Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
What about Nyerere?Swali likaja...Jibu langu: About what?Ukumbi mzima ukaangua kicheko.Hawa ni wajuzi ukiwafumbia fumbo wanategua hapo hapo.Nikawapa na pp nilotoa Chuo Kikuu Zanzibar kuhusu Sheikh Hassan bin Amir."...and Mohamed you knew all these people who made history?"Baru mie nimesimama mbele yao nacheka tu na kumshukuru Allah.Ati anasimama mtu hapa free for all anataka kunitisha mimi na kitabucha kufikirika...
Mh! Mwaka 1948-1950 haukuwepo duniani. Hata mimba yako haikuwepo. Wazungu gani hao ulikwenda kuwazuga kwa simulizi hizi nao wakakukubali? Mzee Mohamed Said unatisha.
WC,
Sikiza hii.
Mimi nimezaliwa Mtaa wa Kipata na Nyamwezi huku Swahili.
Nyuma ya nyumba yetu ni Mtaa wa Kirk Street (Lindi) yuko Mashado Plantan
na Saleh Muhsin na Somali Street yuko Zuberi Mtemvu na Omar Londo.
Mbele ya Mtaa wetu Kipata na Congo yuko Mzee Ibrahim Hamisi muasisi wa AA.
Chini Kipata na New Street huku Livingstone yuko Ally Sykes.
Mama yangu Bi Baya na mkewe Abdu Sykes Bi Mwamvua mashoga.
Abdu Sykes nakwenda kwake kwa mama yake Bi Mluguru mimi na mwanae Ebby
ambae tumepishana kuzaliwa kwa siku moja Ebby mkubwa kwangu kwa saa chache.
Sheikh Hassan bin Amir namuona Dar es Salaam msikitini na maulidini na kwingi
tu.
Ni wengi nimewaona bila ya kuwatafuta.
Kuzaliwa mjini dawa.