Mohamed,
Si kweli kwamba EAMWS ilipigwa marufuku Tanzania kwa sababu ilitaka kujenga chuo. Hili umelirudia mara kadhaa kwa dhana kwamba uongo ukirudiwa mara kwa mara watu wataanza kuamini kuwa ni kweli. EAMWS ilipigwa marufuku baada ya kuingilia mambo ya siasa. EAMWS ilitumika kuchanga fedha ili Nyerere aondolewe uongozi wa TANU. Hilo katu hautalisema. Zilichangwa fedha kwa ushawishi wa Tewa Said Tewa. Na pia hujataja mchango wa Adam Nasib. Unamfahamu huyu Muislamu mzalendo? Hujatuambia juu ya Iringa National Islamic Conference ya 1968. Hujataja kauli ya Sheikh Abeid Karume, makamu wa kwanza wa rais wa Tanzania, kwamba EAMWS ilikuwa inafuata siasa zinazopingana na TANU na AFP. na kuonya juu ya "religious pretenders from outside," na kuwataka uongozi wa Waislamu ukabidhiwe mikononi mwa watu wenyewe. Hebu tuambie ni waziri gani aliyetangaza Desemba 20 1968 kupigwa marufuku kwa EAMWS nchini Tanzania. Hakuwa Muislamu huyu?
Jasusi,
I knew right from the outset it is going to be my word against theirs.
(Samahani natumia Kiingereza kurahisisha) na mimi nikajizatiti vilivyo.
Nimejizatitii vipi?
Nimetafiti na kuandika kiasi nimwachie mtu yoyote atumie ''premise'' ya
''the standard of the reasonable man'' kunihukumu.
Angalia hapa chini:
[1]Rashid Kayugwa Afisa wa Usalama Taifa, Dar es Salaam ndiye aliyepewa
kazi ya kudumisha mawasiliano kati ya kundi la Adam Nasibu serekali.
Kayugwa ndiye aliyekuwa akielekeza kundi la Adam Nasibu mbinu za propaganda
na nini kifanyike na kwa wakati gani ili kuvunja umoja wa Waislam.
Kayugwa alikuwa amepata mafunzo yake ya ukachero Israel, Checkoslovakia na
Marekani.
Katika kuhakikisha mafanikio ya mkutqano wa Iringa, Kayugwa ambae ni mzaliwa
wa Iringa alipendekeza mkutano wa Waislam wa Taifa ufanyike Iringa kwa kuhofu
vurugu na upinzani kutoka kwa Waislam wa Dar es Salaam.
Baada ya kusoma kitabu cha Padri John Sivalon kilichoeleza kuwa Kanisa baada ya
uhuru liliendesha hujuma dhidi ya Uislam na Waislam kwa kupitia serikali, ndipo
ilipomdhihirikia ukweli na kuona kuwa alipokuwa akitumiwa kuhujumu EAMWS hakuwa
akitumikia serikali kama alivyokuwa anadhani bali alikuwa akilitumikia Kanisa, kama
kuomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu, aliamua kueleza mchango wake katika
kuwahujumu Waislam na Uislam ili iwe fundisho na onyo kwa Waislam watakao
kuwa katika utumishi wa vyombo kama hivyo siku za usoni.
Kabla ya kufa kwake alieleza masikitiko yake kwa kukandamizwa kwa Waislam na
akatoa mfano wake mwenyewe wa kutopandishwa cheo katika Usalama wa Taifa
kwa sababu tu yeye alikuwa Muislam.