Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

mbona mnaanza kuhamaki nyie kizazi cha nyoka?

Tunawapeni kile alichowanyima mohamed said na kuamua kuwapa ngano za masika.

Mwambie awape ukweli, hao wazee wake akina sykes walitengwa au walijitenga kwa minajiri yao ya kiimani?

Mohamed anajua kila kitu lakini kaamua kuwapotosheni kwa laana ileile.
yericko vibaya hivoo,
una haribu mnakasha,jazba za nini?
Tushakuwa kizazi cha nyoka mara hii?
Twende pole pole,kidogo kidogoo.
 
hahaha. Andikeni basi makala kuping historia? Kama nyerere mwenyewe alijificha uso. Mtaweza nyinyi?

Kulikuwa na Kamati ya Usuluhishi ya Waislam chini ya Mussa Kwikima na ilikuwa na makabrasha na nyaraka nyingi sana.
Baada ya mgogoro kwisha na BAKWATA kuundwa na serikali.

Wakawa sasa wanapitiwa wanakamati na kutishwa makabrasha yote yakakakusanywa.

Waikela hakuweza kutishwa na yeyote.
Yeye akaficha makabrasha yake kwa miaka 20.

Akayaweka hadi yaliponifikia mimi katika miaka ya 1980s.
Nyaraka za Bilal Rehani Waikela ndizo nilizotumia kuandika shemu ya mwisho ya kitabu changu.

Historia ya Waislam Tanzania ni nzito.
Hakuna nje ya sisi anaeweza kuwa na ujasiri wa kuiandika.
 
kulikuwa na kamati ya usuluhishi ya waislam chini ya mussa kwikima na ilikuwa na makabrasha na nyaraka nyingi sana.
Baada ya mgogoro kwisha na bakwata kuundwa na serikali.

Wakawa sasa wanapitiwa wanakamati na kutishwa makabrasha yote yakakakusanywa.

Waikela hakuweza kutishwa na yeyote.
Yeye akaficha makabrasha yake kwa miaka 20.

Akayaweka hadi yaliponifikia mimi katika miaka ya 1980s.
Nyaraka za bilal rehani waikela ndizo nilizotumia kuandika shemu ya mwisho ya kitabu changu.

Historia ya waislam tanzania ni nzito.
Hakuna nje ya sisi anaeweza kuwa na ujasiri wa kuiandika.

natamani wazee wa tanu watoke wakanushe na sio hawa waliosomeshwa na pesa zetu walipa kodi kupitia mradi wa kifisadi wa kanisa (mou). Hawajui chochote badala ya jazba
 
halafu kibaya zaidi anataka kutuaminisha ya kuwa mateso wanayoyapata masheikh leo yana mfanano na wakati ule wa nyerere alivyowafanyia waislam na hasa masheikh. Hoja hafifu kabisa.

ndugu yericko kaishiwa hoja,sasa anaanza kuonyesha vyake viroja kwa kututamkia wazi wazi ya kwamba sisi ni kizazi cha nyoka,yaani tumelaaniwa?
Je,anautendea haki mnakasha huu??
 
yericko vibaya hivoo,
una haribu mnakasha,jazba za nini?
Tushakuwa kizazi cha nyoka mara hii?
Twende pole pole,kidogo kidogoo.

Unajua maana halisi ya KIZAZI cha NYOKA?

Uliza mkuu usikimbilie kulaumu tu!

Kizazi cha nyoka ni binadamu wote wakizazi baada ya Eva/Hawa kula Tunda la mti wa mema na mabaya!

Hivyo mimi, wewe na yule ni kizazi cha nyoka.
 
Ndio ni jibu la hoja, unayo fursa ya kupinga au kukubali mkuu!

Waambie ukweli wafuasi waku kuwa wazee wako waliasi serikali.
Serekali ipi ya Muungano wa ya KANISA? kama ya MUUNGANO WAMEFANYA KOSA. LKN KAMA YA KANISA hawakufanya kosa. wewe na WAZEE WA TANU NANI ANAJUA HSTORIA? HISTORIA ULUIOSOMA WEWE SI NDIO HII INAYOSOMESHWA KATIKA SHULE ZA ST ZA KUMTAKASA MWALIMU? HONGERA SHEIKH SAID
 
unajua maana halisi ya kizazi cha nyoka?

Uliza mkuu usikimbilie kulaumu tu!

Kizazi cha nyoka ni binadamu wote wakizazi baada ya eva/hawa kula tunda la mti wa mema na mabaya!

Hivyo mimi, wewe na yule ni kizazi cha nyoka.

umepanchi ili kuweka mambo sawa na kutunza heshima ya mnakasha,na tuendelee,mimi najitambua kama ni kizazi cha adam na wala si cha nyoka,tafsida uliyoificha pale ilishatambulika mkuu,
anyway kuwa kizazi cha nyoka ama adam si mantiki ya mnakasha huu,tunaiweka pembeni na kuendelea kuinamisha vinywa vyetu chini kwa maalim moh said ili aendelee kumwaga darsa kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho..
 
ndio ni jibu la hoja, unayo fursa ya kupinga au kukubali mkuu!

Waambie ukweli wafuasi waku kuwa wazee wako waliasi serikali.

si kweli ya kwamba waliasi serikali,si kweli hata kidogo,
lakini pia,,ndio kusema ya kwamba mara baada ya wazee hao kuasi serikali kama ilivokuwa fabricated hiyo ikawa ni justification ya kufutwa kwa historia yao ya ukombozi wa taifa hili moja kwa moja?
 
Naona neno uchochezi umeshindwa kulitumia tena baada kushindwa kuthibitisha.

Ni vizuri kujifunza hebu tupe hicho kisa kidogo cha wazee waliofanya uasi na kutaka kumpindua Nyerere. Kwa faida ya JF na wasomaji tupe
na majina yao.

Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa,
kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislam
wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Wakristo
serikalini. Mashuhuri miongoni mwao walikuwa:

Sheikh Hassan bin Amir, Abdillah Schneider Plantan, Sheikh
Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi
Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein
Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela,
Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh
Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah,
Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha
Mbuzi na wengine wengi.

Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa
na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa.

Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana
na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa Nyerere.

Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu
walihusika na msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako
Sheikh Hassan bin Amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo
roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa
yake kila magharibi pale msikitini.

Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba walihamishiwa Kenya,
walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika
harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa
waangalizi wa msikiti wa Badawiy.

Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara
alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa
kivuli cha sheikh.

Hakuna katika orodha hii ya masheikh hata mmoja aliyefikishwa
mahakamani kwa kesi ya uhaini.
Jina lenye mstari Salum Abdallah ni babu yangu.

Salum Abdallah aliongoza mgomo (General Strike) wa 1947.

Salum Abdallah alikuwa mfadhili wa AA hadi TAA Tabora.

Salum Abdallah alikuwa katika kamati ya siri ya kuibuka na TANU
1954akihudhuria mikutano yote ya ''uchochezi'' dhidi ya Waingereza.

Salum Abdallah alitoa fedha nyingi kupita wote kumpa Germano Pacha
kuja Dar es Salaam kuwakilisha Western Province katika kuasisi TANU.

Salum Abdallah ni mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU
Salum Abdallah 1955 alikuwa rais muaisisi wa Tanganyika Railway
African Union (TRAU) chama hiki kilipigana bega kwa bega na TANU
katika kupigania uhuru.

Katibu wake akiwa Chrisant Kassanga Tumbo.

Salum Abdallah aliongoza mgomo wa Railway wa 1960 uliodumui siku
82 mgomo kama huu wa miezi 3 haujapata kutokea.

Viongozi wa TRAU walipokea msaada kutoka chama cha wafanyakazi wa
Reli Uingereza na chama cha wafanyakazi kutoka Ujerumani ya Mashariki.

Hiki ndicho kilichoiwezesha TRAU kudumu katika mgomo kwa miezi 3.
Wafanyakazi wakipata posho kuzikimu famila zao.

Salum Abdallah katika mkutano wa Moshi 1962 alimpinga Nyerere
katika suala la kuweka vyama vya wafanyakazi chini ya TANU.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kuzuizini.
Babu yangu hakuwa haini.

Babu yangu alikuwa mzalendo mpigania uhuru kwa vitendo toka
enzi za African Association akiwa akiwa Dar es Salaam.

Nyerere alipata hofu ya wazalendo kama hawa waliokuwa na uwezo
wa kuwakusanya wananchi pamoja kudai haki zao.

Mgomo ule wa 1960 ndiyo uliomfanya Nyerere apate hofu na Salum
Abdallah.

Akiwa jela ya Uyui taarifa zikamfika Salum Abdallah kuwa ya TRAU
na vyama vyote vya wafanyakazi vimevunjwa na Nyerere na chama
kimoja cha vibaraka NUTA kimeundwa kuwawakilisha wafanyakazi wa
nchi nzima.

Salum Abdallah hadi anaingia kaburini alikuwa na orodha ya watu wake
akiwaita waongo, vibaraka, wasaliti na wengi katika hao walikuwa katika
NUTA, TANU, na serikalini...

Michael Kamaliza...

Wanaukumbi tafuteni majina ya watu hawa si shida kuwajua.

Alipokufa 1974 TANU walifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
babu yangu na kumwita mzalendo aliyejitolea kwa hali na mali yake
kuipigania nchi yake.

Huyu alikuwa Mmnanyema kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika baba
yake Samitungo Mwekapopo aliingia nchini kama askari katika jeshi la
Wajerumani.

Nanyi kama mna wazee huko kwenu wana historia kama hizi hebu ziwekeni
humu nasi tuzisome.

Salum Abdallah alizaliwa Shirati pale bomani.
 
si kweli ya kwamba waliasi serikali,si kweli hata kidogo,
lakini pia,,ndio kusema ya kwamba mara baada ya wazee hao kuasi serikali kama ilivokuwa fabricated hiyo ikawa ni justification ya kufutwa kwa historia yao ya ukombozi wa taifa hili moja kwa moja?

Hawakufutwa kama unavyodai/mnavyodai,

Historia inawafahamu wote, ni wewe tu na wengine ndio mnaoamini kuwa wazee wenu walifutwa.

Hakuna tamko mahala popote lililotamkwa na kiongozi wa nchi hii kuwa amefuta rasmi historia ya wazee hao, ila Uchochezi na propaganda za akina Mohamed Said tu ndizo mnazoozisikia na kuamini.
 
Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa, kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislam wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Wakristo serikalini. Mashuhuri miongoni mwao walikuwa:

Sheikh Hassan bin Amir, Abdillah Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha Mbuzi na wengine wengi.

Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa.

Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa Nyerere.

Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusika na msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa yake kila magharibi pale msikitini.

Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa waangalizi wa msikiti wa Badawiy.

Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh.

Hakuna katika orodha hii ya masheikh hata mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa kesi ya uhaini.
Jina lenye mstari Salum Abdallah ni babu yangu.

Salum Abdallah aliongoza mgomo (General Strike) wa 1947.

Salum Abdallah alikuwa mfadhili wa AA hadi TAA Tabora.

Salum Abdallah alikuwa katika kamati ya siri ya kuibuka na TANU 1954
akihudhuria mikutano yote ya ''uchochezi'' dhidi ya Waingereza.

Salum Abdallah alitoa fedha nyingi kupita wote kumpa Germano Pacha
kuja Dar es Salaam kuwakilisha Western Province katika kuasisi TANU.

Salum Abdallah ni mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU
Salum Abdallah 1955 alikuwa rais muaisisi wa Tanganyika Railway African
Union (TRAU) chama hiki kilipigana bega kwa bega na TANU katika kupigania
uhuru.

Salum Abdallah aliongoza mgomo wa Railway wa 1960 uliodumui siku 82 mgomo
kama huu wa miezi 3 haujapata kutokea.

Salum Abdallah katika mkutano wa Moshi 1962 alimpinga Nyerere katika suala la
kuweka vyama vya wafanyakazi chini ya TANU.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kuzuizini.
Babu yangu hakuwa haini.

Babu yangu alikuwa mzalendo mpigania uhuru kwa vitendo toka enzi za African
Association akiwa akiwa Dar es Salaam.

Nyerere alipata hofu ya wazalendo kama hawa waliokuwa na uwezo wa kuwakusanya
wananchi pamoja kudai haki zao.

Mgomo ule wa 1960 ndiyo uliomfanya Nyerere apate hofu na Salum Abdallah.
Alipokufa 1974 TANU walifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia babu yangu
na kumwita mzalendo aliyejitolea kwa hali na mali yake kuipigania nchi yake.

Huyu alikuwa Mmnanyema kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika baba yake Samitungo
aliingia nchini kama askari katika jeshi la Wajerumani.

Nashukuru sana ndugu yangu Mohamed Said kwakuamua sasa kuwapa ukweli halisi wanajamvi wanaotufuatlia hapa!

Ndugu zangu wanajamvi, Mashehe aliowataja hapo juu na baadhi ya makasisi wa kikristu, ndio wali ASI serikali ya TANU iliyokuwa chini ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,

Tuipongeze serikali ya TANU kwakuzima maasi yale ya chini kwa chini na kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi na waambata wao wote wa maasi dhidi ya ukombozi wa nchi yetu takatifu.

Mohamed Said, mimi ninajua mengi huenda kuliko hata kukuzidi wewe, kinachonishangaza, mbona hukutaka kuwaambia ukweli kwenye Kitabu chako mashabiki wako hasa waislamu wenzio wanaokuunga mkono?

Waambie tu usiogope, waambie kuwa "wazee wetu akina Sheikh Hassan bin Amir waliasi, na wakakumbana na mkono wa sheria ya nchi"!

Hongera kwa vijana wa wakizalendo wa usalama wa taifa Sawaya na Kayugwa waliojitolea nafsi zao kupambana na mashehe hawa walioasi, kwakuwa walifanya kazi nzito katika mazingira magumu na wakafanikiwa.
 
Bwana Nyerere,

Ahsante sana kwa michango yako lakini naona kama
mnakasha unaanza kupoteza ladha yake kama chai
iliyopoa au mchuzi usio ndimu.

Sijui kama hii ni dalili ya uchovu au kitu gani.

Mimi kwa sababu ambazo nadhani ziko wazi huwa sina
kawaida ya kumuuliza mtu swali lolote labda kama
nataka ufafanuzi.

Nimeweka vitu vingi ambavyo nilidhani ukumbi watavichangamkia.

Kuna mtu alisema EAMWS ilikuwa inamchimba Nyerere.

Mimi nikasema hiyo ilikuwa propaganda ya serikali na nikamueleza
na hata kuweka jina la bingwa wa propaganda wa zama zile.

Rashid Kayugwa.

Nilitegemea hapa pangenogesha barza.
Wapi mmetishika.

Mmetishika kwa kuwa mmepata mshtuko kuwa Mohamed hakika
haya mambo anayajua.

Nilitegemea mtaunganisha na jina la mgawaji hongo kwa wanafiki
waunge mkono BAKWATA.

Mgawaji hongo yaani rushwa aliyekuwa akizunguka na mikoba iliyojaa
fedha alikuwa...

Geoffrey Sawaya.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai.

Hii ndiyo serikali yenyewe na vyombo vyake vya ukandamizaji vikiwa
kazini.

Waislam walikuwa yatima.
Walichokipigania kimeporwa na kanisa.

Nilitegemea angalau mniite muongo mpiga soga nk. nk.
Lakini hadi sasa kama vile nimekumwagieni maji ya baridi ya kuzizima.

Turudishe mnakasha katika reli tuache hii kutupiana madongo kama vijana
mnavyopenda kusema.

Huu ni mjadala mzuri sana.
Si muda mrefu viongozi wa dini zetu kuu hizi watakaa mezani kuzungumza.

Itakuwa vyema sisi wafuasi tujue chanzo cha chokochoko na fitna hii inayogawa
taifa letu.

Kubwa zaidi tuwajue walosababisha hii fitna.

muogope Mungu wako mzee Said;
ukiambiwa uthibitishe unakimbilia kusema wazee wangu walinihadithia
 
Nashukuru sana ndugu yangu Mohamed Said kwakuamua sasa kuwapa ukweli halisi wanajamvi wanaotufuatlia hapa!

Ndugu zangu wanajamvi, Mashehe aliowataja hapo juu na baadhi ya makasisi wa kikristu, ndio wali ASI serikali ya TANU iliyokuwa chini ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,

Tuipongeze serikali ya TANU kwakuzima maasi yale ya chini kwa chini na kufanikiwa kuwatia nguvuni viongozi na waambata wao wote wa maasi dhidi ya ukombozi wa nchi yetu takatifu.

Mohamed Said, mimi ninajua mengi huenda kuliko hata kukuzidi wewe, kinachonishangaza, mbona hukutaka kuwaambia ukweli kwenye Kitabu chako mashabiki wako hasa waislamu wenzio wanaokuunga mkono?

Waambie tu usiogope, waambie kuwa "wazee wetu akina Sheikh Hassan bin Amir waliasi, na wakakumbana na mkono wa sheria ya nchi"!

Hongera kwa vijana wa wakizalendo wa usalama wa taifa Sawaya na Kayugwa waliojitolea nafti zao kupambana na mashehe hawa walioasi, kwakuwa walifanya kazi nzito katika mazingira magumu na wakafanikiwa.

Bora umekuja kwa mtindo mwingine kuja kwa njia nyingi za kujifunza siyo mbaya.
 
Darwin,Soma haya machache kutoka paper yangu ''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania'' (Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin. Paper hii niliiwasilisha Ujerumani 2011:''It took a decade to bring the Muslim movement back on track and the irony for that was, it was not CCM the old enemy which was responsible for that but an opposition party, Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) seemingly under the tutelage of Catholic Church out to oust a Muslim president, Mrisho Jakaya Kikwete, which broke the camel’s back. The Catholic Church prior to election issued an Election Manifesto and a document of guidance on how Christians should vote. The presidential candidate for CHADEMA was a former Roman Catholic priest. That said it all. Muslims mobilised for the general election in a manner never seen before to oppose CHADEMA and the Church. Muslims irrespective of their political affiliations campaigned for the return to office of a Muslim president Jakaya Mrisho Kikwete.''Siasa zetu ndipo zilipotufikisha hapa. Wakati umefika wa kujiuliza vipi tumefikia hali hii ilhali wakati wa kupigani uhuru wa nchi hii tulikuwa wamoja?
Mzee Mohamed Said kama kuna siku umepiga msumari mzito ni leo yani hapa ndio ni likuwa nataka nadhani YERICKO NYERERE yuko hoi mimi nilikuwa nataka ajibu hii point yako hapa
Moh' Said na vijana wako akina Boko Haram!Sometimes huwa tunajiuliza weledi wenu nyie kama wasomi hasa mnaposhabikia vitu mnavyojua kabisa kuwa ni propaganda.Moh' Said, unasema habari za EAMWS kuhusishwa na radical islamists miaka hiyo mpaka kupigwa marufuku kwake, ilikuwa ni propaganda tu.Yes, ilikuwa ni propaganda kwa sababu unataka kuhusisha kanisa na Nyerere kwamba ndio wali-collude.Lakini kuhusu Chadema kuwa chama cha kikatoliki kwa vile tu mgombea wake aliwahi kuwa Padre- hizi sio propaganda, si ndio?Kwa mtaji huo mtaendelea kutumiwa na wanasiasa mpaka mchanganyikiwe (kama bado hamjachanganyikiwa).

Hivi hamjui kuwa ni CCM iliyotuma state agents (mashushu) ndani ya misikiti mwaka 1995, wakijifanya maustaadh, huku wakipiga kelele kuwa waislam wachague CUF ambacho kilikuwa na mgombea muislam? Hamjui kwamba walikuwa wanafanya makusudi ili wapiga kura wakione CUF kuwa chama cha kidini? Njama kama hizo walizifanya na kwa NCCR-mageuzi ionekane ni ya wachaga. Na ndio propaganda kama hizo zinatumika dhidi ya Chadema. Lakini nyie ni wepesi wa kuamini lolote lile mnaloambiwa na viongozi wenu, hata mnapoingizwa chaka! Na ndani ya chaka mmeingizwa! Si waliwaambia CCM itawapa mahakama ya kadhi, tutajiunga na OIC, msichague chama kinachoongozwa na padre, na mpaka sasa bado mnaamini hivyo?

Boko Haram na wafuasi wenzio:
Mnaaminishwa kwamba waislam wamekuwa sidelined kwenye maendeleo hapa nchini. Yet, tunaona matajiri wakubwa ni waislam. Eti wanaonewa na NECTA kwenye elimu, yet, tunaona maprofessor wengi waislam (hasa wenye asili ya bara) ambao wamepitia mfumo huo huo wa elimu. Mnasema waislam wengi ni maskini kwa sababu ya mfumo kristo, lakini sisi tuliotembea vijijini tunaona hakuna tofauti ya umasikini kati ya wanavijiji wa imani mbalimbali. Mnaaminishwa kuwa uhuru ulipiganiwa na waislam. Tukikosoa na kuwapa ukweli kuwa ulipiganiwa na wazalendo bila kujali imani zao, nyie mnasema tumekaririshwa kumsifia Nyerere na kwamba tunampinga Moh Said kwa vile yeye ni Muislam na sisi ni wakristo (hata sijui mnajuaje kuwa members ni wakristo au waislam-kwa kuangalia majina kama alivyofanya Moh kwenye simulizi zake?). Moh' Said akiwaambia nchi hii haina wapagani, ila ina waislam na wakristo, nyie mnaamini tu, almradi aliyewaambia ni ustaadh MS aliyefanya "research". Hata hapa jamvini wala hamumsomi vizuri. kiasi kuwa mmeshindwa kujua kuwa huyu mtu ana hidden motive iliyopelekea yeye ku-fabricate stories ambazo anaziita historia. Hamuwezi kumkosoa Kikwete eti tu kwa sababu ni muislam, Kimsingi, ni watu kama nyie ndio mtatucheleweshea maendeleo ya nchi. Stuka, fikirieni nje ya boksi la dini, mpate ukweli.
 
Bora umekuja kwa mtindo mwingine kuja njia nyingi za kujifunza.

Ndugu yangu Ritz, mnakasha huu tutakufunza mengi ambayo naamini toka moyoni mwangu tena upande wa kushoto ulipo moyo, haungeyapata popote mpaka safari yako duniani inaisha na unaingia kaburini, si wewe tu bali ni wengi tu hapa wanazidi kufunguliwa!

Ishukuru JF
 
Ndio ni jibu la hoja, unayo fursa ya kupinga au kukubali mkuu!

Waambie ukweli wafuasi waku kuwa wazee wako waliasi serikali.

Bwana Nyerere,

Wazee wangu hawakuwa waasi kwa serikali kwani hiyo
serikali waliiweka madarakani wao wenyewe kwa mikono yao.

Nakuwekea hapa kwa ufupi kipi kilimpeleka babu yangu jela.

Nawaachia wanaukumbi waseme kama babu yangu alikuwa msaliti
au mzalendo.

Soma ukiwa akili yako umeifungua.

Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa,
kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislam
wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Wakristo
serikalini. Mashuhuri miongoni mwao walikuwa:

Sheikh Hassan bin Amir, Abdillah Schneider Plantan, Sheikh
Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi
Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein
Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela,
Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh
Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah,
Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha
Mbuzi na wengine wengi.

Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa
na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa.

Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana
na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa Nyerere.

Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu
walihusika na msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako
Sheikh Hassan bin Amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo
roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa
yake kila magharibi pale msikitini.

Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba walihamishiwa Kenya,
walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika
harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa
waangalizi wa msikiti wa Badawiy.

Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara
alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa
kivuli cha sheikh.

Hakuna katika orodha hii ya masheikh hata mmoja aliyefikishwa
mahakamani kwa kesi ya uhaini.
Jina lenye mstari Salum Abdallah ni babu yangu.

Salum Abdallah aliongoza mgomo (General Strike) wa 1947.

Salum Abdallah alikuwa mfadhili wa AA hadi TAA Tabora.

Salum Abdallah alikuwa katika kamati ya siri ya kuibuka na TANU
1954akihudhuria mikutano yote ya ''uchochezi'' dhidi ya Waingereza.

Salum Abdallah alitoa fedha nyingi kupita wote kumpa Germano Pacha
kuja Dar es Salaam kuwakilisha Western Province katika kuasisi TANU.

Salum Abdallah ni mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU
Salum Abdallah 1955 alikuwa rais muaisisi wa Tanganyika Railway
African Union (TRAU) chama hiki kilipigana bega kwa bega na TANU
katika kupigania uhuru.

Katibu wake akiwa Chrisant Kassanga Tumbo.

Salum Abdallah aliongoza mgomo wa Railway wa 1960 uliodumui siku
82 mgomo kama huu wa miezi 3 haujapata kutokea.

Viongozi wa TRAU walipokea msaada kutoka chama cha wafanyakazi wa
Reli Uingereza na chama cha wafanyakazi kutoka Ujerumani ya Mashariki.

Hiki ndicho kilichoiwezesha TRAU kudumu katika mgomo kwa miezi 3.
Wafanyakazi wakipata posho kuzikimu familia zao.

Salum Abdallah katika mkutano wa Moshi 1962 alimpinga Nyerere
katika suala la kuweka vyama vya wafanyakazi chini ya TANU.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuwekwa kuzuizini.
Babu yangu hakuwa haini.

Babu yangu alikuwa mzalendo mpigania uhuru kwa vitendo toka
enzi za African Association akiwa akiwa Dar es Salaam.

Nyerere alipata hofu ya wazalendo kama hawa waliokuwa na uwezo
wa kuwakusanya wananchi pamoja kudai haki zao.

Mgomo ule wa 1960 ndiyo uliomfanya Nyerere apate hofu na Salum
Abdallah.

Akiwa jela ya Uyui taarifa zikamfika Salum Abdallah kuwa TRAU
na vyama vyote vya wafanyakazi vimevunjwa na Nyerere na chama
kimoja cha vibaraka NUTA kimeundwa kuwawakilisha wafanyakazi wa
nchi nzima.

Salum Abdallah hadi anaingia kaburini alikuwa na orodha ya watu wake
akiwaita waongo, vibaraka, wasaliti na wengi katika hao walikuwa katika
NUTA, TANU, na serikalini...

Julius Nyerere...
Michael Kamaliza...
Rashid Kawawa...

Wanaukumbi tafuteni majina ya watu hawa ambao babu yangu
aliwaorodhesha kama waongo, vibaraka na wasaliti.

Si tabu kuwajua.

Alipokufa 1974 TANU walifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
babu yangu na kumwita mzalendo aliyejitolea kwa hali na mali yake
kuipigania nchi yake.

Huyu alikuwa Mmnanyema kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika baba
yake Samitungo Mwekapopo aliingia nchini kama askari katika jeshi la
Wajerumani.

Bwana Nyerere huyu ndiye babu Salum Abdallah yangu ambae kaanza
harakati za kupigania uhuru wa nchin hii wala hamjui Nyerere.
 
Ndugu yangu Ritz, mnakasha huu tutakufunza mengi ambayo naamini toka moyoni mwangu tena upande wa kushoto ulipo moyo, haungeyapata popote mpaka safari yako duniani inaisha na unaingia kaburini, si wewe tu bali ni wengi tu hapa wanazidi kufunguliwa!

Ni kweli najifunza mengi sana wala ilo halina ubishi.
 
Hawakufutwa kama unavyodai/mnavyodai,(SASA WAKO WAPI??MBONA NIMEJITAHID KUSOMA VITABU VINGI SANA VYA HISTORIA LAKINI SIJAKUTANA NA HAWA NDUGU ZANGU KAMA WALIVOAINISHWA NA MKWASI WA HISTORIA NDUGU MOH' SAID??

Historia inawafahamu wote, ni wewe tu na wengine ndio mnaoamini kuwa wazee wenu walifutwa.(KAMA INAWAFAHAM WOTE,KWANINI SASA JULIUS PEKEE NDIE AWE KINARA NA WENZAKE WALIOMKARIBISHA MJINI NA KUMUUNGANISHA KWENYE HARAKATI WAKAPUUZWA NA KUACHWA NJE YA ULINGO HUO MOJA KWA MOJA??

Hakuna tamko mahala popote lililotamkwa na kiongozi wa nchi hii kuwa amefuta rasmi historia ya wazee hao, ila Uchochezi na propaganda za akina Mohamed Said tu ndizo mnazoozisikia na kuamini.(KWANI YAHITAJI TAMKO ILI TUWEZE FAHAM KUWA HISTORIA YAO WALE WAZEE IMEFIFISHWA??MADHARA YA KUKAA KUSUBIRI TAMKO NDIO HAYA YALIYOPELEKEA HADI JULIUS KUVESHWA UBABA WA TAIFA HILI,YERICKO UPO??BILA SHAKA TUNAENDA SAWA SASA,
UBARIKIWE SANA YERICKO NDUGU YANGU,UZI WAKO HUU UMEWAFUNGUA MACHO WENGI,USHUKURIWE YERICKOO..
 
Halafu kibaya zaidi anataka kutuaminisha ya kuwa mateso wanayoyapata Masheikh leo yana mfanano na wakati ule wa Nyerere alivyowafanyia Waislam na hasa Masheikh. Hoja hafifu kabisa.
Haya maneno yananikumbusha uzalilishwaji wa masheikh wetu kama Sheikh Nurdin Hussein na Sheikh Mohamed Nasoro wa Zanzibar.Sheikh Nurdin Hussein na familia yake walitolewa Lindi na kuhamishiwa Muheza,Tanga kwa mabavu chini ya maagizo ya Nyerere.Katika maeneo yaliyokuwa na uislam au kuonyesha ustawi wa maendeleo yenye kuwagusa waislamu Nyerere aliyavuruga na kigezo cha vijiji vya ujamaa na kuyaacha huku upande wa pili kuyapa fursa za maendeleo maeneo yanayokaliwa kwa wingi ma wakristu.
 
Back
Top Bottom