Tatizo likawa moja: Akina Sykes na wazee wake Mohamed walipigania uhuru wetu hapohapo mitaani kwao. Wengi wao, kama sio wote, hatukuwasikia kwenda bara kusaka uhuru wetu, kuwaunganisha WaTanganyika, wakazidiwa kete hata na mwanamke, Bibi Titi Mohamed!
WC,
Ondoa tu lugha hizo za ''kuzidiwa kete,'' zitatuondolea majadala wa watu makini.
Usinitazame mimi.
Tuna wasikizaji 80,000 plus wametutegea masikio.
Tuwape heshima zao.
Umesema kweli kuwa Abdulwahid hakupanda jukwaani kuhutubia wala hakuonekana
kokote katika majimbo.
Abdu Sykes, Hamza Mwapachu, Dr Michael Lugazia na wengine wengi hawakutoka
New Street kwenda Masasi, Newala na kwingineko kupambana na Kanisa liwaruhusu
Wakristo wajiuge na TANU.
Huko walikwenda Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani.
Na huko kusini wakaungana na akina Salum Mpunga, Shariffa bint Mzee, Sheikh Yusuf
Badi, Yusuf Chembera, Suleiman Masudi Mnonji na wengineo wengi.
Lakini ukweli ni kuwa Abdu Sykes na mdogo wake Ally, Dossa na Rupia ndiyo ''party
financiers'' wawezeshaji wa mengi katika harakati.
Sasa ikiwa unataka kumlenga Abdu peke yake na umjue hayo ni mengine.
Yapo mengi yaliyofanyika hadi kufikia pale TANU inaundwa na ni historia iliyoanza nyuma
sana toka miaka ya 1920s.