Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

What about Nyerere?Swali likaja...Jibu langu: About what?Ukumbi mzima ukaangua kicheko.Hawa ni wajuzi ukiwafumbia fumbo wanategua hapo hapo.Nikawapa na pp nilotoa Chuo Kikuu Zanzibar kuhusu Sheikh Hassan bin Amir."...and Mohamed you knew all these people who made history?"Baru mie nimesimama mbele yao nacheka tu na kumshukuru Allah.Ati anasimama mtu hapa free for all anataka kunitisha mimi na kitabucha kufikirika...

Mh! Mwaka 1948-1950 haukuwepo duniani. Hata mimba yako haikuwepo. Wazungu gani hao ulikwenda kuwazuga kwa simulizi hizi nao wakakukubali? Mzee Mohamed Said unatisha.

WC,

Sikiza hii.
Mimi nimezaliwa Mtaa wa Kipata na Nyamwezi huku Swahili.

Nyuma ya nyumba yetu ni Mtaa wa Kirk Street (Lindi) yuko Mashado Plantan
na Saleh Muhsin na Somali Street yuko Zuberi Mtemvu na Omar Londo.

Mbele ya Mtaa wetu Kipata na Congo yuko Mzee Ibrahim Hamisi muasisi wa AA.

Chini Kipata na New Street huku Livingstone yuko Ally Sykes.
Mama yangu Bi Baya na mkewe Abdu Sykes Bi Mwamvua mashoga.

Abdu Sykes nakwenda kwake kwa mama yake Bi Mluguru mimi na mwanae Ebby
ambae tumepishana kuzaliwa kwa siku moja Ebby mkubwa kwangu kwa saa chache.

Sheikh Hassan bin Amir namuona Dar es Salaam msikitini na maulidini na kwingi
tu.

Ni wengi nimewaona bila ya kuwatafuta.
Kuzaliwa mjini dawa.
 
Nguruvi,

Umehamaki.
Mimi sitafuti umaarufu kwa yoyote kwa kuwa sina shida ya umaarufu.

Umeandika Africa Now la Peter Enahoro.
Hili letu lilikuwa Africa Events la Mohamed Mlamali Adam.

Uhariri wa Enahoro si wa Mlamali.
Sera za magazeti yao zilikuwa tofauti kama mbingu na ardhi.

Ngoja nikuongezee kingine kikuudhi zaidi.

Mimi na Mlamali tuliondolewa katika gazeti hilo kwa shinikizo...

Vinginevyo gazeti lisingefunguliwa fedha zake kutoka BOT kwenda
Uingereza.

Ni kisa kizuri.

Ahmed Yahya akashika nafasi ya Mlamali lakini hakuacha kunipa kazi
ambazo AE walichapa bila ya jina langu nikawa ''Special Correspondent.''

Kisha nikenda pale ofisini kwao Banner Street London tunacheka sana.

Ukisoma habari zangu kila siku utaghadhibika na kila siku utaniita ''muongo
mkubwa.''

Watazamaji ndiyo waamuzi kama mie nawavunga ama nawapa khabari za kweli.
Hiyo ilikuwa mwaka 1988?
 
Baada ya hao anatakiwa kumshukuru sana Allah.

Mara nyingi ahamaki za namna hiyo zinasababisha heart disease and stroke.

Ritz,
Allah amnusuru.

Unajua akili yake inakataa kuamini.
Akinidhania mie jinga lao.

Mtego wa Yericko umenasa mamba.
 
Ilimradi useme tu.
Ulichokanusha na kukubali ni kitu hicho hicho.
Ikiwa serikali kusemwa kuhusu kujenga uwanja mkubwa wa ndege ilifanya nongawa,sembuse kusemea jambo kubwa kama historia ya nchi ikimshushua Nyerere!.
Ilimradi haijatajwa ni gazeti toleo namba ngapi na liliandika kuhusu nini kati ya yale serikali iliyotaka yasisomwe basi kauli ya Mohammed Said itakuwa na uzito zaidi kuliko kukanusha kwako hasa kwa vile yeye alikuwa akifuatilia nyendo za hayo magazeti kinyume na wewe ambaye hukuwa na shauku yoyote nayo.
Sasa hivi kumekuwa na kasi ya kasi ya kuwakamata waislamu kwa makosa yanayoanza kulalamikiwa na maaskofu.Nani utamdanganya kuwa waislamu hawajakamatwa kwa shinikizo la mfumokristo?.
Wakristo kusema kweli mnatia aibu kwa kuogopa hata vivuli vyenu.
Nyerere asisemwe kwa yale aliyofanya tena maovu.
Waislamu wasitoe maoni kuhusu Muuungano
Waislamu wasilalamike kuhusus NECTA
Waislamu wasioneshe uozo wa takwimu za sensa
Waislamu wasidai mali zao zilizoporwa
Halafu waislamu wakubali kula nyamafu,wakikataa wanatiwa ndani na kusingiziwa magaidi.
Nyinyi muko Ovyo kabisa!.Ndio maana Ulaya watu wamekimbia hii dini yenu na kujiunga na Manchester
Hata Yesu angerudi angewashangaa wafuasi wake mlivyobadilika
Bwana mdogo, usisome vitu bila tafakari. Nadhani wakati huo ulikuwa hujaanza shule. Mimi nimesoma magazeti hayo nikiwa na ufahamu wangu.
Haya mambo si kudandia ni maji marefu mwacheni Mohamed akabiliane na hoja.
Hata hivyo kwavile wewe na Ritz mnaonekana kuwa ''mnafahamu'' zaidi kile Mohamed alichoandika, swali hili hapa

Je, magazeti anayosema Mohamed yamechomwa moto, hiyo ilitokea mwaka 1988 kama alivyodai.
Mkishanijibu hayo kwa kuunganisha nguvu na Mohamed, nitawaeleze habari msioijua.

Nijibuni kwanza.
 
Ritz,
Allah amnusuru.

Unajua akili yake inakataa kuamini.
Akinidhania mie ----- jinga lao.

Mtego wa Yericko umenasa mamba.
Mohamed, usikwepe swali muhimu sana, je hiyo ya kuchoma magazeti ilitokea mwaka 1988. Msilete habari nyingine twendeni hoja kwa hoja.
 
Ritz,

Umesahau kitu.
Umesahau kumwelekeza namna ya kunywa maji.

Kwanza akae kitako.
Kisha anywe maji funda tatu.
Mohamed hayo yote ya nini, swali ni kuwa magazeti yaliyochomwa moto kutokana na makala zako, je hiyo ilitokea mwaka 1988?

Mtaendelea na matusi, kejeli na dharau lakini swali hili lipo pale pale.

By the way mimi nikikaa kitako huwa nakuacha bila nguo. Hapa nimesimama nakunywa maji huku nikisubiri jibu la magazeti kuchomwa mwaka 1988, baada ya hapo nitakaa kitako.
 
Mohamed na vijana wako Ritz na Ami, vipi mna jibu au hamna?
Je, magazeti yenye makala za Mohamed katika AE yalichomwa moto mwaka 1988?

Wote nawaona mpo jamvini, lakini hamtaki kujibu kulikoni?
Sina hamaki, nimetulia katika mti nakunywa maji.

By the way nashukuru kwa dua yako ili mwenyezi mungu aninusuru!
 
Wanajamvi naomba msaada inawezekna kiswahili changu kina matatizo.
Kwa anayenielewa naomba aweke sentensi hii katika lugha nyepesi ili Mohamed, Ritz na bwana mdogo Ami wanielewe.

Mohamed anadai magazeti ya AE yalichomwa moto na serikali kutokana na makala zake.
Nainachotaka kujua ni kuwa magazeti hayo yaliyochomwa moto mwaka 1988?

Msaada wenu tafadhwali
 
Hiyo nini?
Mohamed wasomaji 100,000+ wanakusoma unavyobabaika kwa swali dogo wala usidhani ni ujanja!

Swali ni kuwa wewe Mohamed na vijana wako Ritz na Ami, tuelezeni magazeti yalichomwa moto mwaka 1988 kutokana na makala zako!
 
Nguruvi,
Usidhani nafanya maskhara.

AE March/April 1988 makala yangu ''In Praise of Ancestors.''
Ilimtaja Abdu Sykes kama ''brains behind founding of TANU.''

Gazeti likikusanywa kutoka ''news stand.''
Unadhani mie nina uwezo wa kutunga visa kama hivi?

Ningekuwa Ernest Hemingway ingawa wewe unataka kunitia
kundi la JHC crude author!
 
Kwanza umeweka sawa kuwa lilikusanywa kutoka ''news stand'' kama ilitokea hivyo na sikuwa lilikusanywa kila mahali kwa msako maalumu kama ulivyotaka kuulaghai umma.
Nashukuru kwamba record imekaa sawa na wanajamvi wame note hilo.

Tuendelee, kwahiyo gazeti ''lilikusanywa'' kwasababu lilimuudhi nani kwa makala hiyo!
 
Wanajamvi naomba msaada inawezekna kiswahili changu kina matatizo.
Kwa anayenielewa naomba aweke sentensi hii katika lugha nyepesi ili Mohamed, Ritz na bwana mdogo Ami wanielewe.

Mohamed anadai magazeti ya AE yalichomwa moto na serikali kutokana na makala zake.
Nainachotaka kujua ni kuwa magazeti hayo yaliyochomwa moto mwaka 1988?

Msaada wenu tafadhwali

Hii dramatisation sijui ya nini...
Ona hapa:

''In Praise of Ancestors'' Africa Events,
London, March/April 1988, uk. 37-41.

Ahmed Rashad Ali ndiye alikuwa mwakilishi
wa Library of Congress, Tanzania aliwapelekea
''cutting'' ya makala hii.
 
  • Thanks
Reactions: Ami

Hakuna drama, tayari umeshajibu kuwa gazeti lilichomwa moto mwaka 1988 baada ya kukusanywa kutoka katika ''news stand'' na si kukusanywa nchini na majumbani kote kama ulivyodai mara nyingi.
Hilo limeshapatiwa jibu.

Swali linalotokana na jibu hilo ni kuwa makala yako ilimuudhi au kumkerehesha nani hadi kuamua serikali ikusanye na kuchoma moto?
 
Kwanza umeweka sawa kuwa lilikusanywa kutoka ''news stand'' kama ilitokea hivyo na sikuwa lilikusanywa kila mahali kwa msako maalumu kama ulivyotaka kuulaghai umma.
Nashukuru kwamba record imekaa sawa na wanajamvi wame note hilo.

Tuendelee, kwahiyo gazeti ''lilikusanywa'' kwasababu lilimuudhi nani kwa makala hiyo!

Nguruvi,

Hilo swali unataka nilijibu mie?

Lakini majibu makali dhidi ya makala yangu yalitoka
CCM Dodoma na aliandika Dk Kataroge Mayanja Kiwanuka.

Africa Events, May 1988 barua ya Dr K. Mayanja Kiwanuka.

Wakati ule alikuwa katika Idara ya Uhasishaji Umma.

Unalo?
 
Mohamed wasomaji 100,000+ wanakusoma unavyobabaika kwa swali dogo wala usidhani ni ujanja!

Swali ni kuwa wewe Mohamed na vijana wako Ritz na Ami, tuelezeni magazeti yalichomwa moto mwaka 1988 kutokana na makala zako!

Nguruvi3,

Naona unazidi kuchanganyikiwa unawaita vijana wa Mohamed Said mimi siyo kijana kama umeamua kuniita ivyo ili ujenge hoja zako na mie sitafanya makosa kukuita mtoto wa Nyerere ili twende sawa.
 
Nguruvi,

Hilo swali unataka nilijibu mie?

Lakini majibu makali dhidi ya makala yangu yalitoka
CCM Dodoma na aliandika Dk Kataroge Mayanja Kiwanuka.

Africa Events, May 1988 barua ya Dr K. Mayanja Kiwanuka.

Wakati ule alikuwa katika Idara ya Uhasishaji Umma.

Unalo?

Mtoto wa Nyerere jibu ilo au ulitaki? Wafahamishe uliowauliza.
 
Mohamed, usikwepe swali muhimu sana, je hiyo ya kuchoma magazeti ilitokea mwaka 1988. Msilete habari nyingine twendeni hoja kwa hoja.

Usipoangalia huu uzi unaweza kukuacha na BP.
 
Nguruvi,

Hilo swali unataka nilijibu mie?

Lakini majibu makali dhidi ya makala yangu yalitoka
CCM Dodoma na aliandika Dk Kataroge Mayanja Kiwanuka.

Africa Events, May 1988 barua ya Dr K. Mayanja Kiwanuka.

Wakati ule alikuwa katika Idara ya Uhasishaji Umma.

Unalo?
Mohamed, gazeti lilichomwa kwa amri ya serikali wala si Kiwanuka.
Swali ni nani aliamuru hilo kutokea na kwasababu gani.
 
Hakuna drama, tayari umeshajibu kuwa gazeti lilichomwa moto mwaka 1988 baada ya kukusanywa kutoka katika ''news stand'' na si kukusanywa nchini na majumbani kote kama ulivyodai mara nyingi.
Hilo limeshapatiwa jibu.

Swali linalotokana na jibu hilo ni kuwa makala yako ilimuudhi au kumkerehesha nani hadi kuamua serikali ikusanye na kuchoma moto?
Uliporudia rudia swali la kutaka upate jibu iwapo gazeti lilichomwa mwaka 1988 nilidhani una jibu kubwa kukanusha.
Kwa bahati Mohammed kakujibu kwa kujiamini.Naona sasa umeingia mitini.
Angalia Jibu ulilotaka

Hii dramatisation sijui ya nini...
Ona hapa:

''In Praise of Ancestors'' Africa Events,
London, March/April 1988, uk. 37-41.

Ahmed Rashad Ali ndiye alikuwa mwakilishi
wa Library of Congress, Tanzania aliwapelekea
''cutting'' ya makala hii.
Baada ya jibu hilo angalia ulivyobabaika
Hakuna drama, tayari umeshajibu kuwa gazeti lilichomwa moto mwaka 1988 baada ya kukusanywa kutoka katika ''news stand'' na si kukusanywa nchini na majumbani kote kama ulivyodai mara nyingi.
Hilo limeshapatiwa jibu.

Swali linalotokana na jibu hilo ni kuwa makala yako ilimuudhi au kumkerehesha nani hadi kuamua serikali ikusanye na kuchoma moto?
Hili swali lako hata ukienda ofisi ya Kanumba hawawezi kukupa jibu.Ikiwa kweli lilikusanywa na kuteketezwa inatosha kuwa kuna kitu serikali imekwepa kisisomwe.
 
Back
Top Bottom