Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndiyo maana Mohamed Said anaulizwa...je, anakubali au anapinga hii hotuba kutolewa na Mwalimu Nyerere mbele ya wazee wake wa Dar es Salaam? Akishajibu tutaendelea...mpaka sasa bado anaomba muda, anadai hajaiona! Je kama ilitolewa, imekuwaje afanye utafiti wote huo miaka yote hiyo asiwe nayo? Ritz unataka video clip, sawa, je ngano zote anazomwaga Mohamed Said kama peremende, kwa nini unaziamini? Alitoa video?
Naongea kama Ritz, hayo ni mawazo yangu Mohamed Said naye ana mawazo yake, wewe nikunasibishe na nani ukoo wa Nyerere?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Maalim Mohamed Said, hotuba imewekwa kwa maandishi, neno kwa neno!.
"Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Sasa kama yalioandikwa yote ni kweli ndiyo yaliyotamkwa, then wewe kuitwa mchochezi sio kutukanwa bali huo ndio ukweli halisi wa "the motive behind" kitabu chako!.

Ila pia kwa sisi Waafrika tunaoamini imani za mizimu, kumsingizia marehemu kunaleta laana ya aina fulani, nakushauri utubu ungali hai ili kuiepushia "bad karma" familia yako utakayoiacha nyuma baada ya wewe kutangulia mbele ya haki, isije kuadhibiwa kwa makosa yako!. Huu ni ushauri tuu na only if you belive the universal law of "cause and effects", "karma" haina mswalie Mtume wala haina huruma kwa wasio na hatia!.
Pasco.

Hahaaa Pasco nimekuwa muumini sana wa michango yako hasa ile ya hoja tata, daah hapa sina mbavu kwakicheko.
 
Haya mambo ya kujenga hisia kuwa dini moja inaonewa na dini nyingine yanahatarisha usalama wa taifa letu. Hapa Tanzania kuna fursa ambazo zaweza kutumiwa na yeyote na hakuna mtu anazuiliwa kwa sababu ya dini yake. Kuna tofauti kati ya watu kulingana na kanda zao na si dini. Mfano Bukoba, Arusha na Kilimnjaro waislamu na wakristo hawatofautianani kwa hiyo hakuna kulaumiana kule. Watanzania mitaani wanajichangaya hawabaguani na matajiri wapo pande zote. kulikuwa na tatizo la kimtazamo na utamaduni hasa miongoni mwa watu wa pwani siku za nyuma kuhusu elimu. kwa vile wengi walikuwa waislamu walijikuta hawako katika mfumo wa kishule na hivi wakajikuta hawapo wengi katika mfumo wa ajira na utawala. kwa sasa hayo hayapo na watanzania wote wanaenda shule.
Sidhani kama kuna uamuzi rasmi wa kisera wenye nia ya dini moja kuhujumu dini nyingine.
Dunia innabadilika watakaoishi miaka 50 ijayo watakuwa hawana ujinga huu wa udini tulionao sisi tena watayashangaa sana haya mawazo ya kibaguzi tuliyonayo. Ishara imeanza kwa kasi ya vijana wa kikristo na kiislamu kupendana na kuamua kuwa wanandoa japo wazazi wanakuwa kikwazo. ingekuwa si wazazi na na viongozi wa dini tungeshuhudia mengi. kwa hiyo udini uko kwa watu wazima/wazee kama Mohamed Said na si vijana. Vijana kataeneni kasumba za udini
 
samahani moderators,kama itakuwa ni kosa,nimempa mtu password yangu hili aingize audio ya ile hotuba ya nyerere-tuvumiliane but within 24 hours itakuwemo humu cause we need to get to the bottom of this-kanidokezea kwamba the omens are not good for ms

dah,this is so childish.
Sasa kama umempa mtu pasword yako ili aweke link ya hiyo hotuba ya saut,sasa unawaomba moderators unawaomba samahani kivipi??

Pole sana,kaa chini kwa adabu upewe darsa huru hili.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, hotuba imewekwa kwa maandishi, neno kwa neno!.
"Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Sasa kama yalioandikwa yote ni kweli ndiyo yaliyotamkwa, then wewe kuitwa mchochezi sio kutukanwa bali huo ndio ukweli halisi wa "the motive behind" kitabu chako!.

Ila pia kwa sisi Waafrika tunaoamini imani za mizimu, kumsingizia marehemu kunaleta laana ya aina fulani, nakushauri utubu ungali hai ili kuiepushia "bad karma" familia yako utakayoiacha nyuma baada ya wewe kutangulia mbele ya haki, isije kuadhibiwa kwa makosa yako!. Huu ni ushauri tuu na only if you belive the universal law of "cause and effects", "karma" haina mswalie Mtume wala haina huruma kwa wasio na hatia!.
Pasco.

Ndugu yangu una haraka sana.
Vuta subira vielelezo vyote viwekwe hapa kisha tutajadili.

Sasa hivyo vitisho vya kazi gani?

Usishangilie goli kabla mpira haujatinga wavuni.

Sauti itawekwa tutasikiza sisi wenyewe.

Liko hili la ''TAA kusinzia'' si kweli lakini hili tuliache kwa sasa tutalizungumza tukimaliza hotuba.
 
samahani MODERATORS,kama itakuwa ni kosa,nimempa mtu password yangu hili aingize audio ya ile hotuba ya nyerere-tuvumiliane but within 24 hours itakuwemo humu cause we need to get to the bottom of this-kanidokezea kwamba the omens are not good for MS

Tutashukuru sana mkuu, Nitawaomba MODS waiweke pale chini ya hotuba ya maandishi ili walimwengu wote washuhudie
 
unaposema gazeti la serikali, daily news lilirekebisha cheo cha abdul, na katika hotuba ya mwalimu ya kuaga mbele ya wazee wa dar mwalimu alisema wazi kuwa abdul alikuwa katibu wa tanu, je unataka tukuamini wewe kwa uthibitisho upi?

weka sauti,
tafadhali.
 
Sasa ni kweli abdu alikuwa ''katibu wakati huo?''
ukweli ni kuwa Nyerere alimkuta Abdulwahid akiwa rais wa TAA.
(kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
Sasa unaanza kuchanganya mambo...kwanza unaanza kwa kunukuu kitabu ulichokiandika wewe mwenyewe, duh! Pili ni kikao gani kilichomchagua Abdulwahid Sykes kuwa Raisi wa TAA na kama alikuwa Raisi, katibu alikuwa nani? Kumbuka baada ya Raisiwa TAA wa kuchaguliwa, Dr. Kyaruzi, kupewa uhamisho wa nguvu mwaka 1951 na wakoloni, hakuwahi kuchaguliwa Raisi mpya...tuanzie hapo.
 
Unaposema gazeti la serikali, Daily News lilirekebisha cheo cha Abdul, na katika hotuba ya Mwalimu ya kuaga mbele ya Wazee wa Dar Mwalimu alisema wazi kuwa Abdul alikuwa Katibu wa TANU, Je unataka tukuamini wewe kwa uthibitisho upi?

Tutakaposikiza hotuba jibu litapatikana Insha Allah.
 
tutashukuru sana mkuu, nitawaomba mods waiweke pale chini ya hotuba ya maandishi ili walimwengu wote washuhudie
sasa kumbe hata wewe mwenyewe umeicopy na kui-paste bila ya kuwa na uhakika wa uhalisia wa hotuba ya sauti??
Jamii ya watu ambao wanacopy na ku paste nchi flani huwa wanaitwa (vi- la - za)
 
Sasa unaanza kuchanganya mambo...kwanza unaanza kwa kunukuu kitabu ulichokiandika wewe mwenyewe, duh! Pili ni kikao gani kilichomchagua Abdulwahid Sykes kuwa Raisi wa TAA na kama alikuwa Raisi, katibu alikuwa nani? Kumbuka baada ya Raisiwa TAA wa kuchaguliwa, Dr. Kyaruzi, kupewa uhamisho wa nguvu mwaka 1951 na wakoloni, hakuwahi kuchaguliwa Raisi mpya...tuanzie hapo.

Mag3,

Mimi naomba haya yasubiri Insha Allah nitayajibu.

Tusubiri hotuba iwekwe tusikize sote.
Baada ya hapo Insha Allah mnakasha utaendelea.
 
vipi nitakuwa na hamu ya mnakasha wakati ndugu yangu umehamaki
unanitukana.

Mchochezi, mchochezi, mchochezi.

Sasa heshima yangu iko wapi?

Niwekeeni hotuba.

bado sijaiona.

sisi tunashangaa sana,matusi ya nini na kejeli hali ya kuwa hapa watu wanajibishana kwa hoja?
Inaleta picha tofauti sana kwa kweli.
 
ushaanza kuogopa hata audio haijaingia-the truth will always prevail

niogope kuhofia nini?
Wewe unaetoa lugha za kejeli na jazba ndie mwenye uwoga,kama unajiamin una ushahid na hoja zenye mashiko lazima utakuwa mtulivu na mwenye hekima kwa kauli kama afanyavyo ndug moh' said.
Chukua mfano wa majadiliano ya hoja kutoka kwake.
 
Hahaaa Pasco nimekuwa muumini sana wa michango yako hasa ile ya hoja tata, daah hapa sina mbavu kwakicheko.
Mkuu Yericko, lengo ni kujaribu kumuepushia Mzee wetu Maalim Mohamed Said na laana ya kumsingizia marehemu!, kuna watu wana hatari sio kuchomwa na moto tuu wa jehanum, bali kugeuzwa kuni!. Uchochezi tuu peke yake ni dhabi tosha, achilia mbali kumsingizia marehemu!. Tunasubiri audio mzee aanze kutubu dhambi zake!.
Pasco.
 
Asante sana Son of Alaska lakini kama uonavyo, wapo watakaodai hata video...hawajui hata mwaka kituo cha kwanza cha Television kilipofunguliwa nchini! Ritz tayari anadai aliwahi kuisikia lakini...hatuamini hata sisi tuliokuwapo na kuipata "live".

Hata mimi nilikuwepo nikuamini wewe ili iweje ngoja hotuba tusikie sauti.
 
sisi tunashangaa sana,matusi ya nini na kejeli hali ya kuwa hapa watu wanajibishana kwa hoja?
Inaleta picha tofauti sana kwa kweli.

Yapo wapi matusi? unajua sheria za JF? Kama kuna mtu katukana Mods wangeshamtendea haki yake.

Kejeli ni sehehemu ya burudani ya mnakasha.
 
Mohamed Said,

Mwaka 1985 Nyerere alitoa jumla ya medali 3,979 kwa Watanzania waliochangia maendeleo ya Taifa.

Wazee wazalendo waliopigania uhuru walipewa wangapi medali.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom