Uchumba wa Jackline Wolper wavunjika

Uchumba wa Jackline Wolper wavunjika

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
ULE uchumba wa mwigizaji Jacqueiline Wolper na Mkongo ambao ulipamba vyombo vya habari kwa miezi kadhaa iliyopita, hatimaye umevunjika rasmi huku daktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dk. Fadhili Emily akitajwa, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

Wolper alivalishwa pete ya uchumba kwa mbwembwe katika hoteli moja moja maarufu jijini Dar ambapo mwanaume huyo raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo aliahidi kumuoa hivi karibuni huku akijiweka karibu na ndugu wa Wolper.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Wolper, kabla Dk. Fadhili hajatia ?saundi?, tayari Wolper alikuwa ameshapishana na Mkongo huyo hivyo Dk Fadhili alipata kazi rahisi kuvunja uchumba huo maana amekuta unasuasua.

?Wolper alikuwa ameshatofautiana na jamaa, lakini jamaa alikuwa hakubaliani na matokeo akawa anaendeleza uchumba kwa tabutabu sasa alipotokea Dk. Fadhili na kuingiza nyavu, fasta tu Wolper akawa amevunja uchumba wa awali na kuunga uchumba mpya,? alisema mtu huyo wa karibu na Wolper.

Mara baada ya ubuyu huo kutua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda, mwanahabari wetu alimtafuta Wolper ili aweze kuzungumzia taarifa hizo ambapo alipopatikana alikiri uchumba wake na kutofafanua vizuri kama uchumba huo umevunjwa na Dk. Fadhili.

?Ndiyo uchumba umevunjika kwani tatizo liko wapi? Kuhusu suala la nani ameuvunjia mbona sioni umuhimu wake, iwe ni huyo dokta (Dk. Fadhili) au mwingine yeyote sawa tu kwani haya si ni maisha yangu binafsi,? alisema Wolper.
 
Nilijua tu, hayo mambo ya kuvishana pete uchororoni uishia uchochoroni, mwenyewe yuko busy na ukawa sasa hivi
 
Huyu demu hatareee....dyudyuu ya ngapi hiyo?
 
Haaa chezea sala za mkewe akae afanyaje

Ndio wakome wanaodanfia waume wa watu

Na huko nako analo lazima kama hajaoa.
 
Atajijua....matokeo ndio habari ya mujini.
 
DOKTA-FADHILI-AMZAWADIA-ZARI-BAISKELI1.jpg
 
Atajijua....matokeo ndio habari ya mujini.

Wakati wa kampeni mbona alikuwa anaitwa majina matamu ya kikamanda na anayemsema anasakamwa.
Kampeni zimeisha na hata matokeo hayajatoka imekua 'atajiju' 😃😆
 
Mmh maisha ya movie hayo sijui imefikia part gani? Wacha nishangilie ushindi kwanza
 
Wakati wa kampeni mbona alikuwa anaitwa majina matamu ya kikamanda na anayemsema anasakamwa.
Kampeni zimeisha na hata matokeo hayajatoka imekua 'atajiju' 😃😆

Hahahaha umenichekesha sana
 
Back
Top Bottom