Uchumi Mamboleo; Timu haijengwi na Washambuliaji Pekee

Uchumi Mamboleo; Timu haijengwi na Washambuliaji Pekee

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kumetokea Kasumba ya Watengeneza Sera kuwa Wauza Sura na Wapiga Brah Brah; Kama vile walivyo wapiga ramli wanatafuta mchawi kwa kuwaambia wadau makosa ni yao kwa kutokufanikiwa...

Wanasema kila kitu ni Biashara kana kwamba vingine vyote havina maana; Yaani hata Timu sababu Mfungaji ndio anafunga magoli lakini hata kipa anazuia na ma-middle wanagawa pasi... (Ndio Biashara ni Muhimu ila ni muhimu kama kiungo cha Mchakato Mzima)

Sasa iweje mkulima anapokosa masoko tumalaumu mkulima ? Je tunataka Mkulima huyu ndio awe marketing, au salesman n.k. ? Tunawaambia watoto hiki au kile hakilipi someni hiki au kile ndio kitalipa (Ukulima au wakulima wanaotulisha value yao tunaipima vipi) ? Umasikini wao haimanaanishi wanachofanya hakina Tija kwa Jamii....

Turudi kwenye basics kila kitu kina maana na manufaa; Specialition and Division of Labor (Kila mtu afanye kwa upande wake kwa ufasaha na sio kulaumu wengine kwa shortcomings zetu) Mazao yakiwa machache tumalaumu mkulima lakini masoko yakikosekana watunga Sera wawajibike
 
Turudi kwenye basics kila kitu kina maana na manufaa; Specialition and Division of Labor (Kila mtu afanye kwa upande wake kwa ufasaha na sio kulaumu wengine kwa shortcomings zetu)
Exactly, hapa ndio penyewe.

Kila mtu akifanya kazi anayojitambia kuwa ni yake papo hapo tayari tunakuwa wenye maendeleo.

Mi nnasemaga kwa maendeleo ya vitu tuliyofikia hatuhitaji vitu saaana sasa hivi zaidi ya uhakika wa vitendo.

Msomi na auishi usomi kweli
Fundi ufundi kweli
Mwanasiasa vilevile
Mwananchi vilevile
Mkulima, mfanyabiashara, mwanafunzi, mfagiaji barabara, askari, hakimu, daktari nk
Kila mtu akitimiza wajibu aaaah mbona maisha matamu tu.

Tusipotimiza wajibu yaani unaweza kupata taabu hadi katika jambo la raha kabisa. Ukisikia wanaosema ndoa ni mateso chunguza utimizaji wao wote wa majukumu yao. Yaani hadi vitu vitamu kama sex mtu anaweza tu kuiona chungu.

Consequently; Nchi ya maziwa na asali inaweza kuonekana chungu kama shubiri (shubiri yenyewe ata sijawah ionja😁😆) ikiwa tu wenye nchi hawataki kutimiza majukumu kwa nafasi zao.

Nchi yoyote ikifikia hatua kila mmoja anatimiza majukumu yake inakuwa watu wake wanaishi 'mbinguni'!

Sasa ushauri: usisubiri hadi nchi yote itimize ili wewe mwananchi uishi mbinguni. Anza na familia tu, jitengenezeeni mbingu yenu wenyewee🙃. Na ikikushinda familia yako how the hell do you expect to do it nationwise!?
 
Sasa ushauri: usisubiri hadi nchi yote itimize ili wewe mwananchi uishi mbinguni. Anza na familia tu, jitengenezeeni mbingu yenu wenyewee🙃. Na ikikushinda familia yako how the hell do you expect to do it nationwise!?
Iwapo famili hii ni ya mkulima ambaye amelima kwa kudhani kwamba atauza nje na soko litakuwepo alafu anamaliza anaambiwa mpaka uwe na vibali..., wakati mwaka juzi alilima soko halipo na vitu kuonzea mashambani hata kushindwa kupata chakula....

Je ataweza vipi wakati amekosa pesa ya kutimizia familia yake kutokana na uzembe amabao sio wake ? Au aanze kusoma tuition ya masoko na kabla hajalima ajihakikishie masoko ? Na masoko haya atayapata vipi wakati wao wanataka mzigo mkubwa wakati yeye ana gunia mbili ?

Utasema labda ajenge ushirika na ashirikiane na wenzake wawe na nguvu (labda amejaribu lakini wanamuona tapeli) ?

Je katika hayo kweli Watunga Sera hawahusiki ?; Kwa manufaa ya mmoja mmoja ni jukumu la mtu binafsi ila kwa manufaa ya wote ni either wote wanaungana au watunga sera kuwaunganisha ili waunganishe nguvu na kuweza kuwa kitu kimoja - Sio kutafuta mchawi (Ingawa mchawi anajulikana na ni hao tunaowalipa ili waweke mambo sawa na hawafanyi kazi zao)
 
Utasema labda ajenge ushirika na ashirikiane na wenzake wawe na nguvu (labda amejaribu lakini wanamuona tapeli) ?

Je katika hayo kweli Watunga Sera hawahusiki ?; Kwa manufaa ya mmoja mmoja ni jukumu la mtu binafsi ila kwa manufaa ya wote ni either wote wanaungana au watunga sera kuwaunganisha ili waunganishe nguvu na kuweza kuwa kitu kimoja - Sio kutafuta mchawi (Ingawa mchawi anajulikana na ni hao tunaowalipa ili waweke mambo sawa na hawafanyi kazi zao
Wote wanaohusika, wanahusika haachwi mtu. Mambo hayatokei tu bila sisi, sisi(wote) ndio tunaoyafanya mambo yatokee
 

Attachments

  •  Emurasta.jpg
    Emurasta.jpg
    46.3 KB · Views: 2
Wote wanaohusika, wanahusika haachwi mtu. Mambo hayatokei tu bila sisi, sisi(wote) ndio tunaoyafanya mambo yatokee
Binadamu sio kisiwa..., Ni kama vile timu; kama wewe ni Kipa na umezuia mikwaju yote na kila kona zikipigwa unaenda mbele na kubahatika kufunga mawili mwisho wa siku kama mlihitaji kufunga tatu ili muendelee na mkashinda mbili bila..., huwezi kusema ni kosa la kipa (kuna washambuliaji pia yaani outfield players hawakufanya kazi yao)..., mashabiki walifanya wajibu na wewe kama kipa ulifanya zaidi ya wajibu....

Ndio hayo nayosema peasants kule kijijini anafanya na ameendelea kufanya zaidi ya wajibu wake katika hii jamii yetu ila wengine ndio wanaomuangusha..., hata ukisema kuendelea kwake kutumia nyenzo za kizamani na kutumia / kusubiri mvua huenda sio efficient; ila ni lini watunga sera wamemsaidia kujenga Bwawa na kupeleke tractor na combined harvesters akakataa..., Unaweza kusema pesa zitoke wapi ?!! (Huenda zile wanazomlaghai wakati wa uchaguzi wangempa wakati wa maandalizi ya kilimo wala hasingehitaji kulaghaiwa....)
 
Back
Top Bottom