Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
generaly JAMII YA KIISLAMU IMEPUNGUKIWA UWEZO WA KUFIKIRI..
Nakushauri ungeanza kusoma kuanzia post ya kwanza ungejifunza mengi sana kuliko ulivyokurupuka kupost.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
generaly JAMII YA KIISLAMU IMEPUNGUKIWA UWEZO WA KUFIKIRI..
yapo wapi matusi? Unajua sheria za jf? Kama kuna mtu katukana mods wangeshamtendea haki yake.
Kejeli ni sehehemu ya burudani ya mnakasha.
generaly jamii ya kiislamu imepungukiwa uwezo wa kufikiri..
Mohamed Said,
Mwaka 1985 Nyerere alitoa jumla ya medali 3,979 kwa Watanzania waliochangia maendeleo ya Taifa.
Wazee wazalendo waliopigania uhuru walipewa wangapi medali.
kwa hiyo nilikuwa naijua tanganyika african association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za taa. Sasa niliporudi, baada ya kukaa pugu siku chache, nikaja mjini dar es salaam. Nikauliza nani wanaongoza taa? nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa abdul sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.
Ndugu zangu nimekata kipande cha hiyo hotuba alipotajwa Abdulwahid Sykes.
Sasa shuhudieni mambo.
Mimi nilisema Nyerere kasahau cheo cha Abdu.
Mwanae kaleta ushahidi kuwa baba yake alikuwa hadhir.
Hakusahau cheo cha Abdu.
Sasa ni kweli abdu alikuwa ''katibu wakati huo?''
Soma hii hapo chini:
Nyerere mwenyewe kamwe hajazungumzia kuhusu uchaguzi huu au namna alivyokuja kuongoza taa dar es salaam. Kiasi cha karibu sana alichofika kumhusisha abdulwahid na historia yake kilikuwa katika ile hotuba ya kuwaaga wazee Dar es Salaam, na kwa bahati mbaya nyerere alipojaribu kumueleza Abdulwahid, alishindwa kwa kuwa kwa kauli yake alisema hakumbuki cheo alichokuwa akishika abdulwahid katika taa wakati yeye Nyerere alipojiunga na chama mwaka 1952. Hata hivyo gazeti la serikali, Daily News (6 Desemba 1985) [1] lilijaribu kurekebisha historia kwa kutaja cheo cha Abdulwahid, ingawa kwa makosa, kwa kusema kuwa nyerere alipojiunga na taa makao makuu abdulwahid alikuwa katibu. Ukweli ni kuwa Nyerere alimkuta Abdulwahid akiwa rais wa TAA.
(kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
Sasa bwana Nyerere hatuna sababu ya kuandikia mate na wino upo. Sasa tupatie hotuba katika sauti tumalize huu ubishi.
Ritz,
Hakuna aliyepewa medali.
Ila siku ya pili Dossa Aziz aliitwa peke yake akapewa medali.
Kumbe aliwanyima wote hata wakatoliki wenzake! Sasa hizo shutma za udini unaingiaje humu? Hasa baada ya wewe mwenyewe kukiri kuwa aliwanyima WOTE ( wamisheni, waislamu, wahindu n.k.) lakini baadae akampa muislamu peke yake! Wenye haki ya kulalamika si sisi ambao tungependa wakina Kunambi, Kyaruzi, Mwanjisi na wengine wa enziwe?
Amandla......
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.
Nyerere mwenyewe kamwe hajazungumzia kuhusu uchaguzi huu au namna alivyokuja kuongoza taa dar es salaam. Kiasi cha karibu sana alichofika kumhusisha abdulwahid na historia yake kilikuwa katika ile hotuba ya kuwaaga wazee Dar es Salaam, na kwa bahati mbaya nyerere alipojaribu kumueleza Abdulwahid, alishindwa kwa kuwa kwa kauli yake alisema hakumbuki cheo alichokuwa akishika abdulwahid katika taa wakati yeye Nyerere alipojiunga na chama mwaka 1952. Hata hivyo gazeti la serikali, Daily News (6 Desemba 1985) [1] lilijaribu kurekebisha historia kwa kutaja cheo cha Abdulwahid, ingawa kwa makosa, kwa kusema kuwa nyerere alipojiunga na taa makao makuu abdulwahid alikuwa katibu. Ukweli ni kuwa Nyerere alimkuta Abdulwahid akiwa rais wa TAA.
tarehe 27 aprili, 1985 nyerere alitoa jumla ya medali 3,979 kwenye sherehe kubwa katka viwanja vya ikulu unajua aliowapa hizo medali.
Tarehe 27 Aprili, 1985 Nyerere alitoa jumla ya medali 3,979 kwenye sherehe kubwa katka viwanja vya Ikulu unajua aliowapa hizo medali.
Tulia ndugu yangu.
Tape inawekwa angalia post za wahusika.
Lakini kwa faida yako.
Hiyo "burden of proof" mie mzigo huo wa
nini?
Siko mahakamani sini.
Wala sitaki kumshinda mtu.
hakuelewa huyoo,,
yan kaja kichwa kichwa pasi na hata kuingalia hoja imeanzia wapi,bora umemwekea ili kama inawezekana aanze kuchuttama sasa na kuficha aibu yake.
alivyosema nyerere
hapo juu ndivyo ulivyotaka kutudanganya.
Nyerere alijiunga na taa akiwa makerere. Aliyemvuta kuingia taa ni mmisheni mwenzake na sio wazee wa gerezani. Alipokuja dar es salaam alikuwa tayari mwanachama. Haiwezekani nyerere alikuwa katibu wa taa makerere na milambo bila kuwa mwanachama. Kwa hiyo kudai kuwa nyerere alijiunga na taa alipokuja dar ni uongo mtupu.
Sasa kama katika hiki kiduchu unataka kutupotosha kwa nini nikasome kitabu chako ambacho bila shaka kimejaa upotoshaji zaidi?
Usitufanye wote wajinga.
Amandla.......
kasema kitu kipi kipya? Au kwa vile muislamu mwenzio basi kila semalo unalishabikia?
Kweli debe tupu......
Amandla...
Haikuwa hivyo.
Mambo yalikwenda kama nilivyoandika kwenye kitabu.
Mag3, Hotuba ile nilisikiliza na nakumba alisema hivyo ndivyo tulivyofanya ..kama hamtawaheshimu wazee na kuwasikiliza hamtafanikiwa.Asante sana Son of Alaska lakini kama uonavyo, wapo watakaodai hata video...hawajui hata mwaka kituo cha kwanza cha Television kilipofunguliwa nchini! Ritz tayari anadai aliwahi kuisikia lakini...hatuamini hata sisi tuliokuwapo na kuipata "live".
Pasco,ohamed Said alienda mabli na kusema eti katika hotuba ile Nyerere alitamka hamjui Abdul Sykes. Nadhani umma unaona ni kwanini wengine tumesimama kidete kuhakikisha umma haupotoshwi.Mkuu Maalim Mohamed Said, hotuba imewekwa kwa maandishi, neno kwa neno!.
"Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.
Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.
Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao wa TAA.
Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana cha matatizo.
Sasa kama yalioandikwa yote ni kweli ndiyo yaliyotamkwa, then wewe kuitwa mchochezi sio kutukanwa bali huo ndio ukweli halisi wa "the motive behind" kitabu chako!.
Ila pia kwa sisi Waafrika tunaoamini imani za mizimu, kumsingizia marehemu kunaleta laana ya aina fulani, nakushauri utubu ungali hai ili kuiepushia "bad karma" familia yako utakayoiacha nyuma baada ya wewe kutangulia mbele ya haki, isije kuadhibiwa kwa makosa yako!. Huu ni ushauri tuu na only if you belive the universal law of "cause and effects", "karma" haina mswalie Mtume wala haina huruma kwa wasio na hatia!.
Pasco.