Wickama,
Ikiwa umeridhia na BAKWATA hilo hakuna wa kukuzuia.Binadamu lazima tughitilafiane hatuwezi kukubaliana kwa
kila jambo.Ila ngoja nikupe kitu huenda hukijui.Wale wote walioleta fitna ya kuvunja umoja wa Waislamwote wamekufa dhalili chini ya unyayo.Kuna waliotubia hadharani.Kuna waliosafiri hadi Zanzibar kumshika miguu SheikhHassan bin Amir na kutaka radhi.
Wapo wengine miili yao ilitahayar muda tu baada ya
kukata roho.Wapo waliosalitiwa na hao waliowasaidia kuivunja EAMWS.Lakini kubwa kuna aliyeomba dua Allah amuweke hai ashuhudiewote waliotia fitna wakidhalilika na Allah alimkubalia dua yake.Katika kundi lile la fitna alipokufa wa mwisho haukupita muda yeye akafa.Huyu ni Shariff Adnan mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Hassan bin
Amir.
Mohamed, kifo ni ahadi ya mwanadamu na Mola wake.
Hakuna anayejua kifo kitamkuta wapi na mazingira gani.
Mwenye uwezo wa kupanga hatima ya mwanadamu duniani na akhera ni mwenyezi mungu peke yake.
Mola ndiye anayejua atamchukua mja wake kwa namna ipi, lini na wakati gani.
Mohamed, acha kufur! wewe ni mwanadamu. Hao waliotangulia mbele ya haki wamekwenda kwa mola wao.
Hukumu ya mema na mabay yao yapo kwa mwenyezi mungu. Wewe hupaswi kusema hayo usemayo.
Mohamed, wewe ni mwanadam narudia! siku mola akipenda hujui utakuwa katika hali gani ya kicheko au kutahayari.
Hii ndio saikoloji unayotumia kuwatisha watu huko mitaani na vijijini. Kwamba atakayekataa maandiko yako ambayo umefikia mahali pa kuyapa hadhi ya dini, huyo atakufa katika dhalili au akitahayari.
Mohamed, Uislam ni dini wala si siasa au liwalo.
Dini inasimama yenyewe kwa miongozo yake, haihitaji uongo au uzushi na wala afanyaye hayo hana thawabu.
Ndio maana nasema matisho kama haya yanawatisha waislam wenye weledi na elimu kusimama na kuongoza matokeo yake ndio kama hivi.
Inasikitisha sana.