Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wild Card,
Kama kubadilika ndiyo nishaibadili.

Leo historia ya TANU na Nyerere mwenyewe watu wanaisoma vingine.
Haya ndiyo mabadiliko yenyewe.
Hujaibadili, Bado inasomeka muasisi wa Taifa ni Julius K. Nyerere, Muasisi wa TANU ni Julius Nyerere,

Hilo linathibitishwa na kukaziwa na maamdishi yako pia hasa unaposema, Kadi namba Moja(1) ya TANU ni ya Julius K. Nyerere,

Vivyohivyo inazidi kukidhihirisha ukuu wa uasisi wa TAifa pale wewe mwenyewe katika maamdishi yako unaposema rais wa kwanza wa Tanganyika/Tanzania ni Julius Nyrerere.

Hilo halitafutika wala kuwa badiliko la kikemia au kiumbo ndugu yangu Mohamed Said.

Ngano zako zitasimama Kama ngano za Mohamed Said, kamwe hazitageuka kuwa historia ya kweli ya uhuru wetu.
 
Mohamed

Huhitaji kujua zaidi yaliyomo mwenye kitabu changu kiitwacho "Vita dhidi ya Ugaidi"?
 
Hayo maneno ungemwambia Joseph Selasini Mbunge wa Rombo Chadema.

Wapi mie nimewachukia Wakiristo acha kuniwekea maneno mdomoni dini yangu inanikataza kuwachukuia watu wa dini zingine kwani sikuwaumba mimi.

Mimi kuelezea dhulma tulizofanyiwa wewe tafsiri yako ni kuuchukia Wakiristo.
Mkuu dhuluma ipi mlodhulumiwa?
Wanao kula inchi hii ni ccm na jamaa zao kwa ujumla.
Hawa ccm ndo tatizo ila cha kushangaza mzee Ms, alitudokeza kipi cha uchaguzi waislam walinong'onezana wamchagu Jk, wa chama kilekile chenye kulea mfumo kristo.
Na wakawaagiza mpaka mashekh wapite miskitini wakimuombea kura Jk, na mmoja wa masheikhe hao alikuwa ilunga.
Sasa mkuu kama mnajua mmezulumiwa na utawala huu kwanini wakati wa uchaguzi huwa mnawaludisha ccm walewale waliowadhulumu?
 
Hujaibadili, Bado inasomeka muasisi wa Taifa ni Julius K. Nyerere, Muasisi wa TANU ni Julius Nyerere,

Hilo linathibitishwa na kukaziwa na maamdishi yako pia hasa unaposema, Kadi namba Moja(1) ya TANU ni ya Julius K. Nyerere,

Vivyohivyo inazidi kukidhihirisha ukuu wa uasisi wa TAifa pale wewe mwenyewe katika maamdishi yako unaposema rais wa kwanza wa Tanganyika/Tanzania ni Julius Nyrerere.

Hilo halitafutika wala kuwa badiliko la kikemia au kiumbo ndugu yangu Mohamed Said.

Ngano zako zitasimama Kama ngano za Mohamed Said, kamwe hazitageuka kuwa historia ya kweli ya uhuru wetu.

Yericko,
Hayo yote uliyosema ni kweli kabisa na wala mimi sijapinga hilo.

Tatizo ni kuwa huwezi kuishia hapo.

Utakaposoma sasa historia ya TANU ndipo hapo utakapokutana
na Abdu Sykes, ndipo hapo utakapokutana na Chief David Kidaha
Makwaia.

Vipi unakutanananao?

Kitabu kitakuambia kuwa kabla ya Abdu kuonana na Nyerere 1952
fikra ya kumpata kiongozi mpya wa TAA na kisha kuunda TANU
alizungumza na Chief Kidaha 1950.

Akili ya msomaji akifika hapo itamuuliza ehe ikawaje Abdu na Chief
Kidaha?

Hapo anasonga na kurasa za kitabu anasoma yale ambayo kwake ni
mageni kabisa - ni mambo mapya.

Ninaposema historia imebadilika mabadiliko yeynyewe ndiyo haya.
Si kama tutabadilisha uasisi wa Nyerere katika ujamaa na vijiji vyake
kuasisi CCM nk. nk.

Historia hii ya vijiji vya ujamaa hakika hana mpinzani ila hii ya kuasisi
TANU ndiyo panapo maneno ya kuzungumza.
 
Mohamed

Huhitaji kujua zaidi yaliyomo mwenye kitabu changu kiitwacho "Vita dhidi ya Ugaidi"?

Yericko,
Kwa kweli kwa yale niliyosoma...

Yamenitosha sana.

Nadhani umenisoma kuhusu suala la ugaidi mada niliyowasilisha Chuo
Kikuu Cha Ibadan.

Ikiwa umesoma utakuwa umeona maswali niliyowauliza Wamarekani.

Dunia nzima wasomi wanaandika kwa staili ile msome Chomsky ikiwa
una wakati.

Maandiko yake yatakufaa kwa siku za baadae.
Mwandishi hajikombi kwa mtu.

Anaandika kama akili yake inavyochambua mambo.
Wewe unataka kuwafurahisha Waamerika.

Mimi nimewashambulia Waamerika na juu ya hayo yote wamenita
kuzungumza kwenye vyuo vyao.

Hao ndiyo Waamerika hawana uadui wa kudumu wala urafiki wa
kudumu.

Pokea hilo somo la kwanza.
 
Pole sana ndugu yangu Mohamed,

Nasikitika kwa wewe kuiweka akili yako ikaamini kile iaminicho bila kufingua milango ya fikra mpya,

Ugaidi ninaouongelea mimi sio huo wa chuki dhidi ya imani za kiroho bali ni ule wenye ukupe wa kimagharibi dhidi ya misimamo ya vikundi vyenye kubeba bendera ya kiroho.

Nimelisoma vela bandiko lako ulilohadhiri huko ibadan,

Bahati nzuri hukuficha asili ya sura yako kitabia katika uhadhir huo, ndiomaana Nasikitika kwa www kuturuhusu jambo geni ndani ya medula zako

Nipo tayari kukupa mapya juu ya vita dhidi ya Ugaidi
 
wickama,
nadhani unajua kuwa sie wamanyema wawili uzito
wetu unatosha kuzamisha jahazi na kina kasulwa
ni ndugu zangu...

Sasa ile mie kusema "nilijua" sikukusudia wewe.
Nilikusudia wote watakaosoma kitabu changu.

Hili la uislam limerefushwa kuliko kusudio lenyewe
na baya zaidi ndio mwiba wenyewe.

Ama kuhusu yericko ulosema sawa tunawajibika kumtia
ghera na huo ndiyo utu.

mzee ms you have earned my deepest respect for this courage. Na kwa kweli this is maturity at its best. There are no enough words to describe it. Thank you.
 
Sheikh Mohammed Said,

Salaam sana.

Hapa pana mambo mengi mno yenye kuleta rabsha kiduchu na vichekesho vingi. Nafikiri unakumbuka ile bayana yangu ya awali kwako,sababu nilichelea kuingia mambo kama haya ya udini,kutaja majina na kuwaadhiri jamaa zetu toka family mbalimbali tunazozistahi na mikanganyiko mingi saana,na matokeo yake tupo nje kabisa na hii mada/shutuma dhiki yako.

Imekua kama mtego wa panya sasa,anangia alokuwamo na asokuwamo!ahaha!!

Nimecheka pasi kiasi na yale majibu ulotoa kuhusu hiyo habari ya mmanyema mkristo. Nafikiri Sheikh Mohammed labda kitambo hujenda tembea pale Ujiji kuona "mabadiliko". Mimi binafsi pia pana pahala kwingi nahitaji nikatupie jicho Insha Alaah penye uhai na maajaliwa.

Hii habari ya makabila, ama kwa hakika imenichekesha kiduchu hasa ulipotaja Wangazija Wakristo. Unajua pale Comoro siku hizi pana wale "Wangazija pori" ambao huenda pale "kununua baraza" na kujinasibu Ungazija pasi kiasi. Ukizungumza na Bwana Ahmed Rajab atakuchekesha zaidi juu ya habari hizi.

Nafikiri hata ndugu zetu wa kiZaramo zamani nao walikua na dasturi na ustaarabu kama huo wa kukaribisha "wabweshu" na kuita "udugu wa khiyari". Tena walikua wakifanza na sherehe kubwa mno siku ya kutimiza huo "udugu". Napenda saana tamaduni na mapenzi yalokuwapo zamani baina yetu.

Sijui lini utapata fursa tuwekee na habari za mapinduzi ya Zanzibar,hasa wale wamakonde wa Kipumbwi,Ushongo na Sakura walotumiwa kuua ndugu zetu na kumuweka madarakani yule Mnyasa alokuja Unguja mtoto wa mgongoni(yaleyale ya Musharaf kuja Pakistani mtoto wa mgongoni halafu kuwafanzia watu hadaa). Ndugu na jamaa zetu wengi walitolewa roho na yule dhalim.

Uncle yangu Commando Amour Dougheish,ndo alokua akamkamate yule Mnyasa toka pale Ikulu na kumpeleka pale Idara ya habari - Rahaleo, halafu atangaze kuwa nchi isharejeshwa na imo mikononi kwa wananchi wenyewe. Wallahi,lile jambo mpaka leo najuta halikufanikiwa.

Basi Insha Allah tuendelee na mnakasha.

Ahsanta.

Gombesugu,
Hayo hapo chini ni baadhi ya maneno niliyoandika katika pitio la kitabu ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' cha Dk. Harith Ghassany:Kwakipindi kirefu historia ya mapinduzi ya Zanzibarilikuwa ni ile historia rasmi ambayo imeathiri historia nyingi Afrika. Viongoziwa Afrika wanapenda ile historia itakayowakweza na kuwaonyesha wao katikamwanga wa kupendeza.

Vinginevyo historia hiyohaitakiwi.

Wazalendo wenyewe hawakuwa na hamu ya kuandika historia hii na watuwa nje walioandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar hawakupata kuifanyia hakihistoria ya Zanzibar labda kwa ugeni wao na kwa kuyaamini maelezo yaliyokuwa"wazi" kwa wakati ule, mfano mkubwa ukiwa ni kule kuamini kuwa mapinduzi yaZanzibar yalipangwa na makomredi wa Umma Party.
Hapajakuwapo udanganyifu mkubwa katika uandishi nautafiti kama huu.

Dkt Ghassany amekiweka chanouwanjani bila kawa. Akizungumza na Abdushakur Aboud wa Sauti ya Amerika DktGhassany amesema kuwa historia ya Zanzibar ni historia ya kujijuwa maisha yakeakiwa mjukuu wa babu wa mababu Muomani na mabibi wa Kimanyema na Kimwera –mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na Kiafrika.

Hii kwa hakika ndiyo historia yawananchi wa Zanzibar.

Ni tabu sana kumpata huyo Muarabu Zanzibar kila umuonaeMuarabu basi ana mjomba na shangazi Mwafrika.

Maadui wa Zanzibar wakiweka mkazo katika ubaguzi warangi na kuwafitinisha Wazanzibari. Ukweli huu ndiyo chanzo cha matatizo yoteyaliyoikumba Zanzibartoka vyama vya siasa vilipoanza katika miaka 1950 na matatizo yaliyosababishamauaji ya mwisho yakiwa mwaka 2001.
Ilikuwakatika barza yetu ya kawaida ya kunywa kahawa na kula pweza huku tukijadilihistoria ya Tanzaniaambako siku moja Mzee Mkwawa alinambia, "Mohamed nataka nikuambie kitu.

Unajuamimi nimehusika sana katika mapinduzi ya Zanzibar?"

NilimuangaliaMzee Mkwawa kwa makini.

Fikra yangu ya utafiti na uandishi ishashtuka haipo tenausingizini.

Mzee Mkwawa aliendelea, "Mimi ndiye niliyekuwa nikiwavushaWamakonde kutoka Kipumbwi kwenda Zanzibarkuipigia kura ASP na wakati wa mapinduzi mie ndiye niliyewavusha Wamakondekwenda kuipindua serikali ya Jamshid."

Sasa moyo wangu ukaanza kudunda kwanguvu.

Naisemesha nafsi yangu, "Huyu mzee anajua uzito wa maneno haya?"
Tuishiehapa.
 
mzee ms you have earned my deepest respect for this courage. Na kwa kweli this is maturity at its best. There are no enough words to describe it. Thank you.

Wickama,
Mie nakushukuru wewe zaidi.

Ahsante sana ndugu yangu.
 
Mimi ni mkristo lakini mpka leo nalaumu Marekani na vita hii na naipinga kwenda kutumia drones zao Pakistan, somalia Afghan na sehemu nyingine, hata juzi kwenye Boston Bombs niliwaonea huruma wamarekani na felt very bad for kid and those who lost thier lives and i got to think that what they went through is what Pakistan,somalia and other countries go through almost daily and to top up wamerikani wana wabomb na drone zao, i empathize with Iraq and Afghan people. But i have never looked at it as Muslims being oppressed, but i look at it as a Powerfull nation kuonea taifa dogo.

So huo ni udini when you look at it as Muslims being oppressed.

Mundungus, Ritz and Kadogoo; Labda nichangie. Kama mmesoma baadhi ya magazeti hasa ya kutoka Marekani, nia ya Marekani kuleta Jeshi la kusaidia kumsaka Kony kule Uganda, ni actually kutumia DRONES kummaliza huyu bwana. Ila by Extension, wakishaweka msingi Uganda na operations kama hizo, uwe na uhakika kwamba kama wana mtu wanamsaka kwa udi na uvumba na wakaambiwa yuko Maswa, ni kwamba mchezo umekwisha. Watamulika hilo anga na wakati mwingine kuua watu wanaodhani ni wewe. Pakistani analia sana na drones lakini huku ni mpokeaji mkubwa wa misaada ya kijeshi toka marekani. Siasa zinajua maslahi tuu
 
Wild Card,Kama kubadilika ndiyo nishaibadili.Leo historia ya TANU na Nyerere mwenyewe watu wanaisoma vingine.Haya ndiyo mabadiliko yenyewe.
Watu gani hao wanaoisoma historia ya TANU, Tanganyika vingine. Unaweza kuendelea kujifariji kwa namna hiyo hadi mwisho wa maisha yako hapa duniani. Kitabu kile hata kama kingeandikwa na Abdu kwa namna ulivyokiandika bado kingebaki ni simulizi tu. Kitabu kipo tangu 1998 kimekuja kuwa gumzo humu JF mwaka 2013! Historia ya TANU haiwezi kuokotwa kwenye vikabrasha vya familia moja. Mtu mmoja akajifungia chumbani kwa mkewe, akaibuka na historia ya sisi kuamini kama mazuzu.
 
Muheshimiwa Mwanakijiji

Ndugu gombe sugu; naomba uniite "mwanakijiji" tu au kama wengine wanavyoita "MM"; sistahili kuitwa uheshimiwa kwa sababu siamini katika "uheshimiwa" kama hadhi au sifa ambayo wengine wanayo na wengine hawana. Ni muumini wa "Kila binadamu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Nashukuru.

Maswali yako uliyoanza nayo hapo juu kufikia hapa chini nimeyasoma na ninashukuru kwa kuniuliza. Majibu yangu bado yamebaki yale yale. Ila nitaangalia haya mambo kidogo hapa chini.
hivi ndugu yangu wewe binafsi kwa mtazamo wako unakubaliana na mawazo ya baadhi ya wanajamvi hapa,watanzania kadhaa pamoja na Serikali hapo kuwa Waislam wana matatizo na dhiki kadhaa za kihistoria na inalazim Serikali iwatengee sikio japo la upande mmoja kujua kinachowasibu?

Mimi sikubaliani na mawazo au nadharia kuwa Waislamu wana 'matatizo na dhiki kadhaa za kihistoria" hasa kama unamaanisha kuwa dhiki hizo za kihistoria zinaikumba jamii ya "kiislamu" peke yake. Hii ni tofauti yangu kubwa labda na baadhi ya watu; naamini matatizo ya kihistoria ambayo yalisababishwa na ukoloni yalikuta jamii nyingi za Watanganyika na hilo halikujali dini au imani zao. Matokeo yake utayaona ni yale yale. Ukifika Usafwa utakutana na matatizo yale yale ambayo unayaona Mkuranga; ukienda Ndala utakutana na matatizo yale yale unayoyaona Masasi; ukienda Bunda utakutana na matatizo yale yale ambayo unaweza kuyaona Mtwara. Matatizo ambayo wananchi wetu wanakabiliwa nayo hayana dini. Kudai kuwa matatizo haya yamejali sana dini kiasi kwamba kundi moja la watu (Waislamu) wadai upendeleo wa pekee ni kutokuwa wa kweli wa historia.

Nitakupa mfano mmoja mzuri ambao hatujaujadili sana hapa. Kabila kubwa Tanzania ni Wasukuma/Wanyamwezi. Wanaishi katika mikoa minne (Mwanza, Shinyanga, Geita na Tabora). Wasukuma peke yao wanakadiriwa kuwa karibu milioni 5.5 (sawa na kama asilimia 15 hivi ya Watanzania wote); ukijumlisha na Wanyamwezi (ambao ni milioni 1.5) utaona kuwa Wasukuma ni wengi kweli kweli.

Kulinganisha nao:

Wachagga - milioni 2 hivi
Nyakyusa - milioni 1 hivi (bila kuhesabu wale wa Malawi)
Haya - milioni 1.5 hivi

Utaona kwa haraka tu kuwa makabila ambayo yamepata nafasi kubwa zaidi (katika elimu, ajira n.k) katika Tanzania tangu ukoloni (haya matatu) hayafikii kwa ujumla wake idadi ya watu wa kabila moja - Wasukuma. Tulinganishe tena kidogo:

Wazaramo - 700,000 hivi
Ndengereko - 150,000
Zigua -580,000

(makabila haya matatu yamepokea Uislamu kwa wingi; karibu asilimia 90 ya watu wake ni Waislamu).

Wasukuma hata hivyo Wakristu ni asilimia kama 43 hivi na Imani za jadi asilimia 42 waliobakia ni Waislamu.

Lakini tuangalie makabila mengine ambayo yana Wakristu wengi na tuone nayo kama yako yanawakilishwa vizuri katika utawala na mafanikio ya nchi:

Wahehe wako kama milioni 1.2 na Wakristu ni kama asilimia 90 hivi
Wagogo milioni 2 hivi asilimia 70 Wakristu
Wamatengo 300,000 na asilimia 80 Wakristu.

Sasa namba hizi (unaweza kuangalia makabila mengine hapa) ni lazima zikufanye ujiulize maswali:

a. Ni kweli Wakristu wanapendelewa? Hili lingeonekana kwa jamii zote za Kikristu kuwa na mafanikio kuliko zile za Kiislamu.
b. Je jamii za jadi (zenye waamini wengi wa jadi kuliko wa dini zetu mbili kubwa) zimefanikiwa kiasi gani kulinganisha na Waislamu (ni lazima uwe na sehemu ya kucompare)? Wasafwa wana tofauti gani na Wazaramo?
c. Wasukuma kwa kuwa ndio kabila kubwa nchini kwanini hawana elimu sana kama jamii na hawaonekani katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini (underrepresented)?

Kusema Waislamu ndio pekee wenye matatizo na kuwa matatizo yao yamesababishwa na wao kuwa Waislamu SI KWELI.

Sijui kama unakubaliana na ile kauli ya Bwana W. Mkapa ya kuthibitisha na kuwa wengi kati ya Waislam wana matatizo na dhiki zilizosababishwa na kurithiwa toka kwa wakoloni?

Kama nilivyosema hapo juu sikubaliani na maono hayo kwani hayana msingi wa kihistoria tukichukulia all the other factors into consideration.

Unakubaliana na mimi kuwa Sheikh Mohammed Said alipoandika Historia ya Tanu/Tanganyika, hakuwa na madhumuni potofu au kukusudia uchochezi kama mnavyodai bali labda ni khitilafu kiduchu na dhahama tu za kitaaluma na kiuandishi na pia hakukusudia nia dhalili dhidi ya nchi yake na wananchi wenzie.

Sikubaliani na wewe kabisa. Nimemsoma Mohammed Said vya kutosha na ninaifahamu historia ya Tanzania vizuri tu. Mohammed Said aliandika kama Mwanaharakati wa Kiislamu; lengo lake (pamoja na wale wengine wa WARSHA) ilikuwa ni kuwapandikizia Waislamu hisia ya kuwa duni na kujihisi wanadhulumiwa. Hivyo kufikia lengo hilo ameandika historia upya, akipotosha matukio mbalimbali na akiweka hisia zake juu kuliko ukweli wa historia.
Nashukuru, na niwie radhi kama kuna masuala nimekuuliza tena. Najaribu kuangalia kama mpaka hapa mnakasha ulipofikia labda kuna majambo umeyaona na umepata kubadili fikra zako japo kiduchu.

Ahsanta.

Kwa kweli baada ya kusoma sana sijaona chochote ambacho Mohamme Said au mtu mwingine mwenye kutetea histohisia hii amesema kuweza kunishawishi fikra zangu. Nilichokiona ni kuwa tuna tatizo kubwa zaidi katika kufikiria, kutafuta ukweli, kupima ukweli na kuutetea. Kimsingi nimeamini kuwa wapo kati yetu ambao wanaogopa ukweli kwa sababu utawaondoa katika kile walichokiamini au kile ambacho wanaamini ni kweli. Kuogopa ukweli siyo sawasawa na kuujua ukweli. Ukweli unafungua. Mohammed Said ameficha historia, kapotosha matukio na kwa makusudi kabisa amechafua na kufunisha mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa nchi yake kiasi kwamba wapo baadhi ya watu wakiamini simulizi la Mohammed Said wanamuona Nyerere kama adui wa Waislamu na wanamlaani huko kaburini aliko.
 
Gombesugu,
Hayo hapo chini ni baadhi ya maneno niliyoandika katika pitio la kitabu ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' cha Dk. Harith Ghassany:Kwakipindi kirefu historia ya mapinduzi ya Zanzibarilikuwa ni ile historia rasmi ambayo imeathiri historia nyingi Afrika. Viongoziwa Afrika wanapenda ile historia itakayowakweza na kuwaonyesha wao katikamwanga wa kupendeza.

Vinginevyo historia hiyohaitakiwi.

Wazalendo wenyewe hawakuwa na hamu ya kuandika historia hii na watuwa nje walioandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar hawakupata kuifanyia hakihistoria ya Zanzibar labda kwa ugeni wao na kwa kuyaamini maelezo yaliyokuwa"wazi" kwa wakati ule, mfano mkubwa ukiwa ni kule kuamini kuwa mapinduzi yaZanzibar yalipangwa na makomredi wa Umma Party.
Hapajakuwapo udanganyifu mkubwa katika uandishi nautafiti kama huu.

Dkt Ghassany amekiweka chanouwanjani bila kawa. Akizungumza na Abdushakur Aboud wa Sauti ya Amerika DktGhassany amesema kuwa historia ya Zanzibar ni historia ya kujijuwa maisha yakeakiwa mjukuu wa babu wa mababu Muomani na mabibi wa Kimanyema na Kimwera –mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na Kiafrika.

Hii kwa hakika ndiyo historia yawananchi wa Zanzibar.

Ni tabu sana kumpata huyo Muarabu Zanzibar kila umuonaeMuarabu basi ana mjomba na shangazi Mwafrika.

Maadui wa Zanzibar wakiweka mkazo katika ubaguzi warangi na kuwafitinisha Wazanzibari. Ukweli huu ndiyo chanzo cha matatizo yoteyaliyoikumba Zanzibartoka vyama vya siasa vilipoanza katika miaka 1950 na matatizo yaliyosababishamauaji ya mwisho yakiwa mwaka 2001.
Ilikuwakatika barza yetu ya kawaida ya kunywa kahawa na kula pweza huku tukijadilihistoria ya Tanzaniaambako siku moja Mzee Mkwawa alinambia, "Mohamed nataka nikuambie kitu.

Unajuamimi nimehusika sana katika mapinduzi ya Zanzibar?"

NilimuangaliaMzee Mkwawa kwa makini.

Fikra yangu ya utafiti na uandishi ishashtuka haipo tenausingizini.

Mzee Mkwawa aliendelea, "Mimi ndiye niliyekuwa nikiwavushaWamakonde kutoka Kipumbwi kwenda Zanzibarkuipigia kura ASP na wakati wa mapinduzi mie ndiye niliyewavusha Wamakondekwenda kuipindua serikali ya Jamshid."

Sasa moyo wangu ukaanza kudunda kwanguvu.

Naisemesha nafsi yangu, "Huyu mzee anajua uzito wa maneno haya?"
Tuishiehapa.

Mzee MS, tatizo la kitabu unachosema ni bei. Nilikinunua Tanga pale Mwongozo shop kwa takriban 35,000 au 47,000/= moja kati ya bei hiyo. Na hii ni miaka 2/3 huko nyuma. Sijui kama imepungua au ndiyo imepaa. Akitaka watu wakisome kwa wingi lazima aangalie bei. Pia, kama unataka kujenga hii hadithi jaribu kumhoji upya Mzee Mkwawa kama yungali hai bado. Inaniwia vigumu kufikiria kikawaida alifanya "trip" ngapi za "wapiga kura" wake hadi ilete impact kwenye uchaguzi. Sikumbuki kama marehemu Ali Muhsin alitaja hiki kisa cha wapiga kura kuletwa. Nimesoma kitabu chake zamani. It could be walikuwa wanakodishwa wakiwa kama mashua nyingi kwa mpigo na sio yeye peke yake. The operation just seems to be too big for one canoe. Huyu baba na Field Marshall Okello je vipi? nakumbuka tuu kusoma katika kitabu cha Okello akisimulia kubakia na jeshi dogo la wapiganaji wakati wa mapinduzi na kufanya mitambiko ya kuchinja paka na vitu kama hivyo. Lakini kitabu cha Muhsin kinaonyesha kuwa British police officers waliokuwa zenj walikuwa wenye msaada kwa kuhakikisha local police officers hawana access ya ghala ya silaha siku husika. mi naona kuna gaps ambazo kwa anayetaka anaweza kuandika amother story.
 
Watu gani hao wanaoisoma historia ya TANU, Tanganyika vingine. Unaweza kuendelea kujifariji kwa namna hiyo hadi mwisho wa maisha yako hapa duniani. Kitabu kile hata kama kingeandikwa na Abdu kwa namna ulivyokiandika bado kingebaki ni simulizi tu. Kitabu kipo tangu 1998 kimekuja kuwa gumzo humu JF mwaka 2013! Historia ya TANU haiwezi kuokotwa kwenye

vikabrasha vya familia moja. Mtu mmoja akajifungia
chumbani kwa mkewe, akaibuka na historia ya sisi kuamini
kama mazuzu.

Asante sana mkuu kwaisema kweli,

Kweli hii ni chungu kwa Mohamed Said japo ni dawa kwa Vijana wanaounga mkono ngano hizo
 
Yericko,Hayo yote uliyosema ni kweli kabisa na wala mimi sijapinga hilo.Tatizo ni kuwa huwezi kuishia hapo.Utakaposoma sasa historia ya TANU ndipo hapo utakapokutanana Abdu Sykes, ndipo hapo utakapokutana na Chief David KidahaMakwaia.Vipi unakutanananao?Kitabu kitakuambia kuwa kabla ya Abdu kuonana na Nyerere 1952fikra ya kumpata kiongozi mpya wa TAA na kisha kuunda TANUalizungumza na Chief Kidaha 1950.Akili ya msomaji akifika hapo itamuuliza ehe ikawaje Abdu na ChiefKidaha?Hapo anasonga na kurasa za kitabu anasoma yale ambayo kwake nimageni kabisa - ni mambo mapya.Ninaposema historia imebadilika mabadiliko yeynyewe ndiyo haya.Si kama tutabadilisha uasisi wa Nyerere katika ujamaa na vijiji vyakekuasisi CCM nk. nk.Historia hii ya vijiji vya ujamaa hakika hana mpinzani ila hii ya kuasisiTANU ndiyo panapo maneno ya kuzungumza.
TANU imeundwa na kuasisiwa mwaka 1954. Mwalimu amekuwa kinara wake tangu mwaka huo hadi 1977. Miaka 23 mfululizo. Abdu hakuwahi kuwa kiongozi mkuu wa TANU wakati wowote ule katika uhai wake. Kama kuna ukweli mwingine kuliko huu basi hiyo haitakuwa TANU labda TAA. Historia ni lazima iambatane na tarehe na matukio halisi sio mambo ya kufikirika kama ilivyo kwenye DINI na misahafu yake. Hakuna kinachoweza kuibadili historia.
 
Shukran sana Mwanakijiji. This is one of the best analysis. By the way Nyerere angekuwa mtu wa kanda na dini kama juhudi za hivi karibuni mbona Mara ingekuwa mbali? Wakiristo kibao, waislamu kiduchu, rais Mara, Prime Minister Mara, Mkuu wa Majeshi Mara mbona jamaa kila nyumba ingekuwa na vigae!!!!! Suala hapa ni KAZI. Anayetaka aende Lushoto. Waislamu tele, hard work bila kipimo, maendeleo yao hayana mipaka.
 
Tujihadhar jaman na hizi thread kwani hazijengi zaidi ya kubomoa,

Ila hapo kwenye NECTA ninaweza nikaamini maana nakumbuka uzembe uliopitiliza wa NECTA uliofanywa mwaka jana ktk mitihani ya Islamic knowledge, Hapo sina ubishi kwa kile alichokieleza mzee Mohamed Said na wadau wengine.

Shardcole, ahsante kwa mchango wako. Binafsi nilishapotelewa mtihani (papers 2 wakati wa O level), hiyo ni kwenye late 70s. Nilichofanya ni kufuatilia pamoja na ushahidi wa shuleni kuwa nilikuwa kwenye mtihani husika. Mitihani hii (chemistry na Biology) haikupatikana. Practicals zilionekana. Eventually nilipewa grade stahili kwa criteria wanayoijua. Hili suala la NECTA lilikuja wakati waislamu wengi wanalisubiri kwa HAMU. Binafsi nawapongeza sana NECTA kwanza kusikiliza malalamiko. Pili kubali kupitia colums husika upya na kukiri kulikuwa na dosari. Tatu kukubali wahusika (waislamu) wajiridhishe kuwa sasa maksi ziko sawa. Lakini kubwa zaidi ni kutokutwa na mikingamo kuwa wanabeba baadhi ya shule. Popote, makosa ya data entry sio aghalabu kutokea. Tatizo ni pale kosa likikuta maelfu wanalisubiri ili walipuke.
 
Last edited by a moderator:
Watu gani hao wanaoisoma historia ya TANU, Tanganyika vingine. Unaweza kuendelea kujifariji kwa namna hiyo hadi mwisho wa maisha yako hapa duniani. Kitabu kile hata kama kingeandikwa na Abdu kwa namna ulivyokiandika bado kingebaki ni simulizi tu. Kitabu kipo tangu 1998 kimekuja kuwa gumzo humu JF mwaka 2013! Historia ya TANU haiwezi kuokotwa kwenye vikabrasha vya familia moja. Mtu mmoja akajifungia chumbani kwa mkewe, akaibuka na historia ya sisi kuamini kama mazuzu.

Wild Card,
Sina ugomvi na fikra yako.

Lakini nitakueleza jambo moja.
Kitabu hiki kimependwa sana.
 
TANU imeundwa na kuasisiwa mwaka 1954. Mwalimu amekuwa kinara wake tangu mwaka huo hadi 1977. Miaka 23 mfululizo. Abdu hakuwahi kuwa kiongozi mkuu wa TANU wakati wowote ule katika uhai wake. Kama kuna ukweli mwingine kuliko huu basi hiyo haitakuwa TANU labda TAA. Historia ni lazima iambatane na tarehe na matukio halisi sio mambo ya kufikirika kama ilivyo kwenye DINI na misahafu yake. Hakuna kinachoweza kuibadili historia.

Wild Card,
Hilo ulosema kuhusu Abdu ndipo ilipo nguvu yake.

Kuwa alikuwa nyuma ya pazia akisaidia TANU kwa hali
na mali yake kimya kimya...

Ndipo nilipomtoa uwanjani hapo sasa kikazuka kishindo
hiki ambacho na wewe kimekukumba.

Nani huyu Abdulwahid Sykes...
Sasa unapoanza kumsoma ndipo unaposoma historia ya TANU.
 
Back
Top Bottom