Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kinachotokea Ukraine ndhicho kitakachoipata Israel mbele ya Hamas.Ukraine na Israel wote wanafanana kwa viwango vya kiburi vita vilipoanza.
Ukraine alipoona uchumi wake ni mkubwa akaamua kuichokoza Urusi na vita vilipoanza na misaada ikaamiminika aliamini ataishinda Urusi na kujizolea sifa kutoka nchi za NATO.
israel nayo kwa muda mrefu imejiamini sana kwa maendeleo ya kiteknolojia na urafiki wa hali na mali kutoka nchi za magharibi.
Baada ya kupigwa na Hamas hapo Oktoba 7 imejiamini kuishinda Hamas na kutekeleza mipango yake ya siri iliyokuwa mezani.Imeamua kupingana na ushauri wa kila mmoja kuanzia UN mpaka majirani zake miongoni mwa nchi za kiarabu.
Baada ya wiki moja tangu kuingiza vifaru vyake rasmi Gaza na kupiga kwa nguvu kubwa bado haijaweza kuzuia sauti za wapiganaji wa Hamas ambao wamo ndani ya mahandaki.
Pamoja na kuwakatia chakula,maji na umeme sauti za wapiganaji wa Hamas zimeendelea kusikika kote duniani.Wamesema bado jeshi la ardhini halijaingia katika eneo la kaskazini ya Gaza na kwamba wamevipiga vifaru jumla 24 vya Israel
Iwapo wapiganaji wa Hamas wataendelea kuhimili vita hivyo kwa mwezi mwengine mmoja ujao.Hali inaonesha jeshi la Israel litachoka na silaha zao za kutoboa ardhi zitapungua sana katika wakati viongozi wa Marekani wameonesha kukereka na kiburi cha Israel kutosikiliza malalamiko ya hata wao wafadhili wao.
Kwa upande mwengine upinzani ndani ya Marekani na nje kwenye mataifa mengine kutazidi kupunguza nguvu za mapigo ya Israel ndani ya Gaza.
Katika hali hiyo ushindi wa Hamas unaweza ukaja katikati ya unafiki wa nchi za kiarabu ambazo zimeonesha kutokuwa na uchungu wa maangamizi ya ndugu zao wa Palestina kuliko uchungu wa mataifa mengi ya dunia kuanzia Spain,mpaka China na Japan.