Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ritz inabidi sasa tukusaidie wewe kufikiri vizuri ndugu yangu. Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mwaka 1988 lakini Rais alikuwa ni Ali Hassan Mwinyi na serikali yake. Ukisoma hapa Mohammed Said anasema kuwa uamuzi wa kuondoa gazeti lililokuwa na makala yake ulifanywa na CCM (agizo la Mwenyekiti). Na anasema lilitekelezwa na mtu wa CCM - Kiwanuka na kuwa licha ya Kiwanuka kukusanya makala hizo na kuzichoma moto Kiwanuka huyo huyo aliandika makala kumjibu Mzee Said, sawa. Stori imenoga kwa wanaopenda stori; lakini kwa mtu ambaye chembe za Ubongo zinafanya kazi maswali kadhaa yako wazi:

a. CCM haijawai kuwa na mamlaka ya kuzuia kitabu au andiko bila serikali; yaani serkali inatekeleza mapendekezo ya chama. Kumbuka kuwa kama ilivyokuwa mwaka 1988 ndivyo ilivyo sasa; sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ndiyo iliyokuwa ikitumika. MTu pekee ambaye anaruhusiwa kuondoa gazeti au kufungia gazeti ni Waziri wa Habari na mamlaka yake ni ya mwisho (hata mahakamani huwezi kupinga). Sasa, ni Wazirri gani aliyetoa agizo hilo?

b. Tukiachilia hilo la a tujiulize Kiwanuka alikuwa anatekeleza agizo la nani? Kama alikuwa anatekeleza agizo la Nyerere, itabidi ajieleze alipewa na Nyerere wapi? Kama alitekeleza matakwa yake kama afisa mahusiano wa chama je ni lazima Nyerere awe anajua au aliomba baraka? Mtu pekee wa kujibu hili ni Kiwanuka.

c. Lakini kama Kiwanuka alikuwa anatekeleza jambo lililokubaliwa na serikali basi mtu ambaye anapaswa kujua ni Rais Mwinyi ambaye alikuwa kwenye madaraka. JE Mwinyi alitoa agizo hilo? Mtu wa kujibu hili ni Mwinyi, umemsikia Mohammed kaenda kumuuliza?

d. Lakini cha kushangaza na sijui kama umekiona; Mohammed Said huyu huyu anatuambia toleo linalofuatia Kiwanuka aliandika makala kumjibu. Sasa, kama gazeti limepigwa marufuku Tanzania na hakuna wa kulisoma Kiwanuka alikuwa anamuandikia nani?

Naona unakurupuka kujibu mwenzenu Yericko Nyerere kasema mwaka 1988 Nyerere alikuwa hana cheo chochote zaidi ya kwenye familia yake.

Nadhani ingekuwa vyema kama ungemsaidia Yericko siyo mimi.

Mwanakijiji kila siku anandika habari za kuishambulia CCM kuwa ndiyo imeleta ufisadi uoni kama unakuwa unapoteza muda wako badala ya kuishambulia serikali mnawashambulia kina Kinana, Makamba, Mwigulu.
 
Wewe kweli hamnazo, serikali ni nani?? Sio mimi na wewe?? Kwani hata hao wabunge si wanachukua mawazo yetu na kuyapeleka bungeni?? Yani hata hili dogo namna hii unashindwa kupambanua na kuelewa nafasi yako kama mwananchi. Stop non sense kama huna solution ni bora ufunge mdomo wako maana watu wakikupendekezea solution bado utalalamika milele.

Umesoma tamko la Maaskofu wakiilalamikia serikali? Maaskofu nao utawaitaje?

Kweli akili yako ipo kama jina lako kisima unataka nifunge mdomo kisa unachukia nichokiandika JF kuna majukwaa mengi nenda hata Jukwaa la Mapenzi ndiyo saizi yako maneno yako yanafanana na huko.
 
Mohamed unajua wazi kuwa watu 100K wanatufuatilia tunaowasaidia kuona kile kilicho katikati ya mistari yako. Unajua namna gani umma umeelewa nini dhamira na nia yako.

Hili la wewe kusema gazeti limechomwa moto, mimi nimekuambia mchana kweupe kuwa wewe ni muongo.
Mkasema nimehamaki ninywe maji, nimekunywa maji na wasomaji hadi sasa wametambua kuwa si kweli na kwamba ulichokusudia kukisema hakilingani na hadithi uliyotunga.

Ulichokusudia kusema kuhusu gazeti la AE ni kuonyesha jinsi gani makala zako zilivyokuwa moto hadi Nyerere akachoma magazeti moto. Ni kuonyesha jinsi Nyerere alivyomchukia Abdul Sykes.
Kwasisi wenye akili zetu, makala zako hazikuwa sababu kabisa na hilo umeliweka kujifaragua tu.

Nimekuuliza swali kuhusu mwaka 1988 kwasababu wakati nakala zako zinachomwa moto Nyerere alishaondoka madarakani. Umegundua hilo ndiyo maana umekuwa unakwepa kwepa, unakimbia hovyo bila majibu.

Umeamua kumtaja Mayanja ambaye hakuwa serikalini wakati huo huo unaaminisha umma kuwa serikali ilichoma magazeti moto. Umetafuta mahali pa kujitficha chini ya mwamvuli wa CCM

Kwasababu hadithi ni ya kutunga umesahau kuwa wakati huo mwenyekiti wa CCM alikuwa Ali Hassan Mwinyi.
Kama ingekuwa kweli basi serikali iliyochoma moto magazeti kwa makala zako ni ya Mwinyi kwa maagizo ya CCM iliyokuwa chini ya Mwinyi.

Hadi hapo Nyerere hana mkono wake katika kazi zako na umemtetea bila kukusudia ingawa ulikusudia kumhukumu bila mashtaka.

Kama huna majibu ya kwanini serikali ya Mwinyi au chama kilichoma magazeti moto huna moral authority ya kusema hivyo kwasababu hujui! kutoa tuhuma kwa kitu usicho na ushahidi nacho ni uongo na uzandiki usiovumilika kwa mtu mwenye akili sawa sawa na anyezitumia ispokuwa wale walioamua kufunga tela.

Kijana wako kwakusoma bila tafakari amekimbilia kutuhumu kuwa aliyechoma magazeti (tumethibitisha ni hadithi) ni Nyerere. Hapa ndipo tunasema Mohamed unapata tija gani unapozua uongo na kuulaghai umma.
Hivi kitabu hakiuziki hadi utie hoja zisizo na majibu, mashiko au maana!

Kwa wasomaji naomba wafuatilie kwa umakini kuhusu swali la je,serikali alichoma moto magazeti ya AE 1988 kutokana na makala za Mo? na majibu yake ili kuelewa wapi alikwama kama ilivyo kawaida anapopelekwa katika ''kona''

Majibu ya Mohamed hayaonyeshi hilo kutokea na kama lilitokea basi Nyerere hakuhusika.
Uongozi wote wa juu wa CCM haukuhusisha mfumokristo.

Kwa uhakika na usahihi naweza kusema hili la magazeti kuchomwa moto ni;
1. Kujifaragua ili aonekane kama mtu aliyeisumbua serikali
2. Halina ukweli kama alivyoshindwa kulielezea achilia mbali kuthibitisha
3.Kumtuhumu Nyerere na mfumo kristo ili kujenga dhana ya chuki kwa jambo lisilowahusu

Kwa uhakika na uyakinifu nasema Mo hili la magazeti ni uzushi tu.
Wewe jamaa unatia aibu.Kama alivyosema Ritz mmechanganyikiwa na huu mjadala.Angalia jibu lako kutoka kwa Kadogoo

Huo ni uongo wa wazi kabisa (RED)! Nyerere alistaafu uenyekiti wa CCM mwaka 1990! chama kilikuwa kimeshika hatamu hivyo Mwenyekiti wa CCM ndie aliekuwa na kauli ya mwisho ktk maamuzi yote nchini! na hata Mwinyi alikiri hilo wakati anaapishwa kuwa Rais mwaka 1985 kuwa ana deko sababu Nyerere bado ni Mwenyekiti wa CCM na zawadi toka Mbinguni!

Sahihisha uongo wako na wacha kukanusha historia kwani wewe unaonekana bado mtoto sana!
Suala la msingi nililokuwa nikisubiri Mohammed mwenyewe akuulize ni hili.
Ritz,

Hebu muuliza huyu ndugu yetu wapi nilipoandika
kuwa msako wa gazeti ulikuwa nyumba kwa nyumba?

Gazeti unalisaka nyumba kwa nyumba au unayanunua
kutoka kwa wauzaji?

Wameelemewa.
Kama utaweza kumjibu Mohammed basi angalia na nyongeza yangu.
Wachilia mbali na 1988 hii leo 2013 bado tunateseka na mzimu wa Nyerere.Kila anachofanya Kikwete hadi kwanza amfikirie Nyerere.Wapo watu wanamsubiri waone kama ametenda kama Nyerera alivyotaka.
Hivyo mwaka 1988 kivuli chake kilikuwa kikimsumbua hata Mwinyi.Nyerere alikaa pembeni baada ya mambo kumshinda lakini alikuwa ndiye kiongozi.
Hayo si mafanikio ya uongozi wa Nyerere bali ni uovu uliopitilia na roho mbaya.Mfumo kristo aliouwacha mpaka leo unaitesa jamii ya waislamu.
Kwa upande mwengine wacha akina Mwiny na Kikwete yawakute kwa woga wao.Kufanya hivyo kumbe kunaua imani yao na kutuaibisha sote.
 
Naona unakurupuka kujibu mwenzenu Yericko Nyerere kasema mwaka 1988 Nyerere alikuwa hana cheo chochote zaidi ya kwenye familia yake.

Nadhani ingekuwa vyema kama ungemsaidia Yericko siyo mimi.

Mwanakijiji kila siku anandika habari za kuishambulia CCM kuwa ndiyo imeleta ufisadi uoni kama unakuwa unapoteza muda wako badala ya kuishambulia serikali mnawashambulia kina Kinana, Makamba, Mwigulu.

Unahatibu kujwepa kilichodhahiri...
 
CCM haijawai kuwa na mamlaka ya kuzuia kitabu au andiko bila serikali; yaani serkali inatekeleza mapendekezo ya chama. Kumbuka kuwa kama ilivyokuwa mwaka 1988 ndivyo ilivyo sasa; sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ndiyo iliyokuwa ikitumika. MTu pekee ambaye anaruhusiwa kuondoa gazeti au kufungia gazeti ni Waziri wa Habari na mamlaka yake ni ya mwisho (hata mahakamani huwezi kupinga). Sasa, ni Wazirri gani aliyetoa agizo hilo?
Hapa kama kwamba umekubali kuwa waliotaka gazeti lichomwe moto ni Chama ambacho Nyerere alikuwa ndiye mwenye mamlaka nacho.
Suali jee hamjaona kwamba mjadala umewashinda hata mnapotafuta vijineno vya kujifariji eti mumuweke Mohammed Said kwenye kona.
Huu mjadala ulikuwa umeisha akaibuka Yerico kujitangazia ushindi kumbe ndio anazidi kujishindilia.
 
Umesoma tamko la Maaskofu wakiilalamikia serikali? Maaskofu nao utawaitaje?

Kweli akili yako ipo kama jina lako kisima unataka nifunge mdomo kisa unachukia nichokiandika JF kuna majukwaa mengi nenda hata Jukwaa la Mapenzi ndiyo saizi yako maneno yako yanafanana na huko.

Tatizo lako unakimbia hoja...halalisha kutotoa solution kwa hoja...wewe unasema solution itolewe na serikali na sio wewe. Usitutoe kwenye mada ya maaskofu kama unataka uanzishe uzi mpya juu ya maaskofu na sisi tutachangia.
 
Naona unakurupuka kujibu mwenzenu Yericko Nyerere kasema mwaka 1988 Nyerere alikuwa hana cheo chochote zaidi ya kwenye familia yake.

Nadhani ingekuwa vyema kama ungemsaidia Yericko siyo mimi.

Mwanakijiji kila siku anandika habari za kuishambulia CCM kuwa ndiyo imeleta ufisadi uoni kama unakuwa unapoteza muda wako badala ya kuishambulia serikali mnawashambulia kina Kinana, Makamba, Mwigulu.
Ritz nilisha sema na narudia kusema mzee Mwanakijiji yuko kama kasuku kwasababu kasuku kila analolisikia yeye hulisema sasa huyu MM hafanyi bahthi [utafiti] kabla ya kuandika ndio maana nilitoa ombi kwa mods badala yakuweka likes tu wangeongeza na fimbo ingekuwa vizuri kunawatu tunge walamba fimbo mpaka akili zaozikae sawa.
 
1. Namba za mitihani zilianzishwa na Kigoma Malima
2. Africa Events likakusanywa na kuchomwa moto (baadae likaondolewa news stand na kuchomwa moto)
3. Utafiti mujarab wa Taasis ya Warsha (Daily News pia kama source of Data)
4. Kawawa Makamu wa Rais (akihudhuria Maulid Tabora 1988)
5. Daarul Islam kupigwa marufuku na Serikali kujenga Chuo Kikuu lakini ikaruhusiwa kujenga misikiti tu!

Orodha inaendelea.................................

Mzee Mohammed Said endelea kutupa darsa.
Lakini kumradhi kama nimekosea spelling - Daarul Islam. Lakini pia unaweza kuendelea kutupa darsa juu
ya utafiti murua wa Warsha na kama ulishatumika kwingine Duniani kama "reference" n.k.

Usisahau kuweka record straight maana kuna wachimvi fulani wanasema eti wewe umesema News Events
liliondolewa kwenye "News stand" na sio News stands. Lakini pia hayo mengine niliyoandika hapo juu
unaweza kuendelea kutoa darsa pia.
 
Tatizo lako unakimbia hoja...halalisha kutotoa solution kwa hoja...wewe unasema solution itolewe na serikali na sio wewe. Usitutoe kwenye mada ya maaskofu kama unataka uanzishe uzi mpya juu ya maaskofu na sisi tutachangia.

Kumbe ufahamu mpaka huu uzi umefika hapa chanzo ni maaskofu.
 
Ritz nilisha sema na narudia kusema mzee Mwanakijiji yuko kama kasuku kwasababu kasuku kila analolisikia yeye hulisema sasa huyu MM hafanyi bahthi [utafiti] kabla ya kuandika ndio maana nilitoa ombi kwa mods badala yakuweka likes tu wangeongeza na fimbo ingekuwa vizuri kunawatu tunge walamba fimbo mpaka akili zaozikae sawa.

na si tuh kasuku..!
Bali ni kasuku mwenye njaa na kiu kali,,
hali imewaelemea sana..
Wanalia na kusaga meno.
 
Gazeti la Jambo Leo la leo limeingiza hizi ngano za Mzee wetu Mohamed kwenye kesi ya Sheikh Ponda. Kuna shahidi mmoja upande wa Ponda kasema Mwalimu na Abeid Karume waliua Uislam. Kimsingi kesi ya Ponda ni matokeo halisi ya simulizi za Mzee Mohamed. Kwa nini Mohamed Said hajaitwa kama shahidi wa Sheikh Ponda?
 
Last edited by a moderator:

laiti ungalitungamana kiakili na kiupeo usingaliandika hicho ulichokiandika..
Lakini hizi zote ni ishara ya kifo cha mfa maji,
mmeishiwa hoja moja kwa moja,mmebakiza viroja kama hivi..
 
Last edited by a moderator:
Gazeti la Jambo Leo la leo limeingiza hizi ngano za Mzee wetu Mohamed kwenye kesi ya Sheikh Ponda. Kuna shahidi mmoja upande wa Ponda kasema Mwalimu na Abeid Karume waliua Uislam. Kimsingi kesi ya Ponda ni matokeo halisi ya simulizi za Mzee Mohamed. Kwa nini Mohamed Said hajaitwa kama shahidi wa Sheikh Ponda?

WildCard,

Waislam wanaelewa dhulma zote walizofanyiwa hata kabla ya Mohamed Said ajaandika kitabu chake. Kwa mtindo huo mtafunga Waislam wote andaane magereza mengine.
 
Last edited by a moderator:
WildCard,

Waislam wanaelewa dhulma zote walizofanyiwa hata kabla ya Mohamed Said ajaandika kitabu chake. Kwa mtindo huo mtafunga Waislam wote andaane magereza mengine.
Unajua magereza hivi karibuni yameboreshwa sana.Huenda lengo ilikuwa ni huu mkakati ulionza sasa ambapo hata makosa yanayoanza kwa wakristo wanaokamatwa ni waislamu.Ukiangalia ya sheikh Ponda,sheikh Farid na wenzake na Imamu Hamza wa Mwanza utajua ukweli wa mchezo huu.Sheikh mmoja juzi aliniambia wewe Ami ondoa hofu,kama wanajua wanachokifanya hawa jamaa basi wangesitisha mara moja.Hakusema ana maana gani.
Allah (s.w) atuokea na janga walilolipanga,atupe ushujaa wa mapambano kama ule wa Ahlul badri na awahukumu katika mikono yetu kwa kadri anavyopenda.
 
Baada ya miezi miwili na usheee ya mnakasha.... Tuweke pollz sasa tu.... Tuuamue mnakasha huu kwa polls... Tushajua nani ni nani....
 
laiti ungalitungamana kiakili na kiupeo usingaliandika hicho ulichokiandika..Lakini hizi zote ni ishara ya kifo cha mfa maji,mmeishiwa hoja moja kwa moja,mmebakiza viroja kama hivi..
TBS,Fuatilia vizuri kesi ya Sheikh Ponda utaona anachokifanya ni utekelezaji kwa vitendo simulizi za mzee wetu Mohamed. Kiwanja alichovamia ndicho mzee Mohamed anachodai palitakiwa kujengwa chuo kikuu cha Waislam. Baada ya uvamizi ule, msikiti wa muda uliojengwa pale ulipewa jina la Sheikh Amir, mmoja wa wazee wa Mohamed. Sheikh Ponda ni mfuasi mzuri sana wa simulizi za Mohamed Said.Kwanini mzee huyu sio shahidi wa Sheikh Ponda? Pengine angemwokoa kwa kuwa kesi hii imemkalia vibaya Ponda. Hatachomoka.
 
Last edited by a moderator:
Unajua magereza hivi karibuni yameboreshwa sana.Huenda lengo ilikuwa ni huu mkakati ulionza sasa ambapo hata makosa yanayoanza kwa wakristo wanaokamatwa ni waislamu.Ukiangalia ya sheikh Ponda,sheikh Farid na wenzake na Imamu Hamza wa Mwanza utajua ukweli wa mchezo huu.Sheikh mmoja juzi aliniambia wewe Ami ondoa hofu,kama wanajua wanachokifanya hawa jamaa basi wangesitisha mara moja.Hakusema ana maana gani.
Allah (s.w) atuokea na janga walilolipanga,atupe ushujaa wa mapambano kama ule wa Ahlul badri na awahukumu katika mikono yetu kwa kadri anavyopenda.

Ami,

Jana nilikuwa mahakamani kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda.

Kilichonifikisha pale ni kumsikiliza Sheikh Bilal Rehani Waikela ambae alipanda kizimbani
kutoa ushahidi wake upande wa washtakiwa.

Sheikh Waikela amekuja kutoka Tabora.

Hakika mahakama jana walisikia ambayo si wengi wamepata kuyasikia katika maisha yao
yote.

Sheikh Waikela ameanza kwa kutaja umri wake wa miaka 87 na akaieleza mahakama kuwa
ameanza kuutumikia Uislam mwaka 1940 akiwa katika Anjuman Muslim na ilipokuja East
African Muslim Society ( EAMWS) akawa kiongozi.

Akaeleza pia yeye ni muasisi wa Mabaraza ya Misikiti Duniani makao makuu yake Makka.

Akasema yeye Tabora ni mtu wa tatu kujiunga na TANU na katika Tanganyika ni mtu wa 264.

Sheikh Waikela akaeleza kuwa yeye alikuwa bega kwa bega na Nyerere katika kuipigania uhuru
wa Tanganyika na akimchukua Nyerere ndani ya gari yake Tabora na wakila chakula nyumbani
kwake.

Waikela aliichekesha mahakama aliposema wakati ule alikuwa kijana ana fedha na akicheza tennis.

Akaeleza kuwa Gavana Edward Twinning aliingiza fitna nchini kuhusu Waislam kutaka kuwachonganisha
na Wakristo katika suala la elimu ili avunje juhudi za TANU kudai uhuru.

Nyerere alimsihi Waikela kuwa katika hutuba zake ajitahidi sana kuliweka suala hilo vyema ili pasiingie
mtafaruku na nchi ikawa kama India na Pakistani Waislam na Wahindu wakagawana nchi katika misingi
ya dini.

Waikela akasema hilo walilifanyia kazi na hali ikabaki shwari hadi uhuru ukapatikana.

Matatizo yakaja baada ya uhuru kupatikana.

Waikela akaieleza Mahakama jinsi Sheikh Hassan bin Amir alivyomtahadharisha kuhusu njama zilizokuwa
zinapikwa serikali dhidi ya EAMWS na akamweleza kuwa wanafiki ndiyo wanaotumiwa.

Sheikh Waikela aliwataja Mahakamani wanafiki hao kwa majina mmoja baada ya mwingine.

Akaeleza mkutano wa EAMWS katika Ukumbi wa Aga Khan Girls mwaka 1963 alipomsomea Nyerere risala
ya Waislam kuhusu fitna iliyokuwa ikienezwa nchini dhidi ya Waislam na Uislam.

(Risala hii kwa sasa ni maarufu inajulikana kama ''Moto wa Waislam Ukiwaka.'')

Anasema hotuba hii ndiyo iliyosabaisha yeye kuwekwa kizuizini mwaka uliofuatia 1964 na alipotoka jela alipewa
hati ya kifungo ambayo Sheikh Waikela aliieleza Mahakama kuwa ameitundika nyumbani kwake ukutani kama
pambo.

Mahakama ilifahamishwa kuwa mmoja wa washitakiwa ni binti yake aitwae Dentation Waikela ambae alizaliwa
baba yake ikiwa jela.

Sheikh Waikela akaeleza jinsi Nyerere alivyowawezesha kundi la Adam Nasib kwa fedha na ushirikiano wa serikali
kupita majimboni kuwashawishi Waislam kujitoa EAMWS lakini hawakufanikiwa.

Katika majimbo 20 ni majimbo 8 tu ndiyo yaliyokubali kujitoa.

Hata hivyo serikali ilikatumia nguvu na kuitisha mkutano wa wanasiasa Waislam Iringa na Bakwata ikaanzishwa na
serikali ikaweka askari wenye silaha katika ofisi zote za EAMWS na kuzifunga na makufuli na minyororo.

Binafsi Sheikh Waikela akaeleza Mahakama kuwa alihongwa shs: 40, 000 na Geoffrey Sawaya aliyekuwa Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai, hongo ambayo aliikataa.

Hao waliokubali hongo ile ndiyo walioshirikiana na serikali katika kuiweka BAKWATA madarakani.

Kuhusu kiwanja cha Markaz Chang'ombe anasema kile kiwanja ni mali ya EAMWS na madhumuni yake ilikuwa ni kujenga
Chuo Kikuu.

Kwa hakika alisema mengi na mwisho alimuomba hakimu awape Waislam haki yao.
 
Gazeti la Jambo Leo la leo limeingiza hizi ngano za Mzee wetu Mohamed kwenye kesi ya Sheikh Ponda. Kuna shahidi mmoja upande wa Ponda kasema Mwalimu na Abeid Karume waliua Uislam. Kimsingi kesi ya Ponda ni matokeo halisi ya simulizi za Mzee Mohamed. Kwa nini Mohamed Said hajaitwa kama shahidi wa Sheikh Ponda?

Ngoja nilitafute kwanza kisha nilisome, nchi hii tunakokwenda ni kubaya zaidi,
 
Last edited by a moderator:
TBS,Fuatilia vizuri kesi ya Sheikh Ponda utaona anachokifanya ni utekelezaji kwa vitendo simulizi za mzee wetu Mohamed. Kiwanja alichovamia ndicho mzee Mohamed anachodai palitakiwa kujengwa chuo kikuu cha Waislam. Baada ya uvamizi ule, msikiti wa muda uliojengwa pale ulipewa jina la Sheikh Amir, mmoja wa wazee wa Mohamed. Sheikh Ponda ni mfuasi mzuri sana wa simulizi za Mohamed Said.Kwanini mzee huyu sio shahidi wa Sheikh Ponda? Pengine angemwokoa kwa kuwa kesi hii imemkalia vibaya Ponda. Hatachomoka.

Duuh nilikuwa sijaifuatilia hii kesi, kumbe ndivyo picha lilivyo?
 
Last edited by a moderator:
Wewe jamaa unatia aibu.Kama alivyosema Ritz mmechanganyikiwa na huu mjadala.Angalia jibu lako kutoka kwa Kadogoo

Suala la msingi nililokuwa nikisubiri Mohammed mwenyewe akuulize ni hili.

Kama utaweza kumjibu Mohammed basi angalia na nyongeza yangu.
Wachilia mbali na 1988 hii leo 2013 bado tunateseka na mzimu wa Nyerere.Kila anachofanya Kikwete hadi kwanza amfikirie Nyerere.Wapo watu wanamsubiri waone kama ametenda kama Nyerera alivyotaka.
Hivyo mwaka 1988 kivuli chake kilikuwa kikimsumbua hata Mwinyi.Nyerere alikaa pembeni baada ya mambo kumshinda lakini alikuwa ndiye kiongozi.
Hayo si mafanikio ya uongozi wa Nyerere bali ni uovu uliopitilia na roho mbaya.Mfumo kristo aliouwacha mpaka leo unaitesa jamii ya waislamu.
Kwa upande mwengine wacha akina Mwiny na Kikwete yawakute kwa woga wao.Kufanya hivyo kumbe kunaua imani yao na kutuaibisha sote.
Yaani hapa unataka kutuambia kuwa Kikwete hana akili? Kumbe ndiyo maana nchi imo kwenye leadership crisis!
 
Back
Top Bottom