Hii posting ya Yericko Nyerere bado sijaisoma,naona imepata hits nyingi sana. Kuhusu udini wa Mwalimu,Mwalimu alikuwa anaamini sana katika dini, na mtu akiamini katika didi ina maana kwamba anaamini dini yoyote,kwamba dini ndio inaweza mumuongoza mtu katika maisha yake.
Kwa mfano Yesu Kristu, Kristu siyo jina lake. Hali ya ukristu ni hali ya utakaso,hali ya mtu kuishi kufuata maadili ya Mungu,hali ambayo kila Mkristu anatakiwa kuwa nayo,kuifikia..Katika dini ya Budha pia. Ingawa Budha anaitwa Budha,lakini Budha,kama Kristu,maana yake ni mtu aliyetukuka,na kila muumini anatakiwa kuwa Budha. Lakini ndio hivyo,Kristu anaitwa Kristu na Budha anaitwa Budha.
Dini ya kweli inafundisha tu ntu aishi kufuata maadili ya Mwenyezi Mungu,pia awe na jicho la kumtambua mtu anayeishi kufuatana na maadili mema,amtambue kwamba yule ni ndugu yake katika roho,Brotherhood of Light. Yaani kwenda across religious beliefs,kwenda beyond any beliefs, na kumtambua mtu mstaarabu unapomuona.
Vinginevyo utakuwa tu unasema Waislamu ni adui zako,wakati wakristu ndio wamekupiga kabali wamekunyang'anya fedha.