Leo tunawajuwa wazee wa Kiislaam walivyokuwa mstari wa mbele kupigania Uhuru, kupigania haki zao za msingi, walivyo asisi vyama vya kujiunganisha pamoja watetee maslahi yao iwe vya anasa au vya siasa tokea 1920s, lengo lake ndio muhimu.
Leo tunajuwa kuwa Nyerere alikaribishwa na hawa wazee, akala nao, akalala nao, majumbani mwao, ashaakum si matusi, wakamuenzi na hata kumfulia nguo zake kwa dhanna yao ya kuwa ni Mwaafrika mwenzao tena msomi hatokuwa na madhara kwao wala kwa dini yao, walifanya yote kwa nia safi kabisa kudhani kuwa watakuwa nae bega kwa bega.
Matokeo yake ni kusahau yote, hajui hata aliyemkaribisha kwake, pamoja na wazee wake na mke wake. Hivi Kariakoo ya miaka hiyo, ufunguwe duka la mafuta ya taa mtaa wa Mchikichi, hata Kiswahili vizuri hujui utakuwa huna msaada uliopewa na wenyeji? akafuliwa nguo zake na mama'ke Abdul Sykes, akila nae chakula chake, akamjulisha kwa wazee wake, akamuenzi kwa hali na mali, na wazee hawakurudi nyuma wakijuwa wamepata msomi mwenye muono, mwenye kujuwa kuongea, mwenye busara, oohh oohhh oooohh.
Matokeo yake tunayaona leo kwa macho yetu, tunayasoma yalivyoandikwa na Mohamed Said, tunahakikisha ni ya ukweli. Aaaah huyo ndie Nyerere.
Wanakuja humu na kejeli na viroja, leo hii hata wao wanawajuwa hao wazee waliompokea Nyerere, isingekuwa Mohamed Said wangewajuwa?? kwa historia ipi? Inashangza sana, badala ya wao kuona kuwa wameletewa upande wa historia waliokuwa hawaujuwi na watoe sifa kwa Mohamed Said wao wamekazania kulalama na hoja zisizo na msingi wala mshiko. Wanachotetea ni nini? hakijulikani.
Hakuna mpaka sasa, hata mmoja aliyekuja akasema Mshume ni wa kutunga, Said Tewa hakuwepo, EAMWS haikuwepo, Abdul Skes hakumkaribisha Nyerere. Mashado Plantan si kweli. Mama Maria hakuuza mafuta ya taa Mchikichi, Iddi Tosiri ni wa kubuni hakuwepo mtu namna hiyo. TAA haikuanzishwa na wazee wa Dar. AA haikuanzishwa na Kleist Sykes. Mweka hazina wa kwanza wa TANU hakuwa mweka hazina wa Jammiatul Islamiya fi Tanganyika nayo haikuanzishwa na Sykes
Jamani, hivi mnachobisha haswaa ni nini? tarehe fulani? siku fulani? kavaa nguo gani? hakulitumikia kanisa?
Rudini muisome hii historia kwa muono wenye manufaa, kwenu na kwa wenzenu. Itawafunguwa katika ubaguzi wa ujinga mliojifunga nao. Hakika mioyo yenu ina maradhi.