Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

yapo wapi matusi? Unajua sheria za jf? Kama kuna mtu katukana mods wangeshamtendea haki yake.

Kejeli ni sehehemu ya burudani ya mnakasha.

kejeli ni moja ya burudani ya mnakasha??
Kumbe mko hapa kumuenjoy ndugu moh said na si kwa ajili ya kujifunza na darsa lake?
Sasa nimekuelewa mkuu,thanks a lot,kumbe mnamkejeli makusudi ili mumtoe kwenye mstari?
Kwa hilo hamtafanikiwa,ngoja tuisubirie kwanza hiyo hotuba ya julius.
 
generaly jamii ya kiislamu imepungukiwa uwezo wa kufikiri..

sawa,matusi,kejeli na dharau haziwezi kutuondoa kwenye mantiki kuu ya mjadala huu,semeni yote hadi myamalize,ila tukibishana kwa hoja tutakuwa tunafanya jambo la msingi sana,
dharau kama hizi ni kuonesha kipimo finyu cha busara na hekima zako.
 
Mohammed Said; the burden of proof iko kwako sasa. Hata kama huwezi kupata tape ya ile hotuba bila ya shaka utakuwana transcript yake ambayo uliitumia kwenye uandishi wako. Kama ulitumia tape basi bado ipo na ukiwa tayari tunaweza kukusaidia uiweke digital ili watu wote waweze kusikiliza. Vinginevyo, nakili sehemu tu ya hotuba ya Nyerere ambapo anasema kuwa hakumbuki Sykes alikuwa ni nani wakati wanajiunga TAA.

Mzigo wa ushahidi hauko kwa sisi tunaokupinga bali uko kwako wewe unayedai.

Je unayo hotuba ya Nyerere kuaga mwaka 1985 ikiwa katika format yoyote ile?
 
kwa hiyo nilikuwa naijua tanganyika african association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za taa. Sasa niliporudi, baada ya kukaa pugu siku chache, nikaja mjini dar es salaam. Nikauliza nani wanaongoza taa? nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa abdul sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Ndugu zangu nimekata kipande cha hiyo hotuba alipotajwa Abdulwahid Sykes.
Sasa shuhudieni mambo.

Mimi nilisema Nyerere kasahau cheo cha Abdu.
Mwanae kaleta ushahidi kuwa baba yake alikuwa hadhir.

Hakusahau cheo cha Abdu.
Sasa ni kweli abdu alikuwa ''katibu wakati huo?''

Soma hii hapo chini:

Nyerere mwenyewe kamwe hajazungumzia kuhusu uchaguzi huu au namna alivyokuja kuongoza taa dar es salaam. Kiasi cha karibu sana alichofika kumhusisha abdulwahid na historia yake kilikuwa katika ile hotuba ya kuwaaga wazee Dar es Salaam, na kwa bahati mbaya nyerere alipojaribu kumueleza Abdulwahid, alishindwa kwa kuwa kwa kauli yake alisema hakumbuki cheo alichokuwa akishika abdulwahid katika taa wakati yeye Nyerere alipojiunga na chama mwaka 1952. Hata hivyo gazeti la serikali, Daily News (6 Desemba 1985) [1] lilijaribu kurekebisha historia kwa kutaja cheo cha Abdulwahid, ingawa kwa makosa, kwa kusema kuwa nyerere alipojiunga na taa makao makuu abdulwahid alikuwa katibu. Ukweli ni kuwa Nyerere alimkuta Abdulwahid akiwa rais wa TAA.

(kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')

Sasa bwana Nyerere hatuna sababu ya kuandikia mate na wino upo. Sasa tupatie hotuba katika sauti tumalize huu ubishi.

Hapa ndipo unapoleta usanii. Baada ya kumtoa Clement Mtamila aliyekuwa Katibu Mkuu, plifanyika uchaguzi ambapo Dr. Vedasto Kyaruzi alichaguliwa kuwa Rais badala ya Mwalimu Thomas Plantan na Abdulwahid Sykes alichaguliwa kuwa KATIBU MKUU. Alichaguliwa kuwa Rais wa TAA mwaka 1952, mwaka ambao Mwalimu Nyerere alirejea. Kwa hali hiyo inawezekana kabisa kuwa Mwalimu alirejea kabla ya uchaguzi uliompa Abdulwahid Sykes urais. Hili bila shaka ulilijua lakini kama kawaida ukawa selective katika kumbukumbu zako.

Hotuba imewekwa. Sisi wengine tunaamini kuwa ni kweli. Nyinyi mnaodhani kuwa imechakachuliwa ndio mnaowajibika kutuwekea hiyo sauti au video mtubadilishe imani yetu.

Amandla........
 
Ritz,

Hakuna aliyepewa medali.

Ila siku ya pili Dossa Aziz aliitwa peke yake akapewa medali.

Kumbe aliwanyima wote hata wakatoliki wenzake! Sasa hizo shutma za udini unaingiaje humu? Hasa baada ya wewe mwenyewe kukiri kuwa aliwanyima WOTE ( wamisheni, waislamu, wahindu n.k.) lakini baadae akampa muislamu peke yake! Wenye haki ya kulalamika si sisi ambao tungependa wakina Kunambi, Kyaruzi, Mwanjisi na wengine wa enziwe?

Amandla......
 
Tulia ndugu yangu.
Tape inawekwa angalia post za wahusika.

Lakini kwa faida yako.
Hiyo "burden of proof" mie mzigo huo wa
nini?

Siko mahakamani sini.
Wala sitaki kumshinda mtu.
 
Kumbe aliwanyima wote hata wakatoliki wenzake! Sasa hizo shutma za udini unaingiaje humu? Hasa baada ya wewe mwenyewe kukiri kuwa aliwanyima WOTE ( wamisheni, waislamu, wahindu n.k.) lakini baadae akampa muislamu peke yake! Wenye haki ya kulalamika si sisi ambao tungependa wakina Kunambi, Kyaruzi, Mwanjisi na wengine wa enziwe?

Amandla......

Tarehe 27 Aprili, 1985 Nyerere alitoa jumla ya medali 3,979 kwenye sherehe kubwa katka viwanja vya Ikulu unajua aliowapa hizo medali.
 
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Alivyosema Nyerere

Nyerere mwenyewe kamwe hajazungumzia kuhusu uchaguzi huu au namna alivyokuja kuongoza taa dar es salaam. Kiasi cha karibu sana alichofika kumhusisha abdulwahid na historia yake kilikuwa katika ile hotuba ya kuwaaga wazee Dar es Salaam, na kwa bahati mbaya nyerere alipojaribu kumueleza Abdulwahid, alishindwa kwa kuwa kwa kauli yake alisema hakumbuki cheo alichokuwa akishika abdulwahid katika taa wakati yeye Nyerere alipojiunga na chama mwaka 1952. Hata hivyo gazeti la serikali, Daily News (6 Desemba 1985) [1] lilijaribu kurekebisha historia kwa kutaja cheo cha Abdulwahid, ingawa kwa makosa, kwa kusema kuwa nyerere alipojiunga na taa makao makuu abdulwahid alikuwa katibu. Ukweli ni kuwa Nyerere alimkuta Abdulwahid akiwa rais wa TAA.

Hapo juu ndivyo ulivyotaka kutudanganya.

Nyerere alijiunga na TAA akiwa Makerere. Aliyemvuta kuingia TAA ni mmisheni mwenzake na sio wazee wa Gerezani. Alipokuja Dar es Salaam alikuwa tayari mwanachama. Haiwezekani Nyerere alikuwa Katibu wa TAA Makerere na Milambo bila kuwa mwanachama. Kwa hiyo kudai kuwa Nyerere alijiunga na TAA alipokuja Dar ni uongo mtupu.

Sasa kama katika hiki kiduchu unataka kutupotosha kwa nini nikasome kitabu chako ambacho bila shaka kimejaa upotoshaji zaidi?

Usitufanye wote wajinga.

Amandla.......
 
tarehe 27 aprili, 1985 nyerere alitoa jumla ya medali 3,979 kwenye sherehe kubwa katka viwanja vya ikulu unajua aliowapa hizo medali.

hakuelewa huyoo,,
yan kaja kichwa kichwa pasi na hata kuingalia hoja imeanzia wapi,bora umemwekea ili kama inawezekana aanze kuchuttama sasa na kuficha aibu yake.
 
Tarehe 27 Aprili, 1985 Nyerere alitoa jumla ya medali 3,979 kwenye sherehe kubwa katka viwanja vya Ikulu unajua aliowapa hizo medali.

Ala, kumbe Mohamed ni muongo! Kuna wana harakati waliopewa medali? Tutajie basi umuumbue mzee wako.

Amandla........
 
Tulia ndugu yangu.
Tape inawekwa angalia post za wahusika.

Lakini kwa faida yako.
Hiyo "burden of proof" mie mzigo huo wa
nini?

Siko mahakamani sini.
Wala sitaki kumshinda mtu.

Bw. Said, Kyaruzi alipewa nishani lini na Nyerere?
John Rupia alipewa lini nishani na serikali?
Clement Mhando alipewa lini nishani?
Kirilo Japhet alipewa lini nishani na Nyerere?
 
hakuelewa huyoo,,
yan kaja kichwa kichwa pasi na hata kuingalia hoja imeanzia wapi,bora umemwekea ili kama inawezekana aanze kuchuttama sasa na kuficha aibu yake.

Kasema kitu kipi kipya? Au kwa vile muislamu mwenzio basi kila semalo unalishabikia?

Kweli debe tupu......

Amandla...
 
alivyosema nyerere



hapo juu ndivyo ulivyotaka kutudanganya.

Nyerere alijiunga na taa akiwa makerere. Aliyemvuta kuingia taa ni mmisheni mwenzake na sio wazee wa gerezani. Alipokuja dar es salaam alikuwa tayari mwanachama. Haiwezekani nyerere alikuwa katibu wa taa makerere na milambo bila kuwa mwanachama. Kwa hiyo kudai kuwa nyerere alijiunga na taa alipokuja dar ni uongo mtupu.

Sasa kama katika hiki kiduchu unataka kutupotosha kwa nini nikasome kitabu chako ambacho bila shaka kimejaa upotoshaji zaidi?

Usitufanye wote wajinga.

Amandla.......

sasa hapo kipi unachoshindwa kukielewa?mfano cmm ni chama kinachojipambanua ni cha ukombozi wa mtanzania,na wewe ulibahatika kwenda nje kimasomo,kufika huko masomoni ukaamua nawe na group la wenzako kuanzisha chama ili mje mlete ukombozi na unajaribu kufanya mawasiliano na nyumbani kisha huku nyumbani mbona kuna chama tayari chenye nguvu na kinachokubalika?kama vipi wewe fungua tawi tuh huko la chama hiki,nawewe ukafnya hivyo,unapomaliza masomo yako na kurudi nyumbani na ukawakuta wale ambao walikuambia ufungue tawi kipind uko masomoni na wakakuribisha kwenye chama rasmi,wewe utaweza chukua hoja ya kwamba wewe ni kingunge eti kisa ulianza harakati hizo hata kipindi uko nje ya nchi??inaingia akilini?
 
kasema kitu kipi kipya? Au kwa vile muislamu mwenzio basi kila semalo unalishabikia?

Kweli debe tupu......

Amandla...

mkiishiwa hoja huwa mnakimbilia huko,hakuna cha kushangaza katika hilo,naona sasa unaamua kupigana holy wars?
Crusade against jihadi??
Hiyo siyo mantiki ya mnakasha huu..
Ficha umu-lugo wako..
 
Haikuwa hivyo.
Mambo yalikwenda kama nilivyoandika kwenye kitabu.

Mambo hayawi kwa vile wewe umeyaandika; ukiandika kuwa Nyerere alizaliwa Buzuruga na tukasoma hivyo unadhani ndivyo inavyokuwa? Mambo yanakuwa jinsi yalivyotokea katika historia.

a. Umesema kwenye kitabu chako kuwa Nyerere aliianza siasa alipoingia Dar mwaka 1953 tukakuonesha si KWELI alianza siasa akiwa mwanafunzi Makerere - hujakubali unahamisha goli

b. Umesema Nyerere hakuwaenzi wazee wa Kiislamu waliomkaribisha Dar nilikuwekea sehemu ya maandishi yake ya mwaka 1966 alipokiri ukarimu wa pekee wa wazee wa Kiislamu; kwenye kitabu cha We Must Run While They Walk Nyerere anaeleza kwa kirefu hili - hujakubali unahamisha magoli

c. Umesema kuwa Nyerere alisahau Abdul alikuwa na cheo gani TAA wakati anajiunga ushahidi umewekwa na Nyerere anasema yeye aliporudi kutoka Uingereza Abdul alikuwa katibu wa TAA. Nyerere alikumbuka kwa usahihi kabisa hutaki unakataa - unahamisha magoli

d. Umedai kuwa ni Abdul Sykes ndye aliyemshawishi Nyerere kuacha ualimu Pugu na kuingia kwenye siasa; Nyerere amerudia toka zamani kabisa kuelezea kuwa ulikuwa ni uamuzi wake tangu akiwa Uingereza kuwa angerudi na kufundisha kwa miaka 3 na kuingia kwenye siasa na kweney sehemu ya hotuba hii inaonesha ni Nyerere aliyechukua initiative ya kutafuta uongozi wa TAA na baadaye akapelekwa kwa Sykes - na amekiri kuwa ni Sykes aliyekuwa maarufu kwa viongozi na jina alilopewa na yeye mwenyewe akaenda kule akipelekwa na Kasanga Tumbo mwalimu mwenzi - hutaki unakataa - unahamisha magoli

e. Umedai mara kwa mara Nyerere alikuwa na ubaguzi dhidi ya Waislamu; lakini kwenye kitabu chako mwenyewe (na aehemu ya hotuba hii inakubaliana nawe) Nyerere alishirikiana na wazee wa Kiislamu alienda kwenye matambiko ya Jadi na amekubali kusomewa Qurani na wazee wa Kiislamu na wewe mwenyewe unasimulia vizuri sana ile ibada ya kule Bagamoyo. Huyu mwenye chuki na Waislamu na Uislamu kweli kabisa ameenda na kuombewa na mashehe Mkristu akiwa peke yake! Leo umemuona nani kati ya viongozi wetu ambaye anaweza kufanya aliyoyafnaya Nyerere mbele ya watu wa dini nyingine? Kweli mwenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu anakubali kuombewa nao, kukaa nao, kula kwao, kulala kwao na kwenye kitabu chako unasimulia jinsi Waislamu walivyomlinda kule Mtwara wakati ameingia kanisani kusali! Hii chuki ya Nyerere dhidi ya Waislamu ilikuja lini?

e. Umeeleza kwenye histohisia yako kuwa kulikuwa na Kundi la Waislamu 'radicals" ambao walitaka kumuondoa Nyerere uongozi wa TANU kwa sababu ya Ukristu wake lakini hujasema hadi leo Nyerere alikuwa amefanya nini kuwaudhi wazee wako hawa wa Dar kutaka muondoa - tena mara mbili?
 
Asante sana Son of Alaska lakini kama uonavyo, wapo watakaodai hata video...hawajui hata mwaka kituo cha kwanza cha Television kilipofunguliwa nchini! Ritz tayari anadai aliwahi kuisikia lakini...hatuamini hata sisi tuliokuwapo na kuipata "live".
Mag3, Hotuba ile nilisikiliza na nakumba alisema “ ……hivyo ndivyo tulivyofanya……..kama hamtawaheshimu wazee na kuwasikiliza hamtafanikiwa.
hata kidogo!’’
Mkuu Maalim Mohamed Said, hotuba imewekwa kwa maandishi, neno kwa neno!.
"Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Sasa kama yalioandikwa yote ni kweli ndiyo yaliyotamkwa, then wewe kuitwa mchochezi sio kutukanwa bali huo ndio ukweli halisi wa "the motive behind" kitabu chako!.

Ila pia kwa sisi Waafrika tunaoamini imani za mizimu, kumsingizia marehemu kunaleta laana ya aina fulani, nakushauri utubu ungali hai ili kuiepushia "bad karma" familia yako utakayoiacha nyuma baada ya wewe kutangulia mbele ya haki, isije kuadhibiwa kwa makosa yako!. Huu ni ushauri tuu na only if you belive the universal law of "cause and effects", "karma" haina mswalie Mtume wala haina huruma kwa wasio na hatia!.
Pasco.
Pasco,ohamed Said alienda mabli na kusema eti katika hotuba ile Nyerere alitamka hamjui Abdul Sykes. Nadhani umma unaona ni kwanini wengine tumesimama kidete kuhakikisha umma haupotoshwi.

Lakini pia Mohamed lazima aelewe maneno ya Nyerere. Nyerere aliposema “ nikaambiwa naitwa na wazee, …..nikakutana na wazee,………wazee wakasema”
Maneno hayo yana maana sana ya kuwaheshimu wazee wa Dar. Laiti angesema nikakutana na Waislam basi kuna kitu watu wangehoji ambacho kingewadhalilisha wazee wale. Wanajamvi mnakijua kwa kusoma maneno ya Nyerere?
 
Panazidi utamu hapa.
Naipenda hii thread ila nimeona kua wengine wanatumia akili nakufikiria katika kujibu lakini wengine wanajibu kiushabiki tu.
Hao hata ukiwaambia jua linatoka mashariki watakuambia magharibi.
 
Back
Top Bottom