Mohamed kwanza nikuambie kuwa acha kudanganya watoto na vijana.
Hili la African event unalisema sana. Umesahau kuwa kulikuwa na Africa Now na magazeti mengine.
Magazeti hayo yalikuwa yanazuiliwa si kwasababu ya Habari zako muongo mkubwa wewe!
Yalikuwa na habari nyingi za kuusakama ujamaa na pengine kuelezea hali ya mambo ambayo by then ingewatia hasira sana wananchi. Nakumbuka katika moja ya makala ni ile ya ambayo iliielezea kwanini serikali ijenge uwanja mkubwa wa ndege ambazo ni za kigeni badala ya kuendeleza bonde la ruvu ili kujitosheleza kwa chakula.
Lakini unaposema yalikusanywa, yalikusanywa kutoka wapi wakati kuna nakala majumbani kwa watu.
Unachotaka kusema hapa ni kuwa Polisi waliingia kila nyumba kukusanya na kuchoma moto.
Mzee Said, hivi huwa unapata tija gani unapokuwa muongo! Muogope mwenyezi mungu.
Narudia Mohamed, stop this cheap popularity!
You erode the little respect as story teller of our times
Nguruvi,
Umehamaki.
Mimi sitafuti umaarufu kwa yoyote kwa kuwa sina shida ya umaarufu.
Umeandika Africa Now la Peter Enahoro.
Hili letu lilikuwa Africa Events la Mohamed Mlamali Adam.
Uhariri wa Enahoro si wa Mlamali.
Sera za magazeti yao zilikuwa tofauti kama mbingu na ardhi.
Ngoja nikuongezee kingine kikuudhi zaidi.
Mimi na Mlamali tuliondolewa katika gazeti hilo kwa shinikizo...
Vinginevyo gazeti lisingefunguliwa fedha zake kutoka BOT kwenda
Uingereza.
Ni kisa kizuri.
Ahmed Yahya akashika nafasi ya Mlamali lakini hakuacha kunipa kazi
ambazo AE walichapa bila ya jina langu nikawa ''Special Correspondent.''
Kisha nikenda pale ofisini kwao Banner Street London tunacheka sana.
Ukisoma habari zangu kila siku utaghadhibika na kila siku utaniita ''muongo
mkubwa.''
Watazamaji ndiyo waamuzi kama mie nawavunga ama nawapa khabari za kweli.