Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Unaamini kweli ilikuwa ni 'historia rasmi ya wapigania uhuru'. Nani kakuambia kuwa historia ni lazima iwe rasmi ili iwe history?
😛layball:..................:frusty:

:rockon:....................

:high5: :high5::high5:......................

:nono: :nono: :nono::nono::nono::nono::nono:
 
Unaamini kweli ilikuwa ni 'historia rasmi ya wapigania uhuru'. Nani kakuambia kuwa historia ni lazima iwe rasmi ili iwe history?

Mzee MM nikwamba haya yaliyoandikwa huku na mzee MS huyaoni au ni kwamba unamakengeza si dhumuni langu kukueleza hivyo ila unachosha, ngoja nikupe kisa kimoja cha huyu jamaa ndio utapata akili ya kuelewa , huyu jamaa alikuwa ana makengeza na kasuku wake ana makengeza sasa jamaa akawa anamuweka kasaku wake kwenye banda kutokana na yale makengeza akajua kamuweka ndani kumbe kamuweka nje na kasuku na makengeza yake akakimbilia ndani.CCNGURUVI3,MAG3,JASUSI
 
  • Thanks
Reactions: Ami
Unaamini kweli ilikuwa ni 'historia rasmi ya wapigania uhuru'. Nani kakuambia kuwa historia ni lazima iwe rasmi ili iwe history?
Nyerere aliasisi TANU. Kama walikuwepo wengine hiyo ni sawa tu. Lakini sikubali kuwa Nyerere hakuasisi. Chama kimezaliwa 7.7.1954, Rais wa kwanza wa chama asiwe muasisi? Doesn't make sense!
Kuwa wengi walikuwa waislam, ninakubali kuwa wanaharakati hao HASA WA PWANI, wengi wao walikuwa na majina ya kiislam. Sina uhakika sana na uislam wao. Mimi binafsi nina ndugu zangu wapagani ambao wana majina ya kiislam na wengine ya kikristo.

Uchochezi wa Moh Said utauona ukipitia thread hii toka mwanzo, bila jicho la udini. Ningekusaidia ku-extract points zetu zinazomuonesha kuwa ni mchochezi. Bahati mbaya natumia simu.

😛layball:..................:frusty:

:rockon:....................

:high5: :high5::high5:......................

:nono: :nono: :nono::nono::nono::nono::nono::nono:

:A S angel::A S angel:
 
Mijadala mingi niliyoishuhudia ambayo inaendeshwa kwa hisia za kidini ni ngumu watu kufikia muafaka na hii ni kwasababu kila upande huvutia kwake na kujiona kuwa ni bora zaidi kuliko upande mwingine. So naendelea kufuatili inawezekana huu ndo ukawa mjadala wa kwanza kwangu mimi kuushuhudia wadau wakifikia Muafaka.
 
Mzee MM nikwamba haya yaliyoandikwa huku na mzee MS huyaoni au ni kwamba unamakengeza si dhumuni langu kukueleza hivyo ila unachosha, ngoja nikupe kisa kimoja cha huyu jamaa ndio utapata akili ya kuelewa , huyu jamaa alikuwa ana makengeza na kasuku wake ana makengeza sasa jamaa akawa anamuweka kasaku wake kwenye banda kutokana na yale makengeza akajua kamuweka ndani kumbe kamuweka nje na kasuku na makengeza yake akakimbilia ndani.CCNGURUVI3,MAG3,JASUSI

Nimeyasoma maandishi ya MS sana na kama nilivyoonesha sehemu nyingine; ni maandisi yasiyo na msingi katika ukweli. Yanatumia historia kutengeneza hisia zake. Yote yalianza baada ya kufeki utafiti wa WARSHA ambao ulitengeneza kwa mara ya kwanza "dhulma" dhidi ya Waislamu. Bahati mbaya sana kama ilivyokuwepo mwaka 1981 leo hii lipo kundi la watu ambao wanaamini masimulizi hhaya ya MS na wenzake bila kujiuliza kama yana ukweli. Watu huwa wanachojali ni kuwa masimulizi yanasikika kama ni kweli. Hawaulizi ushahidi wa kisayansi na badala yake wamekuwa wakiburuzwa kwa porojo na masimulizi matamu matamu.

Mzee Said mchango wake mkubwa ni kutukumbusha kuwa yatupasa tuwakumbuke mashujaa wetu mbalimbali. HIli tunaweza kulifanya bila kulazimika kumkandia, kumtusi au kumdunisa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
 
Kuna kitu kimoja ambacho wanaolia "dhulma" wanadhani Watanzania hawakijui sana. Wakati wa Nyerere kama kuna kitu kilikuwa kinapigwa vita sana ni kile alichokiita "undugunization" yaani kwa neno la kimombo "nepotism". Tafsiri moja ya nepotism inasema ni "patronage bestowed or favoritism shown on the basis of family relationship, as in business and politics".

Sasa undugunization ulianza kwa kasi baada ya kuanza kuwa na kada ya watumishi wa umma wasomi ambao wameanza kushika nafasi. Kwa kiasi wale waliopata nafasi kidogo walianza kuwaingiza wana familia wao kwenye hizo ajira. Kama Baba alikuwa meneja wa Benki basi mtoto wake akigraduate naye anatafutiwa kazi benki; hii ilikuwa kweli kwenye polisi, na ilikuwa kweli kwenye ajira nyingi sana. Na kwa kadiri watu walivyozidi kupata nafasi za juu ndivyo nao walivyozidi kuwaingiza ndugu zao kwenye ajira na hawakufungwa na ofisi zao kwani waliweza kuwaunganisha na marafiki zao kwenye kada nyingine. Hivyo, mtu anaweza kuwa yuko Ikulu lakini mtoto au jamaa yake akaunganishwa kupata kazi Benki Kuu, au taasisi nyingine.

Lakini hili halikuishia tena kwenye undugu wa damu likawa limeingia hata kwenye undugu wa "kijiji kimoja"; ambapo hapa utakuta watu ambao wanatoka kijiji kimoja (hata kabila moja) wanadai undugu na kuombeana msaada. Hivyo, mtoto atatoka Tarime na kwenda kwa 'mjomba' Arusha ambaye ni afisa wa JWTZ ambaye atamtafuta kazi kujiunga na jeshi. Matokeo yake utakuta watu wa kabila moja nao wakiwa wamejazana sehemu fulani.

Huu undugunization ndio kwa kiasi kikubwa sana umekithiri na sijui kama kuna Mtanzania ambaye hana ndugu au jamaa aliyenufaika na kumfahamu mtu fulani. Lakini katika maana yake pana zaidi huu 'undugunization' ulifika hadi kwa marafiki. Watu waliosoma pamoja wanasaidiana na marafiki wanapeana nafasi na hata kwa watoto wao. Kwa mfano, mtu ambaye ni Mkristu mwenye tafiki Muislamu anaweza kuombwa na rafiki yake kumtafutia "binti" yake ajira na akafanya hivyo. Yule binti ataingia kwenye ajira na hakuna mtu ataweza kuona upendeleo kwa sababu aliyeingia ni Muislamu na kaingizwa na Mkristu (au kinyume chake).

Hili unaliona hata kwenye teuzi mbalimbali. Mtu Muislamu anaweza akamteua mtu Mkristu ambaye anaweza asiwe na uwezo sana lakini watu wasione "upendeleo" kwa sababu wamefungwa na kuangalia dini tu. Ukiniuliza mimi kitu kinachowanyima watu nafasi kuendelea katika ajira siyo "dini" hasa bali 'undugu" ambapo pamoja na nepotism sasa kuna 'cronyism' yaani 'thepracticeoffavoringone'sclosefriends,especiallyinpoliticalappointments.'

Mfano mzuri sana wa haya mawili ni nafasi za ajira kule BoT ambao tuliona majina ya watoto wa vigogo yakijazana na kupeana nafasi mbalimbali. Sidhani kama kuna mtu anaweza akasema wale walipewa upendeleo kwa sababu ya dini zao. Na hivi karibuni tumeona pia kwenye viwanja vilivyouzwa kule Kigamboni ambapo wanasiasa na watumishi wakubwa serikalini wamepewa viwanja hivyo kwa kufahamiana na wahusika.

Ukisikia ngano basi ndiyo hiyo hapo juu.
Jibu la ngano ya Mwanakijiji lipo kwenye paragraph chache alizozinakili Mohammed Said katika kitabu chake kama hivi
Kwenye kitabu cha Developement and religion in Tanzaia cha Bergen uk365 alimnukuu mwalimu Nyerere akisema
" I am a layman but I try to do what I can and will not go against my own church.I want to give the church a better chance here.Tell the bishops that I have established in TANU a department of political education and have put a Lutheran minister in charge;he was not a greater politician. I selected him because of his strong faith"

Sasa hiyo ngano yako Mwanakijiji ya udugunization imeanzaje?.
:violin::violin:

:kev:

:kev:
 
Kwa hiyo wewe ulitaka Waislamu wasome ktk shule hizo ili wale vyakula haramu! na kama unakubali vyakula vilikuwa haramu kwanini Shule inaruhusu kupikwa chakula haramu? halali imekuwa bidhaa adimu?

Mimi kwa mtazamo wangu naona sio vyema kupika chakula ambacho kitaathiri imani ya mwengine kwa namna moja ama nyingine, lakini katika kufanya maamuzi juu ya hili suala, huwezi kumzuia mwanao asiende kupata elimu kisa tu umuepushe na vyakula haramu.

Fanya ulinganishi wa hili suala, ELIMU VS NGURUWE. Kwa upande wangu ningeenda kusoma hata kama kuna hatari ya kula haramu, kwa maana ya kawaida kabisa naweza kusema, sina lengo na nia ya huo uharamu, bali nina nia na lengo la kuelimika na kupata maarifa, lakini kwenye kufanikisha hili, ndio kuna hizo changamoto za kula haramu.

Hayati Mwl. Nyerere hakuwa na imani juu ya mambo ya KUTAMBIKA, lakini wote tumeona kwenye histora alikubali kufanya hivyo alivyokuwa Bagamoyo, kwa lengo na nia ya kuwa na MSHIKAMANO na wazee wale, na alifanikiwa.
 
Sijawahi kuona Mzazi alie very flexible kama wewe! uko tayari kumruhusu mwanao apate elimu hata kama atadhurika kiafya!

Rosemary Alvarez alijikuta akiwa na maumivu ya kichwa na mkono kukosa nguvu. baada ya kufanyiwa scanning ikaoneka kama ni "brain tumor", pindi alipofanyiwa upasuaji alikutwa na "mnyoo (taenia solium)" akiwa hai unakula brain yake. Chanzo hasa cha mnyoo huo ni kula nyama ya nguruwe ambayo kitaalamu anaprotein nyingi kuliko mnyama yoyote na hivyo kuvutia parasite wengi kwa mnyama huyu.
Source : ABC News: It's Not a Tumor, It's a Brain Worm

Angalia hapa Mchina huyu pia akitolewa minyoo mingi usoni ambayo pia ilisababishwa na utamaduni wa kula nyama ya nguruwe:Worm inside your face - YouTube

Elimu hiyo itamsaidia nini mwanangu ikiwa atapata madhara ya kiafya? halafu usidhani Mungu kaharamisha Nguruwe kwa sababu za kiimani! la! kuna sababu za madhara kiafya!
 
Unaamini kweli ilikuwa ni 'historia rasmi ya wapigania uhuru'. Nani kakuambia kuwa historia ni lazima iwe rasmi ili iwe history?

Kitabu cha historia ya wapigania uhuru cha Kivukoni kinachomtaja Nyerere kuwa ndie muasisi wa TAA na TANU na mpigania uhuru wa Tanganyika unakikanusha kuwa sio historia rasmi! sasa historia rasmi iko wapi? uko mbioni kuiandika kama ulivyoombwa na Mohamed Saidi? Kitabu cha MS umekiita HISTOHISIA na cha Kivukoni nacho hukitambui! sikuelewi!
 
110183042.jpg
police.png
 
Ndugu yangu unaonyesha wazi kuwa kitabu cha Historia ya TANU kilichoandikwa na chuo cha Kivukoni hujakisoma kabisa, na zaidi kitabu cha ngano za Mohamed Said nacho hujakisoma,

Hakuna katika Kitabu cha Kivukoni kinapoeleza kuwa Mwalimu Julius Nyerere ni MUASISI wa TAA,

Hata hotuba yake hapo juu inajieleza wazu kuwa TAA aliikuta ikiwa chini ya Katibu mkuu wake Abdul Sykes,

Soma tena vitabu husika ndugu yangu.
 
Kitabu cha historia ya wapigania uhuru cha Kivukoni kinachomtaja Nyerere kuwa ndie muasisi wa TAA na TANU na mpigania uhuru wa Tanganyika unakikanusha kuwa sio historia rasmi! sasa historia rasmi iko wapi? uko mbioni kuiandika kama ulivyoombwa na Mohamed Saidi? Kitabu cha MS umekiita HISTOHISIA na cha Kivukoni nacho hukitambui! sikuelewi!
Hakuna kitu kama historia rasmi. Hakuna mwenye monopoly ya ukweli katika historia. Historia ni uwanja mpana ambako utafiti mara nyingi hugundua vitu ambavyo havikufahamika awali. Kivukoni waliandika chao, Mohamed ameandika chake. Na wewe pia tumia akili zako.
 
Mijadala mingi niliyoishuhudia ambayo inaendeshwa kwa hisia za kidini ni ngumu watu kufikia muafaka na hii ni kwasababu kila upande huvutia kwake na kujiona kuwa ni bora zaidi kuliko upande mwingine. So naendelea kufuatili inawezekana huu ndo ukawa mjadala wa kwanza kwangu mimi kuushuhudia wadau wakifikia Muafaka.
Huu utaisha tena kwakushinda vita kati ya wema na ubaya,

Na kwa halihalisi uzi husika tu hapo juu tayari tumeshawashinda hawa wachochezi
 
Huu utaisha tena kwakushinda vita kati ya wema na ubaya,

Na kwa halihalisi uzi husika tu hapo juu tayari tumeshawashinda hawa wachochezi
Kuna vitu vingi sana ambavyo Nyerere hakukanusha. Yaani mlitaka wakati wote kunapotokea kitabu Nyerere akanushe hadharani? Angefanya kazi yake saa ngapi? Unakumbuka alivyowajibu waandishi habari wa Kenya wakati mmoja kuhusu kuzaa na mama zao? Alitaka watumie akili zao. Nyerere hakujibu madai ya Kambona kuhusu kuwa na fedha katika benki ya Uswiss. Aliyejibu ni Amir Jamal katika interview niliyofanya naye wakati huo natumikia shirika moja la redio ya kimataifa.
Hayo ya kumhoji Amir Jamali ni yako wewe ila Nyerere alihojiwa na waandishi baada ya shutuma za Kambona kusikika nchi nzima! siku hiyo mimi nilihudhuria mkutano wa Kambona Jangwani mwaka 1992 na alipomtaja Nyerere, Kawawa na Amir Jamal kuwa wameweka mamilioni ya dola Uswissi, kulikuwa na mtafaruku na hasira toka kwa Wananchi kusikia kashfa hiyo hasa kumhusu Mwalimu!

wananchi waliwalaani hao viongozi waliotajwa kwa ufisadi na niliona kwa macho yangu na baadae Nyerere alipohojiwa na waandishi kuhusu ufisadi huo, alicheka na kusema kama ni yeye hajali kuhusishwa na utajiri huo, ila anasikitika kutajwa Rashidi ambae umasikini wake anaujua ndani nje!

Jasusi,
Wewe ulikuwa nje ya nchi ukitumikia shirika la kimataifa! mimi nilikuwa nchini na kuhudhuria mkutano huo wa Kambona ambapo ktk mkutano huo Kambona aliambatana na mkewe Flora na kabla ya kuanza hotuba yake Kambona aliwataja na kuwaenzi wapigania uhuru wote waliotajwa na Mohamed Saidi!
Nashindwa kuelewa kwanini mnapinga kila kitu! ukitaka kuthibitisha haya nenda ofisi za Mwananchi, Majira, Uhuru, Daily News na Annur utapata kumbukumbu hizi!
Kumbuka Nyerere akijibu shutuma hiyo alikuwa hana wadhifa wowote ndani ya chama wala Serikali sasa dai lako la kuwa alikuwa bussy na asingeweza kujibu kila hoja halina msingi!

:A S shade: :A S shade: :A S shade:
 
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُواْ سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ
Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini (Qur2:06)
خَتَمَ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ وَعَلَى سَمْعِهِمْ وَعَلَى أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. (Qur2:07)

JEURI YA FIRAUNI ILIVYOSHINDWA

Firauni alitakabari na kujitangazia uungu.Kwa hofu ya kutokea mtu mwengine kuupinga uungu wake akawa anawachinja watoto wote wa kiume waliozaliwa kwenye nchi ya Misri.Kwa hekima za Mwenyezi Mungu hakuweza kumchinja Mussa (A.S) na bila kujua akamlea ndani ya nyumba yake.
Musa (A.S) alikuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyepewa miujiza.Miujiza yake mikubwa ilikuwa kwenye fimbo yake.Akapewa amri aende yeye na nduguye Haruna kwa Firauni wakampe khabari za kuwepo Mwenyezi Mungu aliye mkuu na muumba wa kila kitu.Hii ikawa mwanzo wa ugomvi wake na Musa (a.s).Miujiza ya Musa (a.s) akaita ni uchawi tu.Ikiwa ni uchawi yeye aliamini ana wachawi wakubwa zaidi na wengi.
Upatu ukapigwa kote mjini watu waje uwanjani kushuhudia uchawi wa Musa (a.s) utakavyopondwa pondwa na kumaliza madai yake ya utume.Wachawi wa Firauni wakakusanywa na kualikana.Siku ilipofika Firauni akakaa kwenye kiti chake cha enzi kushuhudia pambano baina ya Musa a.s dhidi ya wachawi wa Firauni.
Uwanja ulikuwa umejaa kweli hata pa kutia mguu hakuna.Wachawi wa Firauni wakaanza pambano kwa kutupa fimbo zao zilizogeuka nyoka wa kutisha.Zamu ya Musa a.s ilipofika akatupa fimbo yake ikageuka joka kubwa likameza wale nyoka wote wa wachawi wa Firauni.
Wachawi hapo hapo wakageuka kuwa waumini wa Musa a.s..Firauni akafedheheka kwa kushindwa kuthibitisha kuwa Musa a,s ni mchawi.
Akahamaki na kuwaambiwa wachawi wake kwanini wamemuamini Mus a.s kabla ya idhini yake.Wachawi wakajibu IMANI KWA MWENYEZI MUNGU HAIHITAJI IDHINI KUTOKA KWA YEYOTE.
ukweli waliouona kwa macho yao unatosha.
Mwenye kujua kiarabu angalia VIDEO HAPA

Mambo Murua sana haya..

Akhsante Sana...
 
Kitabu cha historia ya wapigania uhuru cha Kivukoni kinachomtaja Nyerere kuwa ndie muasisi wa TAA na TANU na mpigania uhuru wa Tanganyika unakikanusha kuwa sio historia rasmi!

Kweli unaamini hicho kitabu kinasema hivyo; au unaamini kwa sababu MS kasema kitabu kinasema hivyo?
 
Kweli unaamini hicho kitabu kinasema hivyo; au unaamini kwa sababu MS kasema kitabu kinasema hivyo?
Unaamini kweli ilikuwa ni 'historia rasmi ya wapigania uhuru'. Nani kakuambia kuwa historia ni lazima iwe rasmi ili iwe history?
Una uhakika alikanusha au unafikiria alikanusha; mtawapata hawa wadogo na watoto zetu na hii historia mpya.
Umejuaje kama Nyerere alisema hicho anachodaiwa kusema kwenye kitabu cha Bergen?
 
Huu utaisha tena kwakushinda vita kati ya wema na ubaya,

Na kwa halihalisi uzi husika tu hapo juu tayari tumeshawashinda hawa wachochezi

Naendelea kufuatilia mkuu kuona mwisho wake na nilikuwa sijajua kama ni vita kati ya wema na ubaya so naendelea kufuatilia ili niweze kutambua upande gani ni wema na upande gani ni ubaya.
 
Back
Top Bottom