Peleka ushirikina wako kwa wajinga wenzako! karne hii bado unashindwa kuelezea mambo kisayansi, bado umeng'ang'a na ushirikiana! aibu.
Nakuuliza, na kwa kunywa kikombe cha Babu sio Ushirikina?
[h=1]MREMA ATUA LOLIONDO KUIMARISHA AFYA YAKE[/h]
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Augustine Mrema.
MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema, ametinga Loliondo kwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Mwasapile kunywa dawa na kutamba ni kwa ajili ya kuongeza nguvu ya mwili kupambana na ufisadi.
Mrema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), alisema jukumu alilokabidhiwa kuzunguka nchi nzima ni kubwa linalohitaji kuimarisha afya yake.
Kazi niliyokabidhiwa ni kubwa, kuzunguka nchi nzima kupambana na ufisadi kunahitaji kuimarisha afya yangu, alisema Mrema na kuongeza:
Bila kuimarisha afya huwezi kufanya kazi hii niliyokabidhiwa, waeleze Watanzania kuwa nimeimarisha afya sasa nikupambana na mafisadi kwenye halmashauri nchini kwa kwenda mbele.
Alisema Watanzania wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuwashushia Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile (76), kwa sababu hawatumii gharama kubwa zaidi ya 500.
Kama angekuwa Marekani tungeenda kwa Sh500? dawa yake haina kuchakachua unakunywa. Dawa nimekunywa na nimerudi na picha nimepiga naye alisema Mrema kwa kujiamini.
Hata hivyo, Mrema hakubainisha magonjwa yanayomsumbua hadi kwenda kwa Mchungaji Mwasapile, ingawa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu.
Mchungaji, Mwasapila juzi alipongeza uamuzi wa Serikali kuondoa tishio la kuzuia kutoa dawa kwani watu wengi wamekuwa wakinufaika na dawa na mahitaji yanaendelea kuwa makubwa.
Tunamshukuru Waziri William Lukuvi kwa kuruhusu dawa iendelee kutolewa na kutoa ahadi ya kuleta huduma mbalimbali muhimu katika kijiji hiki, alisema Mchungaji Mwasapile.
Chakula, malazi
Mmoja wa wasaidizi wa mchungaji huyo, Peter Dudui alisema jana kuwa kuanza kupatikana hudumu muhimu katika eneo hilo kama chakula, vyoo na mahala pa kulala kumechangia kupunguza wimbi la vifo vya wagonjwa.
Sasa vifo hakuna, wagonjwa wanaokuja wanapata huduma kama chakula na maji na pia wanapata mahali pa kulala. Ingawa sehemu za kulala ni chache zinasaidia sana, alisema Dudui.
Tamko hilo lilitolewa wakati ambapo tayari kulikuwepo na tetetsi kwamba Serikali imekusudia kumsimamisha Mchungaji huyo hadi hapo uchunguzi maalumu wa kitaalamu utakapofanywa kwa dawa yake.
Msururu mirefu ya magari yanayotoka Arusha mjini kuelekea katika kijiji hicho ambacho sasa kinaiitwa 'Kijiji cha Babu', jana ilionekana katika barabara ya Arusha hadi Ngorongoro.
Walioshuhudia msafara huo mrefu walisema kitu kibaya walichoshuhudia kwenye msafara huo ni madereva walombele kutoruhusu wenzao wanaookuja nyuma yao kwa kasi kutokana na kila mmoja kujaribu kuwahi kufika kabla ya mwingine kunywa dawa.
Baadhi ya watu walioshuhudia misafara hiyo, walisema ni vigumu madereva kuwaruhusu wenzao wanaokuja nyuma kwa hofu ya kuchelewa kwenye foleni ya dawa.
CHANZO: MWANANCHI MACHI 14, 2011