Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Son of Alaska, huyu mwalimu wa Spike Lee na wenzake angekuwa hakwepi maswali huu mjadala haungefika hapa ulipofikia ila subiri atakavyojaribu kukwepa au "spin" atakazozileta! Hata hivyo nampa hint kidogo tu kuhusu miaka hiyo;

  • Wazaramo ambao idadi yao ilikuwa kubwa, makazi yao ya nyumba za makuti yalikuwa nje kidogo ya City Center kama Buguruni, Tabata na Ubungo.
  • Washomvi waliweka makazi yao Kunduchi na Msasani.
  • Wasukuma waliweka makazi Msasani na Magogoni.
  • Wanyamwezi (idadi yao pia haikuwa ndogo) makazi yao yalikuwa Kindondoni na Bonde la Msimbazi.
  • Wangoni walijikita Keko na Kijitonyama.
Swali langu kwa Mohamed Said ni kuwa wazee wake (wazulu na Manyema) makazi yao yalikuwa wapi? Hapa naongelea mara tu baada ya Tanganyika kutwaliwa na Uingereza kwenye 1920s. Sasa namwomba asiwanyime wanafunzi wake akina Spike Lee fursa ya kufyonza ilmu, awaambie wazee wake waliishi mitaa ipi...hilo tu. Tukumbuke kuwa idadi ya wakaazi wote wa Dar es Salaam wakati huo ilikuwa haifiki 20,000!

Mag3,
Sasa umehamia mipango miji?
JF ina majambo.

Siasa basi.
 
MM,

Huo ni muhali mkubwa sana.
Siwezi hata kidogo kula haram kwa kuwa nayajua madhara yake.

Haram inaathir hadi fikra na hulka za mlaji.
Kwahiyo kamwe siwezi kuigusa.

Achilia mbali hayo makubwa.

Mathalan nina chakula halal kabisa mfano wa kamba, pweza na majongoo ya pwani.
Kwangu mimi hivi vitoweo na delicacy na ukienda Kempisky bei yake ni kali.

Kuna makabila vyakula vya pwani vinawapa shida na mimi najua leo nimemkaribisha
chakuka sahib wangu ambae vyakula hivi haviwezi basi sitavileta mezani ingawa ni halal.
na yeye anaweza akavikwepa akala kitoweo kingine.

Huu ndiyo ustaarabu waliotufunza wazee wetu na ndiyo Uislam khasa.
Sembuse iwe chakula ni haram vipi nitakula hata nikiwa peke yangu?

Shekh Mohamed,

nilikuwa namjibu Mzee Mwanakijiji kama ifuatavyo!

Mwanakijiji alisema hivi:

By Mzee Mwanakijiji
Siyo kwa sababu za kidini bali najua naweza kufikiwa na wageni marafiki zangu Waislamu hivyo sitaki kuwalisha haramu.

Ndipo na mimi nikamjibu hivi:Ndugu, Mzee M,

Jee, ukiwa hauko ktk maeneo yenye rafiki zako Waislamu huwa unakula haramu?

nadhani umenielewa Shekh maana nimeona umejibu mlo halali wa Mzee Mwanakijiji hula pale akiwa na Waislamu na mimi kumuuliza jee, wakati mwingine hula Haramu?

 
Shekh Mohamed,

nilikuwa namjibu Mzee Mwanakijiji kama ifuatavyo!

Mwanakijiji alisema hivi:

By Mzee Mwanakijiji
Siyo kwa sababu za kidini bali najua naweza kufikiwa na wageni marafiki zangu Waislamu hivyo sitaki kuwalisha haramu.

Ndipo na mimi nikamjibu hivi:Ndugu, Mzee M,

Jee, ukiwa hauko ktk maeneo yenye rafiki zako Waislamu huwa unakula haramu?

nadhani umenielewa Shekh maana nimeona umejibu mlo halali wa Mzee Mwanakijiji hula pale akiwa na Waislamu na mimi kumuuliza jee, wakati mwingine hula Haramu?


TK,

Nimekupata.
Ahsante.
 
Mzee Said, hupiganii dhulma iondoke; unatengeneza dhulma nyingine. Qurani inaenda mbali zaidi kwani haiishi kusema hivyo unadai. Inasema pia: Wa Jazā'u Sayyi'atin Sayyi'atun Mithluhā ۖ Faman `Afā Wa 'Aşlaĥa Fa'ajruhu `Alá Al-Lahi ۚ 'Innahu Lā Yuĥibbu Až-Žālimīna (42:40). Ni bora kupatanisha (suluhu) kuliko kulipiza kisasi. Mzee Said umefanya nini ili kuziletea jumuiya zetu hizi mbili pamoja katika kupatanisha? Ni lini umejaribu kukaa na viongozi wa Kikristu au kuwashawisi mashehe kukaa na viongozi wa Kikristu kuyaangalia madai yako? Ni lini umejaribu kutumia majukwaa unayopata kuzungumza lugha ya suluhu na upatano badala ya lugha ya utengano, kisasi na kupasha moto hisia za watu?

Mzee Said iheshimu dini yako na uwe mkweli kwa taifa lako. Usijitahidi kubomoa jaribu kujenga. Wazee wetu walifanya mema kwa pamoja, walishirikiana kwa umoja, na katika changamoto nyingi wametupatia taifa hili tulilonalo. Kwanini leo mwenzetu unajitahidi kututenganisha kwa kupotosha historia? Kwanini leo mwenzetu unaandika historia ya "Wazalendo Waislamu waliosahaulika" badala ya kuandika juu ya "Wazalendo waliosahaulika"? Of course najua jibu lako - hao wakristu siyo wazee wako! Wewe ulitaka kuandika wazee wako - Waislamu tu.

Mola akusaidie kuona dhulma unayoifanya kwa jina la kupinga dhulma. Mzee Said uondoa uovu kwa wema Qurani inasema: Adfa` Bi-Atī Hiya 'Aĥsanu As-Sayyi'ata ۚ Naĥnu 'A`lamu Bimā Yaşifūna (23:96). Ulipe uovu kwa wema; umeona dhulma mzee Said tuoneshhe katika kutenda mema. Qurani haisemi upinge tu dhulma lakini vile vile utende hisani na wema; kwa ndugu, wazazi, jirani, n.k

Mzee Said ukiona watu wanatumia Uislamu kuchoma makanisa uwe wa kwanza kulaani siyo kutafuta udhuru wa kwanini wamefanya hivyo; ukiona watu wanafanya ubaya kwa jina la Uislamu dhidi ya ndugu zao uwe wa kwanza kukataa uovu uovu huo. Vinginevyo, wewe mwenyewe unaonekana ni sehemu ya kutetea uovu huo na kuuchochea kwa jina la kupinga dhulma. HIyo siyo dini.
Katika kujadiliana fanya heshima.Usiwe unazungumzia mambo usiyo na elimu nayo.Tafsiri ya hiyo aya ni hivi
وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ إِنَّهُ لا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ
Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.
Hapo kilichoanzwa kulipa uovu kwa uovu.Halafu ndio ikafuatiwa na kusamehe.
Hivyo kulipa uovu kwa uovu ni bora zaidi ili kukomesha dhulma.Lakini ni kweli kuwa ukisamehe utalipwa na Mwenyezi Mungu.
Jukumu la kulipiza na kusamehe ni la mtu au watu binafsi.Ikiwa ni hivyo kwa tabia za kibinadamu kusamehe kunakuja kwa yule aliyekukosea kidogo na kwa bahati mbaya.
Wewe hufahamu lakini wengine waangalie kwamba uovu wa Nyerere kwa waliomkaribisha kwenye siasa na kwa waislamu ni mkubwa sana.Kwa vipi atasamehewa na kila mmoja wao.Wako waliomsamehe na watalipwa lakini kwa baadhi yetu na hatuna makosa. Hapana !.Sio yeye tu ambaye alifanya kwa kusukumwa na imani yake bali hata Kikwete anayefanya kwa kuwahofu nyinyi na kutii amri za mataifa ya nje naye hasameheki.
Unadhani kila tunachojenga nyinyi mkisaidiwa na Kikwete,Mkapa mnabomoa tutasamehe mara ngapi?.Katika hali ya kuacha dhulma iendelee na kuendelea kusamehe basi kuna ufafanuzi mwengine kuonesha kuwa hiyo ni dhambi pia.
Kuhusu aya ya 23:96 huo ulikuwa ni wito uliomuhusu zaidi Mtume S.A.W ambapo Allah alimuahidi ulinzi na kuahidi kuwashughulikia mwenyewe wabaya wa Mtume wake.Aya ya juu inatuhusu sisi sote ambao tuna jukumu la kujikurubisha kwa Allah S.W kwa kutekeleza kulingana na mafunzo yake.
 
Sina haramu ya kidini; nikitaka kupata kiti moto naenda wanakouza nakula kwa raha zangu. Nyumbani sipiki wala sinunui kuleta.

Kwa kuwa sisi ni ndugu si vibaya nikikushauri uache kula kiti moto kwa sababu zifuatazo:

Rosemary Alvarez alijikuta akiwa na maumivu ya kichwa na mkono kukosa nguvu. baada ya kufanyiwa scanning ikaoneka kama ni "brain tumor", pindi alipofanyiwa upasuaji alikutwa na "mnyoo (taenia solium)" akiwa hai unakula brain yake. Chanzo hasa cha mnyoo huo ni kula kiti moto ambayo kitaalamu ana protein nyingi kuliko mnyama yoyote na hivyo kuvutia parasite wengi kwa mnyama huyu . Je ni watanzania wangapi wanapata uangalizi wa kugundua afya zao na wanakula nyama hii kila siku tena inayofugwa katika mazingira si salama?. soma zaidi kwenye link hii hapa chini

Source : ABC News: It's Not a Tumor, It's a Brain Worm

Angalia hapa Mchina huyu pia akitolewa minyoo mingi usoni ambayo pia ilisababishwa na utamaduni wa kula Kiti Moto:

Worm inside your face - YouTube

Ndugu yetu, mwenzetu, Mwanakijiji unaonaje uache kula nyama hiyo na badala ake ule halali za kila aina! we unajua zaidi si ni Mwanakijiji?
 
Z,

Kwa darsa hiyo wenyewe mipango miji.
Swali langu kwa Mohamed Said ni kuwa wazee wake (wazulu na Manyema) makazi yao yalikuwa wapi? Hapa naongelea mara tu baada ya Tanganyika kutwaliwa na Uingereza kwenye 1920s. Sasa namwomba asiwanyime wanafunzi wake akina Spike Lee fursa ya kufyonza ilmu, awaambie wazee wake waliishi mitaa ipi...hilo tu. Tukumbuke kuwa idadi ya wakaazi wote wa Dar es Salaam wakati huo ilikuwa haifiki 20,000!
kama hilo linahusu mipango miji ni kwanini basi unapenda mipango miji ya gerezani tu ndo itambulike katika harakati za uhuru?
 
Al shabab ni extreme. Taliban ni extreme. Osama bin Laden alikuwa extreme. Rashid Kawawa alikuwa moderate.

Hapa naona tofauti ni majina ya watu wa nchi tofauti! Kawawa Mtanzania na Osama Msaudi na Taliban watawala wa zamani Afgani!
bado hamjajibu swali langu! tofauti ya Muslim moderate na extreme ni nini?
 
Nimeandika historia sikuandika mipango miji.
nafikiri tuishie hapo,
vinginevyo kilichoulizwa na Mag3 hakina uhusiano wowote na mipango miji,
kuulizwa ulipokuwa unaishi na nduguzo au wamanyema walipokuwa wanaishi havina uhusiano na mipango miji,
kuulizwa kwanini jina la mtaa liliitwa new street sio mipango miji, ni siasa na historia, mipango miji hawahusiani na kupanga majina ya mitaa.
 
SHIA na SUNNI wanachinjana IRAQ,PAKISTAN etc etc

Kabla Wazungu kuvamia Iraki na Pakistani ulisikia kuna vita vya kimadhehebu huko? yanayotokea Iraki na Pakistani ni uchochezi wa Wazungu! wanalipua na kuuwa watu huku wakidai ni vita kati ya Sunni na Shia! Zanzibar mapadri wanashambuliwa lakini mtuhumiwa ni magaidi! huku bara wanauliwa Mapadri, albino na kushambuliwa waandishi wa habari lakini wahusika ni Majambazi na wenye Imani za Kichawi!
Unaona Kizungumkuti hicho!
 

kwanini hujiulizi kwanini siku kuu ya IDD inasherekewa kiholela,mwaka jana nilifaidi IDD mara mbili nasafiri nakuta idd wakati nilipotoka ilikuwa jana yake
.

Mbona Urusi Krismasi haisherehekewi 25 december? Wakristo wa Dhehebu la Koptic pia hawali Krismas na Noeli tarehe hizo? Lakini unashangaa Waislamu kugawanyika kula Idi siku tofauti! na kuna ubaya gani hata wakila siku 3? mbona Nyinyi mnaanza Kula Krismasi tangu tarehe 20.december watu wanaanza Kusafiri na kurudi ni mpaka Januari 3! huku ni kufisadi nchi na kurudisha maendeleo ya nchi nyuma!
 
Kwa hiyo haya mauaji wapo sawa kutoa roho za watu.Vipi mauaji ya Joseph Koni Uganda?

Vita vya Wakatoliki wa Nodhern Ireland na WaLuteri wa England vilivyotoa roho za Watu hajui hilo? Vipi na Wakristo wa Kiserbia miaka ya 90 hawakuuwa Maelfu ya Waislamu wa Bosnia na vita baina yao na Wakristo wenzao wa Croesia amesahau mara hii? nadhani inatosha tusiharibu mnakasha wa Jericko Nyerere na Mohamed Saidi! wasitutoe ktk mstari!
 
Ami,

Asichojua Nyambala ni kuwa Prof. Haroub mimi ni ndugu yangu na
mazungumzo yetu hayakuwa na pazia hata kidogo.

Alipokuja kufahamu mchango wa Abdu Sykes katika kuunda TANU
alikuwa kama mtu aliyepagawa kwa kuwa alikuwa anajua hatari ya
habari ile na uzito wake.

Alikwenda kwa Ahmed Rashad Ali kuuliza zaidi.
Huko ndiko alipopata wazimu.

Mzee Rashad akamwambia mimi na Abdu tulikwenda pamoja kumuona
Kenyatta mwaka 1950.

Lakini kubwa lililomshtusha ni zile siasa za Nyerere, Kanisa na Waislam.
Vitu hivi vilimnyima raha sana.

Kuna mengi Ami mimi siwezi kuyasema kwani unasema na kubakiza.

Katika msiba wa Abdu Sykes watu wa protocal walimkalisha Nyerere jamvi
moja na Ahmed Rashad Ali na wakati wa kutoa sadaka ulipowadia Rashad
alikula pilau sinia moja na Nyerere mkono kwa mkono.

Shekh MS,

Habari hii ya Profesa H.Othman kupata mshtuko hata na mimi nimeingiwa na wasiwasi kuhusu kifo chake! jee, alikufa kifo cha kawaida, ama aliugua muda mrefu au kilikuwa kifo cha kutatanisha?
 
Mkuu gazeti la kwanza liliandikwa kijerumani, kuna kipande cha picha yake nimekiweka hapa, 1911 linaitwa USAMBARA lilichapwa Lushoto, (nimeshangaa babu yangu aliishia darasa la 4 lakini anajua kijerumani balaa.
Wewe msambaa kweli akili zako ni zero.
Nilikua nafuatilia post zako kwa muda mwingi nikaona kwamba huprovide chochote bali ushabiki tu.

Wenzio wanaongelea gazeti la mtanganyika wewe unaongelea gazeti la mjerumani?
Tena wajerumani waliokua wanawatemea mate watoto wa kisambaa pale Dochi /Deutch ambapo ni chuo cha mahakama sasa.
Kawaulize mababu zako kuhusu wajerumani huko Usambara.
 
Kuna Waislam hivi sasa wako mahakamani na wako rumande Segerea.

Ni vijana wadogo walikamatwa wakitoka msikitini Ijumaa mbili zilizopita.

Wanashtakiwa kwa kosa la kuandamana.
Vijana wanamuuliza hakimu nini maandamano.

Hakimu akaeleza.

Vijana wakazema hapo tulipokamatiwa sisi wala hapakuwa na maandamano
ila tuliona watu wakiwakamata waliovaa kanzu na mimi nilikuwa nimevaa kanzu.

Ndio maana tunaona una matatizo.. kweli kabisa unaamini watu wenye kuvaa kanzu wanakamatwa!


Kosa langu ni hilo lakini sikuwa naandamana na maandamano yenyewe hayakuwapo.

Hhivi umewahi kukutana na mhalifu ambaye anakubali kuwa kafanya uhalifu? Au kwa vile hawa vijana ni wa "Kiislamu" basi unawapa benefit of the doubt?

Wajerumani Vita Vya Pili Vya Dunia wanawapiga na kuwatesa Wayahudi kisha wanawauliza
hivi mnajuakwa nini tunakupigeni?

Tunajisikia raha tukikupigeni.
Hapa ndipo tulipoifikisha Tanzania.

Angalia sasa! Yaani unathubutu hata kwa mbali kusema walichofanyiwa Wahayudi na Hitler ni sawa na unayoamini yanatokea Tanzania? Really? Kweli we mzee unapenda shari kweli!


Kuonekana na alama za Uislam unahatarisha maisha yako si njiani hata shule, vyuoni na makazini.
Katika hali kama hii nani wa kuonewa huruma?

Yaani kanzu sasa imekuwa "alama za Uislamu"? HIvi ni Waislamu wangapi wanavaa mavazi hayo na hawaulizwi lolote? Kama kweli unaamini hili mlalamikie Kikwete basi, Bilal, Othman na Mwema - wote hawa ni Waislamu na uwaambie kwanini wanawadhulumu Waislamu wenzao.

Mzee Said ulikofika kiakili huwezi kurudi; unaona dhulma kila mahali, unahisi uadui kila upitapo, na ukikutana na Mtu mwenye jina la Kiislamu katiwa pingu wazo lako la kwanza inaonekana ni kuhisi kafanyiwa vile kwa sababu ni Muislamu! Hatuna jinsi ya kukusaidia kwa kweli... Sikutana kukupyschoanalyze you lakini sasa nadhani itabidi nifanye hivyo...
 
Shekh MS,

Habari hii ya Profesa H.Othman kupata mshtuko hata na mimi nimeingiwa na wasiwasi kuhusu kifo chake! jee, alikufa kifo cha kawaida, ama aliugua muda mrefu au kilikuwa kifo cha kutatanisha?

TK,

Kifo kilikuwa cha ghafla.
Allah ndiye mjuzi.
 
Katika msiba wa Abdu Sykes watu wa protocal walimkalisha Nyerere jamvi
moja na Ahmed Rashad Ali na wakati wa kutoa sadaka ulipowadia Rashad
alikula pilau sinia moja na Nyerere mkono kwa mkono.

Kwanini walimkalisha na Dhwaalim? au hawakujua Nyerere ndiye alikuwa adui mkubwa wa Waislamu?
 
Ndio maana tunaona una matatizo.. kweli kabisa unaamini watu wenye kuvaa kanzu wanakamatwa!




Hhivi umewahi kukutana na mhalifu ambaye anakubali kuwa kafanya uhalifu? Au kwa vile hawa vijana ni wa "Kiislamu" basi unawapa benefit of the doubt?



Angalia sasa! Yaani unathubutu hata kwa mbali kusema walichofanyiwa Wahayudi na Hitler ni sawa na unayoamini yanatokea Tanzania? Really? Kweli we mzee unapenda shari kweli!




Yaani kanzu sasa imekuwa "alama za Uislamu"? HIvi ni Waislamu wangapi wanavaa mavazi hayo na hawaulizwi lolote? Kama kweli unaamini hili mlalamikie Kikwete basi, Bilal, Othman na Mwema - wote hawa ni Waislamu na uwaambie kwanini wanawadhulumu Waislamu wenzao.

Mzee Said ulikofika kiakili huwezi kurudi; unaona dhulma kila mahali, unahisi uadui kila upitapo, na ukikutana na Mtu mwenye jina la Kiislamu katiwa pingu wazo lako la kwanza inaonekana ni kuhisi kafanyiwa vile kwa sababu ni Muislamu! Hatuna jinsi ya kukusaidia kwa kweli... Sikutana kukupyschoanalyze you lakini sasa nadhani itabidi nifanye hivyo...

MM,

Waulize Wayahudi walokuwa Poland na wale walopita na kupona
Autshwitz.

Wewe una luxury ya kukaa huko uliko nyuma ya lap top ukafanya
hiyo psychoanalyis yako.

Sisi ni ndugu zetu ndiyo yanawakuta haya.
Tunakijua tunachosema.

Mimi si mjinga ukaja na hicho kibri chako.
Luambano alisema uongo Yesu katukanwa Mtambani.

Serikali ikaua Waislam Mwembechai.
Serikali ilipojua imedanganywa ishachelewa.

Maalim Matar kawekwa kizuizini kwa tuhuma za kupindua serikali.
Walomjua Maalim Matar walipigwa na butwaa kwani Matar hakuwa
anaishi dunia hii.

Kiasi ukimuuliza leo tarehe ngapi atakupa kalenda ya Kiislam.
Hakuwa nasi kabisa.

Fanya tahadhar unapozungumza na mimi kwa hisani yako.
Wewe wa kunisaidia mie.

Kuwa na adabu.
 
Back
Top Bottom