Ritz,
swali lako kuhusu majina ya waasisi wa TANU na pia wanachama 20 wa kwanza wa TANU per post number 2971, majibu yangu ni kama ifuatavyo:
- J.K Nyerere territorial president
- Germano Pacha kanda ya magharibi
- Kirilo Japhet Kanda ya Kaskazini
- Joseph Kimalando Kanda ya Kaskazini
- C. Milinga Kanda ya mashariki
- A . Iranga Kanda ya Ziwa
- L. Bagohe Kanda ya Ziwa
- S. Kandoro Kanda ya Ziwa
- Kisungutwa Gabara Kanda ya Ziwa
- S. Kitwana Kanda ya Ziwa
- Tewa Said Tewa Kanda ya Mashariki
- D. Azizi Kanda ya Mashariki
- A. W Sykes Kanda ya Mashariki
- A. K. Sykes Kanda ya mashariki
- G Kunambi Kanda ya Mashariki
- J Kasessa Kanda ya Mashariki
- John Rupia Kanda ya Mashariki.
Hawa ndio walikuwa ni waasisi wa TANU kwa mujibu wa historia ya taifa letu, wajumbe wa mkutano mkuu wa TAA 1954 uliozaa TANU, na wanachama kumi na saba wa kwanza wa TANU; Wengine waliofuatia katika kundi hili ni pamoja na Paul Bomani na wengine ambao wengi wao waliunda baraza la kwanza la mawaziri la serikali ya TANU;
Wanachama wengine wengi walifuatia baadae lakini wa mwanzo walitokea Dar-es-salaam, Tabora, Tarime, Singida na Mara Kaskazini. Sina majina yao.