Unajua hadithi za kusimuliwa na kuumba umba zina matatizo sana. Gombesugu anadai Kitwana Kondo alikuwa na nguvu zaidi ya rais Mwinyi. Mohamed anasema Nyerere alikuwa anaongoza kwa remote na Mwinyi alikuwa hana ''say''.
Baadhi ya waislam wanasema ni ngumu sana kuvunja mfumokristo kwasababu wakristo wameushika. Gombesugu anathibitisha kuwa Kitwana Kondo ndiye alikuwa na Serikali.
Njozi anamsifu Kitwana Kondo kusimama kidete kutetea waislam. Mohamed anasema CCM ilimsusa akapoteza ubunge kwa msimamo wake wa mambo ya dini. Gombesugu anasema kulikuwa na Ugomvi na Sheikh Yahya kuhusu mabinti enzi hizo.Mohamed anasema walinong'onezana kuichagua CCM iliyomtosa Kitwana Kondo.
It's all confusing huwezi kujua nani anasema nini kwasababu story zinabadilika with time and kind of conversation.
Ndio maana huwaita ''half baked wasomi'' kwasababu nao wameingia katika mkumbo wa hadithi za vijiweni like any othe illiterate in the street.
Muheshimiwa Nguruvi3,
Kama siku zote anavyokuambieni
Sheikh Mohammed yakuwa mambo mengi mno yatakupeni tabu maana nyinyi ni wageni na Wazazi wenu pia ni wageni. Hapa hakuna chaos asilan,ni akili zako tu chechefu zinashindwa ku-comprehend.
Wallahi inastaajabisha,,nyinyi hapa jamvini hamna chochote wala lolote mfanyalo zaidi ya kuwa ma-
armchair/keyboard critics. Kitabu chenu hamtaki kuandika au kutunga,harakati za
Wazee wenu walivyopigania uhuru wa nchi hii hamtaki kutuletea au kutuonyesha,
hadithi za vinyozi wenu pia hamna. Mbona mnatia simanzi nyie wana wa
Nyerere!?
Mimi nimekupeni kiduchu tu na kwa mukhtasari "habari fulani",naona mmebaki midomo wazi kama vile mnaangalia
movies za James Bond.
Nguruvi3,kwa kifupi inakulazim umkubalie
Sheikh Mohammed,yakuwa wakati hivi vitu vinafanyika wewe ulikuwa bado uko kwenu
Magila na
Kicheba unacheza
Mdumange.
Kuhusu hayo matusi na kashfa ulonena dhidi
yetu/Waislam,hiyo wala si siri tena hapa jamvini. Awali nilipojiunga nilistaajabu mno. Ilinilazim kumuuliza
Mwanakijiji(maana yeye ndo kati ya wale Vinara wajifanyao ati wanaheshimu na kuwapenda mno
Waislam),hivi mbona mnashindwa japo hata kukemea kiduchu hii hali hapa jamvini!?
Mwanakijiji akajibu ati hilo tatizo kweli lipo,lakini yeye hana nguvu ya kuzuia au kukemea,maana hata yeye pia hutukanwa. Kwa kifupi nilishindwa kufahamu mantiki alotumia;kufananisha kutukanwa yeye binafsi na kutukanwa
Allah,Mtume Wetu na
Dini isiyopungua watu takriban
1.5bilion worldwide!?
Nyinyi watu mnachekesha,halafu mnadai ati mpo hapa kuondoa "uchochezi na uhaini" wa
Sheikh Mohammed ili kuepusha janga kwa Taifa,na ati nyinyi ndo wapenda amani!? Hapa mnashangilia na kuweka
"LIKE" kila kukicha hao viroboto wenu a.k.a
Abu jahal wanapomtukana
Al Marhum Mufti Sheikh Hassan Bin Ameir kwa kumwita
"ndumila kuwili".
Halafu nyinyi ndo mnadai ati mnatafuta amani ya nchi na
Sheikh Mohammed hana uadilifu na ni muhaini!?
Naona wenzio wanahangaika mno wanauliza, ati wapi watapata reference ili "wakachunguze" hiyo "movie" niliyowapa. Kwa kukusaidieni,maelekezo yenu tayari nilishamtumia
Wildcard jana.
Mmeletewa hoja kadhaa hapa na
Zali la Mentali,naona nyoote mmetokomea. Badala yake mmekaa w'end yoote ati kumzungumzia
Gombesugu...acheni utoto nyinyi watu wazima hasidi.
Ukipata fursa, mwambie
Jasusi akufahamishe kwa kina unyama na ubadhilifu uso mipaka ulofanywa pale
Wizara ya Mawasilianao na Uchukuzi na yule
Augustine Mwingira "
enzi ya Mwalimu". Halafu muulize Nyerere alifanza nini kwa huyo Mwingira na baada ya hapo alimpeleka wapi ili kumstiri!? Na hukohuko alikopelekwa na
Nyerere alifanya nini tena kwa kumtumia muhindi yule yule "
Lord" Rajpar!?
Najua hivi vitu kwenu ni miujiza iso kiasi. Lakini kwa kuwa baadhi yenu mnaamini yakuwa
Nyerere ni Nabii,sasa kwanini msikubali yakuwa hii miujiza aliifanya kwa huo
unabii mlompa!?
Poleni saana kwa maradhi mlonayo na udhaifu wa nyoyo.
Kuhusu habari za
Mzee KK,inalazim mkamuulize
Malecela pale Seaview. Maana Mzee KK ndo alokua
Godfather wa mmoja kati ya wanae wa kiume(amefariki). Na huyo huyo Mzee KK,ndo alompa huyo Malecela u-
Prime Minister baada ya kumwondoa
Sinde Warioba.
Kwa kifupi hiyo hoja mnayojaribu kuidadavua wala si kweli. Kama alivyokufahamisheni
Zali la Mentali kwa kina
;Nyerere alitawala kwa mabavu na kibri kingi wakati wake. Na muda wake "
ulipokwisha",aliingilia na kuvuruga mno tawala za waliomfuatia.
Mzee KK,ilimlazim ainigilie kati ili tu kumnusuru nduguye
Rais Ali Mwinyi,dhidi ya kundi la manyagumi waliobobea kwa fikra za udini na unabii wa
Nyerere wakiongozwa na
Sinde Warioba ,
Daud Ngelatuwa Mwakawago na
Getrude Mongela.
Kwa kifupi
Mwinyi alipata msaada wa dharura toka kwa nduguye...mutoto ya mujini,kitu ya fitna mingi,kitu ya Madrassa,mutu ya
Kariakoo.
Mzee KK,ana sifa nyingi saana na ni mtoto wa mjini anaejua fitna na
system yoote kwa mapana. Nafikiri mliona ghafla kilichowakumba wakereketwa wenzenu wa
Nyerere na jinsi gani Mzee KK alivyowasambaratisha na wako taabani mpaka kesho.
Wakati Nyerere anakuja mjini,
Mzee KK alikua tayari ni askari mwenye cheo kizuri kwenye
serikali ya wakoloni. Wazee woote wa mjini yeye pia ni Wazee wake,
informations zoote za ile
suirvellance ya wakoloni dhidi ya
Tanu,
Julius Nyerere na
Abdilwahid Sykes,ilikua ni
Mzee KK ambae anazileta kwa Wazee wake na hasa
Mzee Mangara Tabu na
Shariff Abdallah Al Attas.
Nyerere analilijua hilo fika. Lakini
Nyerere hakumsaidia asilan
Mzee KK alipopatwa na kesi ya kuchomekewa ya "
corruption", kama alivyowasaidia kwa udi na uvumba nduguze kina
Nyakyoma na
Mwingira. Katika "
kesi/shutuma" hizo
Mzee KK,alishinda kwa kishindo kwenye
Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kwa kifupi
Nyerere baada ya muda fulani alihisi/alijua kuwa
Mwinyi hampatilizi tena kwa kila alokua analazimisha.
Ndipo pale Nyerere,akaanza kucharukwa na kupanda majukwaani huku akizidi kujivunjia heshima. Huku mara kadhaa akitoa shutuma na matamshi machafu kwa Serikali kwenye vyombo vya habari na ati kuuliza huko
Ikulu kuna biashara gani!?
Nyerere vipi yakhe mbona huwachi kujisahau!? Umeacha nchi imeoza baada ya
miaka takriban 30 ya madaraka yako dhaifu,halafu unaanza kutaka kumlaumu
Mwinyi alokuja juzi tu;na kuwapa watu neema,fadhila na kuwatoa
tongotongo za macho na
ukakasi wa vinywa!?
Kwa hiyo wafahamishe jamaa zako,wasipoteze w'end yoote badala ya kujibu hoja za maana wanaleta mambo ya kitoto. Ati ooh! tushapata point ya kuwabana inabidi tuwaulize,je
Mzee KK nae ni mkatoliki? Hivi hamuoni aibu kwa hao wenzenu mnaojihisi ati ndo mpo hapa kwa maslahi yao?
Mfumo aliouasisi na kuucha
Nyerere bado upo mpaka kesho na tulishuhudia kwa mengi jinsi gani alivyoulinda kwa mabavu yoote mpaka mwisho...
Siku nyingine nitakuwekea,kwa kina jinsi gani
Nyerere alivyowatumia watoto wa Madrassa na wanywa kahwa vibarazani
Alhaj Issa Mtambo Gonera na
Alhaj Kitwana Suleiman Kondo ili kumsambaratisha mpinzani wake
Oscar Kambona.
Shukran.
Cc; Ami
Hii ni bashraf tu,maana kuna vitu vingine deep zaidi siwezi kuweka hapa jamvini alivyosababisha
Nyerere baina ya Waislamu tangia enzi hiyo na mpaka leo vinaleta farka baina yetu
Waislamu. Na utaona jinsi gani haohao
"Waislamu wa Mwalimu", Nyerere alivyowatupa baada ya shida/dhiki zake kwisha. Lakini nawastiri majina maana kama
Sheikh Mohammed Said asemavyo yakuwa;hao woote ni
ndugu zetu na ni
Wazee wetu wa karibu mno.