Ami,
Usipate tabu na huyu mtu.
Mwache kama alivyo.
Shughulika na wasikilizaji 100,000+.
Hawa ndiyo wasomaji wa historia hii
ambayo hawakupata kuisikia popote.
Mtego na Chui.
Mohamed unajua wazi kuwa watu 100K wanatufuatilia tunaowasaidia kuona kile kilicho katikati ya mistari yako. Unajua namna gani umma umeelewa nini dhamira na nia yako.
Hili la wewe kusema gazeti limechomwa moto, mimi nimekuambia mchana kweupe kuwa wewe ni muongo.
Mkasema nimehamaki ninywe maji, nimekunywa maji na wasomaji hadi sasa wametambua kuwa si kweli na kwamba ulichokusudia kukisema hakilingani na hadithi uliyotunga.
Ulichokusudia kusema kuhusu gazeti la AE ni kuonyesha jinsi gani makala zako zilivyokuwa moto hadi Nyerere akachoma magazeti moto. Ni kuonyesha jinsi Nyerere alivyomchukia Abdul Sykes.
Kwasisi wenye akili zetu, makala zako hazikuwa sababu kabisa na hilo umeliweka kujifaragua tu.
Nimekuuliza swali kuhusu mwaka 1988 kwasababu wakati nakala zako zinachomwa moto Nyerere alishaondoka madarakani. Umegundua hilo ndiyo maana umekuwa unakwepa kwepa, unakimbia hovyo bila majibu.
Umeamua kumtaja Mayanja ambaye hakuwa serikalini wakati huo huo unaaminisha umma kuwa serikali ilichoma magazeti moto. Umetafuta mahali pa kujitficha chini ya mwamvuli wa CCM
Kwasababu hadithi ni ya kutunga umesahau kuwa wakati huo mwenyekiti wa CCM alikuwa Ali Hassan Mwinyi.
Kama ingekuwa kweli basi serikali iliyochoma moto magazeti kwa makala zako ni ya Mwinyi kwa maagizo ya CCM iliyokuwa chini ya Mwinyi.
Hadi hapo Nyerere hana mkono wake katika kazi zako na umemtetea bila kukusudia ingawa ulikusudia kumhukumu bila mashtaka.
Kama huna majibu ya kwanini serikali ya Mwinyi au chama kilichoma magazeti moto huna moral authority ya kusema hivyo kwasababu hujui! kutoa tuhuma kwa kitu usicho na ushahidi nacho ni uongo na uzandiki usiovumilika kwa mtu mwenye akili sawa sawa na anyezitumia ispokuwa wale walioamua kufunga tela.
Kijana wako kwakusoma bila tafakari amekimbilia kutuhumu kuwa aliyechoma magazeti (tumethibitisha ni hadithi) ni Nyerere. Hapa ndipo tunasema Mohamed unapata tija gani unapozua uongo na kuulaghai umma.
Hivi kitabu hakiuziki hadi utie hoja zisizo na majibu, mashiko au maana!
Kwa wasomaji naomba wafuatilie kwa umakini kuhusu swali la je,serikali alichoma moto magazeti ya AE 1988 kutokana na makala za Mo? na majibu yake ili kuelewa wapi alikwama kama ilivyo kawaida anapopelekwa katika ''kona''
Majibu ya Mohamed hayaonyeshi hilo kutokea na kama lilitokea basi Nyerere hakuhusika.
Uongozi wote wa juu wa CCM haukuhusisha mfumokristo.
Kwa uhakika na usahihi naweza kusema hili la magazeti kuchomwa moto ni;
1. Kujifaragua ili aonekane kama mtu aliyeisumbua serikali
2. Halina ukweli kama alivyoshindwa kulielezea achilia mbali kuthibitisha
3.Kumtuhumu Nyerere na mfumo kristo ili kujenga dhana ya chuki kwa jambo lisilowahusu
Kwa uhakika na uyakinifu nasema Mo hili la magazeti ni uzushi tu.