Uchumi: Nchi zilizobaki za EA kufikia uchumi wa kati baada ya miaka 20 ijayo

Uchumi: Nchi zilizobaki za EA kufikia uchumi wa kati baada ya miaka 20 ijayo

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
WAKATI Tanzania ikitangazwa kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kipato cha kati, Kamisheni ya Uchumi Barani Afrika imesema nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiondoa Kenya, zinaweza kuingia katika kundi la nchi hizo baada ya miaka 20 au 50 ijayo.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Kamisheni hiyo, Carlos Lopes, mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakati alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari baada ya Benki ya Dunia kutaja baadhi ya mataifa ya Afrika kuingia katika uchumi wa kipato cha kati.

Kwa mujibu wa Kamisheni hiyo, nchi zitakazoweza kutafsiri maendeleo ya kilimo yaende sambamba na ukuaji wa viwanda, zinaweza kufikia lengo hilo baada ya miaka 20 ijayo yaani mwaka 2040.

Aidha, alisema nchi ambazo zitashindwa kufanya mabadiliko hayo na kuendelea kukumbatia kilimo cha kizamani, zitayafikia malengo hayo baada ya miaka 50 ijayo yaani mwaka 2063.

Kwa mujibu wa Lopes, mataifa ya Afrika Mashariki yaliyoingia katika orodha ya kuwa na uchumi wa kipato cha kati yamesaidiwa na vipaumbele vya kiuchumi vya nchi hizo kuchangia kiwa kiasi kikubwa kuinua uchumi na pato la nchi.

Kati ya nchi za Afrika Mashariki, nchi zilizofanikiwa kuingia katika orodha ya nchi zenye uchumi wa kati ni Kenya ambayo iliingia tangu mwaka 2014 na Tanzania ambayo imeingia mwaka huu kinyume na matarajio yake ambayo ni kufikia hatua hiyo mwaka 2025.

Katibu huyo ndiye mwenye dhamana ya kushajihisha uchumi wa mataifa ya Afrika pamoja na kuratibu mtangamano wa kiuchumi wan chi hizo kwa kutambua na kuhimiza hatua zaidi za kuboresha mtangamano wa kiuchumi.

“Ninafanya kazi kwa karibu na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) pamoja na Kamisheni ya Umoja wa Afrika, kuna mawimbi makubwa ya maendeleo katika mataifa mengi ya Afrika. Utulivu wa kiuchumi wa Afrika Mashariki unamaanisha mengi sana,” alisema Lopes.

Alisema kilichoifanya Afrika Mashariki ifanikiwe ni kutokana na kutafsiri maendeleo ya kilimo katika mataifa hayo na kuwa maendeleo ya viwanda yaliyosababishwa na ukuaji wa sekta ya kilimo.

Tanzania yaikosha Kamisheni ya Uchumi barani Afrika

MY TAKE: Wakati Tanzania imeingia ktk uchumi wa kati miaka mitano kabla ya ilivyotegemewa, nchi zilizosalia za Rwanda, Uganda na Burundi, zinategemewa kufikia hatua hiyo miaka 15 baada ya muda waliojipangia. Tanzania hoyeeeeee.
 
Duuh kumbe mambo bado sana jaman...Sasa kwa mwendo huu miaka kumi ijayo nadhan Tz itakua upper middle income maana kama leo hii tuko hapa na mambo mengi bado all jikoni sijui yakiiva itakuaje...imagine kabla JPM hajaondoka madarakani vijiji vyote vinaumeme,Tatizo la maji safi litabaki historia,barabara zimebaki wilaya chache tu kwa sasa kuunganishwa,karibu kila kijiji kina zahanati kila kata kuna kituo cha afya kila wilaya one hospital kila mkoa una hospitali ya rufaa
 
Kwahivyo Kenya itakuwa iliwatangulia hawa vibwengo kwa miaka kama 27 hivi? Maanake Kenya iliingia kwenye kundi la uchumi wa kati mwaka wa 2014. Alafu mwaka huu wa 2020 Kenya imeingia kwenye kundi lingine la uchumi wa '3 digits'($100B+). Sijui majirani zetu wengine ukanda huu wa Afrika Mashariki na ya Kati, isipokua Ethiopia ambao wananusia nusia, watafikia hatua hiyo miaka mingapi ijayo? Itakuwa miaka 15,20,25 au labda 30? Yaani kwenye masuala kama hayo Kenya huwa tupo kwenye upweke wa aina yake, mithili ya paka shume. Sio siri bana, ukanda huu Kenya ndio baba lao. [emoji1139][emoji1139][emoji1139]
 
Tanzania yaikosha Kamisheni ya Uchumi barani Afrika
MY TAKE: Wakati Tanzania imeingia ktk uchumi wa kati miaka mitano kabla ya ilivyotegemewa, nchi zilizosalia za Rwanda, Uganda na Burundi, zinategemewa kufikia hatua hiyo miaka 15 baada ya muda waliojipangia. Tanzania hoyeeeeee.
Ġoodluck

@RealHauleGluck
·
Jul 6

#UchumiWaKati: Tanzania ni moja ya nchi kwenye orodha ya nchi maskini zaidi Duniani mwaka 2020!
1594137542958.png
 
Kwahivyo Kenya itakuwa iliwatangulia hawa vibwengo kwa miaka kama 27 hivi? Maanake Kenya iliingia kwenye kundi la uchumi wa kati mwaka wa 2014. Alafu mwaka huu wa 2020 Kenya imeingia kwenye kundi lingine la uchumi wa '3 digits'($100B+). Sijui majirani zetu wengine ukanda huu wa Afrika Mashariki na ya Kati, isipokua Ethiopia ambao wananusia nusia, watafikia hatua hiyo miaka mingapi ijayo? Itakuwa miaka 15,20,25 au labda 30? Yaani kwenye masuala kama hayo Kenya huwa tupo kwenye upweke wa aina yake, mithili ya paka shume. Sio siri bana, ukanda huu Kenya ndio baba lao. [emoji1139][emoji1139][emoji1139]
Itachukua miaka 30 ijayo kwa Kenya kuweza kuacha kutegemea Chakula cha msaada, Kenya ni nchi pekee duniani iliyopo katika kundi la uchumi wa kati lakini bado wananchi wake wanakufa kwa njaa na inategemea Chakula cha msaada.

Kama ambavyo Sudan imeshushwa toka kundi la uchumi wa kati na kurudi katika kundi la uchumi wa chini mwaka huu, hata Kenya kuna uwezekano mkubwa miaka ijayo ikashushwa baada ya kufanyika kwa "rebase" ya uchumi, haiwezikani nchi yenye uchumi wa kati lakini watu wanakufa kwa njaa na nchi itapewa misaada ya Chakula kila mwaka, huo ni "Pseudo economy".
 
Actually Uganda is more realistic go through how Ghana economic growth after oil export started!
Labda hayo mafuta ndio yawaokoe waganda, lakini kwa mwendo huu wa ukuaji uchumi wao, itawachukua muda sana.

Haya mafuta mbona sioni effect yake kwa nchi kama Angola ambayo ni namba mbili kwa uzalishaji wa mafuta Afrika, lakini uchumi wake haufanyi vizuri sana, au Sudan ambayo mwaka huu wameshuka daraja.
 
Kwahivyo Kenya itakuwa iliwatangulia hawa vibwengo kwa miaka kama 27 hivi? Maanake Kenya iliingia kwenye kundi la uchumi wa kati mwaka wa 2014. Alafu mwaka huu wa 2020 Kenya imeingia kwenye kundi lingine la uchumi wa '3 digits'($100B+). Sijui majirani zetu wengine ukanda huu wa Afrika Mashariki na ya Kati, isipokua Ethiopia ambao wananusia nusia, watafikia hatua hiyo miaka mingapi ijayo? Itakuwa miaka 15,20,25 au labda 30? Yaani kwenye masuala kama hayo Kenya huwa tupo kwenye upweke wa aina yake, mithili ya paka shume. Sio siri bana, ukanda huu Kenya ndio baba lao. [emoji1139][emoji1139][emoji1139]
Mkinasuka hapa huu uharo ulioandika utamake sense sana lakini for now you still poorest of the poorer

Endeleeni kupita bakuli la msaada wa chakula msiendelee kufa njaa kwa uvivu.
Screenshot_20200707-190902~2.png
 
Rwanda Uganda wanakwama wapi miaka 20 ni mingi sana[emoji50]
Rwanda haiwezi chukua muda mrefu nawapa miaka tatu,uganda 4, maximum kina Burundi na south Sudan ni shithole inaeza kua ata miaka 30
 
Rwanda haiwezi chukua muda mrefu nawapa miaka tatu,uganda 4, maximum kina Burundi na south Sudan ni shithole inaeza kua ata miaka 30
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Burundi ndio wana per capital ya $309 hawa jamaa sipati picha mwananchi wa kawaida kule anaishi vp
 
Itachukua miaka 30 ijayo kwa Kenya kuweza kuacha kutegemea Chakula cha msaada, Kenya ni nchi pekee duniani iliyopo katika kundi la uchumi wa kati lakini bado wananchi wake wanakufa kwa njaa.
Mkinasuka hapa huu uharo ulioandika utamake sense sana lakini for now you still poorest of the poorer
Endeleeni kupita bakuli la msaada wa chakula msiendelee kufa njaa kwa uvivu. View attachment 1500264
Vijana wa Lumumba buana mna kichaa. Nchi ya Tz na rasimali zake zote bado huwa inapokea misaada kwa wingi zaidi, tena misaada ya kibajeti. Hela za kuwafunza watoto wenu na za kuwalipa walimu wao, madaktari na manesi huwa zinatoka kwa mabwana zenu mabeberu kila mwaka. Kutoka kwa kanchi kadogo kama Sweden! 😁 Mnawakebehi UG ila nyie pia mpo kwenye kapu hilo hilo. FACT: GDP zenu, $63.18B(Tz)+$34.39B(UG)= $97.57B, -ve $3.43B GDP ya Kenya @ $100B.
 
Vijana wa Lumumba buana mna kichaa. Nchi ya Tz na rasimali zake zote bado huwa inapokea misaada kwa wingi zaidi, tena misaada ya kibajeti. Hela za kuwafunza watoto wenu na za kuwalipa walimu wao, madaktari na manesi huwa zinatoka kwa mabwana zenu mabeberu kila mwaka. Kutoka kwa kanchi kadogo kama Sweden! [emoji16] Mnawakebehi UG ila nyie pia mpo kwenye kapu hilo hilo. FACT: GDP zenu, $63.18B(Tz)+$34.39B(UG)= $97.57B, -ve $3.43B GDP ya Kenya @ $100B.
Mshahara ukatoka Sweden? Do you have any idea about this nonesense?
Your gdp is $99B ,n btw Tz is pushing so hard so don't you guys relax
 
Back
Top Bottom