Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Tunampango wa kuanza kuitumia TV Imani na Redio kuhamasisha uchangiaji wa vitu hivyo badala ya kuhubiri "Elimu Ahera" kwa sana maana sasa tuahitaji "Elimu Dunia" kuliko wakati wowote ule katika Historia yetu.
Na haya yatakuwa mafanikio makubwa.
Kwa hiyo kumbe mkiamua inawezekana!? Unaamini hii dhana ya kanisa kuwadhulumu waislam kama anavyosema mohamed said? Kama unaamini , inawezekanaje kanisa likashindwa kuwadhulumu waislam kwenye ujenzi wa kituo cha radio/television lakini liweze kwenye ujenzi wa vyuo?
 
Kuna Mabadiliko makubwa nayaona kutoka kwa Mzee Mohamed, kwenye ile minakasha miwili ya mwanzo, Mzee alikuwa hawezi kukubali lolote, lakini kwenye huu mjadala naona kuna upole na kuna kuadmit ukweli japo sio dhahiri lakini kwa wenye kumjua Mzee Mohamedi, tunaona shock na suprise ndani yake, kuna vitu hakuvitegemea kuwa watu wanavyo au wanavijua zaidi yake,
Tatizo lake liko palepale, sio kweli kama anatetea Wazee wote au Waislamu wote, yeye anatetea Wazee na waislamu wake wa Kariakoo, Wamanyema na Wanyamwezi (Majority), mwisho wa siku hata hao wanaomfuata watakuja kugundua Mzee Mohamed anasimamia nini, kama ilivyokuwa kwa FFox kwenye ule mnakasha wa Pili
Nikweli kabisa ndugu yangu, tulivyoanza mnakasha huu alikuwa na morali ya juu na ujasiri wa kujibu kwakujiamini bila kujua anaojadiliana nao wanajua zaidi yake!

Amrejee muumba wake na kuwaomba radhi watanzania na walimwengu kwa ujumla kwakuwachonganisha na kudhalilisha hadhi ya wanaukombozi wetu
 
Hili tatizo ni kubwa sana.hakuna suala gumu kulitatua kama suala lenye mizizi kihistoria.Mfumo wa maisha tunaoishi dunia ya leo kwa kiasi kikubwa ni kutoka kwa wazungu.waliokuwa wa mwisho kuitawala nchi yetu ni hao hao wazungu na hivyo waliacha jamii yetu ikiwa na mfumo wa maisha yao.wazungu hawa(wakoloni) walikuja na kuwakuta wazungu wenzao kutoka kanisani(wamishenari) waliokuwa wametangulia kuja wakiwa wameshaishika jamii kwa mashule ,hospitali na taasisi mbalimbali.mfumo wa wamishenari ulisababisha mfumo wa wakoloni waliopita(waarabu)kukosa nguvu.Hii ilisababisha utamaduni wao kuwa na influence kubwa ktk jamii yetu hata baada ya uhuru.Ni jambo la wazi kuwa kabla ya uhuru kanisa lilikuwa na nguvu kiasi kwamba hata wakoloni wenyewe walikuwa wakiomba msaada wa kanisa ktk mambo mbalimbali.Baada ya uhuru Nyerere alijikuta akiongoza serikali inayotegemea mambo mengi kwa kanisa.Akaamua kutaifisha mali za kanisa.wafadhili wa kanisa wakaacha kutuma misaada na nyerere akajikuta na majengo matupu.Hali ikawa mbaya,akawarudia maaskofu tena,ndipo likaja suala la MOU hapo!sasa tujiulize,wakristo wana kosa gani hapo?Mie naona tusizunguke sana,Hii MOU ambayo ndio chanzo cha malalamiko ya waislam kwa asilimia kubwa inapaswa kuvunjwa lakini kanisa lirudishiwe mali zake zote na kuendelea kuoperate kama independent entity.serikali ijipange upya na kuanzisha taasisi zake zitakazotosheleza watz wote ili kuua nguvu hii ya ukristo na uislam ambayo ndio inayoiyumbisha nchi.Iache kutegemea sana wakristo maana waislam wanalalamika na isije kutegemea waislam maana wakristo watalalamika,itegemee watanzania yenyewe ikiwa na sura halisi ya utanzania ktk utendaji wake.Vinginevyo malalamiko dhidi ya ukristo hayataisha maana mfumo wa wakristo kusaidiana na kusaidia wasio wakristo kwa kiwango cha kutishia ustawi wa dini nyingine hautaisha,ndio mfumo wao,ndio mfumo ulioijenga tz huko nyuma na ndio mfumo ulioijenga dunia ya leo!kuukwepa ni shughuli nzito maana inahitaji kuanzisha mfumo mbadala utakaokuwa superior kuliko huo na kukubalika na majority,utakaowafanya watz wajione watz na sio wakristo au waislam.WATANZANIA MNALIWEZA HILO?kama hamliwezi waacheni watu waendelee kubatizwa tu because that is the most influential system present and it saves our days. that tells a lot about it's influence!
 
Mzee Mohamed Said,
Umekwenda kutoa maoni yako kuhusu KATIBA MPYA ijayo? Mzee Warioba anapaswa akupe nafasi maalum kama wanayopewa viongozi wetu wa sasa na wastaafu. Leo nilimwona mzee wa vijisenti akiingia pale!

Katika hali ya kustaajabisha, utashangaa zaidi kusikia na kuona kuwa Mohamed Said hajatoa maoni na hatatoa maoni hayo kabisa!
 
Last edited by a moderator:
bwana mdogo acha hizo!
Kama wewe unamtegemea moh said kama source of knowledge basi hiyo ni juu yako. Usifikiri kuwa wote hapa ni vijana wadogo wanaosikiliza hizo simulizi kwa mara ya kwanza. Fyi, tumeisha pambana naye sana hapa katika miaka hii mitatu. Tafuta thread zake za nyuma, utatukuta. Halafu kuwa na adabu kidogo kama alivyo moh said kwenye mnakasha, vinginevyo nenda kacheze chandimu kama alivyokushauri nguruvi3.

bila shaka hili limekuchoma?
Muulize yericko,na mwombe akujibu,tumemuuliza kwanin anakuja na maneno ya kebehi??akajibu ya kwamba anamkejeli ndugu moh said kwa kuwa kejeli ni sehemu ya mnakasha..
Sasa mimi sitoi kejeli umeanza kupiga yowe la nini??
Mnasema sana,tukisema sisi mnasema tuna gubu..!
Basi kama ukweli huu mnaoambiwa umekuwa mchungu ni ruksa tuh kwenu kuutema.
 
hebu endelea mkuu, na mkapa aliurithi toka kwa nani?

mwambie yeye jasusi aendeleze hiyo series mwisho tutafikia tamati tuh.
Kama anamchukia kikwete kwa sababu ya ufisadi,tumuulize vema sasa,ufisadi umeanzia kwa kikwete ama kwa mkapa?madudu haya tumeanza kuyaona kwa mkapa,
sasa anamchukia kikwete pekeake na mkapa anamwacha ili hali lao ni moja ni haki?
Kikwete = fisadi,
mkapa = fisadi,
kikwete = muslim,
mkapa = christian,
by using calculus to differentiate or to intergrate kikwete with respect to mkapa in the case of ufisadi utapata jibu??,,dy dx utapata jibu la aina gani??
Utakuja kuona mkapa na kikwete kumbe wote ni mafisadi,ila hamchukii mkapa kwa kuwa ni mkristu mwenzake na amesema anamchukia kikwete kwa sababu kuu moja tuh,nayo ni uislamu wake.
Hence proved..!!
 
mwambie yeye jasusi aendeleze hiyo series mwisho tutafikia tamati tuh.
Kama anamchukia kikwete kwa sababu ya ufisadi,tumuulize vema sasa,ufisadi umeanzia kwa kikwete ama kwa mkapa?madudu haya tumeanza kuyaona kwa mkapa,
sasa anamchukia kikwete pekeake na mkapa anamwacha ili hali lao ni moja ni haki?
Kikwete = fisadi,
mkapa = fisadi,
kikwete = muslim,
mkapa = christian,
by using calculus to differentiate or to intergrate kikwete with respect to mkapa in the case of ufisadi utapata jibu??,,dy dx utapata jibu la aina gani??
Utakuja kuona mkapa na kikwete kumbe wote ni mafisadi,ila hamchukii mkapa kwa kuwa ni mkristu mwenzake na amesema anamchukia kikwete kwa sababu kuu moja tuh,nayo ni uislamu wake.
Hence proved..!!


Blame never affirms, it assaults.

Blame never restores, it wounds.

Blame never solves, it complicates.

Blame never unites, it separates.

Blame never smiles, it frowns.

Blame never forgives, it rejects.

Blame never forgets, it remembers.

Blame never builds, it destroys.
 
blame never affirms, it assaults.

Blame never restores, it wounds.

Blame never solves, it complicates.

Blame never unites, it separates.

Blame never smiles, it frowns.

Blame never forgives, it rejects.

Blame never forgets, it remembers.

Blame never builds, it destroys.

so what??
Mbona ngonjera nyingi sasa.
 
mjadala umepoa sana!
kwa sababu tunasubiri 'hotuba' ya nyerere kwa njia ya sauti
tuliahidiwa tangu jana kwamba itawekwa lakini kimya mpaka sasa
nimepata tetesi anatafutwa kijana mmoja anaitwa steve nyerere,
huyu ni mzuri sana wa kuiga sauti ya marehemu nyerere.
kama akipatikana,itakuwa rahisi hiyo 'hotuba kuwekwa hapa ukumbini.
Hii ni ahadi ya pili ambayo mpaka sasa haijatekelezwa.
Ya kwanza ni ile iliyoahidiwa na ndugu anayedai ni 'mtoto' wa marehemu nyerere, Yericko Nyerere,
kwamba ataweka majina ya waasi waliosamehewa na nyerere na kupewa vyeo na ubalozi.
Ahadi zote hazijatekelezwa
Njia ya muongo ni fupi sana,
tunaendelea kusubiri,tutaendelea kukumbusha
cc Barubaru THE BIG SHOW mv butiama rizt kichwakigumu
 
Last edited by a moderator:
mjadala umepoa sana!
kwa sababu tunasubiri 'hotuba' ya nyerere kwa njia ya sauti
tuliahidiwa tangu jana kwamba itawekwa lakini kimya mpaka sasa
nimepata tetesi anatafutwa kijana mmoja anaitwa steve nyerere,
huyu ni mzuri sana wa kuiga sauti ya marehemu nyerere.
kama akipatikana,itakuwa rahisi hiyo 'hotuba kuwekwa hapa ukumbini.
Hii ni ahadi ya pili ambayo mpaka sasa haijatekelezwa.
Ya kwanza ni ile iliyoahidiwa na ndugu anayedai ni 'mtoto' wa marehemu nyerere, Yericko Nyerere,
kwamba ataweka majina ya waasi waliosamehewa na nyerere na kupewa vyeo na ubalozi.
Ahadi zote hazijatekelezwa
Njia ya muongo ni fupi sana,
tunaendelea kusubiri,tutaendelea kukumbusha
cc Barubaru THE BIG SHOW mv butiama rizt kichwakigumu

Ndugu yangu nakuomba uweke adabu mbele tunapojadiliana hapa!

Mmemdhalilisha Mwalimu mkakwama na sasa mnageukia kwangu?

Tumia mda mwngi kurudia yale yote tuliyojadili tangu post ya kwanza yatakufunza na kupevuka kimwili kiakili na kiroho mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Na alikuwa katibu wa tawi la AA Tabora kwa mujibu wa kitabu cha Mohamed Said. AA ilianza kabla ya TAAMohamed akasema wameachwa wajifie na kuzikana wenyewe, mwaka 2012 Dr V.Kyaruzi amefariki sijui kama Kikwete alihudhuria! Mzee wa watu naye alijifia kama alivyojifia A.Sykes. Kikwete naye kama Nyerere ni dhalimu kwa mantiki hiyo!Tena eti Nyerere aliyasema mbele ya wazee wa Dar es salaam!
Kasema Nyerere alikuwa anaogopa kupoteza kazi alizopewa na kanisa. Lakini leo tunajua kuwa alinza kulikaidi ''kanisa'' na ukoloni akiwa Makerere, Mwalimu Tabora, Edimburgh na Pugu kabla hajafundishwa kula chapati na kuvaa suruali kariakoo.Tena tumefahamu kuwa si wazee wa kiislam hata wasiokuwa na imani nao walimfanyia tambiko, ushahidi kuwa kupigania uhuru ilikuwa kero ya kila mmoja wetu.Hajawahi kutaja jina hata moja la 'radical' lakini anamtuhumu Nyerere kumuondoa Sheikh Amir. Unless atutajie ma-radical tutabaki kuamini kuwa Sheikh Amir ndiye kiongozi wao na kwanini Nyerere amvumilie hata baada ya kupata uhuru? Majaribio mawili hivi mohamed alitaka yafanyike mangapi ili uungwana wa Nyerere uonekane? Tutajie radicals Mohamed kama hawapo withdraw hiyo statement kwasababu utakuwa uzushi.

hapa hachomoki
 
Mkuu hapa Mohamed hana nafasi yakupata uzima wa milele, sisi tudajitahidi kwa kazi moja tu ya kuwarudisha kundini wale waliopotoshwa na Mzee Mohamed Said kwa ngano zake!

asante mimi ni mmoja wapo mmeniokoa kutoka kwenye histohisia.. Nilitekwa na ngano zake mnamo 14/12/12 kwenye kumbukumbu ya mwl nyerere kupitia kupindi cha "mwangaza wa jamii" radio imaan; hakika nilimuona mwl nyerere na sisi wakristo ni wabaya sana.

Nashukuru mnakasha huu umenifungua macho;
 
Mohamed Said,

..kuhusu "somo la Bakwata," naona umejinukuu mwenyewe.

..unapofanya hivyo tena na tena unakuwa umekiuka maadili ya mnakasha wa kisomi.

..mimi ningeshauri unukuu waandishi independent ambao wanakubaliana na mtizamo wako.

..au, unaweza kutuwekea nyaraka ambazo unaamini zinathibitisha conclusions zako ili na sisi tuweze kujiridhisha.

..mwisho nakuomba utuletee kitabu cha John Sivalon na Van Bergen, itapendeza kama uki-quote zile chapters ambazo unaamini zinahakiki/zinathibitisha madai yako ili na sisi tuweze kujiridhisha.

cc: THE BIG SHOW, Jasusi, Yericko Nyerere, Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
asante mimi ni mmoja wapo mmeniokoa kutoka kwenye histohisia.. Nilitekwa na ngano zake mnamo 14/12/12 kwenye kumbukumbu ya mwl nyerere kupitia kupindi cha "mwangaza wa jamii" radio imaan; hakika nilimuona mwl nyerere na sisi wakristo ni wabaya sana.

Nashukuru mnakasha huu umenifungua macho;

Asante sana mkuu, hiyo ni habari njema sana ndugu yangu!
 
Back
Top Bottom