Uchukuaji fomu usiwatishe. Ni mradi kama mingine

Uchukuaji fomu usiwatishe. Ni mradi kama mingine

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,264
Natatizwa na wanaohofia hili wimbi la uchukuaji fomu, hasa za ubunge kwa tiketi ya ccm. Ni haki yao kulingana na katiba yao na ilani yao. Kadhalika ni takwa la kikatiba mradi tu ujue kusoma na kuandika.

Binafsi naamini kuwa vyombo vya uteuzi ndani ya ccm havitafanya makosa kama awali. Bunge lililopita lilijaa wabunge hewa ambao hawakujua nini lengo lao la kuwa pale. Walijua tu kwamba wataenda kuomba lami na zahanati. Kumbe kuna suala la utungaji sheria na masuala mengine ya kitaifa.

Hizo laki 5 sio ndogo hasa wakiwa watia nia ni wengi. Babati mbaya kutokana na trend ya 2020 kuja 2025, Bunge lilipokea watu ambao sio sahihi. Sasa kuna kundi huku nje wakaona kumbe ni mteremko. Hali hii sio sawa.

Tulitegemea hao watu waonyeshe ujasiri na kwenye nafasi ya urais ila ni waoga. Muhimu hata shule hukusanya sana hela za kujiunga ila huchagua wale muhimu wa wenye vigezo tu. Hivyo ccm na vyama vingine msituangushe. Hatutaki Bunge letu liwe uchochoro wa kupitisha sheria ambazo zitatugharimu huko mbeleni
 
Mheshimiwa Mkojani Bin Daruweshi, Mheshimiwa Jeshii.
Wakenya wana haki kutusimanga baada ya kuona CV za Wabunge wetu.
 
Hata wasomi wanahofia kuchukua fomu sasa kuhofia hawa wenye masihara
 
Yan shilole nae anataka ubunge 😂😂😂😂😂😃 hakuna kazi raisi kama ya ubunge Tanzania... no kupiga meza na kusema ndio mzee na kuruka sarakasi kama unaweza alafu ikifika kipindi cha uchaguzi ni kubwa pikipiki na kofia nyiiingi alafu wapumbavu wanakuchagua tena au unaiba kura unarudi tena bungeni and the loop goes on kazi unakuwa ni kuwatuma kina lukasi kububujikwa na machozi na kina tlaataah kusema gentleman kazi inafanyika kwa Maliki ya ujira mdogo tena wa hela za kodi za watanzania wenyewe. Hakuna sehemu rahis kuitafuna nchi kama Tanzania na CCM ndio mana kuna group kubwa la wapumbavu wengi wamekimbilia kuchukua fomu huko ccm na wanautaka ubunge sababu ukiwa mbunge wa ccm huitaji akili yan ccm kazi yao ni kubebana tu hata kama nchi inazama hakuna kufanya logic na reasoning ya mambo. Kila mpenda urahisi wa mambo anajiita na majizi ili waibe wote vizuri. Inasikitisha sana
 
Baba Levo baada ya kupigwa maswali "magumu" na Kipotoshi sidhani kama atakuwa tena na hamu ya kuchukua fomu. Jamaa alijua kumuaibisha 😁
 
huyu nae kachemka. Sidhani kama alichanga karata zake vyema. Moshi VIJIJINI? Hata mjini sidhani maana sijaona hata akijinasibisha na Kilimanjaro, achilia mbali Moshi, tena vijijini
20250701_171509.jpg
huyu
 
Vipi dimond na harmonize wao hawachukui form za ubunge?
 
Assume ubunge wamechukua watia nia 8000 x 500,000/- Hiyo ni bilioni 4 ndani ya wiki tu.
20250703_141111.jpg
 
Back
Top Bottom