Uchumi wa China ukweli ambao wengi hawaujui

Mchina hapa kabeti vyema aiseeView attachment 2222200
Yani, na nasikia ziko kwenye viwanda vingi viwe vya magari, vya kutengeneza mashine kubwa kubwa. Wakati wanauza hawakutafakari. Kuna kipindi aliwekeza sana kwenye soka naskia alitaka atengeneze league ya kuvutia kama ilivyo ya Uingereza lakini akafail
 
Mchina hapa kabeti vyema aiseeView attachment 2222200
Time ya china inakaribia japo anasogea taratibu ata USA haikuwa super power mara moja ilikaa kmya mpka anguko ya ujerumani, England na Russia kama watawala wa Dunia nae akapata nguvu ndio itakavyokuwa kwa china maana sasa hv anajua nchi maskn ashakamata soko now anapambana awashike na wakubwa
 
Kweli kabisa, uchumi wa kijamaa ulifeli,na ndio sababu Tanzania tumelemaa mpaka sasa. We need to change.
 
Wachina wanawekeza mpaka marekani , nao pia ni wawekezaji wazuri tu. Halafu mbona Tanzania tumefungua mipaka ya uwekezaji toka awamu ya Mwinyi je tumewafikia maendeleo china Basi hata Singapore je tumewafikia maendeleo?🤔
 
Kwa hiyo Sasa hivi kinachokwamisha maendeleo ya Tanzania nini ?🤔 (a) Ni sera za ujamaa zilizoshindwa kufaulu (b) Ubepari nao umeshindwa kufaulu
Unapaswa kujua Tanzania is a mixed economy,na sio 'pure capitalism'
 
Unapaswa kujua Tanzania is a mixed economy,na sio 'pure capitalism'
Kwa hiyo mixed economy pia nayo imeshindwa kufaulu mpaka sasa katika ardhi ya Tanzania hata baada ya Mwalimu kung'atuka
 
Changamoto kubwa iliyopo nchi za Afrika ni suala la urasimu na kutokuwa na uhakika wa nishati hasa hapa Tanzania.
 
Suala la brands za mchina kuteka soko la dunia ni kutokana na low cost of production ikilinganishwa na nchi nyingine ukiacha india. Pia makampuni mengi yanaamua kuoutsource manufacturing kwenda Asia kutokana na theory ya Asia and Automation.
 
Mkuu Namba 5 umedanganya katika Makampuni 10 makubwa ya China yote yanamilikiwa na state au Wachina,hamna company hata 1 kati ya hayo 10 inayomilikiwa na mwekezajj kutoka Ulaya.
 
Mwenyewe namshangaa mtoa mada ili uchumi wako ukue vizuri kayika Nchi,Investment katika Nchi husika lazima zifanywe na wazawa na sio vinginevyo.
 
Binafsi hii ishu niliijua kitambo sana baada ya ku-exchange na American mmoja.

Kwamba, sera nzuri za China ziliwavutia wawekezaji kutoka Ulaya na Marekani kwenda kuwekeza China.

Hao wawekezaji kutoka USA na Ulaya wanaona ni bora kuwekeza China kwa sababu mbalimbali. Ukiachilia mbali sera za China, ila pia China kuna Cheap Labour + Raw Materials. Kwa mfano, ni gharama kubwa kumlipa mfanyakazi ndani ya USA, ukilinganisha na kumlipa Mchina anayefanya kazi ile ile ndani ya China.

Bongo tumeendekeza sana rushwa. Bila rushwa jambo lako halipitishwi na wenye mamlaka mfano kupewa tenda fulani.

Tanzania hakuna uzalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…