Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ni kweli hii ni historia ya wazee wangu.
Hili nalikubali siku zote halina shaka.
Hili nalikubali siku zote halina shaka.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika Darsa lako ni zuri sana kwani umetujuza mengi sana ambayo wengi tulikuwa hatuyajui na umetujuza. Allah akuzidishie zaidi na zaidi insh'AllahHapana labda wewe unaona hivyo. Nimeweka nikiwa hadhir kabisa. Huo ndiyo ukweli. Kama nisemavyo. Simo humu kufanya ubishi. Nipo hapa kueleza ile historia iliyokuwa haifahamiki.
Amin ndugu yangu.Hakika Darsa lako ni zuri sana kwani umetujuza mengi sana ambayo wengi tulikuwa hatuyajui na umetujuza. Allah akuzidishie zaidi na zaidi insh'Allah
Kimsingi huyu bwana said hajui anachokiongea!!!!!
Mohamed Said anadai Raisi wa TAA mwaka 1952 alikuwa ni mtu mwenye akili nyingi, kipaji cha juu cha uongozi, mwenye haiba na mpenzi wa watu, Abdulwahid Sykes...sasa hapa swali linajitokeza, kwa nini uchaguzi ufanyike mwaka 1953 halafu mshamba moja wa bara asiyejua hata kuvaa suruali achaguliwe kuiongoza TAA? Mathalani hilo tuliache, kwa nini walioendesha harakati za kuanzisha TANU mwaka uliofuatia 1954 wampe uongozi huyo mtu?
Ikumbukwe kuwa baada ya Dr. Kyaruzi kupewa uhamisho, Abdulwahid Sykes hakuchaguliwa kuwa Raisi wa TAA, alikaimu tu...je yawezekana hakuwa na uwezo, sifa wala ushawishi kama Mohamed Said anavyojaribu kuchombeza? Itakuwaje vyombo vyote anavyodaiwa kuviasisi, anashindwa kuviongoza?
Hii picha mohamed said hawezi kuitafutia ujiko kama alivyozea maana inamsuta yeye mwenyewe...si ajabu alikuwa nayo lakini hakuitoa kwa sababu haionyeshi kutengwa kwa waislam na Nyerere mara baada ya uhuru...Hiyo hapo juu ni picha ya Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Jamhuri ya Tanzania lililoundwa na Mkristo mwenye chuki na Waislaam, Raisi Mwalimu Julius Nyerere. Kwenye hii picha idadi ya mawaziri Waislaam ni kumi wakati Wakristo ni tisa! Mwalimu mwenyewe kazungukwa na Waislaam tupu kulia na kushoto...linalosikitisha ni kwamba huyu mchochezi hakuwahi kuwahoji wahusika hadi wengine wao wanatangulia mbele ya haki.
Nawaomba wote jamvini wakati mnasoma hayo maandiko ninayoyaita ya kufikirika, kuna mtu anatajwa sana na Mohamed Saidi...huyo ni mzee marehemu Hamza Mwapachu aliyefariki Septemba 17 mwaka 1962, hebu pia pitieni na kumbukumbu hii iliyoandikwa na Andrew Bomani mwaka jana;
Yericho Nyerere. Naona unatumia kila hali kutaka kuonyesha unaedai kuwa ni baba yako alikuwa sahihi lakin alikuwa na mapungufu mengi sana na mara nyingi alipenda sana kujiweka mbele katika kila kitu. Nimebainisha kuwa unayedai Baba yako Nyerere, kwa sababu nilipokuwa RDD Mwanza mara kwa mara nilikuwa nampokea Nyerere alipokuwa akitoka Dar kwenda Butiama na hata familia yake yote. Kwani walikuwa wanatumia ndege mara nyingi za jeshi la anga na kutua Mwanza kisha wanatumia usafiri wa gari kwenda butiama. Nimebainisha kuwa Historia yoyote ni kama pembe la ng'ombe huwezi kuificha na ndio hiyo siri sasa zimefichuka. Na kwa jinsi ninavyojua mimi kama historia hiyo ya Mohamed said angeitoa miaka ya 70's au mwanzoni mwa 80's basi wakti wa utawala wa Nyerere saa hizi nafikiri Mohamed Said Said saa hizi tungekuwa tunamzungumzia mengine. Kwani enzi za Nyerere hakukubali kabisa kufanya kazi na watu wenye akili na wenye kujiamini katika maamuzi yao. alipendelea sana kufanya kazi na waoga. na hilo ni tatizo kubwa linalowasibu wengi huko na kuwa wenye kulalama kila wakti wote. Kifupi alipenda kutukuzwa mithili ya Mungu mtu.
Hapana labda wewe unaona hivyo.
Nimeweka nikiwa hadhir kabisa.
Huo ndiyo ukweli. Kama nisemavyo.
Simo humu kufanya ubishi.
Nipo hapa kueleza ile historia iliyokuwa
haifahamiki.
Nashukuru ndugu yangu, nikweli kabisa umeeleza historia iliyokuwa haifahamiki,
Naomba nikuulize swali moja tu:
Umeamini ushiriki wa kanisa katika harakati za ukombozi Tanganyika kama nilivyoeleza hapo juu?
Naona sasa umeishiwa hoja ndo maana unaleta kejeli. Lakin siku zote ukweli unabaki kuwa kweli na uwongo mara zote unajitenga. Nakupa pole.Kwanza weka adabu mbele ujadilianapo na mimi au mtu yeyote mwenye mang'amuzi ya nera, kisha punguza murkali na ukwale wa fikra! Tuendelee....!
Ndugu punguza hasira,peleka watoto shule na uone kama hawatafaulu kisa ni waislamu! mimi najifikirisha katika mambo matatu kuhusu ustawi wa kielimu kwa dini hizi mbili
1. Kuendeleza mfumo wa kibaguzi katika elimu kama ulivyoachwa na wakoloni. Wakoloni wa kijerumani ndio walioanzisha mfumo wa kuwabagua Waislamu katika elimu baada ya kushinikizwa na makanisa. Ushahidi wa mashinikizo hayo unaweza kupatikana katika rejea zifuatazo: Cameroon and Dodd 1970:56, Kurtz1972:19, Smith 1963:16. Hatimaye kutokana na mashinikizo hayo serikali ilikubali kufaya yafuatayo:-
i. Kuwafukuza kazi Waislamu waliokuwa serikalini na kuwaingiza Wakristo (Tazama Cameroon and Dodd1970: 25, 56, pia Roland 1970:205)
ii. Kuzipa shule za wamisheni msaada wa kifedha kutoka kodi za wananchi huku wakizibagua zile za Waislamu (Tazama Roland: 1970: 205,na Cameroon and Dodd 1970:50)
iii. Kuweka mpango mkakati wa kuwabagua na kuwahujumu Waislamu na Uislamu wao. Tazama Roland 1970:205, Kurtz 1972:29. Cameroon and Dodd 1970:114
iv. Kujenga hoja kwamba Waislamu kwa asili yao si watu wa kuendelea na kuwa ni wavivu. Tazama E.B Castle 1966:37 ambaye anasema, Islam hinders progressive attitude to change in society and a community that accepts Islam is less likely to advance in social welfare and education, Yaani Uislamu ni kikwazo cha fikra za maendeleo na mabadiliko katika jamii, na kwamba jamii ikiukubali Uislamu haiwezi kamwe kupiga hatua za katika ustawi wa na elimu. Pia Abel Ishumi 1980:208 anasema, From the beginning Muslims were opposed to western type formal education, Kwamba Waislamu walipinga elimu. Pia Abel Ishumi 1981:43, Muslims believe highly in fatalism Kwamba Waislamu wanabweteka na kuamini kwao kuwa mambo yameshakadiriwa.
2. Kuhujumu taasisi za Waislamu na kuweka viongozi mamluki. Baada ya uhuru Serikali ya Tanzania imekuwa na muelekeo wa kuziandama taasisi zinazoonekana kuwa na mipango madhubuti ya kuwakomboa Waislamu kuondokana na ujinga na umaskini. Rejea Bergan 1981:26 na Sivalon 1992:3 kuhusu kuvunjwa kwa EAMWS na kuanzishwa kwa BAKWATA. Pia soma Anuur na. 13 la Agosti 1992 juu ya taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ya kuitaka Serikali kuifuta EAMWS. Pia tazama Njozi 2000:31. Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania kuhusu kadhia ya kuvamiwa kwa Msikiti wa Mwembechai na hatimaye kuuliwa kwa Waislamu.
3. Kuhodhi mfumo wote wa elimu nchini. Tangu kuondoka kwa Mkoloni Wakristo wamekuwa kama mabaki ya wakoloni na ukoloni. Ukiondoa shule za msingi na sekondari za Kata, huko katika shule za sekondari za Serikali, vyuo vya kati na vyuo vikuu wanafunzi na wafanyakazi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80. Siku hizi katika shule za Kata wanafunzi Waislamu wameanza kuonekana. Katika taasisi za elimu mfano T.I.E, TEA, NECTA, Bodi ya Mikopo, I.A.E na vyuo vyote nchini, uongozi umekuwa ni mali ya Wakristo. Huko mwanzo walidai kwamba hamna Muislamu mwenye elimu ya kutosha kuongoza. Kwa siku za hivi karibuni madai yao kwa wale Waislamu wachache waliofanikiwa kupata elimu ni kuwa hawafai kwa vile wana, udini. Aidha katika Wizara ya Elimu (MOEVT) tangu Wizara hiyo kuundwa uongozi umekuwa mali ya Wakristo kwa zaidi ya asilimia 90. Nafasi kama ya Kamishina wa Elimu haijawahi hata kuwa na Kaimu Muislamu na wala haitarajiwi chini ya Mfumochristo. Nafasi za wakurugenzi nazo zimemilikiwa na Wakristo. Mfumokristo umejikita barabara. Uongozi wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu nao umemilikiwa vilivyo. Nafasi za Maafisa elimu Wilaya na Mikoa na wakaguzi wakuu wa elimu wa Kanda kwa zaidi ya asilimia 85 zinaendelea kuwa miliki ya hawa Wakristo.
4. Kukataa kutunga sera za kuondoa upendeleo wa Wakristo katika elimu na kuendeleza ulaghai dhidi ya wananchi wasiokuwa Wakristo. Mara baada ya uhuru ilielezwa na viongozi wetu akiwemo Mwl. Nyerere kuwa serikali itachukua hatua kuondoa mpango ulioasisiwa na Wakoloni wa kuwabagua Waislamu. (tazama A. Jumbe 1994:123, Court 1976 na Nyerere in Hansard Desemba 10, 1962). Badala yake hatua zilizochukuliwa hazikulenga kuondoa tatizo la ubaguzi wa kidini katika elimu nchini na kuwaondoa pia katika ajira na madaraka.Mfano wa hatua hizo ni pamoja na:
i. Kufuta ada shule za msingi na sekondari miaka ya 1960/70.
ii. Kuweka kikomo cha elimu ya msingi kuwa miaka 7 bila kusita.
iii. Kuondoa mitihani ya darasa la 4 na 5. iv. Kuanzishwa kwa mpango wa UPE.
v. Kujenga shule za msingi za bweni kwa watoto wa wafugaji na wavuvi wanaoishi kwa kuhamahama
vi. Kutaifisha shule za binafsi zilizokuwa chini ya mashirika ya dini na watu binafsi. Mpango huu haukuhusisha seminari za Wakristo.
vii. Kupeleka wanafunzi sekondari kwa kigezo cha KUCHAGULIWA badala ya KUFAULU kulikoendana na kuyafanya matokeo ya mtihani wa darasa la saba kuwa ni siri.
viii. Kuanzishwa utaratibu wa quota system ambapo kila mkoa ulipangiwa idadi ya wanafunzi watakaochaguliwa kwenda sekondari.
ix. Kuweka utaratibu mgumu wa kuanzisha na kuendesha shule binafsi chini ya sheria ya elimu ya mwaka 1978, hivyo watu wote kulazimika kusoma katika shule chache za sekondari za Serikali
x. Kuanzishwa kwa shule maalum za vipaji katika miaka ya tisini mfano: Kibaha, Kilakala, Ilboru, n.k.
xi. Kutoa upendeleo maalum (Affirmative Action) kwa watoto wa kike kuingia sekondari na vyuo. Aidha kuwepo pia kwa mipango ya kuwasomesha watoto wa kike kutoka familia maskini.
xii. Ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata. Sera hizi zote pamoja na nyinginezo hazikusaidia kuondoa uwiano mbaya au ubaguzi wa elimu kwa Waislamu. Tuangalie mfano michache ifuatayo: Ni ukweli usiopingika kwamba UPE awamu ya kwanza iliyosukumwa na UNESCO na awamu ya pili iliyosukumwa na Malengo ya Milenia (MDGs) na Mpango wa Elimu kwa wote (EFA) zimesaidia kuwahakikishia watoto wengi wa Kiislamu elimu hiyo ya msingi. Lakini sera hii ilikuja katika kipindi ambacho elimu ya msingi haikuwezi tena kumpatia mtu ajira katika sekta rasmi na hata ile ya binafsi.
Ikumbukwe kwamba katika kipindi hicho cha miaka ya 60 hadi 2000 nafasi za masomo ya sekondari ziliendelea kuwa haba. Wakati wote huu watoto wa Kikristo ndiyo walioendelea kufaidika na elimu ya sekondari. Masomo hayo ya sekondari hatimaye yaliwapatia fursa za kuingia vyuo vikuu na hivyo kuwa katika nafasi za kuajiriwa serikalini, kuteuliwa katika vyeo na nyadhifa mbalimbali huku Waislamu waliowaacha shule za msingi wakiambulia ajira za usafi na utarishi.
Naam, Mfumokristo umefanikiwa kuwafanya Wakristo kuwa warithi wa wazungu wakoloni na kuwaacha Waislamu katika hadhi lie ile waliokuwa nayo wakati wa ukoloni. Aidha kutaifishwa kwa shule hakujasaidia Waislamu kupata elimu ya sekondari kama inavyodaiwa kuwa Nyerere alitaifisha shule ili Waislamu wasome.
Kama tulivyoona awali kuwa tangu wakati wa Mjerumani serikali ya kikoloni ilikuwa ikitoa pesa kusaidia ujenzi na uendeshaji wa shule za Wakristo ni dhahiri kuwa shule hizi zilikuwa zimeshalemazwa na pesa za serikali kwa kipindi cha miaka 55, tangu mwaka 1914 hadi mwaka 1969 zilipotaifishwa. Tazama maandiko ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki (TEC) Fr Robinson, D.W 1965:14 kwamba, The Church is now totally dependent on State aid for the administration of these schools. If this aid were withdrawn the church will be forced to close its schools
Yaani, Kwa sasa Kanisa limekuwa tegemezi kabisa kwa serikali katika kutoa pesa za kuendesha shule zake na ikiwa serikali itasita kutoa fedha kwa shule hizi basi Kanisa litalazimika kuzifunga. Ni dhahiri basi kwamba hatua aliyochukua Julius Nyerere ilikuwa na malengo makuu ya kuziokoa shule za Kanisa kufungwa kwa sababu ingekuwa jambo la kiroja kwa serikali ya Tanzania kuendelea kutoa pesa za kuendesha shule za Kanisa kwa wakati ule, na pili kuhakikisha kwamba malengo ya shule zile ya kuwasomesha Wakristo yanaendelea kutekelezwa kwa kutumia pesa za umma.
Kimsingi kilichobadilika ni jina la mmiliki tu uongozi na malengo ya shule yalibaki vile vile. Ndiyo maana hakuna mtu yoyote aliyethubutu au atakayethubutu kudai eti kwamba ukienda katika shule zilizotaifishwa mfano, Pugu, Minaki, Tambaza, Zanaki, Jangwani, Kibasila, Ilboru, Weruweru, Tosamaganga, Msalato, Umbwe, Ndanda n.k, utakuta idadi ya kuridhisha ya wanafunzi Waislamu wanaosoma huko. Lakini hata katika shule za sekondari chache mpya ambazo serikali ilijenga au kujengewa mwishoni mwa miaka ya 70, kama vile: Kibiti, Ruvu, Karatu, Bagamoyo n.k , kote walimu, wafanyakazi na wanafunzi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80.
Watoto wachache wa Kiislamu wanaosoma huko huonekana kama wakimbizi wanaosaidiwa katika nchi ya ughaibuni. Kuhusu kuingia sekondari kwa kigezo cha kuchaguliwa na mpango wa quota system, watendaji Wakristo waliojazana katika mfumo wa elimu nchini wamekuwa wakihakikisha kwamba Waislamu hawasomi kutokana mbinu zifuatazo:-
i. Kufanya matokeo ya darasa la saba kuwa ni siri hivyo kuweza kuibadili nafasi walizoshinda Waislamu na kuwapa wengine. Tazama ushahidi mzito uliotolewa na Njozi mwaka 2000; katika kitabu cha Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania uk. wa 62 -70. Hapa vijana wa Kiislamu waliofaulu darasa la saba walinyimwa nafasi kuingia sekondari na wale waliofaulu kidato cha nne walinyimwa kuingia kidato cha tano. Kazi hii ya kuwakwamisha vijana wa Kiislamu ilifanywa vyema na mawakala wa Mfumokristo waliojazana katika mfumo wote wa elimu nchini.
ii. Kuhamisha wanafunzi Wakristo kutoka maeneo yenye ushindani mkubwa kwenda Mikoa iliyokuwa na alama ndogo za kuchaguliwa kama Pwani, Dar, Lindi, Mtwara na Tanga ambayo pia ni maeneo ya Waislamu . Tazama Malekela 1983 in Access to secondary education in Sub- Sahara Africa
iii. Huko nyuma kabla ya wanafunzi kupangiwa shule za sekondari namba zao za mtihani ziliambatanishwa na majina ili kujua nani Mkristo apendelewe na nani siyo awachwe iv. Kuhakikisha kwamba viongozi na watendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) wote ni Wakristo. Aidha kwa asilimia kubwa kabisa watungaji wa mitihani na wasahihishaji pia ni dini hiyo hiyo. Tazama kitabu cha Miaka Thelathini ya NECTA, 2004 au www.necta.ca.tz
acha vitisho lete ushahidi
mwenzio yericko nyerere alisema ataweka ushahidi mpaka sasa kimya
Kimsingi huyu bwana said hajui anachokiongea!!!!!
Hii picha mohamed said hawezi kuitafutia ujiko kama alivyozea maana inamsuta yeye mwenyewe...si ajabu alikuwa nayo lakini hakuitoa kwa sababu haionyeshi kutengwa kwa waislam na Nyerere mara baada ya uhuru...
Mimi nabaki kumshangaa tu mzee Mohamed Said, nae hajui kuwa mimi namshangaa!
Kwa kauli yako unatuaminisha kuwa wewe huna akili. Kwa sababu uliweza kufanya kazi na kumpokea Mwalimu uwanja wa ndege pale Mwanza, wakati hakutaka kufanya kazi na watu wenye akili. Duuh! Nauona uoga na ujinga wako sasa!Yericho Nyerere. Naona unatumia kila hali kutaka kuonyesha unaedai kuwa ni baba yako alikuwa sahihi lakin alikuwa na mapungufu mengi sana na mara nyingi alipenda sana kujiweka mbele katika kila kitu. Nimebainisha kuwa unayedai Baba yako Nyerere, kwa sababu nilipokuwa RDD Mwanza mara kwa mara nilikuwa nampokea Nyerere alipokuwa akitoka Dar kwenda Butiama na hata familia yake yote. Kwani walikuwa wanatumia ndege mara nyingi za jeshi la anga na kutua Mwanza kisha wanatumia usafiri wa gari kwenda butiama. Nimebainisha kuwa Historia yoyote ni kama pembe la ng'ombe huwezi kuificha na ndio hiyo siri sasa zimefichuka. Na kwa jinsi ninavyojua mimi kama historia hiyo ya Mohamed said angeitoa miaka ya 70's au mwanzoni mwa 80's basi wakti wa utawala wa Nyerere saa hizi nafikiri Mohamed Said Said saa hizi tungekuwa tunamzungumzia mengine. Kwani enzi za Nyerere hakukubali kabisa kufanya kazi na watu wenye akili na wenye kujiamini katika maamuzi yao. alipendelea sana kufanya kazi na waoga. na hilo ni tatizo kubwa linalowasibu wengi huko na kuwa wenye kulalama kila wakti wote. Kifupi alipenda kutukuzwa mithili ya Mungu mtu.