Kadogoo,
Dhana kwamba kuna watu waliliwa na simba kwenye vijiji vya ujamaa ni uwongo mtupu. Na kama watu walikula yanga si ni heri kuliko kufa njaa kama ilivyotokea Ethiopia?
Mzee Jasusi,
Niwie radhi kuingilia majadiano yenu kiduchu na nduguyo Kadogoo.
Lakini roho imenuma nimeshindwa kustahamili,kwanini unataka kupotosha ukweli kwasababu tu ya mahaba yako ya upofu kwa Nyerere a.k.a "Baba wa Taifa"
Mimi binafsi nazijua Family 8,zilizoliwa na simba wakti ule wa ile Social experiment/Sera ya "Vijiji vya Ujamaa" ya Nyerere.
Njia ya kwenda Mtwara/Lindi...pale njia panda ya Nangurukuru nafikiri pana kijiji kinaitwa Sinza,mbele kiduchu kuna kingine kinaitwa Miteja Sinza. Unaingia ndani kama maili sita hivi kuna kijiji kingine kinaitwa kwa Songoro.
Hapo kuna watu/wanakijiji wanne walidhuriwa na kuuwawa na simba. Mmojawapo ya watu waliouliwa na simba katika hicho "kijiji kipya" ni Mke wa Sheikh/Imam wa msikiti Marehemu Mzee Mwinchande Saleh,akiitwa Bibi Mame Koroboi.
Barabra kuu ya kwenda Tanga/Arusha pale Mkata...ukiingia ndani kama unaelekea Handeni pana kijiji cha KwaChaga...ingia ndani kama maili kumi utafika KwaNkonje.
Huko kwenye "kijiji kipya" cha Nyerere nako pia walikufa watu kadhaa kwa kutafunwa au kujeruhiwa na simba.
Kati ya watu maarufu waliokufa/kuliwa na simba alikuwapo pia Mchawi/Mtabibu mkuu wa kijiji wakti huo Marehemu Fundi Idd Khatib Kihongwe na Msaidizi wake John Mwinyikheir.
Kuna mengi mno kuhusu Wananchi kuliwa na Simba kutokana na ile sera mbovu ya Nyerere ya "Vijiji vya Ujamaa".
Alipoamrisha na kulazimisha kuwahamisha Watu/Wananchi kinguvu bila ya ridhaa zao, kutoka kwenye vijiji vyao vya asili na kuwatokomeza kwenye misitu/mbuga,kabla hata hakujawa na huduma zozote/yoyote muhimu inayostahili ili Mwana-Adam kuwezaishi!?
Wananchi wengi walilazimishwa kuacha mali zao,nyumba,makaburi na mashamba yao ya asili nyuma,huku hawajui wendako ni wapi na watakuta nini!?
Inasemekana kuna baadhi ya Wananachi walijinyonga na kupoteza maisha kwa hasira zao na kutojua la kufanza!? Hili sina hakika nalo,lakini nimepata kulisikia mara kadhaa.
Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu kiduchu.
Ahsanta sana.
Cc;Ritz,Kadogoo