Kwa faida ya wanajamvi hebu tuwekee huo ushahidi wa Selasini.
Hicho ndicho aidha Mh Nkamia, Spika ama Lukuvi walipaswa kudai mara baada ya Mh Selasini kutoa zile tuhuma. Badala yake Mh Nkamia akatapika yaliyoujaza moyo wake na kwa kuwa moyo wako pia umejaa udini unaendeleza ujinga huo huo wa Nkamia.
Unachonishangaza zaidi tena ni ati wataka nikupe ushahidi! Nikupe ushahidi gani? Mimi ndie niliyeleta hizo tuhuma za udini UDom? Au umenisikia nikikubaliana na tuhuma alizotoa Selasini Bungeni?
Kinyume chake nimehuzunishwa na GT kama wewe kubeba infirioties za Nkamia na kuanzisha 'vita' ya dhidi ya Ukristo.