Afrika Makelele nchini Uganda, kisha kaenda Scotland Uk ambako ni sehemu muhimu kwa ustaarabu wa mwanadamu, eti leo aje afundishwe kuvaa suruali na shati au kuvaa suti na vijana wa kariakoo???? Hii ni dharau sana!

Mbona hakuiga kuvaa misuli ama kubadili dini yake?

Mohamed Said anahisi watz sote ni majuha!

Yericko Nyerere,

Tupo kwenye huu munakasha toka post ya #1 usitafute pakutokea usitake kumuwekea maneno mdomoni Mohamed Said.

Hakuna sehemu yeyote ambao Mohamed Said kamkosea heshima Mwalimu Nyerere kuyasema hayo maneno ya kuvaa kaptula.

Mohamed Said ni muungwana sana anafanya mijadala bila kejeli wala dharau hata kama akubaliani na mtu.

Mkuu nakumbushia tupe jibu basi la waasi waliosamehewa na Mwalimu Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom