Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Shukran Gombesugu; Point yako imeeleweka. Kuna Baunsa anamkimbia NICHOLAS. Huko kakutana na swaga za saizi yake.Kaumbuka kiroho mbaya kabakia mdogo. Sasa anavinjari kanda ya ziwa. hahhahahahahah. Ngoja nimpe nakala Nicholas just in case

cc Nicholas (kwa taarifa)

Ha ha haa, wewe ndiyo unamuogopa huyo muulize mimi ni nani kwenye nyuzi za Chadema wote wanamtambua Ritz ni nani.

Mimi nimkimbie mtu JF ha ha ha haa, jikusanyeni Wakirsto wote wa Chadema kwangu mtatosha, ha haa ha, njoo kwenye uzi za Chadema ndiyo utanijua vizuri.
 
Wickama,
Basi sina sababu ya kushangaa.

Kuna msemo wa Kiarabu usemao: Ukishaijua sababu ile ajabu hutoweka.
 
Mimi sijakaa kimya wote hao uliowataja nimewajibu, na wewe nimekujibu baada ya kuleta kejeli kama kawaida yenu umeandika kina Sykes wanauza nyumba zao baada ya msiba kisha wanakimbilia mahakamani kugombea.

Mbona unajitoa ufahamu wewe umeaga kwenu kuja JF kumtetea Nyerere na kukashifu Uislam na Waislam pamoja na Wazee wetu hilo kwetu wala siyo tatizo hakuna tusi wala kashfa mpya ambayo utakuja nao kwenye hii sayari.

Unaposikia neno akili, kitu cha kwanza kukifikiria bila shaka siyo moyo, lakini tafiti za kisasa zimethibitisha moyo nao una erevu, ubongo wako ulio kichwani kwako unafanya kazi kwa bidii kwa kutii ujumbe wowote unaotumwa kutoka katika ubongo wako, ha haa ha.

Aiseee, Nimefurahi sana. At last nimepata ushahidi kuwa;

1. Uwezo wako wa kuchambua mambo uko kombo (nakutangulizia samahani kama utaona vibaya)
2. Nimesema sina kipaji cha kuaga wanangu kuja kumtumikia mtu humu JF. Tena MWENYE username na PASSWORD yake. Paragrah yako ya pili ina jibu jambo tofauti kabisa (lini Julius Nyerere akawa na username na password humu JF) waona mapungufu ya uwezo wako RITZ? Naongolea Bwana na mtumishi wake hapa JF wote wako HAI na wote wana username na passwords zao. Hii pia hutaelewa?????

3. Nyumba na Sykes ni habari aliyoandika Nguruvi. Sio mimi. Tena ukiisoma ile post Nguruvi amesema WAJANJA wa MJINI hakutaja jina la familia husika moja kwa moja kama unavyoliweka hapa. Wewe ni mchonganishi. Unataka kuwachochea watu wa familia hiyo ambao wanasoma hii thread wadhani Mchangiaji kawalenga wao majoa kwa moja. Alipomaliza Maelezo yake (Nguruvi) ndipo nimesema watu kugombea nyumba mzazi anapofariki ni kawaida na wengine wakaenda mahakani baada tu ya kuzika. Confusion yako iko wapi Sheikh?

4. Kwa mara ya kwanza leo NAKUTAMKA RASMI KUWA WEWE NI MUONGO. Lete post yangu yoyote kuanzia ya Kwanza ambayo NIMEKASHIFU UISLAMU. ILETE Ndio maana ya reference.

5. Siku zote (MIMI)nimesema wazee wetu walifanya bidii za kukomboa nchi kama wazalendo (kwanza) na kama waislamu/wakiristo (kibinafsi), wewe na wenzako nadhani mnaegemea kuwa walifanya jitihada zao za kuikomboa Tanganyika kama waislamu (kwanza) kwa Wakiristo(mko kimya) na wazalendo (kibinafsi). Hapo SIKUBALIANI NA NYIE, na najua tofauti hii haina tatizo na nguzo yoyote ya kiislamu bali inahusiana na mitazamo tofauti baina yangu na yako na ya MS. Kilio chako ni ili upate support ya wachangiaji wa kiislamu waniangukie kwa kudhani nadhalalisha dini hii. Nakukumbusha kuwa forum hii ni ya siasa na hamna IMAMU humu.

6. Kejeli unaziona tu pale kina Sykes au anapoguswa MS. Wewe unapotumia kebehi na kuwaita watanzania wenzio kuwa ni wakenya kwa sababu wao wanaishi Mara, wala hujijui kuwa UMEWATUKANA kwa vile roho yako umeshaizoeza kutusi watu kwa hiyo huoni tatizo.

7. Mwisho nakufahamisha rasmi kuwa mtu kuwa mwislamu humu JF sio LAZIMA ATII NA AKUBALI KILA LINALOTOKA KWA MOHAMMED SAID. HATA MTUME (SAW) ALIULIZWA MASWALI MAGUMU NA MASWAHABA-JISOMEE MKATABA WA HUDAIBIYA) SEMBUSE MOHAMMED SAID? UTII WA BILA KUULIZA NI UJINGA.

Jioni njema
 
Wickama,
Basi sina sababu ya kushangaa.

Kuna msemo wa Kiarabu usemao: Ukishaijua sababu ile ajabu hutoweka.

Mzee MS; sasa unaniacha nacheka, haya ndugu yangu ufike salama. Ngoja tumchune huyu chui japo tupate kongosho. hahahahahahah. Hukutaja mwenye mtego ni dini gani sheikh!!!!! code ilikuwa hapo.
 
Mkuu Wickama

Unapoteza nguvu kumkamua Ritz, hatoagi maziwa zaidi ya mashudu tu!

Shughulia na wenye afadhari kuliko huyo bora liende!
 
Aiseee, Nimefurahi sana. At last nimepata ushahidi kuwa;

1. Uwezo wako wa kuchambua mambo uko kombo (nakutangulizia samahani kama utaona vibaya)
2. Nimesema sina kipaji cha kuaga wanangu kuja kumtumikia mtu humu JF. Tena MWENYE username na PASSWORD yake. Paragrah yako ya pili ina jibu jambo tofauti kabisa (lini Julius Nyerere akawa na username na password humu JF) waona mapungufu ya uwezo wako RITZ? Naongolea Bwana na mtumishi wake hapa JF wote wako HAI na wote wana username na passwords zao. Hii pia hutaelewa?????

3. Nyumba na Sykes ni habari aliyoandika Nguruvi. Sio mimi. Tena ukiisoma ile post Nguruvi amesema WAJANJA wa MJINI hakutaja jina la familia husika moja kwa moja kama unavyoliweka hapa. Wewe ni mchonganishi. Unataka kuwachochea watu wa familia hiyo ambao wanasoma hii thread wadhani Mchangiaji kawalenga wao majoa kwa moja. Alipomaliza Maelezo yake (Nguruvi) ndipo nimesema watu kugombea nyumba mzazi anapofariki ni kawaida na wengine wakaenda mahakani baada tu ya kuzika. Confusion yako iko wapi Sheikh?

4. Kwa mara ya kwanza leo NAKUTAMKA RASMI KUWA WEWE NI MUONGO. Lete post yangu yoyote kuanzia ya Kwanza ambayo NIMEKASHIFU UISLAMU. ILETE Ndio maana ya reference.

5. Siku zote (MIMI)nimesema wazee wetu walifanya bidii za kukomboa nchi kama wazalendo (kwanza) na kama waislamu/wakiristo (kibinafsi), wewe na wenzako nadhani mnaegemea kuwa walifanya jitihada zao za kuikomboa Tanganyika kama waislamu (kwanza) kwa Wakiristo(mko kimya) na wazalendo (kibinafsi). Hapo SIKUBALIANI NA NYIE, na najua tofauti hii haina tatizo na nguzo yoyote ya kiislamu bali inahusiana na mitazamo tofauti baina yangu na yako na ya MS. Kilio chako ni ili upate support ya wachangiaji wa kiislamu waniangukie kwa kudhani nadhalalisha dini hii. Nakukumbusha kuwa forum hii ni ya siasa na hamna IMAMU humu.

6. Kejeli unaziona tu pale kina Sykes au anapoguswa MS. Wewe unapotumia kebehi na kuwaita watanzania wenzio kuwa ni wakenya kwa sababu wao wanaishi Mara, wala hujijui kuwa UMEWATUKANA kwa vile roho yako umeshaizoeza kutusi watu kwa hiyo huoni tatizo.

7. Mwisho nakufahamisha rasmi kuwa mtu kuwa mwislamu humu JF sio LAZIMA ATII NA AKUBALI KILA LINALOTOKA KWA MOHAMMED SAID. HATA MTUME (SAW) ALIULIZWA MASWALI MAGUMU NA MASWAHABA-JISOMEE MKATABA WA HUDAIBIYA) SEMBUSE MOHAMMED SAID? UTII WA BILA KUULIZA NI UJINGA.

Jioni njema
552673_600966883252741_1976569725_n.jpg
 
RITZ; hili swali hukujibu ndugu yangu;

WHAT ARE YOU?

kindly provide details.
 
Nakufungua akili kwa mara ya pili, japo hili tulishalieleza mwanzo mwa mjadala huu kwa ufasaha zaidi na welevu walielewa!

1) AA ilianzishwa kwa msaada/amri ya Gavana wa Tanganyika Sir Cameron 1929,

Rais wake wakwanza kabisa akawa ni msomi Mwalimu Cesil Matola,

Mkutano wake wakwanza kabisa ulifanyika nyumbani kwa Cesil Matola (Myao)

Uongozi kamili ulikuwa hivi:

Rais: Mwalimu Cesil Matola (Myao)

Katibu: Klest Sykes (Mzulu wa Afrika ya Kusini) mstaafu wa jeshi,

Muhazini: Ramadhani Ally (Mzaramo) mvuvi na mfanya biashara wa samaki

Baada yahapo ilipofika 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake "ikakaimiwa" na Klest Sykes hadi 1948 ilipozaliwa TAA kwa MLENGO uleule wa Sir Cameron!

Narudia, ikazaliwa TAA kwa MLENGO ule ule wa Sir Cameron!

1953 Mwalimu Julius Nyerere anaingia katika uongozi wa juu wa TAA na kuanza mageuzi ya kukifanya kuwa chama cha siasa!

Ni Julius Nyerere ndie aliyeiandika KATIBA ya TAA iliyopelekea kuzaliwa TANU,
Yericko Nyerere,

Mbona haueleweki kila siku unakuja na kauli tofauti tofauti au kwa sababu hakuna anayehoji source ya mabandiko yako.
AA imeundwa 1929 chini ya Mwalimu Cesil Matola,

1933 AA ilimkasimisha madaraka katibu wake bwana Klest Sykes, hii ni baada ya Matola kufariki,

Mwaka 1948 Klest Sykes anaasisi TAA, na mwaka huohuo anapinduliwa na Daktari kijana Vedasto Kyaruzi anashika urais wa TAA,

Katibu anakuwa Abdul Sykes kaka wa Ally Sykes,
Hapa unasema vingine na hapa chini unasema vingine.
1) AA ilianzishwa kwa msaada/amri ya Gavana wa Tanganyika Sir Cameron 1929,

Rais wake wakwanza kabisa akawa ni msomi Mwalimu Cesil Matola,

Mkutano wake wakwanza kabisa ulifanyika nyumbani kwa Cesil Matola (Myao)
ha haa haaa kutokana na watu kumeza kama mamba wanashindwa hata kuhoji source.
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere,

Mbona haueleweki kila siku unakuja na kauli tofauti tofauti au kwa sababu hakuna anayehoji source ya mabandiko yako.

Hapa unasema vingine na hapa chini unasema vingine.

ha haa haaa kutokana na watu kumeza kama mamba wanashindwa hata kuhoji source.

Hautaelewa kamwe kwakuwa haupo tayari kuelewa!

Akili yako imedumaa kwa ngano za Mohamed Said!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Wickama

Unapoteza nguvu kumkamua Ritz, hatoagi maziwa zaidi ya mashudu tu!

Shughulia na wenye afadhari kuliko huyo bora liende!

Tunaanza na hii
Nikubaliane nae kuwa historia ya nchi yetu inamapungufu na inahitaji masahihisho, lakini kwa hili la Mohamed si masahihisho bali ni upotoshaji mkubwa, Uchochezi na ni Uhaini kwa nchi. Kwa bahati mbaya bwana Mohamed Said histori anayoisimamia ameiakisi kuanzia miaka ya 1950+ tu,

Hajajishughulisha kuutazama utawala wa Kiingereza wala kuutazama upya utawala wa Kijerumani ambao ndio uliosimika misingi ya utawala na mifumo mingi ambayo leo tunaitumia! Mjerumani mfumo wake wa utawala kwa ASILI ni wa kikristu na kwa Tanganyika walisimama hivyo bila kutetereka! (Yaani mfumo kristu 100%)

Akaja Muingereza na yeye mfumo wa utawala wake wa ASILI ni wakikristu!

Imenilazimu kitabu cha bwana Mohamed Said kiitwacho "Maisha na nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968" (Historia ya uhuru iliyofichwa ya upande pili) kukiita ni NGANO za masika.

Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.

Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 – 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.

Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake.

Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake,

Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa.

Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.

Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.

Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya mchikichini Mzizima na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 34 tu, hiyo ni mwaka 1880 hadi 1953

Nje ya kuhudumu katika uislamu, alikuwa ni mvuvi aliyevua pamoja na Ally Ramadhan mwekahazina wa kwanza wa AA,

Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL)

Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele za cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu,

Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake!

Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao.

Elimu,

Woga

Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake.

Mnamo tarehe 7/7/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia!

Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 , Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa Kasisi Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni boss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.

Mpaka hapo ndugu yangu Mohamed Said angalau umepata picha kwa KIFUPI tu ya harakati za uhuru chini ya kanisa.

Nikipata wasaa nitakuletea picha za Mwalimu Nyerere na Edger Aristide Maranta

Kwanini Kasisi huyu wa kikatoliki Edger Aristide Maranta hatajwi popote katika historia ya nchi? Kwanini kanisa katoliki halilalamiki kutokuwepo kwenye kitabu cha kivuko?

Yote hayo nitakushushia taratibu kadiri mnakasha huu unavyoenda.

Sasa nini kilifuata baada ya uhuru?
Sources of information?
 
Back
Top Bottom