Mzee Mohamed Saidi, maneno yako haya yananikumbusha kisa cha zamani;
Mtu mmoja alikuwa na tabia ya kutamba kwamba yeye ni mbabe aliyeshindikana, ikaja siku kakumbana na mbabe kumzidi yeye, wakaanza pambano, watu wakajaa kushuhudia pambano, kila mbabe mwenye majivuno alivyozidiwa ndivyo watazamaji waliongezeka kushuhudia pambano.
Ongezeko la watazamaji lilimfanya mbabe mwenyemajivuno kuongeza makelele ya kujisifu badala ya kupambana, alizidiwa kabisa na baadae kuwaamru watazamaji wamshike na kumuondoa uliongoni mpinzani wake amasivyo angemtoa roho! watazamaji waliduwaa kwani wakutolewa roho alikuwa yeye anayepiga makelele!
.......